Kwa walio jiji la London tu
Brother Michuzi habari za leo.
Naomba uniwekee ujumbe wangu mdogo kuhusu akina dada na kaka waishio mjini london uk. Mimi naitwa Fabian na nimefika hapa london for a short course sio muda mrefu, ninakaa london bridge. naomba kuwauliza wenyeji wa mji masuali yafuatayo:
1.MKO WAPI? nakusudia ni wapi mahali ambapo watanzania huwa mnakutana angalau kwa siku za wiki endi kupiga stori, kuchil au hata kutoka jasho kwa kucheza mpira.
2. Niliwahi kusikia kuwa baadhi ya watanzania hukuna ubalozini mara moja kila wiki? jee hii ni kweli? na kama kweli ni kila mtanzania anakaribishwa au ni lazima uwe mwanachama wa ccm?
3. Najuwa kuna umoja wa watanzania, kuna anaejuwa contact za wahusika? ningelipenda kujiunga na umoja huo.
4. KADI FEKI: toka kuja hapa kila card ninunuayo kupiga simu naona zinanitapeli, either sio kweli muda zinaosema unao au ni vigumu kupata connection. ndugu zangu kuna anaeweza ku-recommend card muruwa ya kupiga simu bongo?
Nawashukuru wote na namshukuru brother michuzi kwa kukubali kuweka post yangu hapa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 20 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 09, 2009

    karibu london, tumia card inaitwa talkhome na ni pound tano, hiyo ni uhakika na minutes ni za uhakika. kuhusu ssehemu ya pombe na kutoka jasho(mpira) panda bus 149 towards edmonton(north london) shuka angel cornel.then uliza park ilipo watanzania huwa wanacheza mpira hapo, halafu tukimaliza tunaenda kuburudika kwa waganga(three crown) na kama una nguvu zaidi unaingia club volts just across the road, so karibu sana

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 09, 2009

    Wewe umefika Ulaya sasa,Achana na story BEBA BOX,eeebo.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 09, 2009

    Acha Uzushi wewe mwendawazimu, kama umeweza kuandika humu kwa michuzi, kwa nini usiGOOGLE huo Ubalozi wa Tanzania nchini UK, ama CCM UK, ama Jumuiya za Watanzania UK, hakuna watu wenye vichwa mbovu hapa UK, nia yako haswa ni kutaka kujua kuhusu CCM UK na si lolote, halafu uanze kuleta uwendawazimu wako na kuchafua watu roho, hauna muda mrefu umeshaanza unafiki hapa UK, Watanzania hawana mpango na wapotosha jamii kama wewe. Huna jina kamili wala contact kamili (unakaa kwenye daraja la London)ushauri usichungulie chungulie unaweza kuzama hapo London Brigde halafu Wabongo tusikuchangie kurudisha jeneza lako. Pili nenda kajiandikishe Ubalozi wa Tanzania nchini Uingereza hapo Bond Street, ukishindwa wasiliana na

    Home Office
    Reporting an illegal immigrant or other offence
    If you know someone is breaking immigration laws, for example by being in the United Kingdom illegally or by employing an illegal immigrant, you can email us to give us information about it. We may not be able to acknowledge your email but we will pass it on to the local immigration team in the appropriate part of the country. Where appropriate, they will investigate and take action.

    To enable us to send your information quickly to the local immigration team closest to the offence you are reporting, please help us by putting the specific place (for example Croydon) or the specific postcode (for example CR0) in the subject line (title) of your email. Please also try to give us as much information as possible about the immigration offence (for example names and addresses), to help our investigation.

    We treat all personal information as confidential. This means we will not tell the person involved that you contacted us. It also means that we will not be able to tell you what was done as a result of your information.

    Email: UKBApublicenquiries@ukba.gsi.gov.uk

    Anyway kwa ufafanuzi ama maelezo zaidi piga namba " 999 " kwenye call box utapata majibu sahihi na ushauri wa kurudi Tanzania.

    Ni mimi - Mzee wa Uyagauyaga, No:10 Downing Street,London, Tel: 0800 118 118

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 09, 2009

    tunaomba picha yako tuione kwenye blog hii tujue kama mzushi au vipi

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 09, 2009

    card nzuri ni talk home, ni kama five pounds hivi, utaongea weeee. pili, ukitaka kukutana na wa bongo, nenda club afrique, ndio wamejaa tele huko.
    hope nimekusaidia kidogo. ahsante.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 09, 2009

    Wewe Anon:Tarehe June 09, 2009 5:27AM.

    Acha kuparamia majina ya watu. 'Mzee Wauyauyaga' (na siyo 'Mzee wa uyagauyaga' kama ulivyoandika) haandiki mambo ya kijinga kama uliyoandika wewe.


    Mzee is always 'happy to help' whenever possible (Read: 'whenever possible') and never put down 'poor'/'unprivileged' people like you did to that 'gentleman/woman'.

    Inabidi UKUE wewe Anon hapo juu!

    Michuzi, you always have your own hidden agenda of 'turning your eye blind' on my comments! I hope, this one would go through at last!


    It's me, real Mzee Wauyagauyaga.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 09, 2009

    Kila jumapili ya mwanzo na ya tatu ya kila mwezi, unaweza kukutana na wabongo kibao pale st.Anne's Lutheran church, kanisa liko karibu na kanisa kubwa la katoliki st Paul's cathedral, tube station ni st paul's. muda ni saa nane mchana. unakaribishwa saaana na utajisikia uko nyumbani!

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 09, 2009

    mzushi nunuwa card ianyoitwa royalnomi hii utazuwa siku nne zima uwongo wotte wa ulaya peleka bongo

    ReplyDelete
  9. simbaurangaJune 09, 2009

    Kadi talkhome ama royalnomi ni kiboko zaidi,
    Club Afrique iliopo Cnning town utawapata wabongo ama mitaa ya tottenham kama alivokwambia mdau juu, kama vipi panda treni uende mitaa ya karibu na London, Reading na Slough huko wabongo kwa ndoo.

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 09, 2009

    mjitu kama anonymous wa na wa June 09, 2009 5:27 AMJune 09, 2009 5:23 AM daima itakuwpo tu duniani, ni mijinga, majichwa yamejaa maji, hawafikri lolote ila negative thoughts and negative comments. haina la kufanya na sijui wana lengo gani katika dunia hii.

    mtu kauliza kwa salama kabisa, kama huwezi kumjibu ni lazima ulete utumbo wako hapa?

    Brother michuzi blog ni yako lakini naona kuna haja ya kuwa unaangalia baadhi ya comments na kuzifuta kwani sinatuchafulia hali ya hewa humu.

    ReplyDelete
  11. karibu sana kaka lakini cha ajabu unataka kujua kijiwe cha wabongo cha nini hauna malengo ulipokuja,baa ukatafute nini?nenda ubalozini ndio utapata kila kitu sio humu wabongo wengi wamechanganyikiwa na maisha ya hapa,sasa kama uanataka kuwafuata utaumia fuata yako,nenda kanisani utapata marafiki wa uwakikasio baa,unaenda gesti kutafuta mke//////////

    ReplyDelete
  12. Majibu: 1-Sisi huku huwa hatuna time ya kukutana na kupiga stori, tuko bize na boksi, kwa hiyo kama umekuja huku kwa shoti kozi, bazi malizia kozi yako an urudi nyumbani 2-Huwa tunakutana ubalozini kama kuna shughuli za kichama/kiserikali, siyo kupiga gumzo 3-kama umekuja kwa shoti kozi basi huwezi kujiunga na umoja huo, umoja huo si kwa ajili ya kupiga gumzo, ni kwa ajili ya kusaidia wanachama wakati wa matatizo 4-kadi siyo feki, ukiambiwa una dakika fulani huwa kuna konekshen fiiz na fiiz nyingine ambazo zimejificha. Mwishoni: ukiona umeboreka basi nenda kwenye duka la kahwa na upate kofii kidogo au nenda kwenye mall kusafisha macho, au tafuta boyfrend akupe ubize kigodo - ndiyo maada kila mtu huku ana boifrend au gelfrend - AHSANTE SANA

    ReplyDelete
  13. AnonymousJune 09, 2009

    wewe Tinaa unawazimu sasa? ni wapi aliposema kama anatafuta baa? ndugu anatafuta watanzania ajotowe upweke. labda mwenzagu ulipokuja hapa ulikuwa na wenyeji na hukupata tafrani za kuwa peke yako, tuulize sisi tuliokuja na moja kwa moja chuoni, humjui hata mtu mmoja hapo utafahamu tatizo la dogo hapa.

    Nawe kipojo ushachoka na boksi mchana huu? mbona unaandika utumbo mtupu? kama unayo passport yako hebu soma ndani inashauri ufanye nini unapowasili nje ya nchi. Na kwani kwa vile yeye amekuja kwa short course ndio hawezi kupata matatizo? au akipata matatizo ubalozi hautomsaidia? jinga wewe!

    ReplyDelete
  14. haya umeyataka mwenyewe yaani hawa watu wana hasira zao ,wengi wetu hatujui Bongo ina fanana vipi kwa muda sasa,wengi bills ni nyingi kuliko mapato na zote hizo hapa huitwa stress,sasa wewe kama ni card basi ndiyo hizo ulizo ambiwa mengine tulia kwanza,London wa Bongo kipao uta wapata kazini au college hata kwenye basi usijiingize na urafiki fulani fulani ambao uta shindwa kuja kutoka baadaye kumbuka malengo yako.Usikimbilie kupata MPENZI maana hao wanaweza kukusaidia kujenga au kubomoa sasa tuliza akili yako kwanza,kwa ushauri wangu kama uta penda usipate " rafiki" African hususan Nigerian tafuta mpenzi atakaye kuwa msaada kwako kesho PATA MZUNGU NA HASWA HAO europeans wametulia si kama English.AKILI NI NYWELE KILA MTU ANA ZAKE(NA HUO NI USHAURI WA BURE TU)

    ReplyDelete
  15. AnonymousJune 09, 2009

    panda treni ya jubilee line hapo hapo hadi canning town hapo kuna clib African IKO BARKING ROAD.

    wabongo wakumwaga hapo.au pitia mtandao wa watanzania www.tzuk.com utaona information za kutosha.

    ukienda EAST HAM station utakutana na watu hasa wapemba.ukienda Upton park station opposite na uwanja wa west ham United,hapo kuna kijiwe cha watanzania kwa mr.Abubakar Pailonga.

    na hapo kuna soko ndipo watanzania wanapofanya shopping.
    ubalozi unashughulika na watanzania sio ccm.

    ReplyDelete
  16. AnonymousJune 09, 2009

    Brother eh,wala usihangaike kutafuta vijiwe vya kibongo,watakuyeyusha.mimi nilishajichanganya nao kuna wakati,tabia ni zile zile za kibongo watu umbeya mwingi,,majungu na vimtima nyongo.
    Jichanganye na watu toka nchi nyingine,utapata kujifunza wenzetu wanafikra gani za maendeleo katika vichwa vyao,na nakuhakikishia hutojuta

    ReplyDelete
  17. AnonymousJune 09, 2009

    TUPO KIJIWENI UBALOZINI. HAPO UMBEYA WOTE UNAOTAKA HUYU KALA NINI, KAVAA NINI NA MANGINEYO.
    MAMBO YAKO BADO YA KIBONGO BONGO UNATAKA UWAJUE UPIGE MZINGA. UPO KOZI TAFUTA MARAFIKI WAPYA WASIO WABONGO ILI UPATE MAWAZO MAPYA. AKILI FINYU NA KUDUMAA KAMA NDITI.

    ReplyDelete
  18. maana yangu ni kuwa wabongo ukiwakuta baa wote wamedata,utakutana hata na baba yoko yuko club A.halafu wabongo tunajua kuharibiana badala ya kuelimisha, mambo ya uswahilini tunayaleta huku,negative kibao,upweke maana yake nini si ungubaki bongo au ungekuja na ndugu zako..kuna mabalozi wa hizo club ni watu wazima na familia zoa lakini mambo yao ni bomu hata maongezi yao ni upumbavu kama unawataka hao wewe nenda,utajikuta ulichojia kinakushinda,soma piga kitabu kijiwe cha nini hatuko tegeta hapa,huo ndio mwanzo wa matatizo,mwabie michuzi akuhook na waliosoma

    ReplyDelete
  19. ukiona london hapatoshi njoo basi reading kuna vijiwe vya wabongo,na tuna makatibu wetu wa mkoa unaweza kuwa ona ukifika train station uliza bongo flava utapelekwa,uje hadi paddington ndio upate train ya reading, karibu tukuingize town namba iongezeke ya wabongo waliozamia

    ReplyDelete
  20. AnonymousJune 11, 2009

    kadi nzuri talk home au nunua sim card inaitwa lebara,lyca au nomi uweke top up then piga africa direct mr fabian ok!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...