HILI NI GARI LA FAYA LA KAMPUNI LA KNIGHT SUPPORT AMBALO LILIMPA LIFTI ANKO NANIHII LIKIWA LIMEPAKI KATIKATI YA UWANJA WA CHUO CHA POSTA KIJITONYAMA MAJI MACHAFU, DAR
JUU NA CHINI NI ANKO NANIHII AKIWA NA ASKARI WA FAYA WA KINGHT SUPPORT ALIYEMPA LIFTI KWENYE KIKAPU CHA KUZIMIA MOTO YA GARI LA FAYA LA KAMPUNI HIYO LIKIWA LIMEPAKI KATIKATI YA UWANJA WA CHUO CHA POSTA

ASKARI WA FAYA WA KNIGHT SUPPORT AKITUPELEKA JUU KIASI CHA MITA 100 HIVI.
MAJJENGO YA KAMPUNI YA SIMU YA NANIHII, JENGO LA SAYANSI NA LINGINE LILILO KATIKA UJENZI.
Chemsha Bongo ilikuwa hapa:
chemsha-bongo.html#comments
Wadau kunradhi sana kwa kutotoa jibu jana kama nilivyoahidi. Hii imetokana na jinsi mchuano ulivyokuwa mkali sana. Ila Nina furaha kutangaza kwamba mshindi HAJAPATIKANA kwa sababu ukisoma swali na kurejea tena kwenye kurasa wa chemsha bongo pamoja na taswira na maelezo hapo juu, utaelewa kwa nini.
Swali lilikuwa ni je Anko nanihii kasimama juu ya jengo gani???
Hata hivyo kati ya wadau 79 waliojaribu kujibu, kuna wadau wanne tu ambao wamegusa karibu na ukweli. Nao ni Lulu, Lyimo, na Samweli ambao wametaja anko nanihii kasimama juu ya mnara.
Kiboko yao ni mdau Anonymous wa Fri July 24, 01:24: ambaye angejitaja jina angekuwa kashinda, kwani kwenye karatasi ya mtihani ukisahau kutaja jina inakuwa soo.
Hivyo basi narudisha mpira huu kwa wadau kuomba msaada wa ni yupi kati ya hao watatu anastahili zawadi??? Na je Anonymous anastahili kupata zawadi kwani tutajuaje kama ni yeye???









Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 24 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 28, 2009

    Mshindi ni anonymous! huyo ndo anastahili zawadi.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 28, 2009

    michuzi acha ubahiri hiyo picha umejipinga mwenyewe wala hujapendeza ajili mtu wa kukuchukuwa picha unapohitaji ujuwe mjanja hajinyowi na pili ukimwajiri mtu nae utampa kula sio ule wewe tu oh muone kwanza kicha kama ugali tayari!

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 28, 2009

    Mithupu noma mimi ndo nimeshinda niliyetoa jibu kwamba upo kwenye "UNGO" mimi ndo mshindi na sikubali ninakata rufaa kwani haukua kwenye jengo lolote ila kwenye "UNGO" wa gari la faya. Angalau nilikuwa karibu sana na jibu hivyo ninapaswa kupewa nusu zawadi yangu! Tutafikishana mbali kama hautanipa ushindi wangu.
    Mdau USA

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 28, 2009

    Umepandishwa bila kofia, askari kavaa yake.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 28, 2009

    Mithupu,mimi ndiye Anonymus niliyetoa jibu sahihi.
    Mimi hapo mahala napahafamu sana kwa vile nilifanya kazi Posta Na Simu miaka ya 91/92.
    Mithupu nipe mji tu maana nina stahili,ila nitaendelea kuwa Anonymus maana bado hiyo option ipo katika utambulisho

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 28, 2009

    Michu,

    nipatie zawadi yangu na uache uongo, utakaa vipi kwenye "kijiko" cha faya, kwani wao hawana kazi ya kufanya!! Mimi ndio nimepata jibu sahihi nilisema ulikuwa kariakoo shimoni. na bado nitaendelea kuwa anon.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 28, 2009

    NAONA UKUBWA DAWA, UNAFIKISHA UJUMBE WA DR RICK WA WATU KUJENGA UTAMADUNI WA KUWEKA MAJINA YAO KATIKA MAONI, KI UTU UZIMA. SAFI SANA MITHUPU. USINGEKUWA CCM ,UNGEKUWA JUU KAMA JD ALIVYOSEMA. MASHINDANI ZAIDI YATAWAJENGA WATU.

    ReplyDelete
  8. NautiakasiJuly 28, 2009

    Misupuz acha "bias" zako zakutoa zawadi kwa wanawake tu kila siku, hivi umetumia logic gani kuanza kumtaja LULU wakati yeye ndo mtu wa mwisho kutoa comment inayoakribia na ukweli, tena kama haitoshi, huyo lulu kama ni mtihani alisha feli sababu alishaandika jibu akakusanya pepar then next day ndo anakuja na jibu, hivi unahakika gani kwamba hakudesa kwa waliomtangulia. Kwa haki na usawa na uadilifu sababu mwenye jibu sahihi kiasi ni anonymous, basi mshindi awe huyo alowahi kutoa comment (wa kwanza sijui ndo SAMWEL)) alekaribia ukweli. Huenda waliomfuata wote "wame desa" kwake. Maana ushanza kujipendekeza kwa mdada huchelewi kutwambia na mshindi ni FATMA SHEFA wa Uk (lol) au HABIBA ALMAS wa oman. Hovyooooo!

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 28, 2009

    Hapa michuzi hukufanya haki. swali lako lilikuwa ANKO NANIHII ALISIMAMA JENGO LIPI. wewe umeuliza jengo lipi hukusema eneo gani. Kwa hiyo hata hilo jibu ulilotoa wewe mwenyewe si sahihi. kwa sababu hjataja jengo. umefanya kama wale wnaoset maswali ya mitihani wakisha hawajui hata walichouliza.

    ReplyDelete
  10. Anko nanihii....

    Nimefurahi sana kwa kuwa miongoni mwa waliotoa jibu sahihi. Hii inaonyesha jinsi gani kumbukumbu yangu ya Bongo bado ilivyokuwa kichwani.

    Kwa kuchangia mada hii maoni yangu ni yafuatayo:

    1. Anonymous hakuwa na uhakika na anachokijibu kwa sababu ametaja maeneo matatu tofauti, alikuwa akibahatisha.

    2. Lulu amegelezea, na kugeleze huwa hairuhusiwi.

    3. Lyimo naona amejibu vyema kama mimi. hivyo basi nakumbuka tulivyokuwa shule ya msingi kulikwa kunauwezekano wa washindi wa kwanza kwenye mtihani wakawa WAWILI (Wamefungana) na wote hupewa zawadi sawa.

    Kwa heshma na taadhima, nawasilisha kwako Mkuu ya wilaya ya Nanihii na Balozi wa Nanihino ombi la kuwepo kwa washindi wawili. Mimi (SAMWELI) na Lyimo.

    SAMWELI

    ReplyDelete
  11. AnonymousJuly 28, 2009

    MICHUZI
    KATI YA HAO WATATU HAKUNA MSHINDI KWANI HIYO GARI SIO MNARA NIA CRANE NA ANONYMUS HATUWEZI KUHAKIKI UTAMBULISHO WAKE KWANI WANAWEZA KUJITOKEZA WATU WENGI.LABDA KWA ZAWADI HIYO HIYO TUBUNI CHEMSHA BONGO NYINGINE NA TUWEKE JAPO VIMASHARTI KIDOGO ILI KUONDOA UTATA WAKATI WA KUTOA ZAWADI

    MDAU KUDOJA WA DAR

    ReplyDelete
  12. AnonymousJuly 28, 2009

    lkn mjomba michu ulituchanganya kuuliza kuwa mkuu wa nani hii amesimama ktk jengo ngani? wakati hikusimama ktk jengo lolote vizuri swali lingekuwa mkuu wa na hii kasimama ktk gari gani?
    mdau
    kisiju pwani

    ReplyDelete
  13. AnonymousJuly 29, 2009

    Nimeangalia majibu naona ANONYMOUS WA FRIDAY JULY 24,91.24..NDIYE MSHINDI.

    ReplyDelete
  14. BULICHEKAJuly 29, 2009

    AISEE MICHUZI NAOMBA NIONGEE JAPO SIO MAHALA PAKE..
    JAMANI TELEVISHENI YA TAIFA (TBC1) INAKUAJE HAINA WEBSITE KATIKA DUNIA HII YA UTANDAWAZI, MBONA HATUJIFUNZI JAMANII? WENZETU BBCUNAWEZA STREEM ONLINE VIPINDI(PROGAM)....ANGALI WENZETU WANATUPIGA GEPU KATIKA MAMBO MADOGOMADOGO.LIFIKISHE KWA WAHUSIKA
    ATLEAST HATA UGHAIBUNI TUONE ZECOMEDY... TUJIFUNZE JAMANI
    http://www.bbc.co.uk/iplayer/tv

    ReplyDelete
  15. AnonymousJuly 29, 2009

    ok, ok, mi ngoja nianze kwa kukuuliza swali. Hivi anko nanii kilichokupeleka kupanda hiyo gari na wakakupeleka kule juu ni nini?
    Kwa upeo wangu nahisi kama unaweza kuwaaharibia jamaa waliokuwa duty kazi yao, hasa pindi maboss wao watakapojua kuwa uliitumia gari yako kwa kupata picha za kujiridhisha na kazi yako, unless kama mlikuwa katika kutengeneza promo ya Knight Support. Naomba unielewe lakini siongei kwa ubaya ila nahisi ungeishia kutambulisha kuwa ulikuwa juu ya gari yenye wichi tu. Hata hivyo Big Up sana tu. Nisiwe kapuni tafadhari

    ReplyDelete
  16. AnonymousJuly 29, 2009

    HIVI UNGEANGUKA HUKO SIJUI INGEKUWAJE. MAANA HAYA MAGARI YA SAFETY NAYO MABOVU, SI MMEONA ILE MELI ILIYOENDA KUOKOA MELI YA MOTO NAYO IKAKWAMA? MNARA GANI UNAZUNGUMZIA, U MEAN A MONUMENT? BUT THATS NOT A MONUMENT THO!

    ReplyDelete
  17. AnonymousJuly 29, 2009

    hivi michuzi kwa mfano ukimtaka demu yeyote yule hasa wale waliokaa sana ughaibuni utamkosa kweli???!!!! acha wale wa home make wale mapozi yao bado ya kizamanizamani!!!

    ReplyDelete
  18. sasa bro misupu mim i nasema hakuna anayestahili kupewa zawadi.huyo aliyeshinda hajashinda kwani kwani huyo kadesa kiasi kwamba kashindwa kukumbuka jina lake.hapo hakuna mshindi kwani hata kwenye mtihani usipoweka namba au jina lako NECTA wanatupilia mbali karatasi lako.chaooooooooo

    kiochedi

    ReplyDelete
  19. AnonymousJuly 29, 2009

    mithupu na wewe swali lako halikukaa vizuri, uliuliza umesimama jengo lipi? kwa nini usingeuliza umesimama wapi? umechemsha na wewe halafu usibane haya maoni...

    ReplyDelete
  20. AnonymousJuly 29, 2009

    Anko nanihii, japo unaipenda kazi yako ila hili tukio ni hatari, hauwezi kupanda hiyo lifti ya faya bila kofia ya usalama, na kumbuka hao askari wa knight support ni fire marshal ambao wamekatiwa bima, sasa wewe ukechoropoka toka juu ingekuwaje?
    Next time akikisha safety first at work place. Nawasilisha

    ReplyDelete
  21. Samweli mi sikulegeze ila wakati mtu unapofanya mtihani unakuwa na rough paper na penseli, sasa niliandika jibu langu then nanihii akaliweka mtandaoni kumbe nilikuja kuweka jibu sahihi na kukusanya paper pale ilipokuwa muda wa kukusanya paper. Sasa basi nakubaliana na anon Tue Jul 28, 08:10:00 PM
    kuwa Michu abuni chemsha bongo nyingine na ikiwezekana tuhusike sisi tu wenye majibu karibu na ukweli au hata jopo lote. Tuichukulie hii kama changamoto wanayokabiliana nayo Baraza la mitihani. Kaka Michu lete kitu kingine tukifanyie kazi.

    Waweja sana!!!!

    ReplyDelete
  22. Nautiakasi una machungu kweli ushajaribu kubahatisha akashinda mwana mama nini??? Jina la LULU lisikutie simanzi inawezekana ni mwanaume vile vile amependa tu kujiita LULU au vipi??? Kwani hujaona Witness, Furaha, Neema ambao ni wanaume???

    Utiekasi halafu tafakari!!!

    ReplyDelete
  23. hapo hakuna mshindi.
    Swali limetaka jengo jibu limekuja gari la kuzimia moto.

    Mtihani umevurundwa huu lazima urudiwe upyaa.Eboo!!

    Kisoda2

    ReplyDelete
  24. AnonymousJuly 29, 2009

    ANKO WEWE NDIO ULIKOSEA KUULIZA SWALI, UMEULIZA ULIKUWA JUU YA JENGO GANI, SASA HATA TUNGEJIBU ULIKUWA JUU YA CRANE YA FIRE INGEKUWA TUMEKOSEA MAANA SIO JENGO

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...