Jumuia ya Watanzania waishio Dallas, Texas,  itakuwa na mkutano mkuu wa jumuia tarehe 4, July 2009 jumamosi kuanzia saa kumi na mbili (6:00 pm) jioni.

  Mojawapo ya sababu kubwa za mkutano huu ni kutoa huduma kwa mtanzania yeyote anayehitaji kubadili au kuongeza muda wa "Passport".  Huduma hii, kwa kawaida hutolewa huko ubalozini, Washington DC.  

Hivyo kwa ajili ya kupunguza gharama za usafiri kwa wale waishio Texas na state zingine za hapa kusini, tumeomba ubalozi utume mjumbe kutoka DC ili kuja kutoa huduma hii hapa Dallas.  Ubalozi utatuma mjumbe ikiwa tutakuwa na idadi kubwa ya watu wanaohitaji kuhudumiwa. 

 Tunaomba na kuwasihi muorodheshe majina kwa 
Ndugu Juma Maswanya wa Houston (1-281-989-3724) 
au hapa Dallas kwa 
Simon Nkanda (469-585-8476-e-mail snkanda@verizon.net
au 
Abdul Amiri (214-535-6329:e-mail-abd633ami@yahoo.com

hii iwe kabla ya tarehe 19, June 2009 ili tuweze kupewa fursa hii ya pekee na Balozi wetu.  Ndugu Maswanya ameshughulikia hili swala hapo awali na palikuwa na mafanikio mazuri sana kwa wote waliohitaji huduma ya passport.
 
Asanteni na tunatarajia kuwaona siku ya mkutano, tarehe 4 July 2009.
 
Simon J. Nkanda
Jumuia ya Watanzania, Dallas

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...