Kivuko cha MV Magogoni kilichoundwa hapa Dar kwa gharama ya Sh 8.5 bilioni na chenye uwezo wa kubeba tani 500 wakiwemo abiria 2,000 na magari 60 kikikata maji kutoka Kigamboni. Usafiri mitaa hiyo umekuwa si wa shida tena toka JK akizindue mwezi Juni mwaka huu.
abiria hawabanani tena kama mishikaki

nafasi ya ndinga bwelele
sehemu ya abiria kabla hawajaingia
abiria na magari wakikwea MV Magogoni
MV Magogoni kikielekea kigamboni
MV Alina nacho kinapiga mzigo kama kawa









Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. Duh! ama kweli nchi hii inaliwa na wenye meno. Kivuko hicho kimenunuliwa kwa $9million?, huu sasa ni utani haki ya mungu, nimegoogle kivuko kama hicho kina range $0.5million to $1 million.

    Ama kweli nchi yenu sasa inabidi tuwe transparent kama ni kuliwa imeliwa vya kutosha hebu sasa tuangalie na maendeleo jamani. Ndiyo maana watu wanatoana macho kwenye kugombea uongozi wa nchi hata kama hawana sifa za kuongoza Duh!

    ReplyDelete
  2. hivi wanashindwa nini kujenga daraja pale,yaani tumejaza vilaza wasio na vision yeyote ile,daraja litasaidia sana kukata foleni na kuongeza shughuli za kiuchumi Dar...yaani inasikitisha sana kuendelea kufanya mambo kwa kulipua na kuishioa kununua vivuko tena kwa bei mbaya m,ara 10 bila sababu,watanzania tuamke!

    ReplyDelete
  3. Pamoja na kivuko hicho kutumia pesa kibao lakini pia wahusika kwa usalama wa watu wangeweka sheria inayotenganisha abiria na magari. Nimepanda vivuko nchi za nje sijaona hata kimoja abiria wakichanganyika na magari hata madereva inabidi wote katika magari wakati kivuko kikienda. Hii inasaidi endapo kutatokea tatizo wakati wa safari kama mawimbi na magari kuyumba au kusogea kidogo yasiumize watu waliopo kati ya hayo magari. Tunaomba wahusika walifanyie kazi wakilisha mkuu wa wilaya panapohusika.

    ReplyDelete
  4. HAYA NDIYO MAISHA BORA? MICHUZI UMESAFIRI NCHI NYINGI NA BONGO NINAKUFAHAMU UNAMAISHA DECENT SASA WAELIMISHE VIJANA SIYO KWELI KILA MTU HUKU ANABEBA BOX NA HATA WABEBA BOX HUKU WANA MAISHA DECENT KAMA WEWE TUMECHOKA NA HUU MJADALA. ANGALIA HAYA MATESO YA SEHEMU NDOGO TU KWENDA KIGAMBONI? UMEONA MADALAJA BOSTON NEW YORK CALIFORNIA? UMEONA BALABALA? SASA HUONI KAMA UKIISHI TANZANIA UNAKADILIWA KUFA KABLA YA MIAKA 5O HII NI AVERAGE ULAYA NI 72 KWA NINI? KAMA MAISHA NI TAABU BASI WANGEISHI MIAKA AVERAGE 30 KAMA MALAWI ZIMBABWE SOMALIA CONGO N.K! KWA HIYO MTU AKICHOKA MAISHA YA ULAYA ATARUDI NYUMBANI LAKINI MSIWABUGUZI WALIOCHAGUA KUISHI HUKO!

    ReplyDelete
  5. opps matinde! sio balabala ni barabara
    mdau kifimboplay

    ReplyDelete
  6. Yaani nyie wachangiaji kabla yangu ninawashangaa. Hata kusifia? Mie binafsi nampongeza sana Rais JK kwa kuendelea kutimiza ahadi zake. Pamoja na mazuri hayo bado wakosoaji hawakosekani. Lakini kwa sisi wakazi wa kigamboni ndugu zangu hayo ni mafanikio. Mimi mwakani kura zangu za diwani, mbunge na Rais napelekea CCM!!!Shura ya maimamu na kina Ponda mpo???!!!

    ReplyDelete
  7. heeee feriiii...kweli nimekumbuka nyumbani jamani.nashuru sana aliyetuma picha hizi.zinanikumbusha mbali sana

    ReplyDelete
  8. Hayo ndo mambo kwani nikikumbuka enzi za DEZO hilo lilikuwa ndo kivuko cha mwaka 88 mpaka 91 kwani pantoni liliaribika hilo likawa lina vusha hapo feryy

    ReplyDelete
  9. Hapo mzeee shkran sana kwani wengine hatuja baatika kuliona maana inanikumbusha enzi hizo kipindi cha mkapa!!!!!!!hahaahaaa pantoni likiaribika watoto hawaendi shule

    ReplyDelete
  10. daraja daraja daraja

    vipiii??????????????

    fisadizzz

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...