
Profesa Haroub Othman
Kwa niaba ya familia napenda kutoa shukurani zetu kwako na blogu ya jamii kwa kuwahabarisha ndugu, jamaa na marafiki kuhusu msiba wa mzee Haroub Othman.
Tunawashukuru sana ndugu, jamaa na marafiki wote walioweza kuhudhuria maziko, hitma Zanzibar, Dar, Tabora na Pemba.Tunawashukuru sana wale walioweza kufika nyumbani chuo kikuu na wale wote waliotuma salamu zao kwa njia mbalimbali.
Tunatoa shukurani pia kwa vyombo vyote vya habari vilivyokuwa vinahabarisha jamii katika kipindi chote cha msiba.Shukurani kwake Hamza Kasongo na timu yake ya Channel Ten kwa kurusha kipindi cha kumbukumbu ya mzee jana jumapili.
Leo Jumatatu kutakuwa na hitma nyingine
katika Msikiti wa Mwembechai baada ya sawala ya I'sha.
Tena nasisitiza shukurani zetu.
Familia
inshallah mola apokee dua zetu na zikufikie ulipo, akuondoshee mazito na adhabu za kaburi, akupe nuru katika kaburi lako na kwa uwezo wake mola ulale mahali pema.
ReplyDeleteameen.
Naomba watakao soma wasianze kufokwa na mapovu kisha kunishambulia. Jamani ukweli ni kwamba katika uislam mtu anapokufa ni vitu vitatu vinaendelea kumnufaisha.1-sadaka endelevu yaani kama marehemu ameacha kitu cha kheri na chenye manufaa kwa jamii, ataendelea kula credit akiwa huko.2- mtoto mwema atakaekua anamuabudu mungu na kumuombea mzazi wake na 3- ni elimu yenye manufaa kwa jamii. Tuachane na huu uzushi wa mahitima tutayasoma hata milioni lakini hayana manufaa kwa marehemu. account ishafungwa isipokua kwa vipengele hivyo vi3.kama mna pesa hazina kazi kasaidieni mayatima.
ReplyDelete