
Kundi la TMK Wanaume Halisi linatarajia kukwea pipa kuelekea Mashariki ya kati nchini Dubai kwa maonyesho kadhaa imefahamika.
Kiongozi wa kundi hilo Juma Kassim maarufu kama (Sir Nature) amesema wamepata mwaliko kutoka kampuni ya Consult LB Tard Ltd ya nchini humo.
Sir Nature amesema wanatarajia kuondoka tarehe 3 mwezi Julai kwa ajili ya kufanya maonyesho hayo, ambapo wanatarajia kufanya onyesho la kwanza kwenye ukumbi wa DEIRA nchini humo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...