DJ EDDY SALLY, DJ MASHUHURI NCHINI, AMEFARIKI DUNIA LEO ASUBUHI KATIKA HOSPITALI YA MKOMBOZI JIJINI DAR AMBAKO ALILAZWA KWA MATIBABU TOKA JANA.
HABARI KUTOKA MSIBANI AMBAKO NI NYUMBANI KWA MAREHEMU SINZA KUMEKUCHA HAPA JIJINI ZINASEMA MAZISHI YATAFANYIKA KESHO KIJIJINI KWAO KISARAWE.
HAYATI DJ EDDY SALLY ATAKUMBUKWA KUWA MIONGONI MWA MA-DJ WA MWANZO KABISA NCHINI, AKIWA AMEANZIA DISCO LA SEA VIEW KABLA YA KUHAMIA LUSAKA, ZAMBIA, ALIKOTOKEA KUWA DJ WA KWANZA MMATUMBI NCHINI HUMO.
MIAKA YA 80 ALIREJEA NCHINI NA KUANZISHA LIBENEKE LA 'EM THREE DISCOTHEQUE' KWENYE UKUMBI WA KEYS HOTEL AKIWA NA DJ SWEET FRANCIS AMBAO KWA PAMOJA WALITETEMESHA JIJI KWA VIFAA VYA KISASA NA SOUND SYSTEM ILIYOKUWA BORA KULIKO ZOTE ENZI HIZO

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 28, 2009

    Inna lillaah wa inna illaah rajiun. maskini alikua DJ kwenye harusi yetu mwaka 1996.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 28, 2009

    poleni sana !! ila kaka michuzi ingependeza mmatumbi huyo maana alituma burudani ya muziki miaka hiyo ungetuwekea picha yake watu wapate kumkumbuka miaka mingi imepita

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 28, 2009

    Mungu Ailaze Roho yake mahali pema Peponi

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 28, 2009

    Please allow me to send my condolences to his family and to all music lovers,especially those who enjoyed Eddy`s good spinning of LPs.
    I have just composed a list of oldies which I am sure DJ Eddy Sally used to play in the `80ties. Please log onto: http://www.playlist.com/bmpingo then scrow down to oldies. If you like what you hear, please leave a comment.
    RIP DJ!
    Blackmpingo

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 29, 2009

    HUYO NDO ALIKUWA DJ FAST EDDY AU MWINGINE???? NAOMBA WADAU MNAOJUA MNIJULISHE..

    ReplyDelete
  6. REST IN PEACE! Kweli Eddy Sally alikuwa DJ hasa! Many fond memories! Please Michuzi kama una picha bandika.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...