Kaka Nanihii,
heshima mbele pamoja na wadau'z wote.. Kaka Nimekuwa nikijiuliza kama kusingekuwa na Jehanamu (Moto kwa wenye dhambi) je tungekuwa na Upendo kwa Mola kama tulionao sasa?
Manake mara nyingi viongozi (almost wote) wa kidini huwa wanatuhamasisha kumpenda na kumtukuza na kumweshimu Mungu ili siku ya mwisho tusitupwe motoni. Sasa basi, ina maana kama kusingekuwa na huo moto pamoja na ukweli kuwa Mungu ndiyo aliyetuumba, tungempa nafasi kama tunavyompa sasa kweli?
Just thinking aloud.
Mdau'z wa Mosocw..
Mnh! SINA LA KUSEMA HAPA!! MAANA...! Mnh!
ReplyDeleteHakuna mtu unayemfahamu aliyewahi kwenda Jehanamu na kurudi na kutusimulia. Habari zote unazisoma katika vitabu zinaweza kuwa ni vitisho tu. Wewe usimaindi wala nini, kula kuku wako kwa unono na fanya yaliyo mema. Inawezekana Jehanamu ikawa hapa hapa duniani. Mfano wa Jehanamu inaweza kuwa Segerea! Kuchomwa moto ukikamatwa ukiiba, kukatwa sehemu zako nyeti ukikamatwa katika ugoni. Na vitu kama hivyo......
ReplyDeleteThink about it!!!!!
Mdau wa Moscow,
ReplyDeleteKwa mtazamo wa dini yangu, kumcha au kumtii Mungu kwa ajili ya kuogopa moto, ni imani ya chini kabisa, lakini kumcha mungu kwa kujua kuwa yeye ni muunda wako, na ndiye anayestahiki kufuatwa amri alizotoa kwako kama muumbwa, ni daraja la juu kabisa la kuabudu.
mdau wa moscow inaonekana hali ya kiuchumi imekubana sana,ondoka huko kwa wazungu maskini njoo viwanja vya maana kama USA na Englad,topics kama hizo upate kuzisahau kwa muda
ReplyDeleteBismillah
ReplyDeleteGloria in Excelsis Deo
Mdau wa Moscow umenifurahisha sana maana umeleta suali ambalo linawasumbua watu wengi sana. Kwanza nakujulisha kuwa mimi si maalim msikitini wala padri kanisani
Binadam ana matatizo makubwa sana kwani kila mara ajaribu kumjudge Mwenyezi Mungu by human standards of justice and fairness In the book of Job..who was not happy with Gods injustices and lack of care..he was defeated in his argument not because God is right or wrong but by definition that He is God and thus He is right
Back to your quetion we dont follow religion because of fear of jahanam, but we love Him for what He is.The one who made the earth habitable for you...and produce all kinds of fruits for your sustenance Quran 2:22
Thanks Alan Dershowitz
Wakatabahu
angalia link hii http://www.helltruth.com/free-resources/free-video-library.aspx utakuta kuna option ya watch au listen yenye title Cities Of Ash . hapo utakuwa umepata jibu
ReplyDeleteKama kungekuwa hakuna jehanam na watu wangekuwa hawana hofu kabisa, basi dunia ingekuwa jehanamu. Imagine, jirani yako akikuudhi, ni unamfanya chochote bila ya hofu. Na wewe ukiwaudhi watu, wanaweza kukufanya kitu mbaya bila ya hofu yoyote; dunia ingekuwa ya ubabe kuliko ilivyo sasa.
ReplyDeleteHata hivi leo kuna watu ambao hawana hofu ya Mungu ila wana hofu ya mkono wa sheria. Hatujui wanayofanya gizani (faraghani, ambapo sheria haiwezi kuwakamata). Ndiyo mambo ya ufisadi, nyumba ndogo, ujambazi, wizi, ubakaji n.k. yanashamiri. Mtu mwenye hofu ya Mungu (mcha Mungu) hawezi kufanya hivyo vitu hata akiwa kwenye faragha, kwa sababu anajua kuwa Mungu anaona.
Lakini ukweli ni kuwa jehanamu ipo, na Mungu hataki binAdamu yeyote akanyage huko. Tusipotubu (tusipoishi maisha ya toba) wote tutafika huko, lakini siyo mpango wa Mungu.
Usidanganywe na mtu, jisomee Biblia mwenyewe na muombe Mungu akupe ufahamu uelewe, atakusikia - anamthamini mtu anayemtafuta kwa bidii.
Kwa kumalizia, watu wengi huanza kumfuata Mungu kwa sababu ya hofu ya moto, lakini baadaye huja kugundua uzuri wa Mungu, basi hawa huendelea bila ya kufikiria sana kuhusu moto.
mdau kwa elimu yangu niliyonayo ya philosophy naweza nikakufanya ukaamini kuwa haukuna mungu kabisa.
ReplyDeletelakini tukizingatia ukweli halisi ni kwamba mungu yupo na limuumba binadamu kwa lengo kwamba binadamu amtukuze yeye na kumtii kama muumbaji. lakini kutokana na kuangushwa na kushawishiwa na ibilisi[aliyekuwa malaika mbinguni=LUCIFER na kwa tamaa akanguka] hufanya kujenga hofu dhidi ya huyo muumba.
lengo la muumba ni kurejesha hali ya awali ya mahusiano katiyake na viumbe wake ili wamtukuze na kumtii kama alivyo kusudia tangu awali.kwamsingi huo basi amekusudia kuiteketeza dhambi na sio binadamu,na kwa kuwa hiyodhambi itakuwa ndani ya ibilisi,malaika walio asi na ndani ya baadhi ya wanadamu waliokubali mshawasha wa LUCIFER, basi nao hiyo process itawapitia japo sio lengo la awali la muumbaji wao.kama dhambi isingekuwemo ndani yao nao wasinge kuwa ktk hatari hiyo. JAPO LUCIFER HUTUONYESHA UPANDE MMOJA TU WA SHILINGI yaani faida tutakayoipata kwa kutokujali na kumtii mungu kuwa tutakuwa huru kuishi tutakavyo na kufurahia maisha.lakini haonyeshi upande wa pili nini madhara yake
kwa mfano:atakuonyesha demu,kisha atakushawishi umlaghai(1.useme uongo) ufanyenaye mapenzi(2.uzini),ukishampa mimba anakushawishi uitoe(3.unauwa),kisha msichana anaweza kuishia kutopata mimba tena.na kama akikataa kutoitoa basi atazaliwa mtoto na anaweza kukulia ktk mazingira magumu ya kutelekezwa na baba ambaye hakuwatayari kumzaa nakumlea.
hivyobasi kumcha muumbaji kwa kuhofia kuangamizwa ni uoga na kukosa heshima na kujiamini mbelezake. lakini kumcha kwa kumheshimu kama muumbaji na rafiki kunatija na tunu.
japo tunamkosea mungu amatunaanguka ktk maovu lakini ukweli kuwa yeye ni mungu na anastahili kufuatwa sio kwa woga wa adhabu bali kwa upendo na heshima.
ila napenda niweke wazi jambo moja hapa kwamba wengi wanapatashida kumheshimu mungu kutokana na uhusiano walionao na WAZAZI WAO, HASA BABA!!!kwa kuwa taswira ya baba yako mzazi psychologicaly inakuwa ndiyo taswira unayoipata unaposikia MUNGU BABA)))!!
kama babayako alikuwa sio mwaminifu,hakujali,mtu wa kichapo nk wewe ktk subconscious level unamchukia MUNGU BABA bila kujuwa maana umeathirika kwa mahusiano ya ubaba wa baba yako mzazi.
Mdau wa 3:24 Nafikiri pia unaamini kuwa bears wanatembea mitahani hapa. Warusi sio masikini kama unavyosikiliza ktk redio feki. Hawatupendi, lugha yao ngumu sana, ni wabaguzi na uncultured lakini sio masikini. Angalia nchi ilivyojengwa. Biashara kibao za kimataifa UK na nyingi za US (kuna limitations nyingi) wanamiliki warusi. Na mrusi ni kama wabongo wa 70 na 80, ataiba , atalowea, lakini nyumbani ni must kutesa. Elewa: sishauri mtu kwenda huko kutafuta maisha but sometimes we need to call a spade a spade and to swallow the truth.
ReplyDeleteBila moto kungeweza kuwa na simba kama waliokuwemo kwenye collosium za warumi wa kale. Utasema wamasai wangezini kw sababu hawaogopi simba...wangetishiwa maji...
ReplyDeleteMdau wa Maskava Kakdela?
ReplyDeleteHaihitaji kutumia Falsafa(Philosophy) kumtafuta Muumba wa kila kilichopo.Hahiitaji kwenda University kujadili kuwepo kwa Mola...Kuna mama Sufi wa Baghadad akiitwa Rabia al Adawiyah kwa maneno yake matamu juu ya upendo wake kwa Allah alisikiak akisema kwa uangalifu maneno yake kuwa Ewe Mola Hakika nakupenda si kama nafanya hivi ili unipe pepoe yako ila nakupenda wewe ndio maana nakupenda wewe, laiti kama nafanya hivi ili unijaalie hiyo pepo basi na niikose, na sio kwamba nafanya hivi kuogopa moto wako(Jahanam) kama kuna chembe ya khofu kuogopa Jahanamu hiyo basi nitie humo katika Jahanam.Nayafanya haya(Ibada hii tukufu kwako ewe Mola) kwa mapenzi niliyo juu yako wewe, kwa kuniumba na kunijaalia kila ambalo umenipa wewe pasi nami kukuomba.....''Kuna hekaya nyingine ya kweli ya namna hii, Imam Al Haramain al Juhain(Mwalim wa Imam Al Ghazali) yasemwa kuwa alikuwa na kipaji cha kuweza kukup[a sababu zaidi ya Alfu moja za kuwepo kwa Allah(Wujud wa Allah) alitokea mama mmoja na kumwambia kuwa yaonyesha una shaka alfu moja ndio maana unaweza kutoa hoja alfu moja kuwepo kwa Allah haihitaji hoja kuwepo kwa Allah....Allah yupo kwa kila dalili...
Spasiba
jey4@yahoo.com /jey4@yahoo.co.uk
mdau wa Moscow.
ReplyDeletenimefurahi kwa swali lako zuri.lakini kumbuka,dini ni imani.
korani inasema mwenyezi mungu ameumba viumbe wengi,majini mashetani,na binadamu ili kufanya ibada.sasa hili ndio jukumu letu la kwanza.
sijui wewe mdau ni dhehebu gani?ila uislam ni umma bora wenye kukumbushana memma na kukatazana mabaya.
sasa kwakua binadamu ni viumbe bora na wenye ufahamu wa kutosha tuna mifano mingi sana ya kujua kwamba mungu yupo.na anauwezo mkubwa sana.hebu muangalie tembo alivyo mkubwa,na muangalie nyenyere[mdudu mdogo]na hata [immagine microscopy insect].wote mungu amewapa haki sawa.
Hivyo basi ukiangalia mazingira na mifano kama hii hata kamausingetishiwa jehanamm unatakiwa uamini kuwa mola ni muweza na yupo.
na sikio la kufa halisikii dawa,binaada ni wakosaji ndio maana wanasema si kamili.
mdau washington.
Inshallah mungu ukuzidishie imani.