GLOBU YA JAMII IMEKUTANA NA MDAU LUSEKELO LAZARO MWAKASEGE (PICHANI AKIWA NA ANKO NANIHII) AMBAYE ANASUMBULIWA NA ULEMAVU WA KUWA NA MIFUPA DHAIFU, AMBAPO MIGUU YAKE HUVUNJIKA KILA IPATAPO MSUKOSUKO KIDOGO.
HIVI TUNAVYOONGEA LUSEKELO KESHAVUNJIKA MIGUU MARA 23 KATIKA NYAKATI TOFAUTI TOKA AZALIWE HUKO KIJIJI CHA MPUNGUTI, MWAKALELI, WILAYA YA RUNGWE MKOANI MBEYA MWAKA 1968.

MADAKTARI WAMEMSHAURI LUSEKELO ATAFUTE CHOMBO CHA USAFIRI ILI AENDELEE NA SHUGHULI ZAKE ZA FUNDI UMEME HAPA JIJINI. PIA ANAOMBA MSAADA WA HALI NA MLI ILI AWEZE KUPATA MTAJI WA KUENDELEZA MAISHA YAKE AMBAYO KWA UMRI ALIONAO NA MARADHI INAMPATA SHIDA SANA KUMUDU.

LUSEKELO ANASEMA YEYE HANA MAKUU, ANAOMBA MSAADA WA FEDHA ZA KUMWEZESHA KUPATA KIBAJAJI AMBACHO PAMOJA NA USAFIRI WAKE YEYE BINAFSI PIA ANAWEZA KUFANYIA BIASHARA. BAJAJI MOJA SIKU HIZI NI TAKRIBAN SHILINGI MILIONI 5 ZA KITANZANIA.

ANASEMA NAMBA YAKE YA SIMU YA MKONONI NI
+255 713 195 974
NA NAMBA YA AKAUNTI KATIKA BENKI YA
AKIBA COMMERCIAL BANK NI
ACC NO. ACB 020803951027
SWIFT CODE: AKCOTZ
unaweza pia kuandika nini unachoweza
kumsaidia kupitia email ya globu ya jamii ambayo ni
issamichuzi@gmail.com

Lusekelo akionesha miguu yake ambayo
ikipata msukosuko inavunjika. Tayari imeshavunjika mara 23 na kadri siku zinavyokwenda na majukumu kuzidi hatari ya kupata zahama hiyo ni dhahiri.
Wadau, Kutoa ni moyo. Kwa niaba yake Globu ya Jamii inaomba wadau tumsaidie
apate usafiri wa Bajaji ambao pia utamwingizia kipato ajikimu kimaisha. Globu ya jamii inatoa Tshs. 100,000/- kama kianzio cha harambee hii kwa mdau huyu





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. Pole ndugu, na huu ni ukumbusho kuwa sisi wengine tumshukuru Mungu kwa mili yetu isikuwa na matatizo makubwa ya afya kama haya. Nina swali moja, yeye ni fundi umeme, sasa hata kama akipata kiti cha kuendesha (wheelchair) - bado itambidi asimame, apande ngazi n.k katika process ya kufanya kazi - nafikiri - ndugu angefaa afanye kazi ya ofisini, uwalimu au shughuli yeyote ambayo haitaji kutumia miguu au ketembea. Ufundi umeme mzuri, lakini labda ajifunze ujuzi mwingine au awe na msaidizi ambaye anakwenda nae kwenye kazi na yeye anamwambia nini kifanywe, au atafute shule ya ufundi afunze ujuzi wake.

    ReplyDelete
  2. pole kaka tutajitahidi tukiweza tutatuma. jipe moyo

    ReplyDelete
  3. la muhimu kujua ni kwamba sisi ni wanadamu na duniani hapa tuna pita tu,kama wanyama na wadudu wanaweza kusaidiana kufikia malengo yao kwa nini sisi Binadamu tushindwe? "HUJAFA HUJAUMBIKA" naomba wadau tumsaidie huyu mtu.

    ReplyDelete
  4. we anony Tue Aug 18, 02:34:00 PM ebu ongea kwa herufi kubwa. mahubiri kafanyie jangwani, hapa si mahali pake.

    ReplyDelete
  5. Mr Michuzi, I am really touched by this guy's medical problems...That could have been someone in my family. It is not all about what we think he should do to better his life but rather what he thinks he can do for himself for he knows his ability better than any of us can ever imagine...all he needs from you and I is that help and his dream will (according to his expectations) be realised. For that matter I'm pledging Tshs 100,000/= and will hand it over to you (Mr Michuzi) next month during my short stay in Tanzania. Thank you for sharing this with us (wadau) and I hope others will help too. Thank you guys (wadau) for being charitable

    AP...Mdau wa GB.

    ReplyDelete
  6. Ah! mimi nasubili kupewa mshahala tu,,nakuagizia laki moja shilingi kwa mchango huo.Kweli huyu mtu wadau mje tumsaidie na yeye anastahili kuishi kama sisi.

    ReplyDelete
  7. IT IS A DISEASE THAT HE WILL NOT HEEL, WHAT HE CAN DO IS JUST TO LEARN TO LIVE WITH IT, THERE IS NO CURE FOR THAT UGONJWA.

    ReplyDelete
  8. Suala jingine la kuzingatia Mdau Lusekelo pamoja na vitendea kazi/usafiri n.k ni kujaribu kupunguza uzito, maana ni kawaida yetu tukufikia umri wa miaka arobaini ma kuendelea, huwa tunaongezeka uzito.

    Maana yake ni kuwa na uwiano wa kimo na uzito, hiyo itapunguza mwili uelemea mifupa yako, hivyo onana na daktari na bingwa wa lishe.

    Mdau
    Daktari Mshauri wa Blogu ya Jamii
    Uingereza.

    ReplyDelete
  9. we daktari wa uingereza nahisi unatibu panya.

    sasa ushauri gani huo, ebu kwa akili zako unaona hapo huyo jamaa ana uzito usiolingana na kimo chake? au umeamua kuandika tu!

    ebu ukicheck picha hizo, unaona over-weight problem hapo? Jamaa anaonekana amedhoofu kabisa kinachomsitili ni shati hapo. kama umesoma u-dr. nashauri usitibu, utaua wewe.

    bwana kama huna hela ebu nyamaza bwana! "si unaona wengine tumejinyamzia hapa"!

    ReplyDelete
  10. Pole kaka Mwakasege,
    Nakukumbuka tulikuwa wote IFUNDA (The Glorious...) miaka ya 85-88.
    Nitakutafuta kwa mobile yako, hope we can convince more class mates to contribute.

    ReplyDelete
  11. Sasa wewe anon wa Tue 2.470pm huyo anon unayemshambulia kakosa nn jamani?hakuna hata cha kuhubiri alichoandika hapo, yote ni ya ukweli.Kama unaweza saidia la huwezi kaa kimya na sio kuandika jus for the sake of it!
    Bwana Mwakasege pole naomba mungu akupe nguvu na kwa uwezo wake atakupa wepesi wa maisha inshaalah.

    ReplyDelete
  12. Ndo maana wanasema Wabongo maneno mengi tu..uswahili tu..sasa wote mlioongea hapo ni mmoja tu aliyeahidi pesa. Jamani. Mimi naomba contact nitatuma dola 50.00 Michuzi nipatie contact kuwa natuma hela kwa nani. Haya maneno mengi hayasaidii. Wabongo ingekuwa mmeombwa pesa za harusi au msiba wa kwanza kutoa. Mtu akiugua maneno tu...!!Kwavile hamtakula pilau?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...