kuna wadau hawana habari kwamba anko nanihii hakuanza mwaka huu kutoa zawadi kwa mlimbwende mwenye mvuto wa picha (photogenic), na kwamba mshindi wa kwanza alikuwa wema sepetu kwenye miss tz 2006 ambayo pia aliibuka mshindi wa kwanza. hapo juu anko nanihii akimpongeza wema baada ya kumtangaza kuwa ndiye miss photogenic iliyokuwa inadhaminiwa na photo point.
miss photogenic wema sepetu ambaye pia aliibuka
kuwa miss tz 2006 na anko nanihii na mdau. mambo yakienda mswano mwaka huu kwenye miss tz huenda akapatikana miss photogenic mwingine ambaye si lazima awe miss tz. endapo kama sosi zangu ziko sahihi kambi ya miss tz 2009 inaanza rasmo septemba 7 ama jumatatu baada ya hii ambapo washindi wa kanda zote watakaa pamoja mwezi mzima kujiandaa


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. mwezi mmoja mdogo ndiyo maana wanashindwa shindwa waongezewe miezi sita kabisa waive vizuri wakashinde, maana unajua mambo ya kuanzia ukubwani yanahitaji muda uyazoee acheni kubania vijisenti uto

    ReplyDelete
  2. kaka michuzi naona zipu hapo, ukufunga ulidhamiria au bahati mbaya?

    ReplyDelete
  3. kwakweli haka katoto wema sepetu kalikuwa kazuri sana kipindi kile. kalikuwa na haki ya kumshinda jokate mwegelo ingawa nae yuko tight, lakini wema alikuwa zaidi, tatizo sahivi kasha nyingi mtoto huyu.

    ReplyDelete
  4. Misupu kumbe we andunje! siku nyingine vaa vya mchuchumio ukienda kwenye 'special events' kama hizo

    ReplyDelete
  5. Huyu binti ni mzuri lakini hakufaa kuwa miss wa kutuwakisha nje ya nchi, hips zake kubwa, kwa wenzetu hizo ni mapungufu kwa miss.
    Kuwa miss photogenic ni sawa!!

    ReplyDelete
  6. sasa anko mboni kama unamwogopa kusogelea toto hilo???hahahaaa pozi lako tu picha #1 duuh

    ila umetoka mbali anko ulikua fit no nyama uzembe

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...