Ambwene Yesaya a.k.a AY

habari zimeingia punde zinadatisha kwamba mwanamuziki nyota wa kizazi kipya ambwene yesaya a.k.a AY anaondoka Jumamosi hii kuelekea sauzi katika jiji la johannesburg ambako atatumbuiza kwenye hafla ya Big Brother. Ataongozana na Snare wa east coast.
AY kaiambia globu ya jamii kwa njia ya twitter sasa hivi kwamba yeye kama kawaida yake hana show kubwa wala ndogo na kwamba show zote kwake ni muhimu hivyo anajiandaa kwa makamuzi ya nguvu.
kasema baada ya sauzi ataelekea Malaysia ambako atakuwa na show jijini Kuala lumpur September 24, mwaka huu ndani ya klabu cha Titunium. Pia ataporejea wiki ijayo anatarajiwa kutoa singo ingine mpya iitwayo 'Bed & Breakfast' ambayo imetayarishwa na Hermy B wa B. Hitz Studios.
Wakati huo huo AY anawakumbusha wadau wote popote walipo hapa bongo kumpa taffu kwa kumpigia kura katika tuzo za Mtv Africa. Kumpigia kura andika 'BHH AY' kisha tuma sms kwenda namba 0789 777 333

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. Hongera AY kwa chance hii. Sasa sijui na yeye atasemwa nini au yale aliyosemwa Kanumba yalikuwa ni chuki binafsi tu za watu.....!?

    Kila la kheri.

    ReplyDelete
  2. Mambo vipi AY?

    E bwana Big Up mkuu ila angalia yasikukute kama ya Mh.aliyetoka huko hope unamjua kwa sababu amemake headline sana this week! Pitia Pitia kiinglish kidogo jinsi ya kujitambulisha(kuji=introduce) ukichemka na wewe utazidi kutudidimiza! Kanumba just learn from others like Celin! Walikuwa awajui kiinglish lkn now wanjua coz wamejifinza kwhyo don't feel shy to learn my bro! Ay take it as the challenge! Ndo usupastar huo! Kanumba,you have to pay da cost to be star!

    Bob sambeke--Dodoma-Tanzania

    ReplyDelete
  3. michuzi please!!!!! please!!! wadau wa north america tunaomba ufanye vitu kama usa, kitu kikitokea kama hicho alafu watu kama hawakubali kinachofanyika ni kuweka ile video ya kule south kuhusu kanumba hapo tutajua nani mkweli na hata ikibidi wadau waombe msamaa kama walizusha.
    Mdau Na!!

    ReplyDelete
  4. Ataimba kwa lugha gani?? Nyimbo za Kiingereza??

    ReplyDelete
  5. nenda salama kijana wetu na ukae ukijua kuwa kuna watu wabaya around you life so know the means of managing them, bofya hapa ujue juu ya 8 toxic personalities: http://shine.yahoo.com/channel/life/8-toxic-personalities-to-avoid-461078/

    ReplyDelete
  6. Ay namuamin hata kazi zake zimeenda shule!msimringanishe na Kanumba ubishoo umemponza kwanza AY shule ipo na hata English yake poa ndo maana anafanya kazi zake nyingi kwa shemeji zake Michu Uganda na Kenya poa baby go baby wewe si Ray na Kanumba

    ReplyDelete
  7. ati ataimba nyimbo gani ya kiingereza? we ulitaka aimbe vipi ataimba kifaransa mbona mopao mnakata viuno almanusra vikatike na hamjuji maana mradi anate na biti ukome kuuliza upuuzi

    ReplyDelete
  8. Hello

    kila la kheri AY wabongo hawana wema na wengi wanaolaumu shule hamna nenda baba nendaaa kaimbe kwa KAKA MKUBWA (Big bro.)
    WAO KIDHUNGU NDIO WAMEONA DILI ACHANA NAO

    ReplyDelete
  9. AY yuko fiti sina mashaka naye kwenye kila kitu kuanzia lugha, hana majivuno wala humsikii kwenye mambo ya kijingjinga na makinikwenye sanaa yake hivyo na muaminia tupige kura

    ReplyDelete
  10. Ushauri wa bure kwa bwana AY> Unajua kuimba kiingereza sio kujua kiingereza, unapoimba unakuwa umeclaim, kwa hiyo wimbo upo kichwani. Yoyote anaweza kuimba kiingereza, hata Kanumba anaweza, ila kaka huko kuna mahojiano na maswali ya papo kwa hapo, angalia usije ukaishia kucheka cheka ka bitoz wetu huyo. Jiandae kuperform na pia ujiandae kwa mahojiano. Maandalizi ni muhimu sana kwa kila kitu unachotegemea kufanya.

    AHSANTE KWA KUNIELEWA !

    ReplyDelete
  11. Ish! huyu maimuna mwingine eti ume claim jamani lugha ya watu iacheni kwani ulishindwa nini kusema kukariri mpaka utumie english. Si ajabu ulimnanga Kanumba wa watu maskini kumbe wewe ndio kabsaa hujui watanzania acheni hizo kuchapia kila mtu anachapia hata Richard alikuwa anachapia vilevile saana tu

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...