Sisi watoto wa Familia ya Mzee S. P. Kallinga wa Jakaranda Mbeya kwa Huzuni kubwa tunapenda kuwajulisha wadau wa Globu hii ya Jamii popote pale mlipo kuwa tumeondokewa na baba yetu tuliempenda sana sana Mzee S P Kallinga.
Baba alifariki kwa Ugonjwa wa moyo Jumapili tarehe 14 June 2009 saa 5 asubuhi katika hospitali ya Rufaa Mbeya.
Kwa mapenzi makubwa na ushirikiano wa wapendwa mbali mbali tulifanikiwa kumpumzisha baba yetu mpendwa katika makaburi ya sabasaba Mbeya tar 17/06/2009.
Tunatoa shukurani zetu za Dhati kwa wale wote mlioshirikiana nasi kwa Hali na Mali katika kipindi hiki kigumu sana katika maisha yetu.
ASANTENI SANA
Bwana Alitoa na Bwana Alitwaa
Bwana Alitoa na Bwana Alitwaa
Jina Lake na Lihimidiwe
Poleni sana jamani...Tuliksikia msiba wa mzee wetu! tulihuzunishwa sana na msiba huo...Sisi tuliokulia Mbeya hasa maeneo ya Jakaranda na Uhindini tulimfahamu sana mzee Kalinga!! Poleni sana na Mungu ailaze mahali pema peponi roho ya Marehemu mzee wetu
ReplyDeletePoleni sana Jamaa nzima ya marehemu. Mungu ailaze roho yake mahali pema amen. Je, Ni babake Sekela Kallinga aliyesoma Sisimba na Mbeya Day?
ReplyDeletePoleni sana.. I am not sure if he was related to an old class mate at Sisimba Primary School, Sekela Kalinga.....Poleni tena....
ReplyDeleteG.H.C
Poleni sana kwa msiba huo mkubwa. Naikumbuka sana familia ya mzee Kalinga na hasa Mama Kalinga ambaye alinifundisha Mbeya Primary school (Mbalizi road)
ReplyDeleteNi kweli mmepatia ni baba yake sekela kallinga, tunawashukuru wote kwa ushirikianoo wenuuu wa dhati!!!
ReplyDelete