Timu ya FC BONGO ya helsinki leo imefuta majonzi ya kufungwa na kilimanjaro ya stockholm baada ya kuibamiza timu ya ndugu zao wa finland TAS ya mji wa tampere kwa goli 3-2.FC BONGO iliweza kuumudu mchezo kwa dakika zote tisini na kabla ya mapumziko walikua wakiongoza kwa magoli 2-0.

TAS ya Tampere iliweza kubebwa na refa ambaye ni shemeji ya mmoja wa wachezaji wao kwa kupewa penati tatu, penati mbili wakapata magoli na penati moja iliokolewa na kipa wa FC BONGO Steve Mashallah ambaye alikuwa ni nyota wa mchezo huo uliochezwa katika kiwanja cha mazoezi cha FC Bongo kijulikanacho kama (Vumbi Stadium).

Pichani Kipa wa Fc Bongo Steve Mashallah mwenye jezi ya orange akiokoa kona. Picha zaidi tunamuomba Edo Ndaki wa Tampere atushushie kwa michuzi.

Habari na Michuzi correspondant
Helsinki.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 05, 2009

    Edo Ndaki kaondoka helsinki jana na kilio ataweza kutuma picha kweli?

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 05, 2009

    Steve Mashala ametuonesha kwamba ye ni kipa nambari 1 hapa Nordic na hana mpinzani.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 05, 2009

    Timu ya FC Bongo iliocheza leo,imecheza vizuri na kwa maelewano sana,naombea vijana ndio wangekutana na Kilimanjaro FC

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 05, 2009

    VUMBI STADIUM, ha ha ha ! hilo jina mmenikumbusha chang`ombe jamatini.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 05, 2009

    Sasa na wao watamwekaje shemeji kuchezesha mechi ngumu namna hiyo?

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 05, 2009

    Heheheeeee! Sasa hao Bongo FC walibanjuliwa nane kwa moja (8 - 1)na Kilimanjaro Fc ya Sweden: Kwahiyo kwa hesabu za haraka haraka ni hivi: Kwa kila goli moja walilofunga Bongo Fc dhidi ya THE KILIMANJARO wao (Bongo FC) walimanuliwa manane (8). Lets see: kwahiyo roughly speaking: KWA KILA GOLI WANALOFUNGA BONGO FC HUWA WANATAKIWA WAFUNGWE MAGOLI NANE NA MPINZANI WAO (KUTOKANA NA UBOVU WA TIMU YAO HAWA BONGO FC) THEN FROM THAT BASE: TASS WAO WANGECHEZA DHIDI YA THE KILIMANJARO WANGEMANULIWA (HAWA TASS I MEAN) MAGOLI 8 X 3 TO MAKE IT 24!HENCE PROVED MATHEMATICALLY!!!! OOH NOOOO! MNH, LOL!!!!

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 05, 2009

    Magoli yalikua 4-2, mwandishi kakosea, magoli ya FC Bongo yalifungwa na Sami na John kipindi cha kwanza na kipindi cha pili yalifungwa na Adam na Ali.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 05, 2009

    4-2 sio 3-2

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...