Kaka michuzi,habari ya kazi?
natumaini unaendelea vizuri na shughuli za ujenzi wa taifa.Nimesoma malalamiko ya mdau kutoka Afghanistan anaedai kua simu zake mbili na camera viliibiwa DIA kutoka kwenye bag lake.
Kwanza kabisa ningependa kuwaelimisha wasafiri kua vitu vya thamani(valuable items)haviruhusiwi kuwekwa kwenye mizigo inayokua checked in.Na hii ni kulingana na sheria za ICAO na IATA ambao ndio wanaoweka sheria mbalimbali zinazohusiana na usafiri wa angaa.
Na unapoona kuna ulazima wa kucheck in mizigo yako ya thamani lazima utoe taarifaa unapokua unakabidhii mizigo yako,halafu utaambiwa utaratibu wa kufuata.Utaratibu huo ni pamoja na kulipia mizigo ya ko gharama za ziada na kukatia bima.
Tusiwe wepesi wa kupenda mteremko,lazima tufuate sheria kabla ya kulaumu. Nakuja kwenye swala la madai kua mizigo yake iliibiwa DIA.
Napenda kukufahamisheni kua mizigo inapokua inashushwa kunakua na usalama wa kutosha ikiwa ni pamoja watu wa mamlaka ya viwanja vya ndege,usalama wa taifa,polisi,na wana usalama wa kampuni ya SWISSPORT, wengine ni pamoja na wanausalama wa mashirika mbalimbali ya ndege.Tukio lolote la kuibiwa mizigo ni gumu kulingana na wanausalama wote hao.
Mizigo inaweza kuibiwa mahali mnapobadilishia ndege au mwanzo wa safari kulingana na usalama unaokua sehemu hizo. Bwana michuzi naomba maelezo hayo uyaweke,siyo kwamba nabahatisha,nilifanya kazi katika kitengo hicho cha mizigo iliyopotea na iliyopatikana (lost and found)kwa muda wa miaka mitatu.
Mdau kutoka ughaibuni.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 56 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 27, 2009

    Mdau wa ughaibuni usijaribu kutetea wizi au jambo usilolijua vizuri... Issue iloletwa ni WIZI na kutafuta namna ya kuondoa tatizo hilo..kila kitu duniani ni valuable item na tunagharamia kuvipata isipokua hewa tu tunatopea na Mwenyezi Mungu bure..Nakubaliana na wewe izo sheria za IATA lakin point ya wadau ni kwanini wizi ufanyike JKNIA?? SIkubaliani na wewe kabisa kuwa wizi unaweza fanyika airport kama za UK au USA na hata Amshaterdam au Dubai kwa kuwa wenzetu wana ustaarabu na kuthamini mali za wengine. Binafsi nlisafiri kutoka USA kwenda UK na bag 2 na zote sikuweka kpfuli wala locks; nlijaza perfumes kama 15 kwa ajili ya kufanya biashara bongo lakin nikafika UK kila kitu kilikua sawa, waliniwekea kikaratasi kua wamepekua bags zangu kwa ajili ya usalama lakin hamna hata handkerchief iloibiwa; ingekua ni bongo am sure nisingepata perfume wala nin, wangejizolea zote!!! Muhimu ni uongozi wa aiprorts zetu uwajibike kuhakikisha usalama, staff wao wasidhubutu hata kuiba pipi ya mtu sandukuni!

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 27, 2009

    Mi napendekeza tubadilishe jina la Eapoti yetu, napendekeza tuiite FISADI INTERNATIONAL AIRPORT!! Ili popote ulipo ukiwa unafanya booking yako ya ndege unajua mara moja kwamba destination yako ya mwisho unakumbana na Ufisadi. Ni udhalilishaji wa hali ya juu kuendelea kutumia jina la NYERERE wakati maskini Baba yetu alipinga ufisadi kwa nguvu zake zote mpaka siku ya mwisho. Kwa hiyo jamani, kuanzia leo Eapoti yetu ya Dar inaitwa FISADI INTERNATIONAL AIRPORT!!!!

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 27, 2009

    HABARI MR MICHUZI,
    Nimeona huyu jamaa alieweka maelezo akiwa ametoa maneno ya kupinga upotevu wa vitu,
    Kifupi maelezo yake ni potofu kabisa,yeye kafanya kazi miaka 3 iweje asijue UWIZI wa mizigo unavyofanywa pale airport.Ni muongo na jinsi ya comment zake inaonekana anashiriki wizi huu.yaani ni wazi uwizi wa mizigo umekithiri hapo Dia.Anathubutu kuongelea suala la polisi na usalama,mara swissport afficers.Wao wenyewe wananjaa na niwezi hadi wa chocolates za watoto.
    Hata ajidifence na wezi wenzie,Taarifa ipo kwa wahusika serikalini,arobaini itafika tu,Nini kufanya kazi 3yrs alafu ujui lolote unanyanyua mkono na kuleta hoja potofu na kusingizia issuarance.UPUMBAVU TUKATE BIMA HATA KTK CHOCOLATE.MAANA WANAIBA BILA KUJUA NI NINI WAMECHUKUA,Na ushaidi wa wazi,juu ya upoteaji wa air O2 plastik,sijui walifanyia nini!!!!?
    Lazima wezi watolewe pale,kuna vijana wa Swissport wanajulikana,kila siku wanauza cameras,mobiles,perfumes nk za wizi.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 27, 2009

    Huyu jamaa naye anatetea Ufisadi tu! anaposema "mizigo inaweza kuibiwa mahali unapobadilishia ndege...." ina maana mtu anayebadilishia ndege Dar anaweza kuibibiwa au hapana? au anamaanisha vinginevyo? Pia anaposema "mizigo inaweza kuibiwa mwanzo wa safari...." ina maana mtu anayeanzia safari yake Dar pia anaweza kuibiwa au hapana? Na anaposema kuna watu wa usalama wa taifa, polisi, Watu wa mashirika ya ndege, blah blah......" kwani umeambiwa huko kwingine tunapoanzia safari hao watu hakuna??? Na mwisho, mbona airport za huku ulaya hakuna kesi za udokozi isipokuwa hapo Dar(FISADI INTERNATIONAL AIRPORT)??? Fikiria kabla hujatetea!

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 27, 2009

    Haya dada G, habari za huko? nimeona habari hii nikajua ni wewe tu. Mimi najiandaa kwenda Bongo wiki ijayo.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 27, 2009

    Michu, huyu jamaa si mdau wa ughaibuni wala nini. Huyu ni agent wa JKNIA. Anancho fanya hapa ni obstraction ya criticism kutoka kwa JKNIA kwenda kwa mdau wa ughaibuni.

    Unaposema viyu vya thamani viswekwe kwenye check in luggage unataka kwenye check in luggage watu waweke nini?, majani ya randa?.

    Hao wote uliowataja kuanzi polisi, UWT na walinzi wote ni wezi. Wizi ni wizi tu, hata kama mtu kaweka diamond yake halali kwenye bag kwa nini uibe?.

    Halafu kusema mzigo unaibiwa ulipotoka au kwenye kubadili ndege ni uongo mtupu labla ndege hiyo ibadilishiwe JKNIA kwenye wezi. Hii tabia ya udokozi mbona ni ya kawaida pale JKNIA!. tuache longolongo watu waache kuwa na tamaa ya vitu visivyokuwa vyao. Mimi leo nikikanya JKNIA kila mfanyakazi namuona kibaka tu hata awe ana nyota, ngao mabegani au radio call na kapelo ya kinjagu mkononi. Wote hawa ndiyo chanzo cha kushuka kwa credibility ya JKNIA na Tanzania Abroad.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 27, 2009

    Wizi mtupu,anayetetea Maovu nae ni muovu tena huyo ndo zaidi.huwezi kuibiwa mizigo halafu mtu achukue Perfume yako,Airport za nje hata ukibeba Perfume mkononi/kwenye hand luggage huulizwi kitu,jaribu kuingia nayo JNIA uone,watakwambia weka kwenye dust bin wanaenda kutupa,JE NI KWELI au WIZI mtupu?tamaa za vitu vidogo ziko bongo tuu.
    Pia ticket yako inakuruhusu labda 20kg or 40kg bure,then ulipie garama zaidi kisa kuna vitu vya thamani,itasaidia nini kama wizi utabaki palepale?maana na lenyewe litabebwa na mabegi mengine kama kawaida.?Wizi upo na Usumbufu upo tena wa bila sababu bongo.MNAKERA WEZI WAKUBWA NYIE.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 27, 2009

    USHAURI KWA RAIS WA URT:

    Ninajua kuwa kuisafisha system iliyojaa "Vultures wa mali za watu na Uma" ni ngumu sana. Kwani huu ni mtandao ambao umeonekana wa kawaida, yaani kuanzia polisi, usalama wa taifa na mpaka mawaziri na wanyikulu wote ni watu wenye tamaa.

    Hii tabia ni ngumu sana kuishinda kwa njia za kawaida na hata TAKUKURU wameonekana pia si lolote si chochote. Watu wanaogopa kuchukua hatua kwa kuogopa kulipiziwa visasi, kama kuuwawa na wengine pia wenye imani ndogo wanaogopa kurogwa, kushushwa mishipa na kutiwa vichaa n.k.

    Ili kukabiliana na hili, Mheshimiwa rais nakushauri kwa siri kubwa tena hata bila kuwashirikisha UWT na baadhi ya wasaidizi wako, unda "KIKOSI KAZI CHA RAIS- KIITE NGE WEUSI". Kikosi hiki kisiwe na ofisi popote bali ofisini kwako, waajiriwa wasijulikane, walipwe vizuri sana, Ikibidi hata kukuzidi wewe na walishwe kiapo cha utii na uaminifu kwako. Kazi ya hawa iwe ni ku- identify watu waaminifu wasomi wanaoishi nje ya nchi na hasa Europe na Marekani ili waje kubadili system na kuondokana na wachumia tumbo wengi waliopo bongo.

    Nimetaja watu wa nje kwa sababu ya exposure na kuwa na experience jinsi wenzetu wanavyofanya mambo yao. Hii itabadilisha utamaduni wa kupeana kwazi kwa kujuana na kiitikadi badala ya uaminifu.

    Tukishapata watu hawa ambao watakuwa ni wafuata sheria na haki anza kustaafisha wabongo wote mmoja baada ya mwingine katika sehemu zinazolalamikiwa na jamii. Hii itajenga uaminifu mheshimiwa. Kwa nini Kenya wanaweza sisi bado tuna suasua tu. Juzi nilikuwa naongea na rafiki yangu mmoja alikuwa Kenya holiday nikamuuliza kama anaifahamu Tanzania akasema aliifahamu kupitia Kenya kwa kuonesha mlima Kilimanjaro ila aliambiwa kuwa usalama wetu ni mbovu sana hasa wizi kwenye mahotel na viwanja vya ndege. Iliniuma sana.

    Hivi tukiamua kuajiri graduates waaminifu ambao ni wengi sana mitaani kwa sasa na kuwalipa vizuri sehemu kama hizi za check up, polisi n.k si tutakuwa tumepiga hatua sana?.

    Kikosi kazi chako hi muhimu sana kurudisha discipline, nakumbuka wakati wa Nyerere walikuwa wanahojiwa na kunyang'anywa majumba ambayo waliyapata kwa ubadhirifu, leo hii mfanyakazi wa serikali mshahara wake laki tano kwa mwezi yupo kazini miaka mitatu hana biashara ila anamiliki nyumba ya milioni mia nane!, tunamwacha tu. Hivi ni vitu vinavyochochea wizi sehemu za kazi kwani mtu hawezi kuulizwa kavipataje?.

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 27, 2009

    jama watoa maoni tuwe serious angalau eti mtu anasajest jina la eapoti libadilishwe kuwa FISADI INT AIRPORT.

    Maana yake nini,huyu yuko sirias kweli?huko alipo anafanya jambo la maana kweli?sidhani,usikasirike,ni maoni tuu

    Toa onyo kwa wasafiri wawe makini na vitu vyao.Thus it,embu fikiria jambo la maana dada G.

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 27, 2009

    Mmeidiriki na kuifata njia iliyo mbaya kabisa,mnatamani katika yale yasiyochumwa na mikono yenu...mnadhulumu jasho la wanadamu wenzenu na hali mioyo na nafsi zenu zikishuhudia juu ya myatendayo.Na kwa hakika simanzi,huzuni na vilio vya mnaowazulumu i juu yenu.
    Hakuna faida wala amani ndani ya muyavunayo yatokanayo na mali msiyoivuna kwa mikono yenu .
    Kwanini mnafanya hivo?
    kwanini mnawadhulumu watu?
    kwanini hamridhiki na kile kichumwacho na mikono yetu?
    MSIFANYE HIVO!
    MSIFANYE HIVO!


    ooh.

    ReplyDelete
  11. AnonymousJuly 27, 2009

    Hawa ndio walewale! Eti unasema mizigo inapotea pale inapobadilishwa? Mbona tukisafiri kuelekea sehemu zingine mizigo yetu inafika salama. Unataka kutuambia kwamba hao wanobadilisha mizigo wanaibaba mizigo ya Dar tu! Mshamba kweli! Sheria unazozisema hazipo mahali popote! Tiketi si ingesema jamani au Airliner basi wangekuwa wanatuambia kila tunasafiri. Hivi jamani nasafiri halafu mzigo ninaouweka kwenye begi langu uanze kuwekewa masharti! Wewe mtu lost and found nu typical walewale mlioko kwenye chain ya wizi! Wizi pale AIRPORT ni chain ndefu mpaka hao usalama unaowataja wamo! Kama mzigo wa mtoto wa kikwete ulipatika ya kabwela unapigwa danadana mpkautasema basi!

    ReplyDelete
  12. AnonymousJuly 27, 2009

    Mzigo wa mtoto wa Kikwete unapatikana Mara moja wezi wamekamatwa wamefikishwa mahakamani! Huku si kuchezeana akili jamani! So in a very simple language wez hawa wamefugwa pale Airport, wamepewa masharti ya kwamba wasi-mess na mizigo ya vigogo! Siku hiyo wakakosea! Ningekuwa mimi kabwela nigesahau BB langu sio! Gross injustice!
    Hebu fikiri jitu linatoka nyumbani kwenda kudokoa mizigo ya abiria bila hata chembe ya aibu! Mna roho gani nyie watu! Kwenye mageti huko mnatupekua mpaka mnatuvua mikanda but when it comes to protecting my laggage you dont know me anymore!!!!! Why??????? kwanini lakini?

    ReplyDelete
  13. AnonymousJuly 27, 2009

    ANONY WA 01: 35 AM, Hayo mashairi yako yanafaa kutungia wimbo! Labda wanahitaji uamsho nyimbo ziimbwe redioni manake mimi mpaka nakosa hamu kabisa ya kununulia zawadi wadogo zangu!

    ReplyDelete
  14. AnonymousJuly 27, 2009

    Mdau wa 01:37 Am.

    nafikiri wewe utakuwa wa pili au tatu katika kusema mzigo wa mtoto wa JK ulipatikana. Hii ina maana gani?. Maana yake ni kwamba wezi ambao ni pamoja na UWT walijua kuwa kwa kumuibia mtoto wa Mkulu basi crackdown inakuja, hivyo kunusuru matumbo yao waurudishe mzigo. Hii ni kama ile ya Mama Malecela kuvamiwa na majambazi Dumila na polisi kuwakamata wote. Ukweli ni kwamba wizi wanajulikana sema mamlaka zinawalinda kwa kuwa kuna "quid pro quo"-relationship kati ya wezi na washughulikia wezi.

    Kama mzigo wa kigogo uliweza patikana kwa nini ya walalahoi bado inaibiwa?. JK fagia fagia rais wetu. Utakumbukwa kwa kusafisha system japo uchumi unaweza usipande. Ulianzia uhamiaji, siku hizi passport wiki tu tena bila ya hongo labla utake siku hiyo hiyo, kwa kasi ile ile, nguvu ile ile na ari ile ile angalia pia TRA, bandari, JKNIA na Polisi. Hizi sehemu bado zinanuka kinyesi tena kibichi cha rushwa na wizi.

    ReplyDelete
  15. AnonymousJuly 27, 2009

    Nini kifanyike! Iundwe kamati? wapewe miazi kadhaa ya kuchunguza, watoe mapendekezo yajadiliwe na bunge! and then mambo yaendelee vilevile! Hivo ndivo ilivo! Unaweza amini fida kubwa lile bosi la takukuru eti limepewa onyo tu! Maana hiyo ndio bongo, by the time maamuzi yanakuja tolewa watu walisha sahau!

    ReplyDelete
  16. AnonymousJuly 27, 2009

    msimamo upo pale pale wezi waondolwe tu, waziri mkuu na Rais watapewa taarifa. Asante kwa utetezi.

    ReplyDelete
  17. AnonymousJuly 27, 2009

    hapa mpaka kieleweke, Waziri mkuu atoe tamko la kusafisha JNIA, wezi watoke, wezi tunawajua tu. mtawaona subirini.

    ReplyDelete
  18. AnonymousJuly 27, 2009

    Da G (mdau wa ughaibuni)kwa maelezo yako inaonyesha kweli ulinzi wa pale Ba wa Taifa eapoti ni ovyo kabisa au kuna syndicate kubwa sana ambayo nawe u mdau au ulikuwemo. Udokozi pale si siri tena sasa na wala haitaji usalama wa taifa, au usalama wa nyumba kung'amua hayo. Eti ulikua Lost and Found kwa muda wa miaka mitatu? "GOD IS WATCHING YOU"

    ReplyDelete
  19. AnonymousJuly 27, 2009

    acha kabisa suala la kusema eti vitu vya thamani. hapo bongo watendaji wamezidi. eapoti wezi bandari wezi. sasa mizigo tupitishie wapi. mkiona eapoti na bandari za majirani zetu zinashamiri mnachukia. jichunguzeni na mbadilike.

    msitulazimishe kupitishia kenya mizigo yetu pamoja na kushukia huko

    ReplyDelete
  20. AnonymousJuly 27, 2009

    sijaelewa valuable items au vitu vyenye thamani ni vitu gani. naombeni usaidizi hapo. nadhani hata soksi ina thamani kwa hiyo isiwekwe huko. sasa tuweke nini?

    ReplyDelete
  21. AnonymousJuly 27, 2009

    Huyu mtu mwenyewe katwambia kuwa alishafanya kazi kwenye hiki KITENGO cha wizi akiwa kama kiongozi. Sasa nyie haya maelezo yake yote hamjapata mwanga wa kutosha. FISADI INTERNATIONAL AIRPORT inahidharirisha Tanzania nzima. Make dunia nzima imeisha jua kwa kuwa FISADI INTERNATIONAL AIRPORT haioni ndani mizigo ya watu. Na hili swala Watanzania wenzangu inabidi tulivalie njuga, na buti. Mimi nilichosema siku ikitokea mzigo wangu unapotea watakoma kuzaliwa. Na hapo utakuwa ni mwisho wa siku 40 tosha.

    ReplyDelete
  22. AnonymousJuly 27, 2009

    Mimi nina mbinu na suggestions za kukomesha wizi wa aina hii na kusafisha hii airport. Viongozi wa usalama kama mnasoma message hii naomba mtangaze kwenye hii blog. haya yote yatakwisha!!

    ReplyDelete
  23. AnonymousJuly 27, 2009

    Ulietaka iundwe black scorpion pia ni fisadi mkubwa. Unasuggest watu walioko nje eti wakija walipwe mishahara mikubwa kuliko hata raisi ili wafanye kazi. Inamaana hawa walioko huku bongo ndio wanaostahili mishahara midogo? Huoni hata aibu kwa kusema kwamba mje mpewe mishahara mikubwa kuliko hata raisi? Kaeni zenu huko huko wala msitake kujifanya nyie ndio mnajua hela sana. Tatizo la wizi eapot kama ndio mnataka liwape shavu mmechemsha. Acha kutoa wazo lisilotekelezeka.Kukaa kwako ughaibuni iwe chachu ya kuja na mikakati inayotekelezeka sio ndoto za kulipwa mshahara mkubwa kuliko wote walioko huku bongo,eti kupita hata raisi. Umefulia wewe!

    ReplyDelete
  24. kaka michuzi huyu hatofautishe rost and found na mizigo kuchomolewa hapa swala ni kwamba unacheck mzigo wako kabla haujawekwa kwenye ndege watu wanachomoa baadhi ya vitu ilo ndilo tatizo kubwa tunaloongelea hapa na pili ni pale ndenge inapotua watu kutelemsha mzigo watu wanadokoa si wote bali ni group kuanzia security.maafisa wa usalama pamoja na polisi wenyewe kama hutaki suburi Emirates itue pale Dia uone huo mchezo.kama Ma poter waliofukuzwa majuzi ndo ilikuwa biashara yao kubebeshwa hivyo vitu,mbona digtal camera simu,ipod za kumwaga maeneo ya airport ukitaka sema but no receipt or charge zake. mdau nahisi umenielewa ni hayo kaka.

    ReplyDelete
  25. AnonymousJuly 27, 2009

    Huyu jamaa vipi huyu?

    hivi anadhani sie watoto hadi tuamue kulalamika? mimtu kama hii ndo hata matatizo yanatokea kwenye familia yake badala ya kutatua anatetea akidhani analinda heshima ya familia yake wakati anaipotosha tu.

    Mimi binafsi nishalizwa sana simu pale airport, kawaida tukitoka china hakuna kubadili ndege hadi dar, anataka kuniambia wachina ndo wananiibia? mbona toka nianze kushukia JOmo Kenyatta sijawahi kuibiwa?

    Tuache ujinga jamani, kama ni kurekebisha makosa huu ndo wakati wake.Tuache kutetea makosa yasiyokuwa na maana.

    Naungana na mdau aliesema huyu jamaa yuko uwanja wa ndege anajaribu kutetea wezi.

    ReplyDelete
  26. AnonymousJuly 27, 2009

    NIMEKUPENDA ANONY WA 12:57:00AM,UMENIFANYA NISHINDWE KU KOMENT. BILA SHAKA HUYU JAMAA NI MWIZI AU HICHO KIPINDI CHA 3YRS NAYE ALIKUWA MWIZI HIVYO ANAJARIBU KUSAFISHA PERSONALITY YAKE MAANA ANAKUMBUKA KAMERA ALIZOKUWA ANAUZA MTAANI NA VIZAWADI VYA CHOCOLATE ALIVYOKUWA ANA WAPATIA WATU AIBU ZINAMKUMBA.

    ReplyDelete
  27. AnonymousJuly 27, 2009

    MUME WANGU ANAFANYIA KAZI KITENGO CHA MIZIGO HUWA ANANILETEA ZAWADI NZURI NZURI KUTOKA NJE ANADAI ANA MARAFIKI WENGI NJE YA NCHI NA PIA ANA UZA VIFAA VYA ELECTRONICS KWA BEI POA WAKIMLETEA RAFIKI ZAKE KUTOKA NJE. KWA HAYA MALALAMIKO MNANIFANYA NIWE NA WASIWASI NAMI SIPENDI KUISHI KWA DHURUMA MAANA NAMPENDA MUNGU. NISHAURINI NIFANYE NINI NIIJUE KWELI.

    ReplyDelete
  28. AnonymousJuly 27, 2009

    mie sku hz mabegi yangu na-wrap angalau napunguza kdg hii adha maana FISADI airpot ina wataalam usipime. wrapping za nje ya nchi ni ngumu, begi likifika hapa itakua ngumu kidogo kulifungua ingawa kukukomesha wanaharibu begi lako kwa kuliburuza au kupinda mkono wa kuvuta kuliendesha begi (hili nalo tatizo).

    ReplyDelete
  29. Nashukuru kupatikana kwa nafasi ya kujadili suala hili la matumikio ya wizi uliokithiri katika viwanja vya ndege huko Tanzania.
    Nimeshuhudia watu kadhaa wakiwa na hofu ya kuibiwa mizigo yao wanaposafiri kuelekea Tanzania.
    Napenda kuelezea mfano halisi na ambao unasikitisha mno ambao umenitokea juzi Thursday 23 katika Airport moja wapo pale CANADA.
    nikiwa katika harakati za ku-chek inn mizigo yangu.nilipata ushauri kutoka kwa mwanadada wa kizungu aliyekuwa akinishughulikia pale Airport kuwa niwe macho mno wakati wa kuteremka huko Dar-es- salaam maana kuna wizi wa hali ya juu kwa mizigo ya Abiria.
    Akiendelea kunipa nasaha za kunusuru wizi wa mizigo yangu alinitaka niwe wa mwanzo wakati wa kushuka kutoka kwenye ndege otherwise kwa maelezo yake ni kuwa mizigo yangu itaibiwa.
    Hizo ndio sifa za Airport zetu zinavyofahamika.
    ni hali inayosikitisha.

    ReplyDelete
  30. AnonymousJuly 27, 2009

    Nadhani huyu jamaa anaficha tu ukweli, pale wizi mpaka samaki wa Mwanza wanatoboa maboksi ya abiria. Hakuna cha Polisi, Usalama wa Taifa, SWISSPORT wote wana njaa za ajabu. Jamani ata samaki mnaiba

    ReplyDelete
  31. AnonymousJuly 27, 2009

    Huyu aliyeandika hii habari sidhani kama amewahi kupata ndege kwenda popote..!!

    ReplyDelete
  32. AnonymousJuly 27, 2009

    CHUKUA TIME HUKO, ETI ULIFANYA MIAKA MITATU KUMBE HATA EXPERIENCE YA KAZI HUNA, KILE NACHO NI KITENGO AMA MNAUZA SURA TU PALE......WEWE ONGEA HABARI ZA KIPINDI HIKI...TENA AFADHALI UKO MBALI MAANA NINGEKUWASHA KIBAO....WEWE AIRPORT YA MIAKA MITATU NI YA SASA.......
    UNACHEKESHA SANA , YAANI UMENIUDHI SANA TO BE HONEST..NANI KWANZA WEWE ILI NIKUJUE VIZURI,WATU TUNAONGEA TUKO HAPA HUU MWAKA WA 15 ,YOU ARRE TALKING ABOUT 3 YEARS,DEAD WHAT THE HELL IS THAT....WIZI UPOO TENA MWINGI SANA..SASA TUMESHAMTUMIA MKUU WA NCHI RIPOTI SUBIRI FAGIO LA CHUMA LINAPITA SOON ,WAPE TAARIFA ULIOWAACHA SWISSPORT...HAKUNA KUBEBANA TENA.
    NI MIMI WA HAPA HAPA AIRPORT.

    ReplyDelete
  33. Maadam nae alifanya kazi hapo basi nae ni mwizi. tatizo vitu vinaibiwa Dar tu lakini ukishuka kenya vitu haviibiwi hapo utapata jibu kuwa wezi upo dar na sio unapoaanzia safari. Watz tubadilike jamani inatia aibu mtu kushuka kenya kisa unaogopa kuibiwa dar. wenzetu wanatupiga bao mpaka bandarini mamilioni yanapotea watu wanashusha vitu mombasa sababu wanaogopa kushushuia bandari salama vitu vyao vinachomolewa ni aibu hiii jamani. Wadau wa TRA mpoo! watani wanachukua kilicho chenu amkeni.

    ReplyDelete
  34. AnonymousJuly 27, 2009

    halafu mijitu hii hii wakati inakupekuwa inalalamika ati ina njaa utasikia jamani unaenda nje huna kitu utuachie mbona unaenda na hizo hela tuachie jamani ebo?! kwani za kwenu? yani imekaa kidhikidhiki tu full usumbufu yani ni bora pale ubungo basi linafika mwisho wa safari linasimama unachukua sanduku lako unalala mbele i wish na ndege pale dar zianze utaratibu wa pale ubungo tuchukulie mizigo yetu uwanjani mbona itakuwa shwari tuuuuu kuliko haya manyang'au yafaidi zawadi za wenzao

    ReplyDelete
  35. AnonymousJuly 27, 2009

    Inatia huzuni kweli hii kitu huku tuitwe wabeba ma box huku nako ukifika unaibiwa jamani ifike wakati tumuogope Mungu turidhike na kile kidogo tunachopata!

    ReplyDelete
  36. AnonymousJuly 27, 2009

    Mzee wa Libeneke!!
    Namshukuru sana kaka yangu (sijui ni dada??) wa ughaibuni kwa ushauri wake na majibu yaliyoelekezwa kwangu!!Kwanza napenda kumfahamisha mdau kwamba kwa bahati nzuri na mimi nazielewa sheria hizo anazosema, na ninaelewa taratibu zinazitakiwa kufuatwa na wasafiri ila nitakosa busara nisipomshukuru kwa jitihada zake za kuelimisha jamii!!
    Naomba nimtioe wasiwasi kuwa mimi sihitaji mteremko, sipo katika kundi hilo kabisa, kama wapo wanaopenda miteremko basi mimi sio huko!! Ndiyo maana uliona mimi sikuwa mlalamikaji wa awali bali nimeweka maoni yangu baada ya ndugu yetu mmoja kulalamikia wizi pale Dar Airport!! Kama alisoma waraka wangu niliparuriwa vitu hivyo Mwaka 2007, leo tunaenda 2010, kama ningekuwa na nia ya kulalamika kwa nia ya kupata mteremko mbona ningekomaa tangu 2007!! Jumla ya thamani ya vitu vyote haizidi $1200; sidhani kama hivyo vitu vingenishawishi “kuvificha” ili nisilipe ushuru (mteremko!!) ambao kwa kawaida isingezidi hata pesa zetu za bongo 150000/=!! Nililazimika kuviacha kwenye begi kwa vile nilishop uwanjani Dubai na begi nililinunua hapo na niliona ni rahisi kuweka vitu vyote pamoja nadani ya begi hilo ambalo later lilikuwa checked in!! Kama sheria inakataza ni sawa na nakubali kosa, kwa maana hiyo adhabu yake ndiyo kuibiwa? Ningefurahi sana kama maofisa wa pale wangekagua begi na kunionya nisiweke tena vitu vya aina ile kwenye mzigo unaokuwa checked-in badala ya kunisafisha!! Naomba mdau aelewe kuwa najaribu kukosoa “uaminifu” wa wafanyakazi pale Airport, siyo kwamba napinga sheria au hivyo vitu vilivyopotea ni ishu kubwa sana, kwa nini hatukubali kukosolewa? Kwa nini tusichukue hilo kama ni “chalenji” kwetu?? Mimi nimelitumikia taifa kwa zaidi ya miaka 12 kwa uaminifu mkubwa na naheshimu sheria na ni mlipa kodi swafi, sipo katika kundi la wanaopenda mteremko; lakini napenda kuisaidia nchi yangu, napenda kuwa muwazi kutoa maoni yangu bila woga ndiyo maana nikasema malalamiko haya yanayotolewa kuhusu usalama wa pale DIA ni aibu kwa nchi yetu inayosifika kwa amani na utulivu!! Kwa nini tusiongezewe sifa ya kuwa waadilifu na waaminifu??
    Kuhusu suala la kwamba mzigo unaweza kupotelea pale unapounganisha safari basi nadhani kesi yangu ni tofauti…nilikuja moja kwa moja! YES, wakati na-konekti usafiri kutoka DIA kwenda Tandale kwa Mfuga-mbwa ndiyo baadhi ya vitu kwenye begi langu vikapungua…koneksheni yangu ya kwanza ilikuwa DIA ambapo nilibeba begi langu kwenda zangu Tandale…….!!
    Mzee wa Libeneke, nashukuru kwa nafasi kwenye globu yetu, nashukuru kwa maoni ya wadau na namshukuru mdau wa ughaibuni kwa lekcha yake kuhusu sheria za IATA na ICAO. Nikipata nauli nitamtembelea ughaibuni.
    Hizi ndiyo salamu zangu

    ReplyDelete
  37. AnonymousJuly 27, 2009

    Yeyote anetetea wizi DIA nae ni fisadi, wewe unajua kiasi gani kimenigharimu kunua hivyo vitu?.narudi nyumbani bongo unanisachi na kuniibia mbona nchi za wenzetu hawafanyi hivyo, acheni kuwaibia watanzania wenzenu na kuwadhurumu jasho lao, tubadilike tafadhari hii ni aibu ya taifa

    ReplyDelete
  38. AnonymousJuly 27, 2009

    Anon wa Mon Jul 27, 06:42:00 AM

    Sasa kama wafanyakazi mliopo bongo asilimia kubwa ni wezi. Na hili linadhihirisha katika malalamiko haya ya udokozi wa chocolate mpaka nguo za ndani kwenye ma-bag ya watu unatarajia nini?. Si mmeshindwa kazi?.

    Halafu punguza hasira, Nani kakwambia NGE WEUSI watoke ughaibuni?, ukisoma vizuri jamaa alivyoeleza ni kuwa hawa watu kazi iwe kutafuta watanzania wenye exposure kutoka nje ili waje wabadili system ya wezi waliopewa dhamana ya kuangalia usalama wa mizigo ya watu.

    Vile vile kumbuka huwezi kumtoa mtu alitepo wall street uje umlipe $250 kwa mwezi. Ni lazima uanze na $8,000. Iengo likiwa kusafisha system ili watu wema wanaomaliza pale UDSM, UDOM, MZUMBE,SUA,IFM,n.k waje kubadili kuliko hawa wanaong'ang'ania kazi graduates wakati wana-elimu ya darasa la nne. Matokeo yake wanaishia kuwa wadokozi.

    ReplyDelete
  39. Mdau - BongoJuly 27, 2009

    Hua mwizi anahitaji kujua kilichopo ndani ya begi, ili ajue kwamba thamani ya mali inalingana (kwa maoni yake) na hatari ya kukamatwa akiwa katika tendo la kuiba, pamoja na faida anayotarajia kuivuna wakati wa kuuza hiyo mali.

    Sasa, tukumbuke kwamba katika usafiri wa ndege mizigo yote hua inapitishwa katika x-ray scanner katika airport ya kuondokea na sio ile ya kufikia. Pindi ndege inapowasili Dar, wahusika wanahangaika kuharakisha kuifikisha mizigo kwa abiria wanaosubiri kwenye mikanda ya mizigo. Hakuna scanning hapo, ila watu wa Customs wanasubiri kuvuta malipo ya kodi kwa mali zinazohusika.

    Hivyo, sii sahihi kwa huyo mdau wa kutoka Afghanistan kufikiria kwamba ameibiwa hivyo vitu vikiwa vimeshafika hapa Dar. Pamoja na ukweli kwamba wezi wapo katika nchi zote duniani, hakuna wala muda wala uwezekano wa kubaini mali na kuiiba wakati ndege imeshawasili.

    ReplyDelete
  40. AnonymousJuly 27, 2009

    HUYO JAMAA ANAJITETE BURE MIE NIMSHAWAHI KUJARIBU KUUZIWA VITU KUTOKA AIRPORT NA NIKAKATAA..NA MWIZI ALIKUWA ANAFANYA KAZI DAHACO..HUYO KIJANA ALINILETEA SIMU,NIKAKATAA,AKALETA POCHI NIKAKATAA,VITU KIBAO..UMUULIZA UNAPATA WAPI ANASEMA AIRPORT..HUYO KIJANA ALISHAWAHI HATA KUIBA POCHI YA MJEJA ALISAHAU KWENYE NDEGE..AIRPORT YA BONGO DAR WEZI WATUPU!!ACHA KUJITETEA..HATA AIBU HUNA..MDAU NORWAY

    ReplyDelete
  41. AnonymousJuly 27, 2009

    Huyu jamaa anaongea tu. 2006 nilikuwa Tanzania kuna siku kulikuwa na habari kubwa kweye TV watu waliibiwa vitu vingi kwa mpigo kukawa na malalamiko makubwa sana mpaka kusababisha reporters kwenda uwanja wa ndege koripoti kuhusu hilo tukio. Watu walikuwa wanatokea Dubai (nadhani walikuwa wasafiri wa Ethiopian Airlines). Na huyu mjinga anasema ni kipindi hicho alikuwa kazini pale?!

    ReplyDelete
  42. AnonymousJuly 27, 2009

    Mdau wa Bongo

    Ulichoongea ni sahihi kabisa wala hujakosea. Kwani mtu anayejua kuwa kwenye bag kuna nini lazima atakuwa makini katika kuiba bag lenye nguruwe aliyenona. Kwa kuwa hawa ni vibaka basi wao hufanya pata potea kwa kuhisi tu yaani by chance. Sometimes wanapatia kweli na ila wakati mungine wakosea step na kujikuta wamefungua bag lenye chocolate, kwa kuwa mwizi akiingia ndani basi akikosa cha kuiba hata kijinga cha kuni ataondoka nacho na ndivyo walivyo hawa watu JKNIA.

    Wanaangalia bag na kufanya trial and error, ndiyo maana wakakosea na kuiba la mtoto wa JK, baadaye wakaamua kulirudisha kwa kujifanya UWT wamelipata.

    ReplyDelete
  43. AnonymousJuly 27, 2009

    Mdau asitetee ujinga
    mimi mwenye 9 of march nilikua nikitoka Dar kuja Msterdarm na KLM.na nilikua na Perfume yangu aina ya blue for Men. na niliiweka chini ya nguo katika begi langu.chakushangaza nilipofika Amterdarm niambuli box na Perfume walikuwa waneishainywa wafanyakazi wa hapo dia.kwa hiyo mdau asitetee uhalifu. Tunasema vitu vyenye uhakika na utubahatishi

    REK
    Norway

    ReplyDelete
  44. AnonymousJuly 27, 2009

    hapo nikumdondoshea Fax mkubwa. utaona mabadiliko mara moja.

    ReplyDelete
  45. AnonymousJuly 27, 2009

    Wewe uliyeandika habari hii nina uhakika wewe ni mmoja wapo wa wafanyakazi wa pale airport na mmoja wa wezi wa simu za watu kaa kimya wewe mjinga.

    ReplyDelete
  46. AnonymousJuly 28, 2009

    Huyo anaejiita mdau wa ughaibuni mwenyewe mwizi alafu anatetea wezi wenzie kafanya kazi miaka 3 ndio anajiona mzoefu, tujaribuni kupiga hatua kwenda mbele kwa maendeleo mazuri na sio kwenda mbele kwa ujinga wizi upo na lazima wahusika waufanyie kazi ili ukomeshwe na tupate kuhifadhika kwa aibu kutoka kwa wageni wetu na hata sisi wenyewe tuliokuwa ughaibuni tupate kuwabebea vijizawadi ndugu na marafiki zetu zifike zikiwa salama usalimini.

    ReplyDelete
  47. AnonymousJuly 28, 2009

    Kuna mdau ameuliza swali la msingi. Kosa la kuweka vitu vya thamani kwenye checked luggage adhabu yake ni kuibiwa?
    Japo sio mwanasheria lakini katika sheria kuna kitu wanakiita "intent"...sheria ina nia ya kufanikisha nini. Sijui kama hii ni sheria au mwongozo lakini unapoambiwa usiweke vitu vyako vya thamani kwenye checked luggage, intent ni kutolaumiana kwa sababu ya uharibifu wa vitu vyako vya thamani na usije kulidai shirika la ndege pesa nyingi kwa sababu ya uzembe wako. Tukumbuke kwamba wafanyakazi wa viwanja vya ndege wanahamisha mizigo mingi katika muda mfupi. Ukiweka laptop yako mle bila kuifunga vizuri basi unaweza kushtukia begi limebamizwa laptop yako imeharibika ukaanza kudai watu. Sio vitu vya thamani tu, hata vitu unavyovihitaji mara moja unaambiwa uvibebe mkononi. Masanduku yangu yameshawahi kupelekwa Tasmania kabla ya kufikishwa Tanzania.
    Huu udokozidokozi tusidhanie ni hali ya kawaida. Tunao bongo tu, nchi zilizoendelea hazina hizo. Tubadilike!

    ReplyDelete
  48. AnonymousJuly 28, 2009

    Jamaa anatetea wizi, atuulize sie tulokwisha ibiwa DIA - tena safari ya Dar - Zanzibar tu na ndege ya usiku begi zima lilipotea mpaka kesho! Mdau kaa kimya kwanza unatutia hasira ***&&&& ''''

    ReplyDelete
  49. AnonymousJuly 28, 2009

    Jamani watu wengi tunajua na tumeibiwa sana hapa airport, suala lililopo ni kuwasaidia hao viongozi wao wanawaajiri watu wanadhani ni waaminifu kumbe ni wezi toka hata huku mitaani, watupe nafasi ya kuwataja tunaowajua wanaofanya vitendo vya wizi na kuja kujisifia mitaani na kutafuta wateja wa simu kila siku na simu mpya wewe mtu ushanga haoni na aibu hajui unajua kabisa anafanya kazi Swissport akichacha yuko baa anauza simu kwa bei ya kutupa ili anywe bia na kesho anakuja na simu nyingine, tupe nafasi tuwataje!!

    ReplyDelete
  50. AnonymousJuly 28, 2009

    Mdau wa jul 28,10:11am kama unawajua wewe wataje ndiyo itakuwa mwanzo wa uchunguzi na wao wenyewe pia wataogopa.

    ReplyDelete
  51. AnonymousJuly 29, 2009

    Kwani wewe muaminifu unaweza omba hii kazi ukapewa kama humjui mtu pale? Mimi namuonaga jirani yangu anafanya pale AIPORT ndugu zake huwa hawajui hata kusoma hata chembe, lakini wako pale eaport wanadunda. Mimi nilienda kuomba kazi pale niliambia kama si mjui mtu yeyote pale siwezi kupata nafasi yoyote. Kwa hiyo pale ni pekana pekana tu. Wanazoa vibaka waweka tu, si ndugu wako pale.
    Iliniuma sana huyo mama aliponiambia nimpe TSHS 5000 alipatie hiyo nafasi. Baadae Mungu akaniona akanileta huku Marekani nikabebe maboxes. Nayanalipa kweli make ni haki yangu. Kila ninapoenda Bongo namuangalia huyo mama simuoni, siku nikimuona nitamtemea mate usoni kwa ajili ya ufisadi.

    ReplyDelete
  52. AnonymousJuly 29, 2009

    Kila nikiamka , nashukuru Mungu nimepewa viza ya halali ya kuishi nje na kupewa pasi ya ulaya. Kila nikisoma hapa, nashukuru kuwa naishi nje. Maisha ya bongo ni ya kiwizi wizi tangu zamani sana na hayatabadilika.

    ReplyDelete
  53. AnonymousJuly 30, 2009

    MWIZI MKUBWA WEEE. SWISSPORT,TRA, VITAMBI UHAMIAJI WOTE WEZI WATUPU KUDADEKIIII. NCHI IMEJAA WEZI, RUSHWA, UKABAJI, UPORAJI, UNYANG'ANYI, UMBEA, UBADHIRIFU, UZEMBE, UDAKU, UMWINYI, YAANI HAINA MWISHOOOO.
    NANI ASIYEJUA DUNIA HII KAMA BONGO NI NIGEIA YA PILI? DUNIA NZIMA WANAJUA BONGO IMEIZIDI NIGERIA KWA RUSHWA HIVI SASA.

    ReplyDelete
  54. AnonymousJuly 30, 2009

    Mdau wa Jul 29 01:52 Heri yako ila kumbuka myumbani ni nyumbani hata kama kuna kunguni. Na ukweli wa mambo bado unapapenda licha kuwa upo ulaya la sivyo hata hii hoja usingechangia, si etii eeeee?

    ReplyDelete
  55. AnonymousJuly 30, 2009

    Mdau 03:20 AM:

    Nyumbani ni nyumbani, na napenda sana kutembea familia Tanzania. lakini, sina ndoto ya kuja huko kuishi hata kama nikipata kazi ya maana. Napenda maisha yangu hapa na mwaka kesho, safari itapungua zaidi kwa kuwa familia iliyobaki huko wataruhusiwa kuja hapa kuishi na mimi London. Ila, mishikaki, kababu ninamisi sana, zaidi ya hapo, sina nia yoyote ya kurudi bongo. Nitapapenda Bongo mpaka nikizikwa ila sitaishi tena huko, ila nitakuja (nikipewa viza) kwa matembezi kila miaka mitatu hata kama sita kuwa na familia tena huko. Kama ulivyosema, Home is Home.

    ReplyDelete
  56. Anonymous
    Wizi huu ni Airport ya DareSalaam,siyo point of departure au connection, nilisafiri may sikuamini jinsi watu walivyo na njaa, wanaiba kimacho macho,ukiongea wanakutishia kukuitia polisi.na ni ukweli wanaiba vitu hata wasivyovifahamu,hawana utu,wala hawajiheshimu,wanadhani ni haki yao,waliiniibia mpaka vitu vya urithi, Jamani mwogopeni Mungu.Whats goes round comes round.ndiyo mnatuyanyasa,mnatuibia hadi chupi, siku yeni itafika.nimesafiri sana Afrika na Europe, sijahawi kuona watu wenye tamaa na njaa kama wa Dar-Es-Salaam Airpot,mnajua jinsi tulivyopindika kupata zawadi za kuleta nyumbani halafu nyie mnajisaidia?mie hamnipati tena,nimejifunza.Nyumnani nitarudi sana kusalimia lakini hamtapata vya Ulaya kutoka kwangu.Its A Promise.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...