dk. liky abdallah aongelea mswaki, kanta, zazuu na mengineyo..
Home
Unlabelled
dk. licky abdallah alonga juu ya 'mswaki' na zazuu na mengineyo
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Most read Swahili blog on earth
dk. liky abdallah aongelea mswaki, kanta, zazuu na mengineyo..
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
Dr. Licky unatuvunja mbavu:)
ReplyDelete(US Blogger)
Asanta sana DR Licky,mambo uliyoongea ni ya kweli na kimsingi.
ReplyDeleteTatizo lipo sana lakini huku ughaibuni paliwahi kuzuka mjadala kama huo ikaonekana kuwa kidogo watanzania tunanafuu ukilinganisha na wanaijeria.Wenzetu hata kama wapo kwenye midnight romantic conversation utasikia milipuko ya
sauti zikifokeana kwa kelele za kutisha,na wenzetu sauti za kike na kiume ngoma droo.Ukiuliza
kama kuna ugonvi? Watajibu hapana,huyo ni Babatope anam-turn
on mkewe Olufonke.Nasisi tunaiga
kwenye sinema zetu ambazo unapotazama inapendeza sauti iwe
chini sana vingevyo utamwamsha mtoto.Muigizaji jicho limemtoka
(samahani)utadhani anasimulia Septemba eleven ilivyotokea,kumbe
anamu-engage mchumba wake
Laki pia hata pale UK waheshimiwa wakiwa bungeni shughuli ni zaidi ya hiyo hadi ngumi zinapigwa sasa sijui kama tunaiga au ni utamaduni wetu.
Toto tundu,Upper Marlboro.
Asante kijana wa zamani.
ReplyDeleteWadau mliopo ughaibuni mnapokwenda likizo nyumbani fanyeni mazoezi
kidogo.Mimi nilitukanwa barabarani
na kutaka kupigwa nilipopigiwa honi
na madereva wenzangu wenyehasira
kuwa kwanini nimesimamisha gari kwenye taa nyekundu.Gari langu lilizingirwa na hao madereva wakasema "kama umejifunzia gari Kigoma hebu kabidhi gari..umeingia mjini changanya matako..hizi taa hazibadiriki..mshamba wewe.."Nilichanganyikiwa nikatoa simu yangu na kupiga 911 nikdhani nipo Georgia avenue.Hii inasababisha foleni kubwa,kama likizo yako ni wiki mbili basi wiki moja ni ya barabarani.Wadau wa nyumbani tutofautine kwa kuheshimiana.Ubabe unaongeza foleni
Dereva Tax DC
Dr Licky, smart head.
ReplyDeletemambo gani yakuchekeshana asubuhi asubuhi...Safi sana!kula tano, Michuzi huyo mtu apewe kipindi kwenye TV au clouds wampe air time kwenye redio yao.
ReplyDeleteMjadala mzuri, mada nyingi kwa wakati mmoja, Dr Liky wewe una kipaji cha kuzungumza, Mungu akuzidishie na uko muwazi sana
ReplyDeletesalaam toka zenj
Hongera michuzi kwa kutuletea Dr licky naona anatuchekesha siku hizi. Dr licky naona unawachokoza wa bara je mziki wao unauweza? nirudi kwenye mada.. Sisi watz hatuna utamaduni wa kujifunza sheria kabisa. hata mpirani utakuwa washabiki wanampiga refa kisa kakubali goli. lakini kama tungekuwa tumejifunza sheria za soka na barabarani kusingetokea matatizo yoyote.
ReplyDeletemadau ustadh Saidi
thee teee!!! Nimekuelewa vizuri sana, kumbe hata we Dr ulisha utumia huo mswaki!. Nakubaliana na wewe kabisa lakini ujuwe pia huo uswahili ndo unaotufanye tusiwe na maendeleo na kutufanya tuwe na uvivu wa kufikri. Safi sana African Lyon huo ndo mwelekeo wa mpira wa leo, Mheshimiwa Mo nahamini anazingatia CV.
ReplyDeleteDr kabla sijamaliza swali langu kwako: Je unamtazamo gani kuhusu African Lyon ya Mbagala?
Asante sana Dr Licky kwa kutuwakilishia dukuduku na mawazo ambayo kila mtu analo na linakera sana jamii ila watu namna ya kuelezea na kulitoa kama mada au ujumbe inakuwa ngumu.I like your still for delivering the message kwa kila Mtanzania.Bro Misupu fanya mpango Dr Licky apate kipindi kwenye luninga na radioni kwani ana mada nzuri na still nzuri ya kufikishia walengwa wote popote pale hasa ndani ya Tanzania.
ReplyDeleteKama clip hii ningependa isikilizwe hata kwenye Tv ana radioni kwani itasaidia kupunguza ajali na majeruhi barabarani Tz.
Dr endelea kutunoa kwa kutufungua macho na mauzembe yetu.Naomba uzungumzie kila corner ya maisha ya watu once utakapoona una hoja nzuri kwani Dr kipaji unacho.
Kimz-Edinburgh
Dr kuwa Honest Maximo ndio kocha pekee kulipwa pesa nyingi timu ya Taifa,pia kupata sapoti ya kila aina kuanzia Rais,Fans,sponser lakini bado Timu yetu inasusua.
ReplyDeletembaya zaidi watu wamekuwa wakimsifia na kuwaponda makocha wazalendo waliotangulia na kusahau kuwa hao makocha wazalendo hawakupata hata nusu ya sapoti yoyote kama anayoipata Maximo sasa hivi.
Unazunguziaje Maximo kama kocha wa t stars.
kwa upande wako DR licky MAXIMO anafaa au hafai.
soka yetu inapanda ,inashuka au ipo pale pale.
plzz nijibu kwa mikasa ya nguvu tu duniani.
by MBONDE
Naomba kutofautiana na hoja - ni hoja nzito ya Dr. Licky. Asante kwa kazi nzuri Licky. Ni kweli, sisi watanzania tunamshambulia mtu badala ya hoja. Kumbuka watu wanaomvamia Ndugu Mashaka...nk.
ReplyDeleteAsante Licky. Ongeza tena hoja nyingine...inayoendandana na hii
Doc nimekukubali.Kama utapata muda nilikuwa naomba utueleze sisi waungwana wapenda soka haya yafuatayo,mosi inakuwaje TFF hawana website,kwa sisi tuliombali na home kupata matokeo ya ligi bado hadi usubiri magazeti ya kesho kujua kaitaba ilikuwaje au mbeya Prisons ilikuwaje,kweli kupata mtu wa IT imekosekana,mbona Mtibwa na African Lyion wameweza?Pili tatizo likowapi hizi Simba na Yanga washindwe kujitegemea?Inamaana wakikosekana watu wenye "good heart" mpira ndo utakuwa umekwisha?
ReplyDeleteTatu kuna tatizo la hawa wachezaji wanapotaka kuuzwa,mizengwe ya viongozi,Mrisho angekuwa Norway au Sweden kama sikosei lakini ilitokea zengwe bado anakipiga hapo nyumbani,mimi nacheza timu ya mtaani hapa Copenhagen lakini kuna waghana na wasenegal wametoka kwao wakaja hapa wakacheza series 3 kama daraja la 3 bila kulipwa na sasa wamesajiliwa 2nd division,nadhani bado inalipa pia na huo ni mwanzo tu.Naomba uwape ushauri wachezaji wanaposaini mkataba waweke vifungu mfano wakipata trials nje waweze kuondoka wakati wowote na waweke bei inayojulikana kwamba mimi nikiuzwa itakuwa kama USD 10k au 20k ilikupandishiana bei kusiwepo wanapopata timu nje zikawazibia nafasi.Mwisho nampa big up Henry Joseph.Nimesoma kwenye website ya timu yake wanasema atakuwa na kipindi kwenye tv ya timu mwezi wa nane.
Bib up balozi wa nanii.Mbona vakesheni zako hazikuelekezi huku Scandinavia.Karibu kwenye summer party ya watz tarehe 15 august copenhagen.
Mdau kalokola
Shukrani kwa maneno yenye busara, Dr. Na napenda kuchukua fursa hii "kutopenda kutofautiana" na hoja yako kuhusu ukosoaji!
ReplyDeleteUkibaki kwenye hoja hiyo hiyo, kuna wale marafiki zetu (labda na sisi pia) ambao tunapenda kukosoa tu. Kwa maneno mengine, tunaonesha wapi kwenye kasoro au hapafai, bila kutoa mawazo ya jinsi ya ku-improve au kutoa hoja mbadala. Mfano, ni mijadala ile ya kina Mashaka. A significant portion of us tukamtungua mawe yeye na hoja zake, na tukasahau kutoa mawazo yetu ambayo labda yangeweza kutupatia midahalo ya kutufungua macho.
Ukiacha hayo, Michuzi endelea kutuletea clips za huyu gwiji; jamaa haishiwi maneno. Licky, hivi ulizaliwa tayari ukiwa unaweza kuzungumza? Kwasababu vijana wengi tunampenda Licky, msukume kidoooogo azungumzie mambo ya elimu ughaibuni, kufanya kazi ughaibuni na mikasa mengine inayowapata vijana wa siku hizi.
Nawasilisha.
Winga Tereza.
DK Liki Mashallah Baba yetu umependeza na Umetuelimisha mengi sana. Tunakuhaidi Inshallah tutapunguza Jazba na tutafurahi Kila Mwisho wa Week au Mwezi Tukio kubwa lenye Ugomvi au uzuri ukaliweka chini tukusikie, Wewe Ndio kama Mzee Mangara Mdogo.
ReplyDeleteDK Liki Ndio Kifimbo cheza Bila Fimbo au Mdomo cheza Kutoka kwa Pazi.
Dr Licky Pamoja na maneno yako mazu ri mimi napenda nikuambie kuwa unakosea. Ni kweli kuwa hoja hujibiwa kwa hoja ila kama mtu anatoa hoja mbovu anastahili kuambiwa hivyo. Kwamba anachoongea ni upuuzi.
ReplyDeleteItakuwa vizuri ukawa unaangalia Prime Ministers Questions(PMQs) uone maana ya maneno yangu haya. hupatikana tu katika tovuti ya no 10 Downing St.(http://www.number10.gov.uk/number-10-tv/prime-ministers-questions)
Kibaya ni kumtukana mtu au kumkashifu lakini kusema "Waziri fulani anachoongea ni upuuzi au ujinga" ni sawa kabisa kama ni kweli(A spade is a spade).
Tatizo la Bongo ukisema hivyo basi Waziri huyo au kiongozi mwingine anakuwa adui.
Nakumbuka katika PMQs moja Kiongozi wa Liberal Democrat alimuambia Gordon Brown amekuwa kama Mr Bean sasa kwa Bongo hapo ingetosha kukuweka Segerea.
Kwa hiyo Dr Licky naona kwenye hili nashindwa kukubaliana na wewe fungua macho yako na masikio zaidi uweze kuona tofauti.
Mzawa
The guy is very smart! Thanks Dr.
ReplyDeleteI came across with a book titled HOW TO WIN FRIENDS AND INFLUENCE PEOPLE, by DALE CARNEGIE, an old boy from MISSOURI - USA (I was doing an MBA at one of Universities in UK), this book was one recommendant by my professor for HUMAN RELATIONS subject (careful not HUMAN ROSOURCES,)in there one paragraph says that (It is an old true maxim) I quote "that a drop of honey catches more flies than a gallon of gall" end of qoute, HONEY = ASALI, GALL = NYONGO. So with men, I mean BINADAMU, if you would win a man or a woman to your cause, first convince him or her that you are his or her sincere friend. Therein is a drop of honey that catches his or her heart; which, say what you will, is that great road to his or her reason. Here what I mean you can not win a man or women to your way of thinking by attacking him or her, try to reason with them then you come to an amicable solution. KUNA HII STORY YA JUA NA UPEPO WALIKUWA NA UBISHANO WAO UPEPO AKISEMA MIMI NINA NGUVU SANA NAWEZA KUMFANYA BINADAMU AVUE KOTI LAKE JUA AKASEMA HAPANA MIMI NDO NAWEZA KUMFANYA BINADAMU AVUE KOTI LAKE, HAYA ANZA BWANA UPEPO TUONE, UPEPO UKAPULIZA KWA NGUVU ZAKE ZOTE NA KUANGAUSHA MAJUMBA NA MITI LAKINI NDO KWANZA BINADAMU AKAWA ANANG'ANG'ANIA KOTI LAKE LISIMTOKE, MUDA WA UEPO UKAISHA BILA KUFANIKIWA KUMVUA KOTI BINADAMU, SASA ZAMU YA JUA, JUA LIKACHOMOZA NA KWA MBALI KIDIGO TU NA KUJA TAMU SANA BINADAMU AKAVUA KOTI LAKE NA KUANZA KUOTA JUA - nachotaka kusema hapa huweza ku-influence waatu au mtu to you way of thinking kwa kushambulia kwa kashifa, kejeli , dharau na vitisho, sana sana atakuwa adui yako try to reason, think about him or her don't and never ever think about yourself when dealing with people. I RECOMMEND THIS BOOK EVEN TO AFRICAN PRESIDENTS, MANAGERS, SUPERVISORS, EVEN INDIVIDUAL PEOPLE WITH SMALL DUKAS, HUSBANDS AND WIVES AS WELL AS TO KIDS, IT IS AN AWESOME BOOK.
ReplyDeleteDr.ricky kaongea ukwei ntupu,watz na waafrika wengi tumekosa kijibusara cha kutumia lugha nzuri wkt tunatofautiana hoja,kwaleo mi naongelea swala la watu wa usalama wa taifa ambalo ricky kaliongelea,mi niko hapa USA kimasomo,na watu wa CIA wanakuja vyuoni kurecruit watu wanaotaka kufanya nao kazi na mambo km yale,ni vitu vya kawaida 2,huko hm mtu anafanya kazi usalama wa taifa watu kujua inachukua muda mana ni siri utafikiri ana ufunguo wa kwenda mbinguni,ni hayo 2 kwa leo,naamini dr.rick kaleta changamoto,tubadilike wakuu
ReplyDeleteDr Licky you are one smart head na unayo ile suna ya kwamba ni mtoto wa mjini. Michango yako tunaihitaji katika kuelimisha jamii, kuburudisha, kujenga constructive arguments etc.
ReplyDeletenimefurahi umegusia hili suala la kutumia organic materials, wazungu wanajua kuwa bidhaa hizi za kemikali na additive ndio sababu kuu ya maradhi mengi, cancer, kidney failure nk. Huku ughaibuni utakuta wengi wanapenda hizi bidhaa za organics ila ni ghali mno kulinganisha na non-organics, sisi Bongo tumejaaliwa unaweza kula vyakula ambavyo ni organics lakini utakuta mtu pengine kwa kutoelewa ama kujionyesha kwamba ana uwezo ameingia katika dimbwi la kutumia mabidhaa ya kemikali kuanzia vyakula vya makopo, juice hadi vipodozi, ndio ukaona maradhi kama Cancer, kisukari na moyo yameongezeka wakati zamani yalikuwa ni machache.akina dada na mikorogo yao ndio inawauwa polepole masikini, Juzijuzi nilikuwa likizo Bongo ambapo nilishangaa kukuta familia yangu wana desturi ya kununua mivyakula ya makopo Supermarket? Nililetewa Juice za maboksi ambapo walishangaa nilipozimwaga zote na siku ya pili kuenda Sokoni na kununua fresh fruits and Vegs na nilitengeneza fresh home made juices. Inafaa tuelemishane juu ya Organic produce na faida zake.
Dr. Licky spoke the truth, nothing but the truth. Ukweli wa mambo soka la bongo si la kulipwa. Ili kupata vijana wataojitolea kucheza soka kama ajira kamili bila kuwa na uswahiba na wafadhili hakuna kitachoendelea ila kudumaza soka.
ReplyDeleteTatizo lingine ni kuwa hatuna viongozi wa klabu mpaka viongozi FAT ambao wako tayari tufike huko. They just their for their personal gains achilia mbali makundi madogomadogo ndani ya klabu ambayo vilevile wanategemea klabu kuishi.
DR. licky said it all without reforming our soccer we will still be doing business as usual like them old days.
Keep it up bro tell them loud and clear.
Dr Liky,Karibu sana Washington DC.
ReplyDeleteUtakapopata vakesheni.Tutakupokea na kukuhudumia.Tutakuonyesha jinsi tunavyobebe mabox.Tunauhakika utafurahi sana kama jinsi wewe utakavyotufurahisha na kutuelimisha
Hebu fikiria halafu utupapie mawazo yako.
Mdau DC