NAOMBA MSAADA WA WADAU KUHUSU RIWAYA YANGU YA KISWAHILI:
"ZIMWI LIKUJUALO"
na
Swallehe Msuya
Pan African Publishing Company
P.O. Box 4212,
Dar es Salaam.
Mnamo mwaka 1986 nilitoa riwaya yangu ya kwanza kwa lugha ya Kiswahili iliyojulikana kama "Zimwi Likujualo..." kupitia Kampuni ya Uchapishaji ya Pan African Publishing iliyomilikiwa na hayati Kanyama Chiume (ex-Malawi).
Baada ya kifo cha Mh. Chiume, sina hakika kampuni hiyo sasa inaendeshwa na nani. Nimekutana na watu toka Kenya wanaonithibitishia kuwa kitabu changu walikisoma katika shule za sekondari huko kwao, na pia kuna jamaa mmoja wa Kijerumani aliniambia kuwa kitabu hicho kimetafsiriwa kwa lugha ya Kijerumani.
Naomba msaada toka kwa yeyote mwenye taarifa juu ya wapi kinapatikana au kinauzwa kitabu hiki anijulishe ili niweze kufuatilia kwani wapo watu wengi wanakihitaji ili nitoe toleo jipya.
Natanguliza shukrani zangu kwani kidole kimoja hakivunji chawa na masuala haya ya "Intellectual Property theft" yameibuka kwa wimbi kubwa siku hizi!
Nawasilisha.
Ndugu yenu
Swallehe Msuya
e-mail address: ssmsuya@yahoo.com

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 04, 2009

    Mzee michuzi..I am really sorry to express my optimism to this information from this ex-Minneapolis guy.How can someone write a book,still he/she has not have even one copy..??!! It doesnt matter how long he/she published the book.This is not coming in my head Michuzi.I am so skeptical of this wadau.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 04, 2009

    Hivi michuzi ni kwamba unataka kupima ufahamu wa wana blog yako au na wewe unataka kuingia kwenye gunia la huyo mjinga? inaingia kichwani kweli kwamba mtu aliandika kitabu ila hana copy yake!!! acheni wizi wa kijinga jamani

    Sony-a-town

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 04, 2009

    mbali ya aliyosema mchangiaji wa mwanzo, hivi inakuwaje kitabu chako kinatafsiriwa bila ya idhini yako? iko wapi copy right? Haki miliki ya vitabu haikuwepo tanzania miaka ya nyuma? i don't think so!!! tena inakuwaje kitabu kinaendelea kuchapishwa na mwandishi hajui wala hanufaiki na mauzo ya kitabu chake? does this make sense?

    Ningelifurahi sana kama ndugu yetu huyu angelirudi tena hapa na kutuelimisha zaidi.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 04, 2009

    is this serious or some kind of a crazy joke here?hii ni blog ya jamii alaaaaah

    what?

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 04, 2009

    Mzee hebu mbona haueleweki??. wewe shida yako ni kitabu au shida yako ni kutaka kujua walipo wale wanaouza au kureproduce kitabu chako????
    Wewe ni mtu mzima sasa na akili zako timamu, kwa hivyo basi hebu jaribu kutueleza vizuri tukuelewe shida yako ni nini haswa?

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 04, 2009

    Jamani tuwe makini na misaada mingine. isijekua jamaa katumia jina la muandishi kutaka kupata kitabu kwa manufaa yake binafi. sababu haiingii akilini kitabu ulicho andika mwenyewe usijue nani wanasambaza,au hata nakala huna?

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 04, 2009

    michuzi ndo huwa nasema wateja wako wengi ni masenene na vichwa maji. anachhomba mheshimiwa ni kupata taarifa ya wapi wanatumia kopi zake, na ikiwezekana apate kopi moja. wanaombeza kuwa inakuwaje hana kopi, waulize wao hata material yao ya chuo kikuu wanayo. huyu kaandika kitabu 86, hadi leo ni miaka mingi sana, na nani anajua alitumia njia gani kwenda huko. computer kipindi hicho hazikuwepo, sasa wanamlaumu nini. mie nitaulizia tz, nikipata nitakutaarifa mheshimiwa. usikate tamaa.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 04, 2009

    pia hao jamaa walioandika wote hapo juu, wanaifahamu tanzania na haki miliki. wanasema tu kwa sababu wapo nje. wasanii wangapi wapo tanzania, wanalilia haki zao. juzi tu maprof wa mlimani, walilalamika kutotunga vitabu kwa sababu ya kutokuwa na uthibiti, leo wajinga fulani wanamlaumu mtu aliye nje ya nchi kuwa kwa nini hana hata kopi moja ya mwaka 86. watanzania safari ndefu kweli, na hawa ndo wako nje!

    michuzi msaidie kijana huyo kupata anachoulizia. wasikukatishe tamaa hao wabeba mabox.

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 04, 2009

    Bwana Swalehe kitabu chako nimekiulizia na hakijatumika hapa Kenya kabisa.

    Kwa wale wasiofahamu,inawezekana kabisa kitabu kikachapishwa na makampuni na kikauzwa bila ya mwandishi kufahamu.

    Uandishi ni kazi nzuri lakini hauna malipo mazuri.

    Kuhusu kitabu kutafsiriwa kwa Kijerumani, sidhani kwani utaratibu wa tafsiri ni kuwa lazima mwandishi uulizwe kwanza.

    cku nyinine ukitaka kuandika books lookf for reputable companies kama Oxfor, Macmilan na kadhalika japo pia faida siyo kubwa kama kuuza kitabu chako mwenyewe au kukiuza ulaya.

    Lakini kwa wanaomdoubt huyu jamaa the fact is uandishi wa aina yoyote Afrika ni wa kutafuta jina tu hamna hela as such be it journalism, text books, story books, lyrics etc.

    Mdau Swaumu

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 05, 2009

    Hellow Wadau,
    Hapa kuna kitu nimegundua kuwa kuna watu wana uhelewa mdogo wa mambo.Kwa suala hili kutokana na Bwn. Msuya tunaongelea kitu kinahitwa "Intellectual Property Theft" na sio "Wealth property theft". Sasa huyo mdau hapo juu anayeoji eti kama material yako ya shule,University bado unayo,hii inakujaje hapa..???!!!Kwasababu material yako umeenda kuyanunua Book store,tayari yameishaandalia,so hiyo sio "Intellectaul Property" its just Individual wealth property.Mwenye haki ya kudai "Intellectaul property" hapo ni Sir Isaack Newton au Galileo kama ni kitabu cha physics au chemistry,au Shabani Kandoro kama ni riwaya ya "Penzi kitovu cha uzembe" n.k. , na si mtu ambaye ameenda kukinunua dukani na kukitumia ndugu mdau hapo juu.Kwahiyo tusichnganye mambo hapa.

    ReplyDelete
  11. AnonymousJuly 05, 2009

    anony wa 24.00am hukutaka kumuelewa aliyeongelea material ya vyuo. alichomanisha ni uwekaji kumbukmbu zetu, na sio wealth property kama unavyotaka isomeke. waandishi juu yako wameelewa. aidha intellectual propety sio za kina kama ulivyotafsiri mzee, so long as kazi fulani inafaa kufundishia, kuelimisha na umeifanya wewe, inaqualify kuitwa hivyo. desertations, article, journal zoten na ndo maana zinalindwa na zuio la pregialism.
    MSUYA ENDELEA KUULIZIA KILICHO CHAKO KAKA, USIKATE TAMAA.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...