KAKA MICHUZI POLE KWA KAZI NA ASANTE KWA LIBENEKE LAKO HILI LINALOTUBURUDISHA KILA SIKU.
MIMI NI MDAU WAKO MKUBWA HAPA USWIDI, BILA KUSOMA MARA MBILI KWA SIKU BLOG YAKO SILALI.SASA KAKA MICHUZI MIMI NANAOMBA UNIFIKISHIE UJUMBE WANGU HUU KWA WAKAKA WALE TU WENYEWAATOTO NA AMBAO WAKO SINGLE, PIA WASIOTEGEMEA KUPATA WATOTO TENA.
MIMI NI MDADA WAKITANZANIA NINAYEISHI HAPA KWA MDA SASA. NILIOLEWA NA MWANAUME WA KISWIDI KWA BAHATI MBAYA TULISHAACHANA NA NINA WATOTO.
NINATAFUTA MCHUMBA WA UKWELI NA ALIYEKO SERIOUS.ANAYEISHI SWEDEN NA ISIWE NI CHINI YA MIAKA MITATU.
KAMA KUNA MTU MWENYE SIFA HIZO BASI TUWASILIANE KWA EMAIL: mbetaz1@hotmail.com
ASANTE
MDAU WA USWIDI.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 17 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 03, 2009

    OT: Mbona kaka michuzi that damn icon ya kuonyesha page view imedisapper?

    Na lini umeudisha hii word verification tena. Kweli unaspam msgs au kutuchosha tu?

    Sorry I didn't mean to hijack the topic.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 03, 2009

    Mh!!!!!!!!! wewe umegonga mwamba,Yaani atakae jipendekeza atakufa.Mabinti walio Ulaya haswa wa kiAfrica hawafai wengi wao,Kwani wanaweza kukunyonya na ukaishiwa akakimbia sembuse wewe na watoto wako?????.Kama kashindwa huyo fala wa kiswidish sasa unataka kuuwa Mbongo?Tafuta wawest Africa mascam wenzenu.Ukiwa na mwanamke wakizungu hata ananunua chakula na mambo mengine,wadau kama nikuowa Home unaweza kidogo Ulaya imekuwa ngumu kama jiwe.{MDAU}

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 03, 2009

    Hello bibie,
    Mimi nipo tayari na nina vigezo vyote unavyovitaka,ila tu naomba unifahamishe yafuatayo.

    1.Ni sababu gani zilikufanya uachane na mwenzako ili "jumbabovu" licje likaniangukia.

    2.Hao watoto wa huyo jamaa watanipa hesma kama heshma wanayoipata mababa wa kufikia huku Tanzania,au wataniita "step-monkey!"

    3.Kama chanzo cha kuachana kilikua ni tabia zako mbaya,je umeshajirekebisha?

    4.Nilitegemea tupate taarifazako zaidi ikiwa ni pamoja na picha yako ili tuone hau siriasi yuu aa!

    5.Wewe unafanya shughuli gani huko mbali na kulea hiyo familia yako.

    Naomba ujibu hayo hapo juu,sababu mimi nikipenda huwa napenda kama bwege na hata mke niliyekua naye aliniacha sababu ya kupagawa kwangu na mapenzi na nikawa zezeta kabisa.

    Mkulima-kijijini Gezaulole.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 04, 2009

    mimi nakaa houston texas na mdate mswedish wewe utakuwa umeshindikana kwa sabu zifuatavyo
    -Hawa watu waswede wanamapenzi yakweli na sio kama wanaume wa kitanzania.
    -wanaume wakitanzania wako nyuma sana kimapenzi sanaa. hawana experience.
    -wanaume walitanzania hawarespect mapenzi yaani hawaapreciate.
    -wanaume wakitanzania wanabagain mapenzi na pesa. kutwa nzima kuplann vitu hela hawana .
    -wewe hao watoto watakuwa sio wamswed mzungu damu yake haichezewi kama yawaafrika kutwa nzima kutelekeza familia.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 04, 2009

    aaah dada hili sio tatizo njoo rinkeby Alle tunapofanyia mazowezi ya football kuanzia kuanzia saa kumi na moja jioni tupowengi na tena kwa vile una makaratasi dada kama kumsukuma mlevi.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 04, 2009

    tafuta teja jingine la kiswidi. wewe utakuwa haufai kabisa maana wanawake wengi wa kiafrika walioolewa na waswede wanainjoyi iweje wewe uachike?

    ReplyDelete
  7. Al MusomaJune 04, 2009

    ...hawarespect...yaani hawaapreciate...

    Nijulishe kama ulishawahi kuona kauli ya kufurahisha kuliko hii toka mwaka huu uanze na ilikuwa inasemaje...

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 04, 2009

    We mdada fafanua vizuri wanaume wa kitanzania hatuna uzoefu gani? Au uzoefu wa pesa ambazo ndizo zinafanya msitulie na mwanaume mmoja kwa tamaa zenu tu!

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 04, 2009

    kweli Annoy 12.02 Am natumai atakuwa mdada anachekesha sana. Maskini ayakutana na mwanaume wakibongo wakampa mambo mazuri. Mie naamini wanaume wakibongo wanatrue luv isipokuwa mabinti wenyewe wanatamaa kupitiliza.Wanacopy life.wanataka mwanaume aliye na mali,mfano Awena gari,nyumba na pesa ndio anataka awe naye. Inshort hawataki tabu ya kutafuta au waanze chini kutafuta na boyfriend wake, bali kutaka amkutenavyo tayari. Narudi kwa anayetafuta mchumba. Ukweli mnaotafuta hamsemi ukweli sababu ya kuachana na kama ni wewe ndio chanzo cha tabia mbaya. Embu fikiria umezaa na jamaa watoto inawezekana wawili au watatu mda wote mmeishi leo akuache bila sababu wala uchungu na watoto wake. We unamatatizo tena itakuwa tabia yako mbaya haivumiliki wala kuonekana kubadilika. Halafu unataka mchumba mwingine aliye serious wakati we usiserious wako hatuujui, Pili umeweka masharti makubwa awe na miaka mitatu sweden Umetega nini kwake kama sio pesa na unaamini atakuwa na uzoefu wakutafuta cash hapo sweden. Hapo hakuna cha mchumba serious unamtaka kwa mapenzi bali Unataka mtu wakukusaidia kulea watoto mambo umeona yamekuwa tight. USHINDWE WIZI MTUPU. NANI AKALEE WATOTO WA MWANAUME MWENZIE. BYE

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 04, 2009

    Pole sana dada...kutokana na maelezo yako inaonekana umemiss sana mapenzi ya kitanzania/kiafrika ...kwa uzoefu wangu ni vigumu sana kuishi na hawa watu wa scandinavia awe wa kike ama kiume kwani mfumo wao wa maisha ni tofauti sana na wazungu wengine ama nchi nyingine.. hauko peke yako... wapo wengine wengi sana waliokwisha divorce japokuwa wengine waliingia kwenye ndoa kwa sababu zao nyingine..
    tukirudi kwenye ombi lako.. ni kuwa unahitaji kutoa taarifa zaidi.. kama unafanyakazi ama unategemea UB40,wewe una umri gani? sababu zilizosababisha muachane na huyo Mswidi.. n.k otherwise nafikiri itakuwa ngumu kwa mjamaa waheshima zako kujitoa mhanga...

    ReplyDelete
  11. AnonymousJune 04, 2009

    he he heeee kazi kweli kweli. Haya mama tafuta usichoke utapata. Ingekuwa unataka wakitanzania ningetoka mimi hapa ningevumilia hata kama una visa. Lakini kwakuwa unataka wa huko haya endelea.

    ReplyDelete
  12. AnonymousJune 04, 2009

    hahahaha, huyu mdada nyie wote hamjagundua kua anafanya practical joke.kasema mtu asiwe chini ya miata mitatu.
    halafu kama ni kweli anataka mume wa kibongo,tatizo liko wapi, mnaongea negative,bla bla bla! acheni hivi.
    Hey,dada yangu ya wa swidi,pole kwa kuachwa na pia kuachiwa watoto. nakuombea Mungu upate mume unayemtafuta.

    ReplyDelete
  13. AnonymousJune 04, 2009

    WANAUME WA KITANZANIA HAMNA PESA KUTWA NZIMA KELELE NDIO MAANA WALIONAZO WANAJULIKANA KWA MAJINA ..wewe nataka kukujibu hamna uzoefu wa mapenzi . hamko desired, suruali chini ya tumbo mambo gani hayo . PESA HAMNA KWANI UONGO ,HAMNA KABISAAA KELELELEL KUJISHAUA.COLOGNE YENYEWE TABU

    ReplyDelete
  14. AnonymousJune 05, 2009

    Mimi ni mdada wa kitanzania na nina mume mtanzania pia.Napenda kumjibu mdada anayesema wanaume wa tanzania hawana pesa,hawajui mapenzi,bla bla.wewe umedate wanaume wangapi wa kitanzania?halafu nikukumbushe,pesa haijengi mapenzi hata siku moja.kumbe ndo maana unaona wanaume watz hawajui mapenzi coz hawana pesa.pole sana,"miss gold digger"!hapo umewatukana baba yako,mama yako,shangazi,mjomba,nk.Dada,Pesa au material possession haijengi mapenzi.na pia kwanini unamsema vibaya huyo mdada,kwani wewe umedate waswidi wote duniani?utajuaje huyo mswidi wake ana tabia gani! hahah,inaonyesha unawekwa kama slave na huyo mswidi wako.wewe nani kakwambia wanaume wa kz wanavaa suruali kiivyo,labda ambao wamekuzunguka,coz tokana na mawazo yako,inaonyesha umezungukwa na watu wenye mawazo kama wewe,narrow minded.

    ReplyDelete
  15. AnonymousJune 05, 2009

    Napenda kumjibu huyo dada anaesema wanaume wa kitanzania hawafai,hawana pesa,nk.Inaonyesha wewe dada mtoto wa uswahilini,shule hujaenda na ilia ni dream yako kuolewa na mzungu kwasababu ya stereotype. kama baba yako alikutelekeza,pole sana.mimi mwanaume wa kitanzania,nimeoa mswidi na hawajahi pata mapenzi na care ya hali ya juu kama ninayompa.she is stunning,tall,smart,sexy body na wanaume wote wa kiswidi wanamtolea macho.tokana na experience yake,wanaume wa kiswidi wako selfish,full of themselves. kwahiyo dada,usichukulie experience yako ukadhani ni waswidi wote wako hivyo au watanzania wote wako hivyo. halafu wewe kama mwanamke,badala ya kumshauri na kumhurumia huyo mdada,unakua against nae.Put yourself in her shoes!!! kwahiyo kama wewe familia yako ilikutosa,na pia watu wanaokuzunguka ndo wanavaa suruali chini ya tumbo, basi pole sana. wewe subiri kilio chako hapo huyo mswidi wako atakapo kudivorce, kwani si ndo westerners walivyo,divorce kila siku,hawathamini ndoa na hawawezi ku compromise.nimefurahishwa na maoni ya mdau mmoja,kakuita "miss gold digger".inakufaa kabisa.kwa kifupi,unaonyesha hujaenda shule.

    ReplyDelete
  16. AnonymousJune 05, 2009

    huyo mdada anaesema ana mdate mswidi na kumpondea huyu mama anaetafuta mwanaume wa kibongo na kuponda kua watanzania wanaume hawana hela,hawajui mapenzi!!
    Nina uhakika huyo mswidi unaemdate ni kibabu hivi, kishachoka maisha,basi ndo umejibebea. acha kuwakandia wanaume wa kitanzania. i've met many of them who are smart,educated,doing well with their lives,doctors,pilots,accountants,lawyers,entrepreneurs. wewe kama umezungukwa na wanaume watanzania wenye mawazo kama ya kwako,pole sana.

    ReplyDelete
  17. AnonymousJune 05, 2009

    Mimi ni msichana wa Kitanzania nataka nijibu dada zangu ambao wamesema kuwa wanaume wa kitanzania hawana pesa, maneno mengi mdomoni. Lakini kumbuka kabla hujapata huyo uliyekuwa naye sasa hivi ulipitia kwa wanaume wa kitanzania. Kwa hiyo msiwakandie kaka zenu. Mwanamke wa kitanzania hapendi mwanaume wa kiobongo kwa mapenzi anafuata hela aliyokuwa nayo. Kama hana hela ni lazima urafiki wa mapenzi utaisha tu. Kumbuka ulikotoka usiendelee kukandamiza wenzio. Asipokupa hela ya kununulia mafuta ya kupa basi unaona hakundi, lakini ni lazima uonyeshe penzi. Na mara nyingi wanaume wenye akili kama anataka anania nzuri na wewe pengine itafika mahali atataka muoane, lakini akiona unapatient ya penzi ni hela tu, ni lazima na yeye atakutpilia mbali tu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...