Marehemu Rais Omar Bongo
Kiongozi aliyedumu madarakani kwa muda mrefu kuliko wote barani Afrika, Rais Omar Bongo wa Gabon, amefariki dunia Jumatatu mchana wakati akipatiwa matibabu ya moyo katika hospitali moja huko Spain. Alikuwa na umri wa miaka 73.

Utata wa hali yake kiafya ulimea mwezi jana ambapo alipolazimika kuachia hatamu za madaraka kwa mara ya kwanza tangia mwaka 1967.

Alikimbizwa katika hospitali ya Quiron jijini Barcelona ambako alikata roho majira ya saa sita hivi na ushee. Ameacha pengo kubwa katika jamhuri ya hiyo tajiri kwa mafuta ya Afrika ya Kati.
Vyama vya upinzani nchini Gabon vimesikika vikilalamika kwamba mtoto wa kiume wa Hayati Bongo, Ali Ben Bongo, ambaye pia ni waziri wa ulinzi, amekuwa akiandaliwa kuchukua wadhifa wa baba yake, na wamehoji endapo kama ingekuwa vibaya kufanyika uchaguzi mkuu upya.
Habari za kifo cha Rais Bongo kimekanushwa mara kadhaa na serikali hadi pale Waziri Mkuu wa nchi hiyo Jean Eyeghe Ndong alipothibitisha katika taarifa ya maandishi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 14 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 09, 2009

    habari si za kweli,HAJAFA

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 09, 2009

    MAY THE ALMIGHT GOD REST YOUR SOUL IN PEACE. NI YEYE PEKE YAKE MWENYE HAKI KUHUKUMU.

    MFANO MZURI KWA AKINA MUGABE. YOU WILL NEVER OUTLIVE YOUR COUNTRY.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 09, 2009

    I shed no tear for this tyrant. Africa will do well without him. I can't wait to see Mugabe and Gaddafi kick the bucket as well. It is time for the new generation of Africans to steer our future not some tyrants who steal our money and buy houses in Europe. Gambia is an oil rich country but the people have nothing to eat. What a shame!!

    Mdau, Tokyo, Japan.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 09, 2009

    Africa will be better place without him. One less thief of state to worry about. Maybe now teh Gambians will have enough money to eat.

    I quote the BBC:

    Mr Bongo was one of three African leaders being investigated for alleged embezzlement by a French judge. The others are Denis Sassou-Nguesso of the Republic of Congo and Teodoro Obiang Nguema of Equatorial Guinea.

    It is alleged that the properties owned by Mr Bongo's family in France could not have been purchased with official salaries alone.

    Mr Bongo denied any wrongdoing.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 09, 2009

    It's very interesting story....

    I would like to see these scrapped tyrants to follows:

    1. Mugabe - Zimbabwe
    2. Museven - Uganda
    3. Gaddafi - Libya
    4. Tom Biya - Cameroon
    5. Hosni Mubaraka - Misri (Egypt)
    6. Abdulaziz Butafrica - Algeria
    7. ...

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 09, 2009

    One Down,Nine to Go!Gabon Unite for Democracy.Hii Biashara ya Kurithishana Uongozi wa Nchi lazima IKOME!

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 09, 2009

    Nakubali, huyu kiongozi alikuwa ni dikteta mkubwa mwenye ubinafsi wa hali ya juu sana na kutojali wananchi na yeye akajitajrisha kutumia mafuta na rasilimali za Gabon. Yeye na Mobutu, Banda na Mugabe wote wamedhalilisha nchi zao na kutia aibu bara letu. Ndio, hakuna machozi - miaka 42 ya kunga'nga'nia utawala na kukaba yeyote yule ambao angempinga, Afrika haitaji tena viongozi kama hutu. Hakuna ufalme hapa ya viongozi kutawala kwa maisha, we need new blood and ideas from the new generation of leaders! I bet you Bongo did not even know how to use a computer !!!!
    Sam -ATL

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 09, 2009

    this dude ruled Gabon as it was his. He only let it go after being sick! He is gone, change has come.

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 10, 2009

    Waziri wa Usalama wa Gabon ni mtoto wake, usishtuke kama kesho atakuwa "kiongozi" mpya wa Gabon. Wanafuata mifano mibovu ya Kongo DC. Madikteta wa Misri na Libya pia wanawatayarisha watoto wao wachukue madaraka wakifa. Afrika lazima tuamke.

    Mdau, Tokyo, Japan.

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 10, 2009

    sawa tu wanae washike madaraka

    nyie shida yeni nini?mbona sie tuna tawala za kitemi/kichifu?ndo asili yetu
    sio mimambo ya western countries

    wezi watupu wazungu+obama

    ReplyDelete
  11. AnonymousJune 10, 2009

    wanawaletea matatizo watoto wao tu

    kwakweli

    ReplyDelete
  12. AnonymousJune 10, 2009

    Mdau wa Japan that is so myopic to think that it is only Gabon that cronyism is rife! Watoto wa vigogo wangapi wako kwenye system Bongo.... huo ushabiki mhishimiwa. The big man in Libya is doing fine!

    Mdau Mkulanga.

    ReplyDelete
  13. AnonymousJune 11, 2009

    Ndio,unaweza kua na monarch lakini pia lazima kuwa na serikali inayochaguliwa na watu,lazima kuwe na demokrasia. huyu jamaa aliua demokrasia na ukumbuke,yeye hakua king,au kiongozi wa jadi(mtemi).yeye alikuwa President na pia hakutaka kuachia madaraka hadi anakufa.hiyo ni soooooooooo. wewe mdau unasema wazungu+Obama wezi, utaishia kusema hivyo hivyo na nchi za kiafrika bila demokrasia hatutafika popote.sasa jiulize,huyu jamaa wa Gabon,katika uongozi wake wa miaka 42,Gabon imenufaika na nini? ni mojawapo ya nchi maskini duniani! amka mdau.

    ReplyDelete
  14. AnonymousJune 15, 2009

    Surprise! Surprise! Mtoto wa Bongo, Ali ben Bongo, Waziri wa Ulinzi, anataka "kugombania" uraisi wa Gabon. Baba yake ameshaweka njia safi tu kwake kuiba kura na kendeleza ufisadi.

    Hii habari kutoka BBC:

    No current or former member of government should stand in forthcoming presidential elections in Gabon, say civil society groups in the country.

    A correspondent in Gabon says the organisations are particularly concerned the son of the late President, Omar Bongo, will take over.

    Elections are due to be held in the West African nation within 45 days.

    Mdau, Tokyo, Japan

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...