Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 16 mpaka sasa

  1. Al MusomaJuly 21, 2009

    Is there any truth in the rumour (which I am starting now) that people like KP are paid huge sums of money to incite religious acrimony for the benefits of nobody?

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 21, 2009

    Hii kweli kabisa udini unanukia vibaya sana,hii yote ni kuiyumbisha serikali iliyopo madarakani thats it nothing more. Ila hakika wenye husda allah atawadhalilisha

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 21, 2009

    Haya `Udini unaanza kutweta' eti kwasababu kuna chama kinaanzishwa kwa mfumo wa dini. Nafikiri ni heri kusema ukweli, `nyie' hamtakiwi kusema, au kuanzisha,`nyie' ni bendera fuata upepo, kwani toka lini `mswa....aka...(jaza sehemu zilizowazi)

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 21, 2009

    Michuzi,

    Hongera Masudi kwa kukumbushia hili,wale wanaojifanya hawaioni hatari hii subirini chakula kiwekwe mezani. Acheni unafiki.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 21, 2009

    Hongera na pongezi kwa kuliona hili. wapo wanaopuuzia lakini ukweli utakuja kubainika muda si mrefu, pale tutakapoanza kunyenyepeana kwa sababu ya udini. wabunge wetu wana acha kujadili mambo ya maana bungeni wao wanakumbatia ajenda za udini, wakati serikali wanayoitumikia inasema kuwa aina dini.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 21, 2009

    KP naona umahiri wako katika sanaa
    Hongera sana
    salam toka zenj

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 21, 2009

    kabla sijasoma habari hii nilikuwa sijaelewa ujumbe wa kipanya, habari nimeipata kule darhotwire kayajue mengiEhh udini wanyemelea Mjengoni!
    Huku kukiwa na kila dalili za wazi kwa baadhi ya wabunge kuonesha dalili za kujisahau na kuanza kupandikiza mbegu ya udini miongoni mwa Wabongo, Mbunge wa Singida Kaskazini Bw. Lazaro Nyalandu, (CCM), amevunja ukimya na kuwaonya wabunge wenzake kuwa Bunge si Msikiti wala Kanisa kwa huku akitaka Serikali kufuta kabisa wazo la Tanzania kujiunga na Jumuiya ya Kislamu Duniani (OIC).

    Akichangia hototuba ya bajeti ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa bungeni jana, mbunge huyo alisema katiba ya nchi inakataza Serikali kujihusisha na masuala ya dini na kwamba atawasilisha hoja binafsi wiki ijayo kulitaka Bunge kutojadili tena suala linalohusiana na dini yoyote kama njia mojawapo ya kulinda amani na utulivu uliopo nchini.

    “Katiba hii inakataza kabisa Serikali kujihusisha na suala lolote la kidini, Katiba hii hairuhusu Serikali kuanzisha chombo chochote chenye uelekeo wa dini, Zanzibar ilipotaka kujiunga na OIC Mwalimu Nyerere hakusita katika hili alisema hapana," alisema.

    Alisema hali hii ikiachwa iendelee Bunge litageuzwa kuwa sehemu ya kujadili masuala ya kidini, udini na utagawa nchi hii. Alisema ukabila unamaliza Kenya na udini unanyemelea Tanzania na kuongeza kwamba anakusudia kuwasilisha hoja binafsi ili Bunge hili lisijadili tena suala la dini yoyote.

    Alisema katika hoja yake atayowasilisha atapendekeza kamwe
    fedha za walipa kodi zisitumike kuanzisha suala la dini yoyote na kuitaka serikali kuacha mara moja kufuatilia masuala ya OIC kwa kuwa Katiba ya nchi hairuhusu taifa kujiunga na jumuiya yoyote ya kidini.

    Kwa upande wa Mbunge wa Maswa Bw. John Shibuda aliunga mkono hoja hiyo ya Bw. Nyalandu kwa kueleza kwamba mbunge yeyote anayetaka kuwa wakala wa dhehebu yoyote au dini yoyote ni mhaini wa kikatiba na hafai kuwa mwakilishi wa wananchi kwa kuwa atapandikiza mbegu mbaya.

    koku

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 21, 2009

    Kwangu mimi M/Kipanya ni celebrity halisi Tanzania,ana uelewa wa juu sana huyu mshikaji,hii unaweza kuiona katika kila jambo analolifanya kwa jamii,sio wengine ucelebrity wa kuandikwa ovyo kwenye magazeti.
    keep it up man,big up.

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 21, 2009

    Hapa sio kp wala nini. kp kama msanii anaakisi yaliyo kwenye jamii. tatizo kubwa sana la wabongo (hususan watawala wetu) ni kwamba huwa hatupendi kukukiri kwamba kuna tatizo. na ni vigumu kutatua tatizo kama hukubali kuwa tatizo halipo. mifani ni mingi na leo tupo tunaanza kutumbua mimacho tu. tumekataa kukubali kuwa katiba yetu imechoka, yanayotokea tunayaona. tumekataa kukubali kuwa muungano una matatizo uangaliwe upya, matokeo yake ni kamati geresha ya kujadili kero za muungano. tumekataa kukubali kuwa zanzibar kuna mpasuko wa kisiasa, matokeo yake ni muafaka-feki. tumekataa kukubali kuwa nchi inatafunwa na ufisadi, matokeo yake ni kesi za geresha za watuhumiwa wa ufisadi. na SASA TUNAKATAA KUWA HAKUNA TATIZO LA UDINI?!?! kp uko sahihi kabisa ebu tusubiri chakula kilicho jikoni kiive ndipo tutakapotambua utamu wa kuuza tabasamu!!!!!!

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 21, 2009

    Niukweli tukisha ukaribisha udini tumekwisha. Watanzania tunaheshimiana kidini ndiyo utamaduni wetu, hatari twaiona ispokua tunapuzia.

    ReplyDelete
  11. I salute you Kipanya...you the best! I don't want you to die so I can say what I feel. Hear it while you are still alive, Keep it up!!!!!

    ReplyDelete
  12. AnonymousJuly 22, 2009

    Jamani mimi nauliza dini zina ubaya gani, kama watu tutaishi kama dini zinavyotaka mimi sidhani kama kuna ubaya,labda tuseme watu kutumia ubaya wao kupitia mlangowa dini!
    Tunapoogopa dini zisiwe na nafasi katika siasa ina maana sisi ni wapinga dini, na unajua anayepinga dini ni mpenzi wa shetani,sasa tunataka tutawaliwe na `ushetani'
    Kwa mfano waraka uliotolewa ulikuwa unakataza mabaya, ufisadi nk,je kuna ubaya gani hapo, mnataka matatizo yatokee ndiomseme, viongozi wa dini njooni mtusaidie! Halikadhalika vyama vya dini, ambavyo vipo, lakini nia sio kuingia madarakani vina ubaya gani, nia zao ni kuongeza imani za umini, na imani zikiongezeka, amani inatawala. Mimi nahisi tunaogopa sana `maamurisho ya mungu'.

    ReplyDelete
  13. AnonymousJuly 22, 2009

    yani hakuna siku nilompenda mtu kama uyo mbunge NYALANDU aliposema kweli yote...

    mara zote wasababishi wa vurugu/vita ktk nchi ni wanasiasa na viongozi wa dini,vyombo vya habari(pale vikitumika vibaya km rwanda)

    serikali ya Tanzania haina dini basi!!!
    anaetaka dini yake/imani yake ishike hatamu ktk nchi basi si budi atengeneze nchi yake/sio tanzania kabisa uko aabudu kulingana na imani yake imtakavo

    sio kelele apa

    ReplyDelete
  14. AnonymousJuly 22, 2009

    Huyo Nyalandu amejaa chuki na Udini, Mbona hahoji suala la Tanzania kuwa na mahusiano ya Ukatoliki(kuwepo na mahusiano na Vatikan)?Yaani inapokuja waiaislamu kudai haki zao kujiunga na OIC au kuwepo Mahakama za Kadhi(zilikuwepo udini wa Mwalim ukazivunja) sasa Waisilamu wakidai maslahi yao ndio inakuwa Udini?????!Hebu kuweni wakweli wa Nafsi zenu!!
    Maranya Mkoani Mara

    ReplyDelete
  15. AnonymousJuly 22, 2009

    Serikali 90% duniani zinashikisha dini hatamu. Zile za kidini ziko wazi na za kisekula kwa siri. Kila afisa atatenda kwa mamlaka yake bila kuhojiwa.

    Mikutano ya mipango hii hufanyika kwenye nyumba za ibada kwa waumini watumishi wa serikali bila ya watu wengine kujua.

    Kutokuwa na ushahidi wa hili hasa ndo lengo la wakutani, wamefanikiwa.

    Serikali zisizo na dini ni chanche saana, mf. china.

    ReplyDelete
  16. AnonymousJuly 23, 2009

    someni waraka wa kanisa na serikali kwenye gazeti la RAIA MWEMA.www.raiamwema.co.tz

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...