askari polisi wa dar, hasa wanaolinda sehemu nyeti kama vile mabenki, wapo makini sana na kazi yao. hapa huyu anamhoji dereva wa hili gari kwa nini kapita njia isiyo sahihi. yaani jamaa alikuwa anatokea sehemu za luther house barabara ya sokoine na wka vile ni jumapili magari si mengi sana akala kona kulia kuingia azikiwe... toba! ghafla askari huyu ambaye alikuwa amebana mahali akachomoza na kumpiga mkono. hakuna zawadi ya kukisia kilichojiri baadae kidooogo...

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. Michuzi hao jamaa ndiyo mchezo wao. Wapo makini kuhesabu magari yote na ndiyo maana mabank yanaibiwa. Mi iliisha nitokea na jamaa yangu, hapo wanachowinda ni hela yaani sisi walitung'ang'ania tuwape Shs 50,000. Tukamwmbia tupeleke kituoni hatulipi hata shs moja akashuka mpa buku tano tukamwambia yeye ni askari katukamata atupeleke kituoni ili tukalipie hela mahakamani, ikabidi aanze kubembeleza sasa tumpe hata hela ya maji, hali ngumu sana. Tukamwambia kwanza pale hakuna alama ya barabarani inayoonesha usipite, hivyo kwa mtu ambaye ni mgeni wa mjini itakuwa ngumu.

    Jamaa akashindwa kutupeleka kituoni kwa kuhofia kuacha lindo. Ukweli inabidi wakuu wa hawa jamaa wawaeleze wazi kuwa ipo siku majambazi yatatumia mtego huu ili kuvamia hapo NBC, maana akiisha kukamata mawazo yote yanahamia kwa dreva nakupata rushwa badala ya kufikiria lindo.

    Nafikiri madereva wengi hawajui haki zao. Kwanza kabla hujababaishwa jiulize je alama za barabarani zipo?, na je zipo visible?, kama haya majibu ni ndiyo mpe rushwa kama na wewe ni mpenda rushwa ila kama wewe ni mzalendo kataa mwambie akupeleke kituoni ukalipe fine kwa maendeleo ya nchi.
    Kama jibu ni hapana kataa katakata mwambie akupeleke mahakamani na ukaeleze hali halisi, huenda hii itafanya city fathers waboreshe miundo mbinu na kuweka alama zilizo clear barabarani.
    Kila ajali ikitokea tunalaumu madereva lakini wanasiasa wanasahau kuwa majuku ya kuweka miundo mbinu iliyo bora ni ya kwao kwani wao ni watunga sera na watekelezaji vilevile

    ReplyDelete
  2. Asante kwa hili Kaka.
    Mimi nilikuwa mhanga wa sehemu hiyo. Na nilikamatwa hapohapo na kwa kosa hilo hilo. Ndio ilikuwa mara ya kwanza kuendesha eneo hilo baada ya miaka kadhaa ya nje ya mji. Nilipokamatwa niliulizwa kama nimeona alama inayoashiria kutokata kona kuelekea kulia nikasema hapana. Wakaingia askari wawili na bunduki zao kisha wakanizungusha mpaka pale kwenye kibao na "bahati mbaya" kilikuwa kimefunikwa. Lakini wakahimiza kuwa nilitakiwa kujua kuwa siruhusiwi kukata kona. Nikasema sikuona bango na nina makosa kwa hiyo sheria ifuate mkondo wake. Wakaniambia nielekee mpaka polisi na tulipofika kwenye maegesho ya polisi (mbele ya stesheni ya reli) wakanieleza kuwa wakiniingiza ndani naweza kuonekana na makosa mengine mengi na itanigharimu pesa nyingi, kisha wakaniuliza "TUKIKUSAMEHE ITAKUWAJE?" nami kwa moyo mweupe na mkunjufu nikawaambia kuwa NTASHUKURU NA NAAHIDI SITORUDIA TENA. Hawakuonekana kufurahia jibu, wakaniuliza registration na mengie mengi na nilipompigia simu mwenye gari wakahisi "wako mtegoni" wakaniambia niwarejeshe nilipowatoa na mpaka nawashusha walikuwa wakiuliza swali hilohilo kuwa WAKINISAMEHE ITAKUWAJE.
    Niliishia kuwashusha lakini niliwahakikishia kuwa sitorudia tena. Niliamini ndivyo walivyotakiwa kufanya (kuonya na kuelekeza hasa kwa anayeonekana kushirikiana nao na kukiri kosa) lakini nilishangazwa na trip ya kuelekea polisi kisha kunieleza kuhusu gharama ninazoweza kukumbana nazo nikiingizwa ndani na kisha mwisho wa swali kuwa TUKIKUSAMEHE ITAKUWAJE???
    Lakini nadhani jamaa wana full-time job ya kulinda benki na part time ya "kupiga mabao"
    Niliambiwa wanapeana zamu / wana foleni ya nani anafuata kukamata gari. Nadhani zamu ya hawa "haikuzaa matunda".
    Blessings

    ReplyDelete
  3. KAACHA LINDO KUKIMBILIA GARI APATE VIJIPESA VYA UGALI NA MAHARAGE NYUMBANI, NDO MAANA WANAULIWA MALINDONI, HAJUWI MAJAMBAZI WANAWEZA KUTUMIA MTINDO HUO ILI KUWAZUBAISHA NA WAWAVAMIA KISAWASAWA, RUSHWA NI UGONJWA MBAYA SANA TIBA YAKE NI NGUMU KAMA UKIMWI HIVI, UNAJUWA HII YOTE IMEPANDWA VICHWANI MWAO NA WAKUBWA ZAO, HIVI WANAPOONA WAKUBWA ZAO WANA MAGARI SITA NYUMBANI NYUMBA KUMI ZIKIWEMO A GOROFA, MBEZI BEACH, BOKO BEACH NA MISHAHARA YA WAKUBWA ZAO WANAIJUWA UNATARAJIWA WAO WATAFANYA NINI, SOMETIMES WANATUMWA NA WAKUBWA KUKUSANYA PESA, WASIPOLETA HAWAPANGWI KWENYE MALINDO HAYO. MIMI MWENYEWE NILISHAPATA AJALI KUNIANDIKIA RIPOTI ILI NIKADAI INSURANCE YANGU WALITAKA TSHS 500,000.00 NILIKATAA NA NILITUMIA WANASHERIA KWA PESA NDOGO TU NA KULIPWA MAPESA NA BIMA YANGU, NI OVYO SANA HAO JAMAA

    ReplyDelete
  4. Hiyo sehemu inajulikana sana wengi wamenasa hapo na wametoa kidogo dogo hao polisi wa hapo ndio kazi yao kubwa kula kidogo dogo cha wanaokosea njia hiyo mimi mwenyewe niliwahi kukamatwa hapo mwaka 1998 na polisi akanidai kitu kidogo nikamtosa akanitishia tufike kituo cha polisi akaingia ndani ya gari na kumuacha mwenzake kwenye lindo basi tulipokuwa njiani nikamtisha kuwa babangu ni mtu mkubwa sana serikalini na kama ataiweka gari kituoni basi atajuwa jinsi ya kujielezea kwa wakubwa wake wa kazi aliposikia hivyo...akajifanya urafiki na mimi na akasema hebu nirudishe pale bank kwenye lindo langu kijana usije kunipotezea kazi yangu nikamrudisha na kuanza kula kona kiulaini mtoto wa kariakoo mjini shule....mdau uholanzi kama kawaida nawakilisha

    ReplyDelete
  5. afande aliacha lindo na kuingia ndani ya gali wakaenda kumalizana juu kwa juu then afande akarudi katika mtego wake kama kawaida .

    ReplyDelete
  6. hawa jamaa msiwalaumu sana tatizo mishahara midogo,wanalipwa kwenye 150-200 elfu.huwez kukiz mahitaji yako na wao ndo dili zao tutoane jamani.maana hata vigogo wana dili zao.
    usibane kaka ndo ukweli halisi.

    ReplyDelete
  7. IMEWAHI KUNITOKEA MIE NA MDOGO WANGU.MDOGO WANGU ALIKUA AKIENDESHA,MIE NILIKAA NYUMA,ULIKU A USIKU KAMA SAA TANO HIVI.TULIKUA WATATU KWENYE GARI.WAKATUSIMAMISHA,MMOJA AKAINGIA KWENYE GARI NA BUNDUKI KUBWA,NILISHANGAA SANA,SIJUI KAMA KUNA SHERIA POLISI KUINGIA KWENYE GARI YA MTU BINAFSI TENA USIKU,NILISHANGAA SANA.WAKAWA WANABISHANA NA DEREVA(MODOGO WANGU),HUKU POLISI AKIMUELEKEZA ,KATA HUKU,ALEKEA KULIA.BAADAE NIKAMUULIZA POLISI,UNATUPELEKA WAPI?AKADAI NIKAMUONYEHSE DEREVA NI WAPI ALIPOKOSEA.

    NIKAMWAMBIA,HATUNA HAJA YA KUONA NI WAPI TULIPOKOSEA,TUAMBIE TARATIBU NI ZIPI BAADA YA KUMKAMATA MTU,NIKAONA ANAANZA KUTETEMEKA PALE.AKAOMBA ASHUKE ILI WAONGEA NA DEREVA.BAADAE DEREVA ALIVYORUDI KWENYE AKATUAMBIA JAMAA ALIKUA ANAOMBA HELA YA SODA BUKU 2,BAHATI MBAYA NIKAMWAMBIA SINA AJE AONGEE NA WEWE,POLISI AKASEMA BASI YAISHE.

    NILICHOKIONA,NI HATARI HATA KWA USALAMA WAO,MAANA ANAINGIA KWENYE GARI USIKU HUKU AKIONA KUNA WATU WATATU.MAJAMBAZI WANAWEZA TUMIA SYSTEM KAMA HIYO,POLISI AKAINGIA KWENYE GARI,BAADAE WAKAMNYANG'ANYA NA HIYO BINDUKI ILI IKATUMIKE KWENYE UHALIFU.SASA HAPA SIJUI TATIZO NINI?TANZANIA BADO TUNA SAFARI NDEFU.

    ReplyDelete
  8. Michu hawa jamaa ndio zao yaani unafikiri pale wanalinda benki! No wao zao ni kusubiri nani afanye kosa wachukue chao ndio mchezo wao huo, kilichojiri baada ya hapo ni kapozwa tena unaweza kuta kapewa elfu mbili tu.

    ReplyDelete
  9. ..Nimesoma maoni yenu wote.Kwanza ni hatari kwa maisha yake asakri alivyosimama na silaha ikiwa ni mtu mbaya askari hana muda hapo wa kuweza kupiga risasi ghafla akionyeshwa pistol hapo.atatekwa na bunduki inakwenda.Wewe angalia tu hiyo picha vizuri mikono kaweka nyuma sasa wakati gani atajiandaa kuweka kidole kwa trigger? huo muda anakuwa hana na jmabazi atachukua bunduki.

    ReplyDelete
  10. Hao askali washenzi san, wanaacha kazi yao ya kulinda benki wanajifanya traffic, mie ilishawahi nitokea siku za nyuma lakini waliambulia vumbi, nilingia hio barabara bila kujua mara nikaona askari wawili wanibuka kwa mbele na kupiga mkono, hapohapo nikastuka nimechemka nikasimama na kuweka reverse fasta, wakabaki wamepigwa butwaa kudadadeki, mwanaume nikaishia. Wengine huwa wanavizia maeneo ya taa za agakhani kam unaenda chicken tikka, ile njia nayo ni one way ukichemka tu hasa mida ya usiku au weekend utakutana nao, be aware.

    ReplyDelete
  11. Ni kweli askari wanaopangiwa kulinda Benki wameligeuza eneo hili kuwa sehemu ya kupata rushwa kwa kuwaonea wageni wasiogahamu kwa hakuna 'kupinda kulia'. Mimi pia nilishishaingia mtegoni lakini nilipowa piga mkwara kwamba wao kazi yao ni kulinda benki na sio barabara hata hivyo walitakiwa kunielimisha kwa vile sikujua badala ya kuniomba pesa na kunihukumu, wakaona nawapotezea muda wakaniachia. kwa kweli wanatia aibu sana. Imekuwa tabia sasa askari wa kawaida kuingilia masuala ya usalama barabarani wakati jukumu hilo wamepewa 'traffik policeme'

    ReplyDelete
  12. Majambazi walikuwa hawajashutukia hii trick, lakini sehemu zote zamalindo ya benki, Askari hufanya kazi hambazo hawajatumwa ni hatari sana, Mzee kova tumia gari binafsi siku moja ucheck vijana wako wanvyo acha malindo yao na kukimbilia dealz za kijinga, malindo ambayo yako affected ni NBC - Samora, KCB & CRB (from steers towards askari mourment), Posta banks (towards Bilcanas)

    ReplyDelete
  13. Hata wanaokamatwa wenyewe (madereva) mara nyingine huwa wanaanzisha hizo rushwa si askari peke yao. Utakuta mtu anafanya kosa, akikamatwa anashika hela kabisa mkononi kabla hata hajaongea na huyo askari.Pamoja na askari wengine kuonyesha dalili ya kutaka rushwa kuna baadhi ukikiri kosa na kuwa limetendeka bila kukusudia wanatoa onyo na wanasamehe.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...