hasheem Thabeet akiingia katika mnuso wa kumpongeza kwa kuwa NBA draft pick 2 usiku wa kuamkia leo jijini New York, ikiwa ni masaa kadhaa kabla hatujajua Hasheem atachezea timu gani
Hasheem akila pozi mbele ya bango lililoandaliwa rasmi kwa ajili yake kwenye mnuso huo
hasheem akiwa na balozi wetu wa kudumu katika umoja wa mataifa dk. augustine philip mahiga
hasheem akiwa na rais wa shirikisho la mpira wa kikapu nchini (TBF) richard kasesela ambaye yuko new york kuwakilisha wabongo katika siku hii ya kihistoria




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 33 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 26, 2009

    Oklahoma huyu...

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 26, 2009

    hongera dogo kwa kutuwakilisha watz mdau uk

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 26, 2009

    Kapata ulaji Memphis Grizzlies akashirikiane na kina Gasol.
    Hongera sana, liletee taifa sifa ufungulie milango na wengine.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 26, 2009

    Kokote kule mradi NBA na bendera itapepea, sasa Watanzania Wataingia Olimpic Basketball South Africa? Wataalam toeni maoni inakuwaje nchi ingine inashirika mchezo fulani Olimpic na nchi ingine inakuwa haina muwakilishi? Yao ming ndio anafaya China iingie Olipic a kunakuwa na factors zingine? Tunapenda kuomuona Hasheem akicheza na Watanzania wenzie pia. Cha maana si kutizama TV NBA cha maana ni changamoto kuinua michezo yote kwa ujumla ndani ya Tanzania. Msitegemee sana mpaka watu waje kuokota vipjai na kuviuza. Endelezeni na kugundua na kuuza vipaji vyenu wenyewe. Mfano Ray Allen alikataa kuwa na Agent kanegotiate deals zote mwenyewe. Hasheem kuwa na agent mzuri kumesaidia, tunamshukuru sana agent wake aliyemleta Marekani na kumfanya ajulikane na kuanzia high school hadi College na leo kuingia NBA draft. SHAQ NA LEBRON IN ONE TEAM? HASHEEM NA KG IN ONE TEAM? HASHEEM FOR CELTICS BOSTON, OKLAHOMA WATAMUUZA KWA CELTICS NA KUMCHUKUA PIERCE!!

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 26, 2009

    Hii habari haijatulia. Huwezi kusema anakuwa 2nd draft pick halafu hujui ni timu gani anayoenda. Memphis Grizzlies ndio wana rights ya 2nd draft pick, na wao ndio wenye rights za ku trade pick hii incase they choose to. Kwa mfano, Hasheem hawezi kuwa drafted namba 2 halafu akaenda LA Clippers kwani Clippers hawana namba 2 wanayo namba 1.

    Congratulations to Thabeet and your family and go to Memphis and become the BEAST!
    All the best,

    ReplyDelete
  6. PhatlorenzoJune 26, 2009

    Congrats Hasheem, what a day! All your hard work has finally paid off. Now keep working hard.. Go out there and make us proud.
    Phatlorenzo, MN

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 26, 2009

    Teh teh treeeeeeee
    With the second pick in the draft, the Grizzlies take Hasheem Thabeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeet.

    Tumuombe kwa mwenyezi mungu afanye vizuri

    ICTM Mapendo

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 26, 2009

    Teh teh treeeeeeee
    With the second pick in the draft, the Grizzlies take Hasheem Thabeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeet.

    Tumuombe kwa mwenyezi mungu afanye vizuri

    ICTM Mapendo
    Mr Suavito

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 26, 2009

    http://www.nba.com/video/channels/draft/2009/06/25/nba_090625_draft_pick2.nba/

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 26, 2009

    sasa huyu raisi wa TBF amekuja huku kufanya nini?
    amehusika vipi na Hasheem kuja hapa? alipokuwa bongo mbona hawakumuona? na sidhani hata kama wangempa number kucheza pazi or timu ya taifa something
    leo vitambi mbelembele kuja kwenye draft ningekuwa mi ndo hasheem ningewatosa tu

    ReplyDelete
  11. AnonymousJune 26, 2009

    duh hongeara sana dogo. mungu akusaidie ushine sana NBA ili sisi tuendelee kujivunia wewe. nampongeza girlfriend wako pia yule mtoto wa kimarekani natumai hutamtosa baada ya kuwa maarufu!
    Antony

    ReplyDelete
  12. AnonymousJune 26, 2009

    MZEE WA SINZA USHATOKA HIVYO TENA,AT LEAST WAJENGEE WABONGO HATA UWANJA WA BASKET WA MAANA MANAKE NAJUA AFTER SEVERAL YRS U WILL BE ABLE TO DO SO KIRAISI TU,TAIFA INDOOR IS ALL "STINKING",BIG UP BIG DAWG!!

    MDAU,ATL!!

    ReplyDelete
  13. AnonymousJune 26, 2009

    you go boy..gud luck 2 u...

    ReplyDelete
  14. AnonymousJune 26, 2009

    Good move, nilikuwa naombea apate Oklahoma sababu wana guard mzuri. Lakini still anaweza kudevelop quick

    ReplyDelete
  15. AnonymousJune 26, 2009

    hongera hasheem! Tunakutakia mafanikio makubwa katika safari yako.

    ReplyDelete
  16. AnonymousJune 26, 2009

    Hongera Hasheem, Wakilisha mwana, kwa wasiojua vitu vyake chekini hapa http://www.youtube.com/watch?v=5GFC5892OTs

    Michuzi inyonye hiyo weka kwa baraza.

    ReplyDelete
  17. AnonymousJune 26, 2009

    Heko sana Hashim Thabit.

    Jitahidi sana kufanikisha kilichokupeleka huko ila usisahau ulikotoka (Unafahamu mwenyewe maisha yako kabla hujafikia mafanikio hayo). Wekeza nyumbani kwasababu itafikia muda ni lazima urejee huku (usiwe na mawazo ya walio wengi wasiopenda kurudi Dar). Nyumbani ni nyumbani tu Hashim.

    Hongera sana. Tena Hongera.

    ReplyDelete
  18. AnonymousJune 26, 2009

    Memphis Grizzlies ndio timu yake...

    ReplyDelete
  19. Hongera sana kwa kazi nzuri na bidii.

    ReplyDelete
  20. AnonymousJune 26, 2009

    mmh na joto lote hilo na hiyo four piece ni kazi kweli kweli

    ReplyDelete
  21. AnonymousJune 26, 2009

    wakondya mwan wise! maana yake asante mtoto wa dad!

    ReplyDelete
  22. AnonymousJune 26, 2009

    inapendeza kuwa Tanzania inawakilishwa vema.. ila bado ni kupitia juhudi za mtu binafsi.. serikali bado haijafanya mkakati wa makusudi kuinua michezo mingine inayoweza kuletea nchi sifa kama basketball au riadha, ingawa naipongeza serikiali kwa kuinua soka.

    BIG UP Hasheem!

    ReplyDelete
  23. AnonymousJune 26, 2009

    hashim angalia usije ukanunua uraia wa USA, maana tunapenda uendelee kutangaza bongo land

    ReplyDelete
  24. AnonymousJune 26, 2009

    dah! wacheki hawa wanyamwezi wa memphis wanavyomuua mchizi wetu...kweli kazi ipo !!..

    gonga hapo..http://www.memphisflyer.com/BeyondtheArc/archives/2009/06/25/the-case-against-thabeet

    ReplyDelete
  25. AnonymousJune 26, 2009

    jamani hapa ninabishana na mkenya naambia heti sio mtanzania niyakweli haya

    ReplyDelete
  26. AnonymousJune 26, 2009

    Wadau Kolikoli ameishia wapi ?

    ReplyDelete
  27. AnonymousJune 26, 2009

    jamani uyu ni MTANZANIA?????

    why hakuna profile yake apa??

    michuzi fatilia ilo,uyu ni celebrity sasa so mambo ya kuanika kilakitu chake-backgroud zake ni muhimu tupate pa kujitambia,,,maana mt kilimanjaro na serengeti ziko kenya sasa

    ReplyDelete
  28. AnonymousJune 26, 2009

    Hasheem hongera sana. Ila itakapofikia suala la mchumba na kuoa urudi nyumbani- uoe mwanamke wa nyumbani. Huyo demu wako wa kimarekani umuache.Kwa kweli sipendi wanamichezo maafuru toka Africa wanapooa wageni. Africa kuna wanawake pia. Na hii itasaidia kuwekeza nyumbani. Angalia Yao Ming- mkewe mchina Mwnzie, Dikembe Mutombo-mkewe Mkongo mwenzie.Fuata nyayo hizo.

    Kila la kheri.

    ReplyDelete
  29. AnonymousJune 26, 2009

    Hasheem kilichokupeleka USA ni kucheza basketball zingatia hilo kwanza na mengine yatafuta. pia kumbuka familia yako, mama na wadogo zako, kwa sasa hivi.

    kwa watanzania wenzangu muachane huyu mtoto afanye kazi yake. acheni kumzonga na matatizo yenu, mara mambo ya kuwekeza nyumbani, sijui ajenge uwanja wa basketball. inakera sana.

    NAKUTAKIA KILA LA HERI.

    ReplyDelete
  30. AnonymousJune 26, 2009

    Huyo Bibo na hiyo TBF yake anawakilisha watanzania kivipi jamani? Watu kurukia mafanikio ya wengine tu. Nani kalipia nauli yake! Hasheem ndio anayetuwakilisha wengine ni kumsupport tu. Huyu jamaa ataitangaza nchi yetu kuliku safari zote za JK za kutembeza sahani!

    ReplyDelete
  31. AnonymousJune 26, 2009

    Ananymous wa June 26, naona upo nyuma kidogo Gasol hayupo tena Memphis kwani alishaendaga LA Lakers

    ReplyDelete
  32. AnonymousJune 27, 2009

    anon wa 10:55 pm,

    Gasol mkubwa ndiyo yuko Lakers. Mark Gasol mdogo mtu alipelekwa Memphis na Lakers akitokea Europe. ndoto ya Gasol brothers ni kucheza timu moja, hivyo labda siku moja Mark aturudi tena Lakers ambao ndiyo walikuwa na rights zake wakati akicheza Europe.

    Mark Gasol na mzungu mwingine Darko wote ni 7ft centers na wako Memphis. Thabeet itabidi akaze msuli kwelikweli ili aweze kuwanyang'anya namba.

    ReplyDelete
  33. AnonymousJune 27, 2009

    bela mnyalukolo Mahiga

    kamwene bee mwagito sa ukoo,wanoge wana na mama

    alee makasi

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...