Kaka michuzi habari,
Leo najaribu tena kutuma ka-post kangu. Sijui na kenyewe katatupwa kapuni!!! Naamini haka UTAKAWEKA sababu siamini kama kaka Michuzi utakuwa mbaguzi kiasi hicho cha kutupa kila posti yangu!!!!
Concern yangu leo ni hawa magraduate hasa wa engineering ambao UDSM yetu huwa inazalisha, sio UDSM tu bali hata vyuo vya nje ambapo watanzania huenda kusomea mfano mechanical engineering, aerospace engineering na aina nyingine nyingi za uhandisi.
Concern yangu ni pale ambapo hatuoni kabisa watanzania wenye utaalam huu wakiweza kuvumbua vyombo mbalimbali kwa kutumia ujuzi waupatao huku vyuo vya juu. Utakuta mtu ana mpaka PhD katika say aerospace engineering and the like, leave alone masters in the same ambazo tunazishuhudia zimejaa.
Swali langu ni je, ni ukosefu wa vitendea kazi, ukosefu wa ujuzi takikana pamoja na kwamba tayari wana ma-degree, ni uvivu, au ni hali ya maisha kuwa ngumu na hivyo wakijikuta hawana muda wa kupoteza kushughulisha utundu wao na elimu zao na ujuzi wao katika kubuni vitu mbalimbali?? Tatizo ni nini hasa??
Hebu tuangalie huyu Kijana wa Kichina mwenye elimu ya shule ya MSINGI TU yeye anadai ametumia kale- kafizikia kake ka primary school akachanganya na mautunduutundu fulani akaibuka na HELICOPTER tena yenye kuweza kupaa 800 metres!!!
Kwa hesabu za harakaharaka huyu kijana hawatamuacha, watamfadhili nje akaendeleze ujuzi ili wamtumie, tena wakimchukua wazungu hawatamrudisha, ndio utakuta kaajiliwa AIRBUS pale France kama mtaalam na kulipwa handsomely!!
Je ma-engineer wetu wako wapi??? hivi kwa kutumia elimu na ujuzi wao hawawezi kubuni vitu kama hivi na hatimaye kujikuta wakipata madili makubwa na kututoa kimasomaso watanzania??
HUYU KIJANA YEYE KATUMIA VYUMA, MBAO NK!!! na sasa ameshakula lulu. Hebu tulijadili hili wadau
ITAKUWA VIZURI TUKIPATA MICHANGO PIA KUTOKA KWA WATANZANIA WENYE MA-DEGREE YA ENGINEERING WATUELEZE TATIZO HASA LINALOWASIBU NI LIPI ILI BASI HATA SERIKALI IWEZE KUONA JINSI YA KUWASAIDIA KUTUMIA ELIMU NA VIPAJI VYAO make hii blogu inasomwa na wengi mawazo yenu yatafika tu pahala husika.
Nawawekea habari kamili ya kijana huyu mdogo 20 yrs of age!!!!
Taarifa zake waweza zipata hapa
AU hapa
Angalia Video ya Kijana huyo akijivinjari kwa
maonyesho na Helicopter hiyo hapa
Inavutia ukiitazama yote inauwezo wa kwenda mbali.
Ahsanteni,
Mdau wa Michuzi blog,
Edinburgh,UK.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 35 mpaka sasa

  1. Hoja hii sio kwa mainjinia tu, umeona wapi ktk vyuo duniani vitabu au machapisho mengine ya maprofesa wa Tanzania yakitumiwa? Hii ni kwa sababu wanaumganisha machapisho ya watu wengine na kuandika ya kwao hawana ugunduzi mpya. Utakuta vitabu vya wahindi na badhi ya nchi za Afrika kama Nigeria, Ghana n.k lakini sijawahi kuona reference ya kitabu cha Prof. wa TZ, je wanastahili kuitwa maprofesa kama wenzao??

    ReplyDelete
  2. Hili tatizo umeuliza kwa wahandisi tu lkn hii ni changamoto kwa kila taaluma. Mfumo wetu wa elimu ni wa ku-Copy & ku-paste, pili wabongo mtu akiwa mbunifu ni hatia.

    shuleni mtoto akionesha uwezo wa soka kwa mfano wazazi, waalimu na relatives watamdiscourage na kumtaka aconcetrate kwenye vitabu.

    Special schools wanapelekwa wale waliooneakana wamepata A's kwenye timing exams, badala ya kutafuta wale wenye ewezo wa ku-apply zile k'ledge wlizozipata kwenye vitabu.

    Nakumbuka enzi za utoto tuliweza kutengeneza mifano ya magari kwa kutumia mabati mabati na matairi tulikata hata kandambili za mama, lakini hakuna aliona kuwa hiki ni kipaji cha kulea. Leo hii tunaagiza midoli ya magari toka china wakati mtoto wa primary anaweza kufanya hiyo kazi hapa hapa bongo akipata support. Huu ni mfano mmoja tu.

    Nenda hapo SUA watu wanasoma kilimo kwa bidii kweli kweli, lakini focus zao ni kwenda kuwa bank tellers. Wimbo unaoimbwa sasa hivi ni "KILIMO KWANZA" lakini sijasikia hata mmoja akizungunza juu ya kuwatumia wataalam wa kilimo pale SUA. Tatizo ni kuwa hata viongozi hawatambui kuwa wapo, na hata walipokuwa wakitumia fedha nyingi tu kuwaandaa hawakujua wanawaandaa ili wawe gani.

    Anyway; tunapaswa kuanza kufikiri upya nini maana ya kwenda shule. Tusipoanza hapo tutabaki na fikra kuwa kwenda shule ni kwenda kujifunza kusoma, kusoma si uliweza kabla hata hujaenda shule?

    Nadhani lengo la shule ni KUJENGA UWEZO UWEZO UWEZO WA KUFIKIRI KUKABILIANA NA MAZINGIRA YAKO. Kwa mantiki hiyo msomi atapimwa si kwa vyeti bali uwezo wa kutumia taaluma yake kuyahandle mazingira yake. Ningeshauri hivi kwa mfano, badala ya kumpima mhandisi kwa exams tu, apelekwe kijiji na apewe tatizo (daraja limebomoka) awezeshe hili tatizo la kutokuwepo kwa daraja liishe.

    ReplyDelete
  3. Serikali ya Jamhuri huwa haitengi pesa za reseach. Kwa bahati mbaya hata wakitenga fungu kama hilo, utakuta watu wanajenga maghorofa badala ya hiyo tukutuku(kopta). Kwetu pia hatuna watu wenye moyo wa kujitolea kama katoto ka ki-china maana wanajua wakijitolea na mambo yakafanikiwa wenye kuja kufaidi ni mawaziri na makamishna. pole pole tutafika.

    ReplyDelete
  4. Mdau nafikiri hoja yako ni nzuri sana na changamoto kwa mainginia na serikali yetu. Tanzania tunamainginia wengi wazuri ndani na nje ya mipaka yetu lakini tunashindwa kuwatumia hata kutangaza jina letu. Mimi binafsi nafahamu mainginia kama watatu au wanne wazuri ambao wanafundisha vyuo vya nje, USA, Germany na UK. Tanzaia tuna hata watu ambao wamegundua machines mbali mbali na sifa wanapata wengine. Kuna huyu jamaa Dr. Alex Paurine yuko UK ni mtafiti wa maswala ya nishati, alinipa B.card yake hivi karibuni kwa mshangao wa visomo nikaamua kupeleleza anafanya nini kwa jamii. Ukweli sikusikia kama amefanya chochote kwa jamii ya kitanzania lakini jamaa ni noma maana kavumbua mtambo wa kupoza kwa kutumia moto (yaani bila umeme), jamaa anafanya kazi hata na EU..amevumbua paa linalopoza nyumba bila kutumia AC ktk nchi za joto (southern Europe), jamaa nasikia anafanya consultation kwa maresearcher kutoka Cambridge university na imperial college, jamaa anashirikiana na maprofessor wengine kuvumbua mitambo ya kupoza london underground, huyu mtu nasikia kwa habari za kuaminika anavumbua mtambo wa kwanza UK wa kusafisha majumba ya kizamani kwa kutumia compressed air na ice badala ya mchanga (ice blasting badala ya sand blasting, Huyu mtu amefeature hata kwenye BBC world service discovery channel na mengine mengi....kuna wengine wako USA kama Dr. Varelian Kwigizile ambaye anafundisha West Virginia University College. Jamaa ni mzuri sana hata ukifuatilia alikotokea huko nyuma. Mpaka hawa wabaguzi wakukubari ufundishe watu wao ujue hawa jamaa wanapotential na wengine wengi wa aina zao wanaweza kusaidia sana nchi yetu kujikwamua kiteknologia. Kuna umuhimu wa serikali kuweka kitengo cha kutafuta wataalam wetu wazuri na kuwarudisha nyumbani maana hawa si tishio la nafasi zao za kisiasa. Hawa ni watendaji na hazina yetu. Mh Kikwete ashauliwe na watu wake kuwatafuta watu kama hawa wakajenge nchi yetu.

    Mkuu wa wilaya ya nanii naomba Niwakilishe

    ReplyDelete
  5. mbona wapo wenginwanaogundua vitu vingi wewe labda ujaona nikwamba wapo waligundua gari linatumia maji na mafutaa.wapo waliogundua maswala ya redio na sasa inaitwa redio mabibo watu wanaipenda,wapo waliogundua umeme kwakutumia mabati na jua na betry bagamoyo,n.kvingine wenzangu watanisaidia hawa hawafiki mbali kwasababu ya hao wanao kagua na kuthibitisha wanaangalia wanaishia hapo kwasababu haiwasaidii wao kupata chochote.

    ReplyDelete
  6. Nadhani hukufanya research ya kutosha kabla ya kuandika.Umeshawishika kuandika baada ya kum-google huyo mchina.

    Kwa taarifa yako,kuna mainjinia chungu mbovu wamegundua vitu bongo,but commercialization bado ni tatizo.Si kila mtu agundue Helicopter.Kwa mazingira yetu,hata mtu akigundua mashine ya kumenya viazi vya chipsi ni sawa.Hakuna kama mainjinia duniani,they are next to God.Angalia kiti ulichokalia,gari ulilonalo na hata laptop unayotumia-ni mawazo yaliyoendelezwa na kuwa products by Engineers.


    Eng.Vinho

    ReplyDelete
  7. ASANTE SANAA KAKA MTOA MADA LEO NAONA NAMI NTATOA KIU YANGU,MIMI KILASIKU NILIKUWA NIKIJIULZA KWANINI NCHINI KWETU VIPAJI NI BONGO FLEVA NA UMISI TU,KILA SIKU UTASKIA LEO TIGO,VODACOM,ZANTEL,CELTEL NA NGO ZINGINE KUTWA KUDHAMINI HAYA MAMBO,JE KWAMTINDO HUU TUTASONGO NA WAANDISHI WAMEMEKUWA MBELE SANAA NDO MAANA WATOTO MASHULENI BAADA YA KUFIKRİA SAYANSI WOTE WANAFIKIRIA KUWA MAMISS NA WAIMBAJI BONGO.NCHI HAINA MIKAKATI NA VIJANA NA SAYASI MI NIPO HAPA TURKEY NAONA WATOTO WA HIGH SCHOOL
    WAVUMBUA MAMBO MAKUBWA SANAA WAKITUMIA MTINDO WA KUSHINDWANISHA MASHULE.NAOMBA TUBADILIKA JAMANII NCHI YETU NITAJIRI SANAA TUKITUMIA VIZURI SAYANSI TUTAFAIDIKA WENYE SASA NA BAADAE SIO KUIBIWA TU RASIMALIZETU MUNGU ALIZOTUPA.MDAU TURKEY

    ReplyDelete
  8. NASHUKURU KUWA WA KWANZA KUTUMA COMMENT: NAOMBA NIKUSAIDIE KUELEWA KUWA MTANZNIA KUWA NA MASTER AU PHD AU PROFESSOR IKIWA ALIANZIA SHULE YA MSINGI ,SEC NA ADVANCED BONGO NA WENGI WAO WENYE MASTER WAMEANZIA BACHELOR TZ KAMWE HAWAWEZI KUWA WATAALAMU WA KWELI KWA SABABU MISINGI YOTE ALIYOPITIWA HAIMUNDAI KUWA MTAALU HATA HAO UNAOWASIKIA WANAONGOZA KATIKA MATOKEO TZ HATA WAKIENDA KUSOMA HAVARD BACHELOR N.K HAITASAIDIA KITU. KAMA UNATAKA KUMUANDAA MWANAO KUWA PROFESSIONAL ANZA MAPEMA MSINGI.KAMA UNAISHI NCHI ZA NJE ZENYE HIGH TECHNOLOGY BASI UKO NDO MWAKE HALAFU AKIMALIZA SHULE MLETE BONGO BAADA YA MIAKA KADHAA TUTAKUWA NA WAATAMU WA KWELI

    ReplyDelete
  9. MDAU HOJA NZURI ILA KWA NCHI KAMA ZETU KWAKWELI LABDA SIKU NABII ISA ARUDI, MAANA WENGI TUNASOMA SIO ILI KUELEWA AMA KUJUA KITU UNACHOSOMA KWA UTAALAMU BALI NI ILI KUPATA VYETI TU VYA KUOMBEA KAZI NA UJUZI UTAUPATIA KAZINI. SABABU HATA WATEGEMEWA WENYEWE WATO HUO UJUZI HUTOA KWA KUKOMOA HUKU WAKIWAJENGEA WANAFUNZI HOFU YA UGUMU WA MASOMO. NAKUAHIDI KUWAKAMATA. TOFAUTI NA MALECTURES WA NJE. ILA KWA WANAOPATA ULIMU NCHE PIA HUJIKUTA KWENYE MAZINGIRA YA KUTUMIA NAFASI HIYO YA KUWA MASOMONI NA KUKITA ZAIDI KWENYE KUPIGA BOX MUDA WA ELIMU HUPEWA ASILIMIA NDOGO. YOTE HAYA NI UGUMU WA MAISHO NA MFUMO USIO NA MTAZAMO WA MAISHA BORA YA BAADAE.

    ReplyDelete
  10. umaskini mwananangu. kua uyaone.

    ReplyDelete
  11. Wadau mmeisoma linki alizoweka mtoa mada?? Kweli kufanya kitu ni imani na determination tu. Yani Dogo anadai wanaishi milimani na shule yake ilikuwa milimani, na yeye alikuwa amechoka kupanda milima kila siku kwenda shule, kwa hiyo alipata ndoto ya siku moja kutengeneza helikopta yake iwe inamnyanyua kumpeleka mlimani shuleni hivyo kumuepushia adha ya kupanda milima kila siku. na ukinuia kitu ukaweka nia na nguvu unakipata, dogo keshatengeneza kopta ingawa ya nondo na mbao lakini inasemekana wiki ijayo anaanza misele teh teh teh
    SWALI, JE WAHANDISI WA BONGO HAMJACHOSHWA NA HII FORENI YA MAGARI KUTUMIA MASAA 3 KIMARA POSTA KILA ASUBUHI NA JIONI?? SASA NA NYIE MNGEBUNI KITU CHA KUWAEPUSHA NA HII DHAHAMA YA FORENI TEGETA POSTA 4 HOURS. UKIWA NA TUKUTUKU/COPTER LAKO MWANAWANE NI DAKIKA 10 TU UNA-LAND PALE VIWANJA VYA GYMKANA MZEE UKO KWA OFFICE TARATIIBU, JIONI TENA TUKUTUKUTUKU 10 MINUTES UKO TEGETA MZAZI. hii imekaaje??

    ReplyDelete
  12. Mdau wa Wed Aug 05, 02:04:00 PM na yule wa Wed Aug 05, 02:40:00 PM nakubaliana nanyi kabisa, Huyu Alex Paurine (sijui kama ameisha kuwa Doctor) nilisoma nae elimu ya secondary PCM alikuwa kipanga na tangu hapo kaenda ulaya kusoma. Hivyo kama kweli ameweza kufanya hayo ni kwa sababu ameendelea na kufundishwa katika mtizamo wa wenzetu wa west. Hawa wenzetu wanaona kipaji na kukiendeleza.

    Alex (Van Damme)nakumbuka ukorofi wako pia. Mimi ni mshikaji wako Salum Maganga nilkuwa nyuma yako mwaka mmoja, niko UAE kwa sasa. Kila la kheli

    ReplyDelete
  13. hebu rekebisha kwanza "kaajiliwa" ndio tusonge mbele. hapa Tz tuna wataalamu aina zote si madktari, maengineer, n.k. tatizo kubwa sana kwetu ni UZALENDO. kila mtu akiipenda nchi yake, ATAJITUMA. watu wataacha kufikiria hela za richmond, EPA n.k sikatai nchi zilizokwishaendelea kuwa bado na zenyewe zina matatizo lkn wenzetu wana UZALENDO. we daktari au engineer unajipinda halafu at the end of day wapo wajanja nyuma yako, ya nini bw wewe? we unafkiri nchi yetu maskini kwamba tuna umaskini sababu hatuna wataalamu wa kuvumbua! Hebu jaribu kufikiri ndio uandikage na wewe. michu siku nyingine ntanyoa kichwa hicho.

    ReplyDelete
  14. Hehehehe Inabidi nicheke kwanza kwa swali lako. Sababu ya wenzetu kuwa wanauwezo wa kubuni ni kwamba technolojia imewazunguka na rahisi kupatikanika katika nchi zao. Sasa basi mtoto mdogo anaweza kutumia vyombo mbali mbali kwa sabau vipo na ana access navyo kwa hiyo Elimu ipo, vyombo vipo mtu anakuwa na time ya kufanya uvumbuzi. Sasa ukija Tanzania, Elimu watu wanayo lakini vyombo hamna sas atavumbua nini wakati vya kuvumbulia huna access navyo na dhiki ya maisha inakupiga bora ulishe watoto kuliko kuhangaika na uvumbuzi ambao unachukua muda, unataka pesa na changamoto. Kwa mfano Mimi nimesoma IT naweza kutengeneza Software amabayo inaweza kutumika kwa kiswahili. lakini sasa huu ni uvumbuzi ambao unataka time, pesa na management, sasa huku ulaya naweza kufanya kazi hiyo kwa sababu vyombo vipi, time ipo na kazi ipo na sina njaa, JEE BONGO NAWEZAAAAAAAA....Kila kitu kinataka time na uwezo, huyo mtoto wa kichina kwa anakula na kulala vizuri, ana vyombo mbali mbali katumia na kuweza kuvumbua, kasoma kwenye internet kajua nini afanye, sasa mwenzangu bongo neno Internet Halijui, yaani umpe pesa mtoto aende internet caffe wakati makaa ya kupikia hamna umechanganyikiwa wewe...

    ReplyDelete
  15. Mh Mtoto huyu kanivutia sana hasa ndoto zake. Nanukuu kidogo
    "Wu, who lives in a mountain village, said: "I had this dream from childhood of not needing to climb mountains anymore. I wanted to go to school in my own flying machine."
    tatizo elimu tunayopewa bongo ni ya kukalilishwa si ya kueleweshwa!!.ukimchukua kijana aliyemaliza form six PCM pale Iliboru au Tabora Boys, ukamwambia a-flow Archimedes principle "Law of Floatation, ataielezea kuliko hata mgunduzi mwenyewe Archmedes, lakini mwambie aweke kwa vitendo mhhhh
    hebu ona kijana yani katumia mbao na tuvyumavyuma na injini ya pikipiki, kitu kinapaa hewani!!
    wewe umesoma Physics+Maths Olevel, ukapiga PCM high school, Ukapiga Bachelor injiniaring yenye maphysics na hesabu ya kufa mtu, ukapiga masters labda ya mambo ya kuelea angani, una utaalamu wa chombo kinatakiwa kuwaje ili kiweze kupaa hewani/kunyanyuka na kiweze kuelea, sasa utashindwaje hata kufanya kitu kama cha huyu mtoto??!!!. aaagh bwana mi nadhani ni either uvivu au hawa mainjinia wetu ni makanyaboya walikuwa haconcetrate darasani zaidi ya kufikilia box.

    ReplyDelete
  16. Wadau naomba niwe mnafiki nitoke nje ya mada kidogo. Hivi huyu Alex mnayetusumbua naye ndiyo Alex Mbaga? na kama ndo huyu haya yote sijui ugunduzi my legs kayafanya saa ngapi?. Msitake kutuyeyusha hapa na misifa sifa yenu ya uongo. Kama kweli ni mtaalam na anapenda nchi yake kwanini tumtafute. Si aende mwenyewe akasaidie tuone.

    ReplyDelete
  17. Mainginia wetu wanajua sio kutengeneza bali kuharibu. Mfano Mv. Bukoba, wao ni kutoboa tundu tu. Aaaah!!!!

    ReplyDelete
  18. ahsante sana kwa kututonesha sisi maengineer lkn mimi leo kwa mara ya kwanza nitasema kwa nini tanzania hatuna maengineer wenye kufanya kazi zao kisawa sawa kwa sababu zifuatazo:-
    serikali haina sheria au haitilii nguvu usimamizi wa sheria, wewe umesikia wapi quality control tz.
    halafu hao maengineer wanatumia utapeli kuwadangaya mazuzu kuhusu utalaamu walokuwa nao kwani hakuna anaesimamia utoaji wa huduma ya engineering
    waziri wangapi katika serikali wana taaluma ya engineering.
    kwa ufupi tatizo lipo serikalini kama hakuna usimamizi wa kitaalamu na kuchukuliwa hatuwa za kitaalam basi hakuna tutakapofika.
    ahsante sana

    ReplyDelete
  19. Utasemaje kuwa taaluma zingine pia hazizalishi watu wenye ubunifu? Jee hujui kuwa joni mashaka ni mtanzania? na obama anataka kumchukua awe mshauli wake wa mambo ya kiuchumi? wamarekani!!! hands off joni wetu.

    ReplyDelete
  20. Mdau,
    Ahsante kwa kuleta mada hii, kwani hata nami nilikuwa nafikiria kitu kama hiki, kwamba kwa nini sisi hatuendelei kwa vitu kusonga mbele. Kwa nini nilipata wazo hili, ni kwa sababu nilikuwa nasoma stori ya kawaida tu kuhusu mfanyakazi katika kampuni ambayo ninafanyia kazi ambayo ni ya wazungu, huyu jamaa kafikiria kitu akapata wazo na kulipeleka kwa wanaousika nao wakalifanyia kazi, matokeo yake ni kuokoa pesa nyingi sana.
    Swali je makapuni na mashirika yetu ya kitanzania yanatoa nafasi ya watu wao kuwa wabunifu, jibu HAPANA. Ukitoa utakatishwa tamaa na msururu wa sababu nyingiiii....
    Mtanzania,
    tmajaliwa@yahoo.com

    ReplyDelete
  21. Eng. Vinho unakosea kusema ma-engineer ni karibu na mungu!

    Sasa kama ni hivyo kwanini hawawezi ku-commercialize?. Entrepreneurship ni kuanzia uvumbuzi mpaka successful commercialization. Kuna link kati ya kugundua na kujua ni kitu gani jamii inahitaji, na kisha kuipatia jamii hicho kitu. Mvumbuzi si lazima awe engineer, na engineer si lazima awe na uwezo wa kudiscover kitu gani society inahitaji. Vinategemeana!

    Ndio maana shule nyingi huko West sasa hivi zinaunganisha idara zao mbalimbali. Utakuta Idara za Uchumi(kwa upana wake),idara ya Uhandisi(engineering) na idara ya Arts and Design zinaungana kufanya kazi pamoja. Watu wanaongelea multidisciplinary.

    Lakini sisi bado tunaulizana, umesoma field gani? bado tuko idiosyncratic, tunafikiria ndani ya fani zetu tu, tunaona fani moja ni bora kuliko nyingine, kitu ambacho tunajidanganya!

    Labda ndio maana wenzetu wanaweza ku "commercialize" na sisi tunebakia kusema" maengineer wazuri ila shida ni ku-commercialize"

    We need to change.

    DMK

    ReplyDelete
  22. Tupe mfano hata wa mtoto wa highschool aliyejenga ghorofa la zege.

    ReplyDelete
  23. Watanzania bwana, kila kitu wanataka kulaumu serikali. Eti mainjinia hawafanyi hivi kwa sababu serikali haifanyi vile. Je private sector TZ inafanya nini?

    Katika nchi zilizoendelea, uvumbuzi mwingi (yaani R&D)zinakuwa funded na makampuni binafsi.

    Hivyo jibu la swala hili ni simple: until serikali na sisi wananchi wenyewe tutakapoamka kutoka kwenye hangovers za siasa zetu za ujamaa za 1970s na kuhamasisha na kukuza upeo wa private sector yetu ili ianze ku-harness ujuzi wa wataalamu wetu, tutabaki tukila serikali serikali, kama walivyokuwa wanalia kule astern Europe kabla ya Gorbachyev na glasnost.

    Tatizo si engineers au serikali au uvivu wa mainjinia. Tatizo ni kwamba watanzania hatujajuwa bado ni jinsi gani wenzetu waliondelea wanavyoanisha private sectors zao na scientific research, halafu ku-commercialise uvumbuzi wao ili wote wanufaike.

    Wafanyabiashgara wetu pia wanabidi waelishwe ili wajue jinsi ya kupata mikopo nje ya nchi ili kuweza kugrow beyond our borders. We are stuck in the past!

    ReplyDelete
  24. jamani tusiongee kwa kujifurahisha kwa maada nyeti kama hii.
    tuwe siliace kidogo, maana mimi naamini mtanzania unayeendaga nyumbani na kuona jinsi mama, baba, bibi, babu zetu, dada na kaka zetu wanavyoishi kwa kulinganisha na huku tunakoishi, kwa kusema ukweli utaacha kufanya utani kzenye maada kama hii na kutoa maoni ambayo kiongozi husika akiyasoma, kama kzeli ni kiongozi mchungu wa nchi yake na mzalendo haswa atayafanyia kazi.

    kwenye hili tusilaumu aina yoyote ya professional hapa, tatizo kuu ni usimamizi wa policy zetu tanzania.
    engineer hawezi kufanya kazi yake vizuri kwa sababu ya system ya uongozi ilivyo, similary mwanasheria, hakimu, jaji etc.

    matokeo yake hao maengineer tunaotegemea kuvumbua vitu wanapoona wanayoyafanya hayadhaminiwi nao wanaamua kuingia kwenye siasa mfano, Dr kawambwa, waziri wa mazingira, zamani technolojia, then maji Prof,,,,, hawa ni maengineer ambao kiukzeli pale udsm walikuwa na mchango mkubwa sana na tafiti zao kama zingekuwa zinafanyiawa kazi na kutolewa support pamoja na wengine kama hao, mimi naamini tusingekuwa hapa tulipo ssasa.

    nitakupeni mfano mmoja, pale udsm kuna jamaa mmoja ameajiliwa pale kama instructor technician, ni engineer, i remember early 1980's alitafiti kitu na akakiandikia kitabu kabisa, unfortunately akakosa pesa ya kukilunch na alipofuatilia hata kwenye utawala wakampiga chini, unajua kilichotokea, akaja msweden mmoja akaondoka na ile kazi akaenda kwao akapata support akaimodofy kidogo akaipublish na serikali yake ikamsupport, ninavyokuambia sasa, ile technologia iliyogunguliwa na mtanzania wa kipato cha chini inawasaidia wasweden na kuwapa pesa na ndio hiyo hiyo wanayoitumia kudai wanatupa misaada.

    jamani issue kubwa mimi naamini na wasimamizi wa policy zetu, kwa maana ya mawaziri na watendaji wakubwa tulionao ndo chanzo kikubwa cha kutokufika pale tulipotakiwa kuwa.
    naomba kuwakilisha, mdau kutoka france

    ReplyDelete
  25. napenda nitoe ufafanuzi ufuatao kwasababu hili nimelipigia sana kelele nikiwa na rafiki zangu hadi leo naliona limetolewa hapa ktk blog.
    -kuna vipaji vingi vipo ktk jamii,lakini vinapotoshwa na jamii yenyewe kuanzia ya wasio soma hadi maprofessor ambao hawana vipaji asilia vya ugundunduzi,maana sio kila mtu kajaliwa kugundua. kwa mfano unaweza kukuta mtoto angekuwa ni mvumbuzi ktk teknolojia ya umeme au mitambo, lakini tangu udogoni anashawishiwa na wazazi aelekee ktk taaluma ya sheria ili awe hakimu na ajitajirishe kwa rushwa. mtoto huyo akianza kupoteza muelekeo anaishia kutumia nguvu nyingi kuitafuta taaaluma ya sheria na anaishia hukohuko.
    - kuna wengine unakuta wamehimili na angalau kufika ktk level za juu ambako wanaweza kuvumbua,lakini kutokana na kuwekwa ktk mazingira ya kutishiwa na maprofessor wao na kutokuwa na uhuru na mda wa ziada wa kujumuisha mawazo(idea),wengi wanabaki kukariri kile tu anachopewa ili apate vyeti. na akimaliza kwakuwa wengi huwa umri umekwenda anaanza kufikiria njia ya mkato kuwin ni kuwekeza ktk siasa.matokeo yake ndio UFISADI unao uona ktk afrika.
    -kama walivyosema walio tangulia,sisi na afrika kwa ujumla ni watu wa matukio na kutokupenda kushughulisha ubongo sana,tunapenda sana starehe,hata kile kidogo kinachokuwepo kinaelekezwa ktk minuso,visherehe,vipombe n.k na matokeo yake hakuna kampuni wala viongozi iwe serikalini,ktk jamii,ama kwingineko wenye vision(maono)ya kuwekeza ktk mkombozi huyu wa kurahisisha maisha aitwaye sayansi asilia.tunapenda mteremko, yaani sherehe,starehe,sanaa za kufurahisha umati na visiasa tu.hapa siilaumu wala hata serikali maana ndivyo tulivyo.
    sasa kifanyike nini hapo ndipo ilipo kazi.maana kila kitu kabla hujafikiria namna ya kukifanya lazima ufikirie ni matokeo gani unayohitaji kupata. itakapofika jamii ikatambua kuwa inahazina ndani yake na inahitaji kuitumia hazina yake ktk nyanja ya kuboresha maisha,basi itajifunza namna ya kukuza vipaji asilia kwa hawa waliojaliwa,na sio kwa wanopata A kwa kuwa wanauwezo wa kupiga misuli usiku kucha na kukariri mistari.maana kuna wengine wana idea ambayo akimpa engineer wa fani hiyo inaweza kuwa rahisi kutekelezeka,japo engineer yeye huenda anautaalam tu ila hiyo idea hana.na uvumbuzi msingi wake huwa ni idea inayochemka toka ndani,na inaweza fikirika kama impossibility,ila ktk mkono wa mtu sahihi inatolewa ktk dreamhadi reality.
    sasa ma engineer wetu nao pia wanaambukizwa ileile kasumba, kwa maana kwamba akishakuwa engineer basi hutamwambia kitu akusikilize hata kama kingekuwa ni jibu la tatizo,maana anajiona tayari yeye ndiye anafahamu yote.tofauti na wenzetu sisi ubishi mwingi(maneno mengi)vitendo kidogo. kuna mmoja hapojuu kalalamika kwa ajili ya muda,vitendea kazi n.k lakini kwa mbunifu hutumia kilekile alichonacho japo atahitaji msaada toka kwa wengine pia ili kufikia malengo na wakati mwingine huchukua muda sana ka kufail maranyingi hadi inapokuja kukamilika.
    wito:tuanze kujaribu. maana huyu mchina angewazia kuanguka na kufa,asingethubutu hata kuruka.angeanza kufikiria laws na principles kibao ktk theory na kuishia kukata tamaa. the risk takers are the winners!!

    mdau-masomoni ughaibuni

    ReplyDelete
  26. tatizo shule zetu ambazo ndio msingi ni kusoma tu darasani na kukariri. Hivyo kuwa creative hatujui.

    Pili shule zetu hazina field trip kwa hiyp mtoto anakua akiwa hajui chochote kinachoendelea nje ya kijiji chake achia mbali ulimwenguni. Tunatakiwa tuwahamasishe walimu wawe wanawapeleka watoto kwenye maofisi, bunge , ikulu na mabwawa ili wakaone.....Raisi Clinton alianza kupenda kuwa raisi mara tu baada ya kutembelea kishule ikulu walivyokua wadogo.

    Unamwambia mtoto wa kibongo adream big wakati hata hajui cha kudream....ndege wengine hata hawajaiona zaidi ya zile rocket zinapita kwa juu na kuacha moshi nyuma.....Sio kosa letu....elimu yetu ni more theoretical. Practical tunachojifunza shuleni ni kusimama na kusalimu mwalimu....na ndio maana tuwapole sana tu

    ReplyDelete
  27. AHSANTE SANA MDAU WA MCHUZIMKWA POST YALO.
    MIMI NI MHANDISI WA UJENZI AMBAYE NINA INTEREST SANA KATIKA UVUMBUZI NA NINA FANYA MAMBO MENGI YA KITAALUMA KATIKA MECHANICAL NA ELECTONIC ENGINEERING.
    TATIZO KUBWA KWA MECHANICAL ENGINEERS WETU NI KUTOKUWA NA UWEZO WA KUTHIBUTU. WENGI NI WAOGA WA KUJARIBU
    WANASHUNDWA KUTUMIA INJINI ZETU NDOGO NDOGO NA ZILIZOPO KWA MANUFAA YA WANANCHI
    UVUMBUZI SI KISOMO ILA NI ULE MOYO WA KUJARIBU.

    ReplyDelete
  28. Mimi kama mmoja wa hao mainjinia,ningependa kukwambia kwamba kuwa na degree za engineering sio hoja, Suala ni kwamba upo katika mazingira ambayo yana promote innovation au vipi? Tanzania hamna research yoyote ambayo iko funded. Research, trial, building prototypes and making a final product can take years. I dont see how Tanzania can support such a thing.

    Engineer USA.

    ReplyDelete
  29. Tatizo la elimu yetu ya bongo ni kwamba watu wanameza maandishi,namaanisha wanakalili,hawako creative..mimi nimesoma bongo nakumbuka nilikuwa star hapo home A kila mtihani lakini ki ukweli zaidi ya nusu ya vitu darasani nilikuwa nameza tu wala maana yakesikujua.hivi sasa niko kwenye watu wenye akili zao kwenye mitihani ya kuandika nafunua ila ukiweka practical ni F .tatizo lengi ni system yetu ya elimu hapo bongo utakuta mwanafunzi analazimishwa kusoma masomo 12 ya secondary ambayo kwa kweli ni mengi kwa mtazamo wangu,hivi kwa nini tusifanye kama A level kwamba mwanafunzi achague anachotaka kusoma anapoingia form one.hivi kama nataka kuwa Doctor kwa nini nilazimishwe kusoma accounts,commerce na masomo mengine ambayo sitakuja kuyatumia hapo baadae wakati huo muda ningeutumia kuingia deep katika kila ambacho naona nina talent nacho.
    Tunao wataalam kibao huku toka bongo ambao hapo nyumbani tulikuwa tunaweka maisha yetu mikononi kwao lakini wakija huku wakipewa mitahani kupata licence ya kupractice wanadunda na kuishia kulalamika ni ubaguzi wa hawa wazungu lakini ukweli ni kuwa ni wachovu. hebu ndugu zangu jiulizeni hivi kwa nini hao wakubwa wetu wakiumwa hawaendi muhimbili? Lowasa alikuwa ujerumani kutibiwa jicho...kisa ni kwamba anajua hakuna Dr bongo...kama anony 2 alivyosema hapo bongo masters wanaipata kwa kukopi toka kwenye vitabu vya watu baada ya kufanya research...ni hayo tu kwa leo.....

    ReplyDelete
  30. wadau wenzangu nimefurahishwa sana na maoni yaliyotolewa,kiukweli tatizo la elimu yetu kwanza lipo kwenye lugha ya kiingereza ambayo inafanya watu wakariri badala ya kuelewa kwa hiyo hawezi kufikiri beyond the content.tunawaona wanafunzi wengi wakija huku ughaibuni kwa masters baada ya mlimani na taasisi zingine za bongo MWE kaazi kwelikweli. na huwa wanakubali kwamba vyuo vyetu bado vinasafari ndefu kama tutaendelea kutumia English kama medium of instruction,wenzetu wachina,wajapan,wakorea n.k wamepiga hiyo hatua kwa kutumia lugha zao mtake msitake hilo ni tatizo kubwa sana.Pili ni aina ya elimu tunayotoa ni ya kikoloni mtoto wa Tunduru unamshindilia physical geography ya North America ya kazi gani badala ya elimu ya madini ambayo yapo hapo tunduru ili innovation ianzie hapohapo Tunduru!!!!

    ReplyDelete
  31. Hapo kare kulikuwepo NYUMBU aliweza kukimbia km80 kwa saa ; Nyumbu si mnyama bali ni Lori la kwanza la Kitanzania, lililotengenezwa na Whandisi wa kitanzania pale Kibaha.
    Hapo kare kulikuwepo na TAMCO ; Hilo si tangazo bari ni kampuni ya Watanzania tuliweza kuunganisha basi na malori hapa Tanzania, kwa mfano tu hivyo ndivyo TATA ya India ilivyoanza kwa kuaunganisha Benzi. Kwa kuunganisha kitu kama gari unaleta vitu ambavyo havipatikani nchini na kadri siku zinavyokwenda unapunguza idadi ya vitu unavyoagiza toka nje mpaka inafika wakati tungepata TATA Nano yetu.
    Hapo kare kulikuwa na SWARA, sio Mikumi lakini ni baiskeri ya kitanzania ngumu yenye uwezo wa kubeba mizigo mizito.
    Hapo kare kulikuwa na TANAREK ; kuliwa na pasi, majiko, mabirika ya umeme ya kitanzania.
    Hapo kare kulikuwa na PHILIPS kule Arusha, NATIONAL pale Chang’ombe waliokuwepo watakumbuka Mkulima, sio shambani bali ni Redio ya bei nafuu ya Kitanzania ambayo kila mkulima aliweza kununua. Hapo kuliwa na feni, redio labda leo kungewa na TV na Projectors. Mnakumbuka Memory Q.
    Hapo kare kulikuwa na STAMICO
    Hapo kare kulikuwa na NDC
    Hapo kare kulikuwa na Eneo la viwa Keko, sio leo eneo la Maghara, (KJ Motors , walitengeneza vifaa vingi vya magari tuliweza kuexport rediator kwenda uraya).Kulikuwa na Eneo la Viwanda Morogoro, (Viatu, ngozi , maturubai, vyombo vya nyumbani, mazuria, engine za treni ohh we acha tu). Pia maeneo yalikuwa Arusha na Mwanza.
    Hii ni mifano, kwa vitu ambavyo kila mtu anaweza kuelewa, mifano hii ipo mingi kwenye fani nyingine za Uhandisi pia, kwenye ujenzi Soko la Kariakoo, katika maji MIanzi miti, n.k.
    HAPO KARE ENZI HIYO INCHII ILIKUWA NA MUELEKEO, ILIKUWA NA LENGO, KILA MTU ALIJITUMA KULIFIKIA LENGO HILO. (MASIKINI MTU ALIKOLIMBIA KWA KUKUMBUSHA HILI). VIONGOZI HAWAKUWA WABINAFSI WA KUTUNGA MILADI KWA FAIDA ZAO NA FAMILIA ZAO.
    Hivi ndivyo nchi kama India na China zilivyoenderea. Mapaka sasa ni vingumu kuingiza vitu kwenye nchi hizi.
    Leo hii Wahandisi Makenika, Kemia hawapati kazi kwa sababu hakuna viwanda.
    UTAONA KUWA SERA ZA NCHI ZINAMCHANGO MKUBWA KATIKA UWEZO NA MCHANGO WA KILA MTU HASA WAHANDISI.
    SISEMI TUJIFUNGIE LEO HII, KWA KUWA KWA HIVI SASA HAITAWEZEKANA LAKINI VIONGOZI WAACHE UBINAFSI NA WAALUDISHI KILE KIDOGO TULICHOKUWA NACHO.
    Wahandisi watanzania TUNAWEZA, ILA HATUWEZESWI AU HATUAMINIWI.
    Tanroads ni Taasisi ya Serikari ya Kiandisi, Katika Wahandisi watatu wa juu ambao walikuwa wapate nafasi ya kuiongoza taasisi hiyo wawili walikuwa wahadhili wanaotegemewa Chuo Kikuu DSM na mmoja ni Mhandisi Mtanzania wa kutengemewa (profesa) huko Afrika ya kusini katika Taasisi ya uchunzi (Reserch) wa ujenzi bora wa barabara. Wahandisi wote hao waliachwa kwa ubunafsi na upendereo mkubwa akachukuliwa MBOHARIA leo barabara zikiharibika tunaraumiwa Wahandisi.
    Huyu kijana hajagundua ila katengeneza kitu kwa bei ndogo na vifaa duni, amejitahidi sana na ni haki kusifiwa, na sasa tusubiri Herikopta za Kichina za bei nafuu, kama ilivyo kwenye pikipiki.
    Uhandisi si kitu rahisi, uboreshaji au urahasishaji wa kitu kama cha huyu kijana wa kichina unahitaji muda na gharama.
    Utaona wahandisi wanaojurika zaidi ni wajenzi kwa sababu kwao hakuna gharama kubwa, ni ubunifu na watu wanagharamia gharama za majengo yao.
    Lakini Uhandisi mwingine, Madini, Mekanikari, Kemia, Umeme mkubwa, Umeme mdogo, Simu, n.k mtu kuweza kungundua kitu inabidi uwe na mahara pa kushughulikia.
    HAPO KARE PALIKUWEPO.
    Na Wahandisi kila siku ya MEI MOSI walikuwa wanapata zawadi kwa uvumbuzi wao. Waliokuwepo watakumbuka wa watoto nawahadithia.
    SIWEZI NIKAKAA NATAFAKARI WAKATI NA NJAA, NITATAFUTA KUSHIBA KWANZA KWA NAMNA YOYOTE RAHISI HATA KAMA NI KOCOPI AU KUSAFISHA NA SIKU ZINAKWENDA, AU NIENDE NCHI NYINGINE NIWEZE KUSHIBISWA ILI NIWEZE KUTAFAKARI.

    ReplyDelete
  32. Hii kitu muhimu kuitafakari vilivyo.Yaani,mimi mpaka sasa hivi najiuliza nini inani interest na kwa ajiri ya maendeleo.
    Shortly,nimefanya yafuatayo:
    O level 10 subject -First Class
    A Level 3 PCM -First class
    Hapo ni nyumbani,haya nimekuja UK
    ACCA-Professional accountant,nimequalify,nimefanya Bsc Economics and Statistics nimemaliza,nikafanya Msc Finance na Investments,pia MBA.Ninafanya kazi,lakini katifa fani moja ya ukaguzi wa vitabu(audit)sasa najiona ninainterest ya computer science na IT,Government studies na politics nafikiria kufanya course.Najiuliza sana Hii DIVERSITY inatokea wapi,Nimekuzwa(Nyumbani) katika mosomo mengi na nimeweza kuyafanya vizuri.Jina langu linafwatwa na FCCA,CIMA,Bsc,Msc,MBA-nikiangalia nimadude kibao ya social sciences na sasa nataka IT,na politics.Sasa sijui NIMEROGWA na ELIMU ya TZ tangu msingi.Inaniudhi sana.Haya bwana baadae.Nimeona nikiingia kwenye fani ya maendeleo ya taifa,nita impact zaidi kwa jamii kwani personally,nimeshafikikia self actualization.
    Mdau uingereza.

    ReplyDelete
  33. Mdau wa Thu Aug 06, 10:56:00 AM,
    Ni kweli umeongea pointi nzuri sana, lugha hii pia ni tatizo kubwa linalofanya wanafunzi waishie kukalili tu badala ya kuelewa. unakuta mtu anakalili "what is matter?" matter is anything that has weight and occupy space hiyo ni kwemye chemistry sasa hako kajidefinition mtu analia nako miezi nenda rudi kukameza, ukimuuliza haya hiyo definition inamaanisha nini haelewi kitu!!!.
    mwisho napenda nikusahihishe nadhani ulimaanisha Regional geography na si physical geography sababu physical geography deals with the scientic aspects/foundations of geography so haitofautiani kutoka sehemu moja hadi nyingine, kwa mfano kwenye physical geography waweza soma jinsi volcanic rocks zinavyotokea au jinsi rift valley lakes like lake Tanganyika inavyokuwa formed, ni sayansi so hata marekani watasoma hivyohivyo, isipokuwa regional geography yenyewe inahusiana na geographical features, locations na vitu kama hivyo, ndo utasoma mto mississipi uko marekani, fiords zipo norway, mto niger uko wapi n.k Kwa hiyo uko sahihi sana kuna haja ya kupitia hii mitaala yetu. sisi mtoto wa kitanzania ukimuuliza mito iliyoko marekani, nigeria, europe yote anaijua, ukimuuliza ujerumani imepakana na nchi gani atakuambia, sababu ya kusoma regional geog lakini je hii inamsadia nini?? wazungu huku unakuta unamwambia ninatoka tanzania, hajui hata tanzania iko wapi, na pengine ndo kwanza anaisikia toka kwako.aaaagh

    ReplyDelete
  34. Elimu ya Tanzania kwa kweli haitayarishi watu kuwa wagunduzi kwa kweli na inapotokea unakuwa na mtu ambaye anajaribu kuja na vitu vipya yaani huwa hafanikiwi hata kwenye elimu yake.

    Yaani watu wengi wenye mtazamo fulani wa kigunduzi huwa wanashindwa elimu ya Tanzania au tuseme hakuna mfumo maalumu ambao unatoa nafasi kwa hawa watu wenye vipaji kuweza kuendeleza vipaji vyao.

    Kwa mfano...mimi nilisoma pale UDSM shahada ya Computer Science na mwaka wa mwisho huwa kuna ile project kwa kweli licha ya mazingira magumu wanafunzi huwa wanafanya projects kibao ambazo zinatatua matatizo ya chuo au makampuni mbalimbali ambayo yanatumika kama case studies lakini tunapomaliza kufanya hizo projects na kupewa awards yaani A,B+ etc ndo inakuwa mwisho.Wakati mwingine project inakuwa na potential kubwa ya kibiashara lakini wapi huwa inaishia hapo hapo na unakuta lecturers wanachukua some of these projects na kuziuza mtaani yaani huwa inashangaza sana.

    Ila kama wangekuwa wanatumia hiyo nafasi kuendeleza projects nyingine nzuri basi tungeweza kuwa na systems nzuri tu baada ya kutegemea systems zote toka india...hii inawezekana kabisa...ila hawa lecturers huwa hawafikirii beyond grades ambazo unapata kwenye hiyo project...

    ReplyDelete
  35. kaka ambaye unahisi umelogwa na elimu kwa kweli umenigusa sana asee.....! mana sometimes i face the same problem ila sema nashukuru sana sasa hivi naanza kujitambua. tuliza kichwa coz mafanikio yanakuja kwa kufanya unachokipenda...........!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...