Mkuu wa Nanihii na Wadau,
Mie nna kero kubwa dhidi ya hawa ma-DJ wanaotumbuiza kwenye minuso hasa ya harusi. Ukiacha kudai pesa kibao kwa kazi yao hiyo, huwa wanakera sana pale wanaposhobokea kupiga manyimbo yale yale utayosikia kwenye karibu kila harusi, yaani utadhani wameambiana.
Nyimbo nzuri, hasa za nyumbani ambazo zimejaa kibao kutokana na jitihada za vijana wetu wa bongo fleva na hata muziki wa dansa, huwa hawazigusi kabisa utadhani wamegombana nazo. Ukimwamba anakuja juu kama moto wa kifuu, huku akifakamia bia zetu za bure....
Utakuta DJ kakomalia kuwapigia mandombolo ya solo ama manyimbo zilipendwa ya sauzi, na wakati wa kula wanakupigia manyimbo ya ughaibuni ya kina miles david na kenny roggers. hivi kweli bongo tuna ukame kiasi hicho wa nyimbo za nyumbani hadi wakomalie manyimbo wanayopenda kusikia wao na sio waliowalipa kuwaburudisha?
Swali langu la kizushi kwa wadau ni je kifanyike nini ili kubadili fikra za maudhi za ma-DJ wetu wa bongo kwenye minuso???
YAANI MA-DJ WA BONGO MNABOA MPAKA BASI!!
Mdau Festo
Mlimani jirani na UDSM

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 16 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 05, 2009

    PIGA VIGELEGELE WEWE MWENYEWE AU KODISHA KUNDI LA ASILI LA KABIRA YENU NA IKISHINDIKANA ONGEA NA KIZAZI KIPYA WAJE WATUMBUIZE
    NA SI LAZIMA ZIPIGWE HOME MUSIC SIUNAJUA BINADAM TUKO TOFAUTI

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 05, 2009

    DJ anapaswa kupiga nyimbo anazaoambiwa na wenye harusi. Kwani si analipwa, basi apige anachoambiwa kama inashindikana basi, maDJ wako wengi mno...
    Itasaidia mkikutana na maharusi kabla ya shughuli ili siku yenyewe kusiwe na mikwaruzano

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 05, 2009

    Ulietoa kero hii umenigusa haswa! Ma DJ wengine ni shida tupu, tulikuwa nashuhuri tulimwelekeza DJ tunataka nyimbo ziwe mchanganyiko ila sababu maharusi wanatoka katika makabila tofauti ni vizuri zipigwe nyimbo za makabila hayo mawili na mchanganyiko toka bakabila mengine ya tz kwani ndo walojaa ukumbini, na ndo walofanikisha mnuso chakushangaza ukawa ugomvi pale alipokumbushwa vipi mbona ndombolo zimezidi kuliko maepatano yetu? ukawa ugomvi eti anawaita wanakamati washamba.

    Wakishabugia bia za bure wanasahau kabisa kuwa wao wapo ofisini.

    Kamati ya music iwe jirani na ma DJ na kuhakikisha kabla ya shuhuri DJ ahudhurie kikao na apewe majukumu yake maana wengine wamezidi hata kuropoka ropoka hata yasiyo faa na kuwaudhi wanafamilia hata maharusi.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 05, 2009

    hata hivyo unaonyesha uko biased. unatakiwa kuwa impartial.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 05, 2009

    Sio swali la kizushi. kwa hakika ni suala pana la kitamaduni katika maana pana (yaani si tu ngoma za asili) ambalo linajidhihirisha katika kila tunachokifanya wabongo. Tanajidumaza, tumezika ubunifu, tunabakia kuiga kama kwamba hatuna akili nzuri, na kuabudu kila kitokacho au kifanywacho 'ulaya'. ukiwauliza watakwambia mambo ya utandawazi/usasa. ukweli ni utandumazi.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 05, 2009

    Makosa mnayo wenyewe wenye sherehe, hao ma dj wako kazini kwa nini mnawapa pombe.Navyojua mimi mtu haruhusiwi kunywa pombe kazini pili kwenye makubaliano imeandikwa lazima ma dj wapewe pombe, kama sherehe ya kwangu ni lazima wafuate yale tunayotaka wanasherehe hivyo sioni sababu ya kubishana nao siku nyingine mnalipa nusu na akimaliza mnammalizia nusu kama mmeridhika na huduma yake.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 05, 2009

    Mnapofanya makubaliano mpe mwongozo wa maudhui unayoyataka katika sherehe yako. Kama unataka nyimbo za makabila ya maharusi zitawale mwambie. Kama hutaki kusikia ndombolo wala kochokocho mwambie. Kama unataka kusikia red light special na nyimbo kama hizo mwambie. Kama hawezi tafuta mwingine.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 05, 2009

    kweli waboa sana hao wandugu,unaweza ukawaambia kabla shughuli haijaanza watakuelewa au uwapatie cd ambazo unajua waalikwa na wahusika watafurahi uwaonyeshe na nyimbo etc ama unaweza kupiga musiki mwenyewe kama unaweza kupata sound system nzuri huwa inanoga sana.
    mdau

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 05, 2009

    Tujifunze kuwa na contract. na kwenye contract hiyo iandikwe ni nyimbo gani unazihitaji kwenye sherehe yako. Halfu iwe mtu anapewa 50% down payment the rest after the job...sasa asipofanya ulivyopenda basi hapati za mwisho. Malawyer wapo bongo kibao? Ndio kazi zao hizo.

    Na pia labda kuna uhaba wa DJs kama ni wengi basi iwe ni mtu anakurefer kwa kazi nzuri uliyoifanya. No good job no reference

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 06, 2009

    Nafikiri mpaka sasa vijana wetu wa bongo flava hawajaanza kupiga nyimbo za wakati wa kula kwa hiyo naona tuendelee kumsikiliza Kenny roggers au akina embe dodo

    ReplyDelete
  11. AnonymousJuly 06, 2009

    Kaka michuzi kama utaweza nitolee hii comment yangu mbele kabisa kwani nahisi ni suuhisho kwa watu walioathirika na kupigiwa nyimbo wasizozitaka katika sherehe zao hasa harusi. Mimi pia nilikuwa nakerwa sana na tabia hii ya ma dj na Mc, na ndipo nilipoamua kuhakikisha kwamba kwenye harusi yangu haipigwi nyimbo yoyote nisiyoitaka. Nilifanya hivi, kwanza nilikusanya nyimbo zooote amazo nazipenda na nimekuwa nikiziota zipigwe siku ya harusi yangu na kuziweka kwenye cd zipatazo 3, then nikachukua kalamu na karatasi na ku note down wimbo upi upigwe sangapi na kwa tukio lipi( huku nikiwa nimezipa namba nyimbo zote) na wiki 2 kabla ya harusi yangu nilikaa na mc na dj nikawaambia mkakati wangu wa kuhakikisha ni nyimbo zile nilizochagua tu ndio zitapigwa huku nukiwakabidhi copy ya cds, na baada ya hapo nilikuwa nimeshaandaa mkataba kati yangu na wao ukiainisha kila kitu ninachotaka kifanywe na wao siku ya harusi yangu, wakausoma na nikawaambia kama wanaukubali wasaini na wakafanya hivyo, kwa makubaliano kwamba kinyume cha makubaliano yetu kutapelekea kutokulipwa balance ya payment, ambapo kati ya laki tano nililipa laki 3 na nusu na kubaki na laki na nusu! unajua nini kilitokea....? mi miziki yangu tu ndio ilipigwa usiku ule. Hili ndio fumbuzi pekeee. na si kukaa kimya then usubiri dj na mc wajue whats ur choice, hapana watapiga walizonazo tu, na si kumwambia siku ya harusi hapo utamchanganya kwani anahitaji muda wa maandalizi na kujipanga.

    ReplyDelete
  12. AnonymousJuly 06, 2009

    eeeh eeeeeh wewe vipi tena sasa we mtoa maoni unataka ipigwe nyimbo gani ambayo unajuwa chakula kitatelemka eeeh bongo fleva..we acha hizo wakina ken roger wacha watuumbizeee ... sasa na kwenye kudansi unataka ipigwe nini msondo ngoma au sikinde eeeeh wewe acha tule mayenu sawasawa bwana maana nikisema fm academia ndio huko huko.....wewe ukitaka kodisha mdumange au mdundiko waje wacheze kwenye harusi yako lala mbele hukoooooooo....

    ReplyDelete
  13. AnonymousJuly 06, 2009

    nawewe unaliye andika kubugia bia za bure sasa unataka wakiwa wanapiga mziki wasile na kunywa ata kituuu nyie kama wanawaboa kwani mlikubaliana kwanza au unatoa comenti tu kufikiria.mimi nafikiri wewe utakuwa umetoka mara au musoma au songea vijini nenda kawalete waje wapige marimba kwenye harusi zenu uone kelele zake ....maaana itakuwa sio harusi bali fujoo muache kenny roger, mayenu yadadishe watu.....kafieni mbele

    ReplyDelete
  14. AnonymousJuly 06, 2009

    mimi nakubali maneno ya mdau hapo juu wa 12:48 maneno yako sahihii. ila mara nyingine wenye shughuli ndio wanaochemkaga unakumta mtu anamwambia Dj nipigie nyimbo flani akiabiwa sina anataka nyingine akaiambiwa sina anaaanza ohh huyu Dj gani, wao wanafikiri Dj anakuwa na nyimbo za ulimwengu zote yaani hata mtu akitaka nyimbo wqakati bibi yake na babu yao walipoowanan atakauwa nao.....jamani sio hivyo ongeeni na ma Dj kabla ya sherehe sio unakurupuka tu ktk sherehe yako unataka nyimbo flani, halafu na ww unaosema km Dj hawapigi B/f ktk sherehe sio kweli Dj siku zote huwa anamsikiliza mwenye sherehe labda kama ww ulialikwa ktk sherehe halafu ukataka kujipaupana wa kumuamrisha Dj wakati hujui Dj aliambiwa apige nyimbo za aina gani na wenye sherehe.

    ReplyDelete
  15. AnonymousJuly 06, 2009

    wewe bwamdogo unataka kutwambia kuwa wewe huwa unafika katika kila harusi hapa dar? ulijuaje kama harusi zote ma dj wanapiga nyimbo hizo hizo?

    ReplyDelete
  16. AnonymousJuly 06, 2009

    Kero hii...ya madj sio wanaopiga harusini tu mpaka baadhi ya maDJ wa kwenye vituo vyetu vya radio, wanatabia za ushamba ushamba za kubabaikia miziki ya kigeni hisio kuwa na maana yoyote hapa nyumbani.
    Pia inakera zaidi mpaka kwa watu tunao wategemea ambao wanamiliki Blogs,baadhi yao wamekuwa nao limbukeni na wanaboa kwa kubabaikia
    habari za wanamziki wageni,mfano blog ya Afrika Bambataa inatia kichefuchefu kwa kuona aslimia 99% ya habari za pale ni za wanamziki wa kikongo.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...