WATEJA WA DAWASCO SASA KUWEZA
KULIPA BILI ZAO KUPITIA VODAFONE M-PESA
Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania kwa mara nyingine imewawezesha wateja wake kulipa bili za maji kupitia Vodafone M-Pesa.Kwa sasa wateja wa vodacom wamewezakulipa bili zao za maji kwa kila mwezi kupitia Vodafone M-Pesa.Ni siku chache tu tangu kutangazwa kwa malipo ya LUKU kupitia Vodafone M-Pesa.
Mkurugenzi Masoko wa vodacom Tanzania Ephraim Mafuru alisema katika makao makuu ya DAWASCO, kuwa kwa niaba ya Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom, Tungependa kuwakaribisha DAWASCO katika ulimwengu wa Vodafone M-Pesa. Vodafone M-Pesa ilianzishwa mapema mwaka jana(2008) kama huduma ya kusafirishia pesa kutoka kwa mtu mmoja kuelekea kwa mwingine.Huduma hii imeendelea kukua na kupanuka hadi kuwawezesha wateja wa Vodacom kulipa bili,ada za shule na ulipaji wa mikopo.
Vodafone M-Pesa ni njia rahisi ya kutuma hela kwa kutumia simu za mkononi.Mtandao huu wa Vodacom M-Pesa uliyowawezesha wateja wa Vodacom kulipa bili zao za maji DAWASCO.
Vodafone M-Pesa ni njia rahisi ya kutuma hela kwa kutumia simu za mkononi.Mtandao huu wa Vodacom M-Pesa uliyowawezesha wateja wa Vodacom kulipa bili zao za maji DAWASCO.
Mafanikio ya huduma hii yamefanikiwa kwa ushirikiano baina ya Vodacom Tanzania na DAWASCO.Kwa Kampuni hii ya simu za mikononi ya Vodacom tunajua huu ni mwanzo tu, Bado tutaendelea kufanya kazi kwa kushirikiana na mashirika mengine katika kukuza na kutoa huduma hii kwa ubora zaidi kwa wateja wetu.alisema Mafuru
Akiongelea huduma hiyo Afisa biashara wa DAWASCO Raymond Mndolwa amesema, Sisi kama DAWASCO tutaendelea kutoa huduma iliyo bora kwa wateja wetu kupitia mitandao tofauti ya mawasiliano.
Tunatumai wateja wetu watafurahia kutumia huduma hii ya kulipa bili ambayo itarahisisha maisha Yao.
DAWASCO imeahidi uboreshaji
zaidi katika huduma zao
Hizo Bili gani za maji yasiyopatikana? Hawa Dawasco wajirekebishe kwanza katika kufanya mtandao mzima wa maji uwe wa kuamininika ndio wajitutumue kuanzisha huduma hii ya malipo. Ninakasirishwa na kitendo cha ugawaji wa maji!
ReplyDeleteKwa hiyo zile foleni za kwenda kukaa kusubiri kulipa bili karibia zinaisha?Cashiers wataisha nyodo,soon tutalipa kila kitu online itakua poa sana.
ReplyDeleteDawasco noma,mnaanzisha kulipa kwa mtandao wakati hamjarekebisha miundo mbinu,tulipe nini wakati maji hamna????
ReplyDeleteKaka Mndolwa hebu tuelimishe kuhusu huo mradi wa wachina maana hatuelewi sisi raia wa kimara nyumba nyingine wanapata maji nyingine hawapati je wanatumia vigezo gani? na je huu mradi wa wachina una uhusiano gani na DAWASCO yetu tuliyoizoea kwani maji yanamwagika ovyo tu mitaani,naomba kuelimishwa nikiwa kama mteja muaminifu na mkongwe wa DAWASCO
ReplyDeleteHey Raymond, keep it up. Tupe maji kila mahali, pesa yenu mtakusanya vizuri tu, si unajua wabongo kwa simu wako radhi walale njaa, simu iwe na vocha.Mosile, hongea Mndolwa. FirePower, UK
ReplyDelete