SHIRIKISHO LA MPIRA WA KIKAPU TANZANIA (TBF) LINAPENDA KUZIPONGEZA TIMU ZA JKT WANAWAKE NA WANAUME NA TIMU YA ABC WANAUME AMBAZO ZILISHIRIKI LIGI YA TAIFA ZA VILABU VYA TANZANIA NA KUSHIKA NAFASI ZA KWANZA NA ZA PILI HIVYO KUPATA TIKETI YA KUWAKILISHA NCHI KATIKA MASHINDANO YA FIBA AFRIKA UKANDA WA TANO YATAKAYOFANYIKA UGANDA TAREHE 27JULAI HADI TAREHE 2 AGOSTI, 2009
NCHI ZINASHOSHIRIKI NI PAMOJA NA UGANDA, KENYA , BURUNDI, RWANDA, ETHIOPIA, ERITREA, SOMALIA, SUDAN NA TANZANIA

TUNAWASHUKURU PIA VIONGOZI WOTE WA JWTZ, JKT NA PATRON WETU MHE. JAJI MKUU KWA KUWEZA VIJANA HAWA KWENDA KUSHINDANA KATIKA MASHINDANO HAYO.
TUNAJUA UGUMU WA BAJETI KATIKA SEKTA ZOTE NA HUSUSAN KWENYE SHIRIKISHO LETU LAKINI PAMOJA NA UGUMU HUO WOTE PAMOJA TUMEJITAHIDI KUHAKIKISHA TIMU HIZI ZINAKWENDA KWENYE MASHINDANO HAYO
TUNATOA WITO KWA BMT KUZIDI KUPIGANIA VYAMA VYA KITAIFA KUPATA RUZUKU ILI WALAU VYAMA HIVI VIWEZE KUJIKIMU KUJIENDESHA NA KUSAIDIA VILABU NA TIMU ZA TAIFA PINDI ZINAPOSAFIRI KWENDA NJE NA MASHINDANO YAKE MENGINE YA HAPA NCHINI

TUNAWATAKIA SAFARI NJEMA NA KILA HERI KATIKA KUTETEA HESHIMA YA NCHI YETU
LAWRENCE CHEYO
(KATIBU MKUU- TBF)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Just curious!
    Nahisi maelezo yaliyowekwa hapo ni juu kuhusiana na Wanamichezo wetu ni mengi mno(too much information)

    Kufahamika majina yote matatu ya kila mchezani pamoja na tarehe zao kamili za kuzaliwa hadharani ni mwanya tosha wa kufanyika Ugharamia.
    Internet zimejaa watu wabaya ambao wanaweza kutumia taarifa hizo kwamaslahi yao.
    kwa mawazo yangu nahisi kulikuwa hakuna haja ya kuchapishwa full date of birth.
    Ahsante mhusika wa blog hii.

    ReplyDelete
  2. Nakubaliana na Sedouf. Hakukuwa na haja ya kuweka taarifa binafsi kama tarehe za kuzaliwa kwani zinaweza kutumika vibaya.
    Lakini suala langu jingine linahusu jinsi gani vyama vyetu vya michezo vinajizatiti kifedha. Kupewa ruzuku ni moja, lakini vyama hivi ninatakiwa kuwa na mikakati binafsi ya kunyanyua vipato vyao. Natumai Cheyo na Kasesela watazingatia hili.
    Mdau
    Faustine
    http://drfaustine.blogspot.com/

    ReplyDelete
  3. Mchezaji wa Zamani - PaziJuly 29, 2009

    Kaka, mie hofu yangu ni kuona kuwa hata wachezaji wa basketball nao siku hizi wanaongopea kuhusu umri wao? Wachezaji wengi wao umri wao uliopo hapo si wa kweli kabisa, tumecheza nao na tumesoma nao. I think we should not allow basketball becoming a cheating game. DARBA & TBF kuweni makini.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...