Tampere African Sports (TAS)
Timu za watanzania zenye maskani yake jiji la Helsinki na Tampere Ufini zimefanikiwa kuanza vema kampeni zao za kutangaza taifa la Tanzania kwenye medani ya soka kwa kutoa vipigo kwa wapinzani wao.
Timu ya Tampere Africans Sports(TAS) yenye makazi yake kwenye jiji la Tampere,chini ya kocha wake George Matovu (mtv) waliibuka washindi kwa goli 4-1 kwenye mechi ya kirafiki dhidi ya timu ya Wakongomani iliyochezwa mwisho mwa juma.

Wakati huo huo ndugu zao wa Bongo Fc wenye makazi yao jijini Helsinki walifanikiwa pia kuwabamiza bila huruma timu ya wacameroon kwa mabao 3-1.Helsinki ambayo inanolewa na mdau mkubwa wa Soka Ezza.
Helsinki inajiandaa kwa mtanange wa kukata na mundu wa kirafiki dhidi ya timu ya watanzania kutoka sweden Kilimanjaro Club utaofanyika June 27,jijini Helsinki.

Kocha wabongo FC amewahakikishia mashabiki wa timu ya Bongo FC ushindi mnene siku ya jumamosi kutokana na maandalizi mazuri waliyonayo.
Mtanange wa Bongo FC na Kilimanjaro Club utaletwa moja kwa moja LIVE na
www.edondaki.blogspot.com
Tutafika tu
Bongo United FC


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 23, 2009

    ...make sure they go to school too. Otherwise the nation will lose a great deal of human resources.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 23, 2009

    Jamani hii ni timu(TAS) ya watanzania ama waafrika waishio Tampere, Finland?

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 23, 2009

    HE bongo Fc Zelu mwaaa inakuaje arooo

    ReplyDelete
  4. mh bALOZI ,
    Bongo tambararee,mbona Bongo Fc yenyewe Wamatumbi wachache au ndio matunda ya zile Vekesheni zetu zileee enzi za mwalim

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...