duka kubwa la helsinki ambamo kazi za jhikoman zinauzwa sasa
CD ya Ras Jhikoman

Mkuu natumaini hali yako ni nzuri.
Siku ya leo imekuwa ni siku ya furaha kubwa kwangu kama shabiki wa miziki ya nyumbani nilipoona CD ya mwanamuziki wetu wa Kibongo Jhiko Manyika (JhikoMan, pichani) ikiuzwa kwenye duka linaloheshimika sana huku Scandinavia (Stockman).

Bila shaka kwa wanaolifahamu duka hilo, huwezi kuingiza bidhaa yoyote ambayo haijakidhi viwango vya kimataifa, na kwa kuona CD ya ndugu yetu na mbongo mwenzetu ndani ya Stockman, bila shaka muziki wetu na wasanii wetu wameanza kukubalika na wanahitaji pongezi.

Hongera sana Jhiko kwa kutuwakilisha.
Mdau (Helsinki-Finland)

kazi ya jhikoman gado-ka-gado na za vigogo wengine





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. mbona wivu hiyo "ZANZIBARA" hujaiona hapo?! mbona huifagilii?

    ReplyDelete
  2. Ndoto ya mchana SwedenSeptember 11, 2009

    Hongera sana Jhikoman,kwa duka kama hilo kama kiwango cha muziki wake ni cha chini kamwe wasingeuza c-d zake.Hii ni uthibitisho tosha muziki wa Jhikoman huko juu sana.
    Mdau ndoto ya mchana Sweden.

    ReplyDelete
  3. Ishu sio kuwa kwenye market, ishu ni kununuliwa hizo cd, wewe mfagiliaji umenunua moja, au unafagilia tu?. Na hapo stockman kwenye sekshen ya world music kuna cd kibao za wasanii wa kibongo sio jhiko peke yake.

    ReplyDelete
  4. Wee anony acha ushamba na roho mbaya. Kama kuna kazi za wasanii wengine, mbona hujapiga picha na kuiweka humu?

    Katika capitalism huwezi kuweka bidhaa isiyonunuliwa kwenye duka, ukiona kazi ya msanii imo kwenye duka lenye jina kama hilo, basi ujue kiwango chake kinakubalika.

    ReplyDelete
  5. Hongera sana Jhiko. Cha kushangaza mbona wanamuziki wanaoshinda kwenye front pages zetu hawaonekani hivyo ughaibuni?

    ReplyDelete
  6. Kwani Zanzibara msaniii? JhikoMam msanii na ndio lengo la mdau kumfagilia.

    ReplyDelete
  7. Hakiwezi kuwa kwenye duka kama Stockhman kama kazi ingekuwa ina kiwango cha chini.Wewe unayesema kuna kazi kibao za wasanii wa kibongo,ni nani hao,wataje.Jhikoman anaperform mara kwa mara kwenye matamasha makubwa huku Ulaya,na sio anakuja kuwapigia tu jumuiya ya WaTanzania kama wasanii wengi wanavyofanya.Ana washabiki wengi huku/audience ya mataifa mengi tu.
    Apewe pongezi zake zinazostahili kwa kufikia kiwango hicho.
    Huu ni mfano kama marehemu Hukwe Zawose wakati dunia inamtambua kwa muziki wake daima amepewa heshima yake na mchango wake umetambuliwa kidogo sana.Lini wabongo tutawapenda na kuwapongeza wasanii wetu?

    ReplyDelete
  8. Michu,
    tafwadhalii Shekhe tuondolee huu mzizi wa fitna kwa kutuwekea angalau 'clip' ya video moja ya Jhikoman hapa ndani ya bulogu ya jamii, maana kwa Kanumba ushaondoa fitna bin fitina.

    amasivyo mzizi huu wa fitna utakua na kuwa 'liji-Mbuyu'.

    Mdau
    Swalihina

    ReplyDelete
  9. salamu mkuu nimefurahi kuona jina la nchi yangu na sio mkoa ZANZIBAR.

    ReplyDelete
  10. Anony hapo juu tafuta mawani, kwani maandishi ya CD hiyo yameandikwa Zanzibara ambayo sina hakika inamaanisha Zanzibar. Kama ilivyo tofauti kubwa kati ya Dar-es-salaam (Tanzania) na Dar-us-salaam (Brunei).

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...