HATIMAYE MDAU WA MILIONI 6 AMEPATIKANA NA HIVI SASA JOPO LA WATAALAMU LINAHAKIKI INGIZO LA MDAU HUYO LILILOTINGA MARA TU BAADA YA HESABU KUTIMIA, NA ATATANGAZWA RASMI SAA SITA KAMILI SAA ZA BONGO LEO.

GLOBU YA JAMII INAPENDA KUTOA SHUKRANI KWA WOTE WALIOJARIBU BAHATI ZAO, NA WENGINE HATA KUTUMA UKURASA UKIWA UNAONESHA KUPITA 6,000,000 NA KUAHIDI KUJARIBU TENA PANAPO MAJAALIWA WAKATI WA KUMSAKA MDAU WA MILIONI 7 ISNHAALLAH KABLA MWAKA HAUJAISHA.


MDAU WA MILIONI 6 AMEPATIKANA SAA 4:42 (10:42am) KWA SAA ZA BONGO. MDAU HUYU AMESHAJULIKANA NA GLOBU YA JAMII INAWASILIANA NAYE KABLA YA KUMTANGAZA KWANI IKIWEZEKANA TUTAHITAJI PICHA YAKE PIA.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 03, 2009

    Hello kaka michuzi. Shindano lilikua kali sana! Kupata tarakimu 6,000,000 kwa spidi ambayo wadau walikua wanafukuzana sio mchezo...lakini bahati ya mtu ni ya mtu tu!! Hongera kwa mdau aliepatikana. Endeleza libeneke kaka Michuzi.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 03, 2009

    KAKA MICHUZI KAMA KUNA KAUPENDELEO FULANI HIVI.

    ReplyDelete
  3. ILIKUWA NGUMU SANA KUPATA UKURASA HUSIKA ANYWAY NITAJARIBU NEXT TIME I SURE NITA WIN

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 03, 2009

    Jamani wabongo kwa lawama...sasa kaka Michuzi amekosea nini? hamna upendeleo wala nini...mwacheni mshindi na yeye anufaike aaaah!! Apooze koo, unadhani kushinda kwenye Cafe ni kazi rahisi eeh?

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 03, 2009

    Kwa kweli ilikuwa ngumu, NEXT time basi weka hata zawadi 3 tugawane kwa atakayekuwa wa 7,000,000-7,000,010 angalau tuvunjiane hizo dola! Tumejaribu kwa moyo kupambana, wengine hata hatukulala tulijua ingetokea usiku, tunastahili hata muda wa maongezi toka VODACOM.... TEH TEH TEH!!!!!!

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 03, 2009

    Ama kweli wahenga hunena, bahati ya mwenzio usiilalie mlango wazi.Maana leo hata sikwenda beba box kabisa nilikuwa naifukuzia kwa udi na uvumba hiyo bahati ya kuwa mdau wa milioni sita.Tulikaa mimi ,mke wangu na mtoto wetu kila mmoja akiwa na komputa yake kuhakikisha tunaisaka hiyo bahati.Chakushangaza mimi nikawa mdau wa 5999999 mke wangu akawa 6000000 na mtoto wangu akawa 6000002.Kipindi mke wangu akiwa katika harakati za kucopy bahati mbaya akaidelete ile page.Sikubalini na matokeo.Mimi nakata rufaa sikubalini na matokeo.

    Naona kama kunakaujanaja flani hivi maana nakumbuka kuna anynomious wa saa 11.06am wa leo alitabiri kuwa mshindi atakuwa fatuma.... hii imekaaje kaka michuzi.

    Mdau wa uswidi

    ReplyDelete
  7. what u did is unfair, yaani nimefungua nikakuta 6999880 then after few minutes eti nakuta 6000141

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...