nanihii akiwa na mpiganaji athumani hamisi ambaye anatibiwa katika hospitali ya netcare rehabilitation centre hapa johannesburg kwa takriban miezi minane sasa kufuatia ajali ya gari aliyoipata kibiti wilayani rufiji  mwishoni mwa mwaka jana. 

hivi sasa mpiganaji huyu anaendelea vyema na matibabu ambayo kwa sasa ni ya mazoezi ya maungo ambayo yemapooza  ama 'mama cheza' ambapo taratibu maungo yake yanapata mazoezi na kuanza kufanya kazi. hivi sasa, tofauti na alipopelekwa hapo mwanzo anaweza kutumia mikono yake na anatembea kwa hicho kiti chenye magurudumu kinachotumia nguvu za betri. 

athumani anatoa salamu zake kwa wote wanaoendelea kumtakia afya njema na ameshukuru sana serikali kwa msaada wa matibabu anayoyapata. anasema panapo majaaliwa atarejea nyumbani hivi karibuni
mpiganaji athumani hamisi akipiga stori na mustafa hassanali ambaye amemtembelea leo akiwa na wadau humphrey wa TBC (shoto) hamisi (kati) na mdau deo mtui (pili shoto) liyepo hapo kumuuguza mdau franco mtui aliyeumia katika ajali hivi karibuni
mpiganaji hamisi athumani akiwa na mzee timothy apiyo, aliyekuwa katibu mkuu ofisi ya rais enzi za mwalimu, na mwanae. mzee apiyo, ambaye yupo hapo netcare rehabilitation centre kwa matibabu baada ya kupooza, anaendelea vyema na matibabu na panapo majaaliwa anaweza kurejea nyumbani muda si mrefu ujao. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 16 mpaka sasa

  1. Assalaamu Alaikum,
    Kuna umuhimu Tuwe na Hospitali yenye vifaa vya kisasa japo moja ili wanyonge wasio weza kusafiri kwenda nje nao wapate huduma kama hizi.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 17, 2009

    nasi tujenge hospitali bora angalau moja au mbili za kisasa tupunguze gharama za kwenda india,south etc. yote yanawezekana kama nia ikiwepo.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 17, 2009

    BAJETI AIJATOA TAMKOLA KUJENGA HOSPITAL BONGO?. NAONA HIZO HABARI AZIJATURIA KABISA.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 17, 2009

    Naam ...ebu sasa imagine hospitali ya Mnazi Mmoja ingekuwa na facilities kama hii hospitali ya Netcare?!

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 17, 2009

    Poleni sana wagonjwa!

    Hizi picha zinanifanya nione kuna umuhimu wa nchi yetu kuhimiza uwekezaji kwenye sekta ya Afya. Tungekuwa na hospitali bora ndugu zetu wasinegkuwa wanaenda kutibiwa nje ya nchi.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 17, 2009

    We need a rehabilitation centre in TZ. naomba mungu mambo yangu yawe poa nitaifungua mimi mwenyewe. This is ridiculous, serikali inafanya nini yaani Tanzania nzima hakuna rehabilitation centre?? Start training some people in occupational and physio therapy!!! Kwa watu wasio na hela za kwenda South Africa ndio inakuwaje?????

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 17, 2009

    mie ni mwandishi wa habari, lakini neno mpiganaji silipendiiiii...

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 17, 2009

    jaman Athumani ucjali utapona, wadau wa TSN 2mekumic saaaaaaana, tupo pamoja.

    ReplyDelete
  9. MUNGU AWAPE NGUVU, SUBIRA NA AMANI WAGONJWA WETU HAWA. JUU YA YOOTE AWAPE UZIMA WAPONE WAREJEE TANZANIA FAMILIA ZAO ZINAWAHITAJI.

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 17, 2009

    du we have long way to go till we have hospital with facilities like these just forget it inasikitisha uchumi tumeukalia na pia hata ikiwepo hospitali kama hii vifaa vake havita chukuwa muda kuuzwa kariakoo sokoni au kuharibika mungu awasaidie wagonjwa wote wapone salama warudi makwao asante madiba kwa kutupa ukimbizi

    ReplyDelete
  11. AnonymousJune 17, 2009

    huu sio muda wake, a hapa sio pahala pake, walakini bandugu bapenzi..yule askari mwenye risasi tumboni alishaenda walau india kutolewa???FOOD FOR THOUGHT

    ReplyDelete
  12. AnonymousJune 17, 2009

    hey deo tuwasiliane mzee mpe pole mzee mi nipo pietermaritzburg my cell no is 0761465037.pole sana nikipata muda nitatokea huko maana me bongo mpaka december or january.ukienda bongo mpe hi sana massawe

    ReplyDelete
  13. AnonymousJune 17, 2009

    Bongo tambarare siyo ahaaaaaaaaaa inatia huruma na aibu kwa Taifa as national kuona the country with population around 23 millions people we dont have such reabilitation centre at least one in Dar, instead of that people are spending a lot of foreign currency in SA for treatment and what so called Tanzania elites tunashangilia ahaaaaa nyumbani tambarare baada ya kujadili how we are going to build our national in 21 st..and to tackle global challenges tunakaria kupiga michapo na machungu...
    Jambo la kusikitisha watu waliolazwa hapa ni ........ what about my dear friends and relatives from mabonde kuinama ambao gari wanaiona mara moja kwa mwaka likija kuchukua mazao... who is going to take care of this people dont forget that we are bearing the same status "WATANZANIA" ......
    Mdau wa kamachumu

    ReplyDelete
  14. AnonymousJune 17, 2009

    Poleni sana nduguzanguni.Inshaalah,wote Mungu atawajalia na mtarudi kuwa fiti kabisa.
    Poleni sana.

    H.Maarifa

    ReplyDelete
  15. AnonymousJune 18, 2009

    annons sawasawa...

    ivi vyombo vya habari kama ambavo milikomalia UFISADI ukafichuliwa bongo!!haiwezekani kukomalia maswala kama haya apo ya afya yafanyike bongo??

    na facilities zote muhimu??ivi mashangingi ya BMW za "watawala" ni costs ngapi na vifaa vya angalau centre moja ya kuhudumia wanainchi??

    au km ni jadi kuomba kwa wafadhili,haya si ndio ya msingi?mtu unampa maekari ya maelfu ya ardhi in exchange of...???tell them jenga hospitali apa yenye kiwango ichi...full stop

    tena ijengwe mkoani sio dar

    ni uonevu na ushenzy sana

    polen mpone mapema

    ReplyDelete
  16. Tunaendelea kukuombea kaka Athumani. Mungu yu mwema naona unazidi kupata nafuu kila siku.

    Na pole kwa Mzee Apiyo pia.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...