Mzee wa nanihii habari ya wewe.
Tafadhali naomba nirushie tangazo langu kwa wadau.

Tunahitaji secretary ambaye ana experience isiyopungua miaka miwili na (asiwe maimuna) mwenye kujua kuzungumza na kuongea kingereza kizuri. Umri wowote lakini usizidi miaka 30.
Yeyote mwenye sifa zilizotajwa hapo juu tafadhali atume CV yake kwenye email: tneema58@gmail.com.
CV zote zitajibiwa ikiwa ni pamoja na kupewa taarifa zaidi na maelekezo zaidi.
Mwisho wa kutuma maombi ni Jumatano tarehe 8 / 7/ 2009.
Wenu Mdau.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 26 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 02, 2009

    Jamani hizi kampuni uchwara nazo kero tupu, muwe mnaajiri ma HR, maana mtumaji tu sijui ndo bosi communication skills zero kabisa, hawajaweka hata location sasa si ni makubwa haya mtatujibu dunia nzima kwa kazi ya kigoma!

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 02, 2009

    Kaka linapokuja swala nyeti hivi la ajira usikubali matangazo "ya hovyo hovyo" kama hili. Hakuna kitu kinaitwa "wenu mdau" katika soko la ajira. Ni lazima muajiri mtarajiwa ajitambulishe vyema na afuate taratibu za kisheria katika usaili na utoaji wa ajira. Swala la kazi ni la kisheria zaidi kuliko la kijamii. Kuna uwezekano mkubwa kabisa mtoa tangazo anataka kuwarubuni dada zetu. Ni hayo tu, usinibanie...

    NDUN'GANI NAKAIYO DONGO S.L.P. 4 KIBAYA-KITETO MANYARA TANZANIA

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 02, 2009

    Secretary Akija JIbaba limoja Tambi hilo miaka 25 msimkatae kama vyeti vyake vimetulia mchukueni msifanye ubaguzi wa jinsia sababu hapo hamjaweka mwanamke au mwanaume ila nafikiri kwa namna mlivyosema asiwe juu ya miaka 30 nyie mnataka mdada nyie. yule aliyekuwa anatafuta kazi humu pengine duwa yake imekubalika mchukueni. au kama naye alikuwa anatusanif atakuja kupata tabu mbele. Pazi.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 02, 2009

    Naona Mdau hapo ana practice age discrimination jiendeleze kimawazo mdau

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 02, 2009

    Age discramanation!!! why under 30 years old?

    ReplyDelete
  6. Mama Lil BJuly 02, 2009

    Kwa yoyote anaehusika. umeweka tangazo la kuhitaji karani, ila cha ajabu hujasema company gani inayohitaji wala sehemu ambayo huyo secretary anatakiwa, tanzania. asia,europe au america? maana mtu anaweza kua anataka hiyo kazi ila hajui ni nchi gani atafanyia.
    hebu jaribu kuongezea information za sehemu anayotakiwa kufanya kazi nk.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 02, 2009

    Hii sio dili kwa akina dada tu kwani haijasema kuwa mwombaji ni lazima awe mwanamke!! kwa hiyo mzee wa libeneke usiwazibie bahati akina kaka. tangazo linataja sifa tatu: tajiriba, kiingereza , na umri. kina kaka pia changamkia tenda!!

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 02, 2009

    Wacha kuchengua watu wewe. Kazi iko nchi gani na wapi? Wewe unadhani mtandao upo hapo ulipo wewe tuu eee?? Acha kulala. Amuka.

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 02, 2009

    aisee hii kali

    Umri wowote, asizidi miaka 30?
    P.E.D

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 02, 2009

    huu ujumbe haijatulia kabisaa

    ReplyDelete
  11. AnonymousJuly 02, 2009

    mtumaji wa ujumbe huu hajatulia. yaani email: yaani kweli; just like that. please acha utani na blog yetu

    ReplyDelete
  12. AnonymousJuly 02, 2009

    Ni vizuri ikijulika na kampuni gani au mtu gani anahitaji hii huduma au atleast ni sector gani husika ilkupata mtu muafaka zaidi. Kwa mfano kama ni hospitali unahitaji mtu anayejua ku handle nyaraka zi ki hospitali.

    ReplyDelete
  13. AnonymousJuly 02, 2009

    Hili tangazo mbona lina ubaguzi wa kijinsia? Kuna wanaume kibao wahazini wana uwezo wa kumfanyia kazi vizuri tu mdau.

    ReplyDelete
  14. AnonymousJuly 02, 2009

    location, location, au ni ujumbe 419 toka nigeria?
    Mdau
    Kiparamoto,
    Mgeni-nani Mbagala DSM.

    ReplyDelete
  15. AnonymousJuly 02, 2009

    hivi bongo bado kuna age discrimination kwenye kazi hata ya u-secretary?na tangazo linarushwa live kwa michuzi bila hofu?hahaha,ama kweli bongo tambarare...

    ReplyDelete
  16. AnonymousJuly 02, 2009

    Hili tangazo kwakweli linachanganya sana.
    je! huyu mtafutaji anatafuta secretary au anatafuta secretary mwanamke? Anasema umri wowote halafu anatoa umri wa juu wa muombaji. Sasa hapo haiwezekani iwe umri wowote. Ameshasema umri usizidi miaka 30.

    ReplyDelete
  17. AnonymousJuly 02, 2009

    Age discrimination!

    ReplyDelete
  18. AnonymousJuly 02, 2009

    Nadhani ujumbe pamoja na mtumaji mwenyewe vyote havijatulia! Kinachotakiwa kujibiwa ni barua au CV? Nisaidieni wadau.

    ReplyDelete
  19. AnonymousJuly 02, 2009

    Mtumaji wa huu ujumbe hujatulia unahitaji Feni.Ok, Sasa wale wasio na utaalam wataupata wapi? maana kila tangazo wana limit awe na ujuzi usiozidi miaka kadhaa. Ni nani atamkubali yule anayetoka chuo asiye na utaalam wowote ndio kwanza anatafuta msingi?

    ReplyDelete
  20. AnonymousJuly 03, 2009

    Huyu anatafuta mke au mchumba?

    ReplyDelete
  21. AnonymousJuly 03, 2009

    SCAM, jamaa anatafuta vibint!

    ReplyDelete
  22. AnonymousJuly 03, 2009

    hakika wewe unatafuta mchumba!!! Mbona wewe umeandika Kiswahili???? Nahisi unataka akufunze kingereza ukiwa nae

    ReplyDelete
  23. AnonymousJuly 03, 2009

    Weweee!!! Hiyo ni Company gani anayetangaza hata haweki vigezo vyovyote??? Wewe mwenyewe unaonyesha ni maimuna kwanza then haujaelimika...Hebu usituchekeshe

    ReplyDelete
  24. AnonymousJuly 03, 2009

    Mtu anayejua kingereza vizuri kamchukue UK kama unataka.......coz wabongo hawajui vizuri najua wengi ni I MEAN I MEAN nyingi kwahiyo hawatakufaa. Weshazoea lugha za kibantu kingereza hawajazaliwa nacho ni chakusomea tuu....

    ReplyDelete
  25. AnonymousJuly 03, 2009

    Salary scale????????? Maana kuongea kingereza si mchezo ukumbuke kuwa sio lugha yetu hiyo mtu atakuwa ametuliza kichwa sana kujifunza.

    ReplyDelete
  26. AnonymousJuly 03, 2009

    I agree with all the anomymous who argued about age!!! In this era kweli we still discriminate about age in Tanzania??? Ingekuwa ni huku nchi za watu ningeelewa kwa sababu wana historia ya kudiscriminate lakini they don't kwa sababu watashtakiwa. We need to change this and give jobs to the people who qualities regardless of their age. Labor rules za kijinga hivi zinabidi kupitiwa and be updated. It's a shame!!! Kama niko 35 but I look 25 nikija hapo kweli ungeninyima ajira citing age?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...