MDAU NJILI MWAKOBA ALYE IPITA ENEO HILO LEO ASUBUHI NA ANASEMA KWA MUJIBU WA POLISI WALIOPO KWENYE ENEO LA AJALI ABIRIA WALIOKUWEMO NDANI YA BASI LA MOHAMED TRANS HAWAKUZIDI 40 AMBAVYO NDIO KUSEMA BASI HALIKUJAA.
POLISI HAO WALIKATAA KUTAJA IDADI YA WALIOKUFA MPAKA SASA ZAIDI YA 28 WALIOFIA ENEO LA TUKIO AMBALO MDAU ALIFIKA KIASI CHA DK.45 BAADA YA TUKIO ILA HALI YA MAJERUHI WENGI IMESEMEKANA SIO NJEMA
Tanzania imekuwa ni moja ya nchi duniani zinazoongoza kwa ajali zenye kuua watu wengi. Sifa hii hatupaswi kujivunia.Soma maoni kuhusu nini kifanyike hapa: http://drfaustine.blogspot.com/2009/01/motor-traffic-accidents-possible.html#links
ReplyDeleteMwisho, napenda kutoa pole kwa wahanga wa ajali na kwa ndugu wa marehemu. Mungu azilaze roho za marehemu mahali pema peponi.Amen
Mdau
Faustine
http://drfaustine.blogspot.com
Tunaomba serikali imchukulie hatua kali mmiliki wa mabasi hayo kwani yamekuwa yakiongoza sana kwa ajali na kupoteza nguvu kazi ya taifa letu.
ReplyDeleteIla serikali utasikia tunafanyia uchunguzi mara hakuna matokeo, jamani vyombo vya usalama tunakufaaaaaaaaaaaaaaaaaa
KAKA ASANTE KWA PICHA HIZI ILA NAOMBA UTUFAHAMISHE LILIKUWA LINATOKA WAPI KWENDA WAPI MAKE HATUJUI KAKA POLENI SANA WAFIWA NA MUNGU AWE NANYI KATIKA KIPINDI HIKI KIGUMU AMINA.
ReplyDeleteUKWELI NI SERIKALI YA KWANZA WA KULAUMIWA,LEO DEREVA ANAFANYA KILA ANACHOTAKA AKIPATA AJALI UTAKUTA ANAACHIWA ANAPIGWA FAINI YA 20,000/= NA MLANGO WA NYUMA ( RUSHWA ) 1,000,000 /= (MILIONI) KESHO ANA GARI INGINE SASA KWA NAMNA HII AJALI HAZITAISHA HATA TUKIPANGA KILA KILOMITA 1 TRAFIC AJALI ZITAKUWEPO TUU ,MADEREVA WAMEKUWA NDIO WATEJA WA MABAA YA NJIANI NA WAZINIZU WAKUBWA ,HELA WANAPATA KWA NJIA YA WIZI KWA KUIBA DIZELI TUU ZA MAGARI YA MABOSS WAO WANAZOENDESHA ,LEO TAJIRI AKIENDA KUSHITAKI DEREVA KAMUIBIA ,POLISI HAWAFANYI LOLOTE,NDIO MATOKEO YA AJALI YA MABARABARANI HAZITA KWISHA MADEREVA WAHATEGEMEI FANI YAO. AKILI YAO YOTE NI KUIBA NDIO UTAKUTA AKIWA BARABARANI AKILI HAIWI SAWA.
ReplyDeleteKama dereva amepona, ANYONGWE MPAKA AFE. Kwa kweli hatuwezi kuendelea kuua vijana, watoto na wazazi wetu kama kuku. Authorities wanaotoa leseni wako wapi? Jamani hii inahitaji mchanganuo ili kupata ufumbuzi wa kudumu.
ReplyDeleteSerikali inapaswa kulivalia njuga suala zima la Usalama barabarani kuanzia mafunzo mpaka kupata lesseni. Utaratibu wa kupata lesseni inabidi ufanyiwe kazi kiukamilifu. Kwamfano kupata lesseni ya kubeba abiria isiwekitu kinachoweza kutolewa na R.T.O tu. Inatakiwa mtu aende shule na akamilishe silabasi yote na afanye mtihani wa wazi afaulu ndio apewe hiyo shahada. lazima hawa madereva waelewe kwamba gari ni mashine inayouwa na kuondoa maisha ya binadamu yeyote pamoja na wao wenyewe. Kwa mtazamo wangu madereva Watanzania wanapokaa kwenye gari wanao gari ni chombo cha kutongozea, vilevile wanachezea gari kama mdori ndio wengi wanaua.
ReplyDeleteNI DHAHIRI MWENYE MAKOSA KATIKA HII AJALI NI DEREVA WA BASI.
ReplyDeleteHEBU ANGALIA LORI LILIKOELEKEA NA BASI LILIKOLIFUATA.
MADEREVA WA MABASI NI LAANA KABISA HAPA NCHINI NA WENGI WAO NI WATOTO WA MIAKA 25HADI 35-HAWANA UCHUNGU WA MAISHA WALA MALI.
MADEREVA WA MABASI WASIPONYONGWA LAMA ANON HAPO JUU WA 2:10PM TUTAKKWISHA KWA HUU UZEMBE
- wadau, naona mnahangaika kutafuta chanzocha matatizo na pia kupendekeza suluhu mujarabu za chanzo. Nimependa maoni ya mtoa maoni Jul 27, 02:04:00 PM: Kuhitimisha asemayo na msemayo wengine na mtakaokuja kusema..Haya ni matokeo ya UFISADI..Watu wengi hutumia neno hili kwa wepesi lakini unapolitafautisha na kitu 'RUSHWA' ni kwenye kina cha matatizo nchi yetu imefikia sasa hivi..hii ndo mdudu "grand corruption"...maana asili/halisi ya neno ufisadi kiarabu ni 'UHARIBIFU'..nchi yetu siyo ile ile, masikini!..hatuna tulijualo kwenda mbele wala kurudi nyuma..yaani thamani ya maisha ya watu imekuwa ni shs. 1,020,000 (mdau hapo juu)..kila eneo matatizo. EWURA wanapiga kelele uongo/kweli na chakachua la mafuta moja kwa mia..bulk procurement na strategic oil reserve ni story tuu- tumeikalia politiki/kiini macho, shirika la stima (makusudi!) wanakarabati nyumba kwa shs. milioni mia 6, ili wauziane kwa milioni 60! (bungeni leo)- wizi mtupu!...EPA/richmond,zebaki na sumu ziwa victoria tufe vizuri kuanzia wanywa maji na wala samaki (na smaki waliwa hadi Dar, patamu hapo!), nk..nk,,nk.....yameshatokea meeengi..huu ndo wakati wa kuchuma, wakati wa mavuno..tumuombe M. Mungu manusura yake lakini tukae tukijua bila miujiza yake, maafa mengi yapo njiani..tumelikoroga....
ReplyDeleteSijui kilichotokea lakini kinachojulikana ni kwamba madereva wa mabasi Tanzania ni vichaa. Yaani mabasi yanakimbia kuliko magari madogo hiyo wewe umeona wapi na kwa barabara zipi hizo. Mpaka hapo serekali itakapoweza kuwathibiti ndipo ajali nazo zitakazopungua. Wewe unaendesha kiubabeubabe wakati umebeba maisha ya watu, sasa yako wapi? labda alikufa lakini madereva wenziwe watajibu. Basi la abiria lisizidi km 120 kwa saa ambayo ni kama miles 75 kwa saa. Pole sana kwa ndugu wa marehemu
ReplyDeleteNi ajali mbaya hakika! Ndugu na jamaa poleni sana,Tu pamoja kuwaombea marehemu wetu na majeruhi wa ajali hii. Nasi wengineo tupate funzo kutokana na ajali kama hizi na tujiulize twaweza fanya nini tuepuke ajali hizi.
ReplyDeletehivi huyu BASI lilikua linafanya nini upande wa kulia mwa barabara
ReplyDeletewadau naomba na mie niongee kwa uchungu.
ReplyDeletejamani hali katika barabara zetu ni mbaya sana.madereva wa mabasi wanakimbia kama wamebeba mawe,na abiria wenyewe tupo kimya tunasubiri ajali ndio tuongee kwa jazba. kwa nini hatuwatii adabu kabla?ukijaribu mtu mmoja kumweleza dereve juu ya spidi abiria wenzako wanakutolea macho na maneno makali juu.mwisho wa siku ndio tunachinjwa tu.yaani safari roho mkononi Bongo.mwezi uliopita nilinusurika kifo kwa kupinduka na basi, na jana hiyo ajali imeuwa watanzania wenzangu kibao na kumuacha rafiki yangu Sele hoi.POLENI WAFIWA MLIOPOTEZA VIPENZI VYENU. POLE KAKA SELE NA MAJERUHI WENGINE WOTE.
Nawakilisha kwa uchungu.
Mdau kyk.
Namuunga mkono mdau was Tarehe Mon Jul 27, 02:10:00 PM, Mtoa Maoni: Anonymous!! Dereva au kondkta wa basi au lori, yeyote mwenye kosa, anyongwe kwa kitanzi mpaka afe.
ReplyDeleteNatoa rambi rambi zangu kwa wafiwa na pia nawatakia mahututi wote wapone haraka, na Mola atazisikia sala zetu.
Basi la kutoka Mwanza kupitia Nairobi, Arusha, Korogwe mpaka DSM linahitaji madereva 4 ( Wanne)
ReplyDeleteMwanza Nairobi dereva wa kwanza anashuka kwenda lala, Nairobi anapanda dereva wa pili aliye freshi atakaeishia Mombo, Mombo anakamata dereva wa tatu mpaka DSM. Dereva wa nne ni wa akiba atakayekuwa lazima awepo ndani ya basi ikiwa kutatokea uchovu wa ghafla au ugonjwa.
Jambo lingine kila basi linapofika sehemu ya kubadilisha dereva, basi lipelekwe gereji kukaguliwa na pia matairi kupimwa joto n.k, ikiwa tairi limezidi joto libadilishwe mara moja, na lazima yatumike matairi maalumu kwa ajili ya nchi za joto.
Mwisho madereva wote wawe wa mabasi, malori na magari madogo wazingatie hizo tahadhari nilizozibainisha hapo juu, kuepukana na uchovu, kutoedesha kilomita 300 bila mapumziko na ukaguzi wa chombo.
Mdau
Rocky
kwasababu trafiki pamoja na watoa leseni wameshindwa wajibu wao! mimi nashauri abiria waanze kuchukuwa sheria mkononi maana wao ndio mawakala wa maisha yao. trafi hana uchungu ukifa yeye anauchungu kama atalala njaa. kwa msingi huo basi abiria ukihisi dereva anakwenda mwendo unaokutia hofu simama useme dereva taratibu kaka! akikupuuza subiri mkisimama tu kituo chochote, mshukeni mpeni kipondo hadi akome kuringa,kisha mnamshusha na kumuacha hapo na kumnyang'anya funguo, mnasubiri likipita gari jingine mmoja anapanda kwenda kumleta trafiki awaendeshe!KAWIA UFIKE.kuzuia ni bora kuliko kutibu!! POLENI MLIOPOTEZA WAPENDWA WENU,NA UGUENI POLE MAJERUHI WOTE.
ReplyDeleteMdau Rocky.
ReplyDeleteUkweli unaousema umeimbwa saana na wengi wamepoteza maisha kutokana na haya. Binafsi nimekuwa mhanga wa mambo kama hayo. Basi la kutoka Dar kwenda Bukoba linakuwa na dereva mmoja. Kibaya zaidi ni kuwa dereva huyo anaendesha kwenda na kurudi na anafika Dar anakuta kuna abiria na posho na anakubali kupiga masaa mengine peke yake. Hili lilipoteza maisha ya ndugu zetu wengi tuliokuwa nao katika Tawfiq.
Lakini sijui ni lini viongozi wetu watakaposikis haya.
Nami nilishaandika (http://changamotoyetu.blogspot.com/2009/01/tumechoshwa-na-salamu-za-rambirambi-na.html)
Mpaka ahusike mheshimiwa ndio tutaona mabadiliko. Si kutafutana uchawi huku? Kutaka kuanza kuombeana mabaya ili waweze kujua uchungu uwakumbao maelfu ya waTanzania?
Heaven Help Us All
Jamani mie nashauri serikali kuangalia routes zote za mabasi na kuzifupisha kama ni ndefu. Halafu kwenye ujenzi wa barara wawewanatenga sehemu za kupumzikia ( rest areas) ambapo mabasi na magari yote yatakuwa yakipaki hapo na siyo barabarani.
ReplyDeleteJamani naomba nitofautiane na nyie wote. Nitakayosema najua ni controversial lakini ukweli ni ukweli lazima uwekwe wazi. Eneo hilo la kutokea Korogwe kuja hadi Segera na kutoka Chalinze hadi Segera kuna nguvu za giza sana. Kuna misukule mingi iliyofugwa na ina kiu ya damu. Kwa hio mara nyingi huyapindua magari na hasa mabasi ikli damu imwagike na yenyewe yakate kiu. Huyo dereva mnamwonea. Ile tairi imetobolewa na hiyo misukule gari likayumba ajali ikatokea. Eneo lile linahitaji deliverance (walokole wananielewa). Mkitaka mkubali lakini pia mna hiari ya kunipinga. Mimi sijali kwa sababu ukweli nimewaambia.
ReplyDeleteTHIS IS BS. JK INABIDI AINGILIE KATI SUALA ZIMA LA HIZI AJALI ZA BARABARANI. WATU WANAPOTEHS MAISHA KIHOLELE NA HAMNA HATUA ZINAZOCHUKULIWA BADALA YAKE RAIS ANAENDA TU KUTOA SALAM ZA RAMBIRAMBI
ReplyDeleteJK PLEASE PLEASE TAKE SOME ACTION.SA SIVYO TUTAKWISHA
GOD BLESS TZ AND IT'S PROPLE
Nadhani ni vema kwanza kuwapa pole wale wote waliopoteza ndugu zao, waliopoteza viungo vyao kwa kweli ni ajali mbaya zilizowahi kutokea katika nchi yetu...chanzo kikubwa kama nlivosikia katika vyombo vya habari ni basi la Mohd lililokuwa likitokea Mwanza kuelekea Dar, lilikuwa likiovertake gari la abiria, Hiace, na kukutana uso kwa uso na Lorry, sasa imagine hio impact inasikitisha sana na kutufanya tuzidi kuwa makini tuwapo barabarani.. Mungu aziweke roho za marehemu mahala pema
ReplyDeleteajari zinazoweza kuepukika,magonjwa,maji machafu ya kunywa,majambazi,mlo mmoja kwa siku=50years mbongo wa leo
ReplyDeleteukivuka hapo basi katambike
Poleni wafiwa na wale wote walioumia katika ajali hii Mungu awe nanyi kipindi hiki cha maumivu makubwa. Kweli inasikitisha sana.
ReplyDeleteChanzo namba moja ni maderva wa haya mabasi.Ni jambo muhimu sana haya mabasi yawe na dereva zaidi ya mmoja. Kweli ukisafiri safari ndefu na dereva asipobadilishwa inafikia kipindi unashikilia roho tu maana yule aliepo anaendesha kwa kasi ya ajabu tena bila hata kufuata sheria mbalimabali mfano za kuovertake ili mradi afike. Watu wengi watakuwa ni mashahidi ni mara nyingi tu ukisafiri mnakoswakoswa sababu ya dereva kuovertake bila kuangalia usalama.
Think in Tanzania there is no NEED of Constructing GOOD Roads, coz in all good roads that's where all these Horrific Accidents are happening. God Bless us!
ReplyDeleteReasons:-
ReplyDeleteRushwa ktk utoaji leseni za madereva
Rushwa kwa ubovu na ukaguzi wa magari
Ufisadi wa pesa za kujenga barabara nzuri.
Tunahitaji double roads na kuwepo na kigawanya njia katikati ama njia zijengwe mbalimbali kuepuka face2face colition.
Kulaumu madereva haitoshi. Kila mtu alaumiwe ikiwamo wewe na mimi ambao hatuwezi kuandamana kuiambia serikali iache rushwa na kujenga barabara bora
Haitusaidii kutafuta mchawi kwakuwa hatuchukui hatua sahihi
Mdomo hausaidii
Of course ccidents happen, HOWEVER, I would say to a large extent traffic police officers contribute to rise the accident bar in tanzania.
ReplyDeleteUSHIRIKINA jamani upo, anayeamini hilo na aamini na asiyeamini halazimishwi.
ReplyDeletehiyo ajali ni nguvu za giza kabisa na huyo mmiliki wa hayo mabasi sio mara ya kwanza magari yake kupata ajali kubwa namna hiyo..
kama alivyosema mwenzangu hapo juu kuwa huu ndio wakati wa mavuno na kutoa sadaka kwa mizimu ili mambo yaende sawa kwa kipindi kingine kijacho mwakani.
UCHAWI UPO NA KWA STYLE HII TUTAKUFA WENGI. HATUNA BUDI KUMLILIA MUNGU KWANI YEYE NDIYE MUAMUZI NA KINGA YA YOTE HAYO
Unajua sheria zetu za mji zimewekwa tu kama geresha, wamekaa wabunge wakala night zao basi imepitishwa ikija kwenye utekelezaji ni kuangaliana usoni.
ReplyDeleteTrafic kama wengefanya kazi zao vizuri, ajali nyingi zingeupukika,lakini pia serikali yetu inatakiwa ibebe lawama, magari mabovu yanaingizwa hayakamatwi na hakuna sheria kali ya kukomesha haya. Barabara nyingi mbovu hela zinatumiwa kununulia magari ya thamani.
Hawa waliokufa na kilio cha wafiwa mtakibeba nyie mliopewa dhamana lakini hamkuitimiza
Tumeanza nusu ya pili na ya mwisho kwa mwaka huu.
ReplyDeleteKatika miezi hii ya kuelekea mwisho wa mwaka kama kawaida tutakuwa tunasikilizia ajali kila kukicha. Sijui kwa nini inatoka hivyo?
Au kama ni mizimu kweli katika kipindi hicho ndo hamu ya kunywa damu za binadamu huongezeka zaidi kuliko miezi mingine?
POLENI SANA WAFIWA...KUMBUKA KUSALI 24/7 VILE VILE KUMBUKA MSIMU WA SHETANI WA KUTOA ROHO ZA WATU KWA NJIA ZA AJALI ULISHAANZA...FUATILIA KWA UKARIBU REKODI YA AJALI UTAONA MILIKI WA MABASI NA MALORI YA MIZIGO NA MALORI YA MAFUTA..
ReplyDeleteKila siku tunasikia tairi la mbele lilipasuka. Kama dereva anaendesha kwa limit inayotakiwa ni rahisi kulimudu basi. Hakuna anayejali safety ya abiria kuanzia tajiri mwenye basi na wafanyakazi wake.
ReplyDeleteKwa ushauri wangu madereva toka Mwanza wakifika Nairobi washuke walale hapo kisha warudi na basi la kuelekea Mwanza. Mabasi yenyewe hayako designed kwa safari ndefu. Huyo dereva mwenyewe atapumzikia wapi? Kiti chake ameuza apate pesa.
Muda wa kuendesha usizidi masaa 4 aidha dereva apumzike au wabadilishane