Bango la Hospitali ya Kolandoto iliyopo Shinyanga
Misaada ya mashine ya kusaidia huduma ya upasuaji na moja ya viti vya wagonjwa vikikabidhiwa rasmi. Toka shoto ni Dk. Emmanuel Mwandu, Mh Janet Kahama, Liliane Mackeja Sykes wa AF Canada aliyeleta misaada hiyo, Dk.Katani, Bishop John Nkola, na Mh. Dk. Mlingwa Mbunge wa Shinyanga.

Lilliane Mackeja Sykes akiwa na Dk Mwandu mbele ya mashine ya kusaidia upasuaji
Bishop John Mkola akitoa hati ya Shukrani kwa kinamama wa Canada waliotoa misaada hiyo.

Hospitali ya Kolandoto ambayo ilianzishwa mwaka 1913 na Wamishenari wa African Inland church Dr. Nina Maynard na mumewe Mchungaji Wiliam Maynard jana ilipatiwa msaada kutoka kwa kikundi cha umoja wa waafrika waishio Canada - African Fellowship Group.

Msaada huo kwa hospital hiyo kongwe mkoani Shinyanga, ulihusu vifaa mbalimbali vyenye thamani isiyopungua Shilingi Million Mia Mbili.

Vifaa hivyo ni pamoja na mashine mpya ya dawa ya usingizi yenye thamani ya Tshs 150 Milioni, vitanda 20 mahususi kwa hospitali viti 28 vya wagonjwa walemavu hundi ya US $ 6000 sawa na Tshs milioni sita, kusaidia ukarabati wa chumba cha upasuaji, zaidi ya vifaa 325 vya aina mbalimbali vya kusaidia shughuli za upasuaji na mashine nyingine.

Bi Lilian Mackeja Sykes ambaye ni Mwenyekiti wa kikundi hicho akiwa ameambatana na Dr. Sam Kwofie mweka hazina wa kikundi ni miongoni mwa wageni rasmi waliohudhuria tukio hilo.

Sherehe hiyo pia ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo wabunge Mh. Dr. Charles Mlingwa mbunge wa Shinyanga mjini, Mh. Tungu Mpendazoe wa Kishapu, Mh. Joyce Machimu viti maalum Shinyanga, Mh. Janeth Kahama viti maalum Dar es salaam; Askofu Nkola wa Shinyanga, Dr. Emmanuel Mwandu, madaktari, wauguzi na wakazi wa maeneo jirani.

Bibi Lilian Mackeja Sykes ambaye alizaliwa Nkolandoto Hospital alistushwa na mazingira duni baada ya kufika hapo mwezi March 2008. akitembezwa na Dr. Emmanuel Mwandu alipata fursa ya kujua mahitaji na mapungufu hospitalini hapo.

Pamoja na kutekeleza dhamira ya msaada huo Bi. Lilian Mackeja Sykes, ana ukaribu mkubwa na Nkolandoto Hospitali. Nyanya mzaa mama yake, marehemu Anna Schubert Mackeja, alilelewa na waanzilishi wa hospitali hiyo na watoto wa Anna Schubert: mary Mackeja (marehemu) ambaye alikuwa katibu mkuu wa kwanza Tanzania Red Cross, Martha Jane Mtebe (mama Mzazi wa Lilian) Janeth Kahama (MB) na marehemu Charles Mackeja walizaliwa Kolandoto hospitali

Mnamo December 2008 kikundi hiki ilifanyika harambee kubwa huko Ottawa Canada na kufanikisha azma yake. Walioshiriki humo Mh. Peter Kallaghe balozi wa Tanzania, Balozi wa Afrika Kusini na mtoa misaada mashuhuri Bw. David Smith ambae alitoa sehemu kubwa ya vifaa vya hospitali. Sehemu ya fedha iliyokusanywa imetumika kusafirisha vifaa hivyo.

Kikundi cha African Fellowship Group chenye makao yake Ottawa Canada chaweza kupokea mawasiliano kwa

Email:
African_fellowshipott@yahoogroups.com





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 24, 2009

    ni msaada mzuri sana, hongerene kwa kutoa msaada huo. sasa wenzetu muvitunze vizuri na musije mkaanza kuvipiga bei maanake watanzania kwa tamaa ya pesa, hamjambo.wenzenu huko canada walipiga harembee kupata pesa za kununua hivyo vitu so please make sure vinatumika kwa wagojwa!

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 24, 2009

    This is a great job...Hongera sana dada, ni mfano wa kuigwa.

    J.
    Toronto Canada

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 24, 2009

    Hi,
    nianzaje? dada ubarikiwe sana.
    kunamedhari yasema mcheza kwako hutunzwa tukupe zawadi gani?
    tutazidi kukuombea ubarikiwe zaidi
    ngwana wa ngwise kulaga uhangame udakunelwe
    by the way hiyo ndiyo kike

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 24, 2009

    Afadhali tuone wenzetu wabeba box wa ughaibuni wanakumbuka na kusaidia makwao.sio THEY BORN IN TANZANIA,THEY SOMESHWA IN TANZANIA,THEY THEN ISHI IN UGHAIBUNI BUT THEY DONT DO NOTHING TO THEIR COUNTRY.Wazazi wao wanatibiwa maili 30 from their villages.Hongereni nyie mlioonyesha mfano..wenzetu waige

    ReplyDelete
  5. jamani Mungu awabariki sana kwa msaada wenu. hospitali hii iliokoa maisha yangu zamani zile nilivyokuwa mdogo japo walifanya mistake kidogo namshukuru Mungu naishi hadi leo.
    nimekumbuka mbali sana japo mengi niliadithiwa na mama yangu mpendwa kwani baba alinikimbiza kolandoto hospital dk za majeruhi.
    Mungu ibariki tz Mungu ibariki Afrika na dunia yote.

    mdau, UK

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 25, 2009

    keep it up wadau wa canada ,naona watau wa uk wanatia kinyaa kila wakionekana kwenye blog kutangaza mikutano ya ccm.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 25, 2009

    Hongera sana dada lilian jamani watanzania tuige huu mfano;Happy to see Dr Mwandu for sure he is a Good Dr by professional

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 25, 2009

    JIS ISH NAISH....

    ReplyDelete
  9. Furahisha MoyoFebruary 14, 2015

    Mimi ni rafiki ya Dr Mwandu katika enzo la 1975 in Shinyanga. Tulikuwa na cheza Basketball na Dr MWandu siku zile alikuwa ana fanya kazi la Nurse.
    Mimi niko Canada since 1980 na nipe pata picha nyingi sana. Dr Mwandu please contact me I am Alnoor Furahisha Moyo I hope you remember me.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...