Alhamisi ya tarehe 04 June 2009, raia (citizens) wa nchi 27 za Umoja wa Ulaya (European Union) watapiga kura ya kuchagua bunge jipya litakalowakilisha umoja huo.

Bunge hilo litachukua kiti cha ubunge kwa muda wa miaka mitano kuwakilisha Umoja wa Ulaya na raia wake wa nchi 27 wapatao 500,000,000 (milioni mia tano).Ukiwa ni raia wa United Kingdom au una makazi nchini United Kingdom, hakikisha siku hiyo isikupite kupigia kura chaguo lako la bunge utakalopendelea.

Kura hii ni muhimu kwa UK kama ilivyo 'General Election'. Kwa maelezo zaidi ya upigaji kura nchini UK, bonyeza hapa.


Zenjydar Community Association

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 03, 2009

    again am back to remind you my muslim brother Muhidin Issa Michuzi...!una nafasi nzuri ya kuiendeleza dini yetu kupitia ufahamu wa computer aliokupa Allah S.W...unaitumia hii nafasi kumtangaza? nakukumbusha kama Allah alivyotuagiza...ukitaka ichukuwe hii msg usipotaka itupe!!

    ReplyDelete
  2. Kawa nini umeileta kwenye blog ya jamii???inatuhusu nini sisi waTanzania????

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 03, 2009

    Mheshimiwa Michuzi, mimi bado sipendezwi na jinsi gani habari za michezo za ndani ya nchi kuwa hazitawali katika blog hii. Nimeshangaa kukuta kwenye website ya livescore, kua timu ya taifa ya Tanzania inacheza mechi ya kirafiki na New Zealand leo. Nina uhakika ingekua ni League ya uingereza,basi ripoti ingetoka mara moja. Jitahidi basi uwe atleast unaweka habari hizo za ndani.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 03, 2009

    Unapotaka kuwaandikia ujumbe raia wa UK, kwani wanapatikana kwa MICHUZI? Kwa nini mambo kama haya msipeleke BBC au SkyNews? Ntashangaa kama kuna raia wa UK kisha hajui kiingereza, labda huyo kajilipua! Waswahili na hasa wa-TZ hatupigi kura kuchagua wabunge wa UK,wla ulaya tafadhali!!

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 03, 2009

    Father tuletee habari za michongo ya kazi au madili ya kupata sheria,hizo habari za kura na vurugu za ubunge kaa nazo mwenyewe,na kura utapiga peke yako,watu tumechoka mbaya

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 04, 2009

    halafu ukishapiga kura...iweje! pua kama msomali wa baajun

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 04, 2009

    Ningependa kutoa maoni yangu kuhusu mdau aliyesema inabidi Michuzi aitumie hii blog kutanganza dini ya kiislamu. Umeonyesha kama vile unamlazimisha "owner wa blog" au kumtishia. Hii blog ni idea yake,mali yake na yeye kutanganza dini yoyote au kutotangaza,ni uamuzi wake. kikubwa hapa tunafurahishwa na habari mbali mbali za tanzania,na sio mahubiri ya dini. wanaotaka kupata mahubiri ya dini, ziko website kibao kwa ajili hiyo. Hapa tunamshukuru tu owner wa blog hii kwa kutupatia habari za nyumbani sisi tuishio nje.Mambo ya dini kando mzee,hapa sio mahala pake.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 04, 2009

    mdau wa pili toka juu, watanzania waishio uk wanahaki ya kupiga kura. ni mfumo wa uingereza, unashangaza kidogo lakini ndivyo ilivyo, kila mwananchi kutoka common wealth countries anaeishi uk anatakiwa kushiriki katika kupiga kura. mimi binafsi mara ya mwanzo nilipotumiwa kadi ya kura nikiwa chuoni nilishangaa sana na hata kufika kwenda kumuuliza tutor wangu.

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 04, 2009

    mchangaiji wa mwanzo, kwanza assalam alayku, pili hongera kwa kuchukuwa uamuzi uliochukuwa kumuandikia michuzi. tatu ni suali tu jee unajuwa kuna blog ngapi duniani ambazo wamiliki wao ni waislamu? jee unakusudia kuwatumia wote ujumbe kama huu? nne, je kwa nini wewe mwenyewe binafsi huanzishi blog yenye lengo la kuwakumbusha mema waislamu wote? naamini ukifanya hivyo hata brother michuzi hatosita kuitangaza hapa kama anavyofanya kwa waanzilishi kibao walioomba awatangazie.
    maasalam

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 04, 2009

    Republic of Ireland, local and European election ni on 5th June 2009.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...