Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo(WAMA) Mama Salma Kikwete akimsabahi Bi.Amina Saidi na mwanaye mchanga Salma Saidi aliyejifungua kwa upasuaji katika hospitali ya Mkoa wa Shinyanga jana(jumatatu).Mama Kikwete alitoa vitanda viwili vya kujifungulia na seti moja ya vifaa maalumu vya kujifungulia.
Wanachama wa SACCOS ya SHIMSA mjini Shinyanga wakishangilia baada ya mke wa Rais Mama Salma Kikwete kutoa hundi ya mfano yenye thamani ya Shilingi Milioni Mbili na nusu kuisaidia SACCO hiyo.Fedha hizo zimetoka katika taasisi ya WAMA anayoingoza. Hafla ya Makabidhiano yalifanyika katika ukumbi wa CCM Mkoani Shinyanga.

Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo(WAMA) akiwa katika picha ya pamoja na wanachama wa SHIMSA SACCOS ya mjini Shinyanga m,uda mfupi baada ya kuongea nao katika fisi zao mjini Shinyanga jana. Picha na mdau Freddy Maro wa Ikulu.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 21, 2009

    Hongereni wa mama wa Shinyanga, kwani mnang'ara yaonekana mambo si mabaya.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 21, 2009

    watu wanaosema vitambi vitambi ooo chuzi punguza tumbo ebo hio ndo miili yetu ya kiafrika unaona mmama alivoshiba pale

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 21, 2009

    Yah,heri mimi sijasema : 2Mama Kikwete= mama Nanihii

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 21, 2009

    miili minene ipo sehemu zote duniani,lakini ukweli ni kwamba sio afya na ni matatizo makubwa kifya,ila kwa kuwa jamii ya kiafrika imezoea kuishi maisha ya dhiki,hivyo wengi hupima halinzuri ya maisha kwa kuangalia unene wa mwili wake. lakini kusema ukweli na bila kumbeza mtu,huu ni ushauri wa bure tu, jitahidini kupunguza mafuta ni hatari sana kwa afya!!! na kama unapata nafasi ya kwenda gym ni bora pia kuushep mwili wako upendeze na uvutie. mambo ya 50/50/100 yalikuwa ya zamani wakati elimu ya afya ilikuwa haijafahamika vizuri kuhusu madhara ya unene.
    ni hayo tu,asanteni.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 21, 2009

    Kweli hawa wamama ni 4 bay 4 by waaaa!!!hongereni jamani kwa kujaliwa unene..mdau norway

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...