SEHEMU YA JIJI LA DAR IKIWA IMEGUBIKWA MOSHI UNAOTOKA KWENYE MELI YA MIZIGI 'MV PEMBA' AMBAYO IMESHIKA MOTO MUDA MCHACHE ULIOPITA BANDARINI DAR. HABARI ZINASEMA MOTO ULILIRIPUKA WAKATI MABAHARIA WAPATAO 20 WA MELI HIYO WAKIWA WAKIIFANYIA MELI MATENGENEZO YA KAWAIDA KABLA YA KUANZA SAFARI YA ZANZIBAR NA PEMBA IKIWA NA SHEHENA YA VYAKULA, MAFUTA NA VITU VINGINE. HAKUNA ALIYEPATWA NA MADHARA
GARI LA FAYA LIKIWA LIMEBEBWA KATIKA PANTONI YA MV ALINA ILI KUIFIKIA 'MV PEMBA' AMBAYO IMESHIKA MOTO
KIKOSI CHA FAYA CHA MAMKLAKA YA BANDARI KIKIWAJIBIKA SAMBAMBA NA FAYA YA MANISPAA YA ILALA KUUTHIBITI MOTO HUO.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 28, 2009

    Bado tupo nyuma sana,yaani hatuna boti maalum ya kuzima moto unapotokea kwenye meli, mpaka gari la kuzimia moto libebwe kufikishwa eneo la tukio? hii ni aibu sana.
    Watanzania mbona hatupo makini? tuna matatizo gani?

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 28, 2009

    Duh! Jamani hizi meli ziangaliwe, tulianza na moja kuzama, jana moja imekatika mlango ikiwa njiani,leo moto! Najua tukitoka hapo tunahamia kwenye ndege!!!

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 28, 2009

    Chanzo hatujaeleza bado, Nishoti ya umeme au kunabaharia alikuwa anapiga jiko la gesi au ni nini? Pili mdau nyingi unatumika kuokoa mali isiteketee. Mpaka fire ije waipandishe kwenye pantoni. Si wangechukua pump wavute maji kibao baharini. simple and clear. to save time

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 28, 2009

    Majanga yamezidi mbona, ikitoka nchi kavu inakwenda majini..well, Michuzi tunashukuru kwa kutupa news kama zinavotokea, Mungu atunusuru maana ni ngumu kupokea taarifa za namna hii..

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 28, 2009

    MSISHTUKE JAMANI HILO NI ZOEZI LIMEANDALIWA NA KIKOSI CHA ZIMA MOTO KUJIWEKA SAWA IN CASE MELI IKIWAKA MOTO NINI KIFANYIKE. BIG UP SANA FAYA.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 28, 2009

    Nilifkiri tulivyofanya D===R===I===L==L hivi majuzi ilikuwa tunajiandaa kwa majanga kama haya? Lakini hatuna vifaa? Duu....kuna kazi hapa.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 28, 2009

    nimependa ubunifu wa kubeba FAYA kwenye pantoni, Tanzanians are very inovatoors, tunatumia dhana na utundu tulionao katika wakati wa dharura, hatuwezi kuwa na technologia ya wazungu.
    jamaa walioosimamisa trip za watu walifikiria ujanja mzuri vinginevyo bandari yote ingewaka

    ReplyDelete
  8. Du Bandari ya Salama TAMBARAREZZZ,
    sa JE KAMA MELI INAUNGUA OVERSEAS KULEE INAKUWAJE ???Tutapakia Fire trucks hadi huko>>>>>??
    BALOZI Gombea Urais Ufanye MAMBOZZZ

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 28, 2009

    Ole wenu kama pantoni yetu nayo ingeshika moto. Inakuwajee mbona bandari na eapoti hapa kwetu ndio wanaaminika katika kupambana na majanga kama haya??

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 28, 2009

    Miaka ya Nyerere wakati nasoma Forodhani Sec, hapo hapo liliungua jahazi. Tabu ilikuwa ni mapipa ya gas yalivyokuwa yakilipuka na upepo ukawa unasukuma hizo fire balls upande wa shule na Wizara ya Maji (enzi hizo). Watu walitoka mkuku maghorofni...Jamaa wa fire hawakutokea kabisa (labda wese halikuwepo au "pumzi" ktk magurudumu haikuwepo) mpaka jahazi likaungua na kubakia frame na majivu tu.
    Blakmpingo

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...