Oya michachuzi,
hawa jamaa FIFA wanatuwekea usiku, ati tusisainishe mchezaji mpya mpaka mwaka two thousand alfu mbili na kumi na moja, sasa hii kweli ni haki au ndio njama zenu wana wa bwawani?
Deku linki hiyo kama vipi imwage kwa jamii.
MdauTrue Blue Helsinki

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. Yani ni noma hii, kama sio umafia ni nini tena. Manu mbona hawakufungiwa walipomteka nyara kijana wa kifaransa juzi juzi tu.
    Hii inaonyesha ni kampeni kubwa mno ya kuwastopisha Chelsea, lakini hata hivyo squadi waliokuwa nayo wanaweza kupeta nayo mpaka hiyo tuu tauzen elfu mbili na moja.

    ReplyDelete
  2. Njama za Platini hizo kupiga vita english clubs.

    ReplyDelete
  3. FIFA wamenukuu vifungu vya sheria vinavyowafunga. Mnabisha ubishi tu au mna vifungu vinawatetea? Mmezidi kuvunja kanuni, hatujasahau mlivyofanya kumhamisha Ashley Cole.

    ReplyDelete
  4. Kama kanuni zinasema hivyo sioni suala la kujadili. Hii inanikumbusha sakata la Athumani Idd "Chuji" ambaye aliomba kuvunja mkataba na Simba na baadaye kusajiliwa na Yanga, kama TFF wangekuwa fair walitakiwa kufanya kama FIFA.

    ReplyDelete
  5. Mpaka 2011 Darajani kutakuwa na care Homes maana wachezaji wote watakuwa vibabu. Poleni ndugu zangu penye kufuka moshi jua moto upo. Unakumbuka walivyomwiba Mikael Omeobi kutoka mashetani wekundu (ManU). Wakazani watakuwa wanafanya hivyo kila siku maana wanabahati kipindi kile ManU waliyamaliza mezani tu lkn kama wanheyafikisha kunahusika basi haya yasingekuwa mapya.
    Roma walishachukua adhabu kama hiyo ila wakapigana ikapunguzwa ikawa msimu mmoja tu wa usajili.
    Kenyon analeta bishara zake haramu hajui morden football siku hizi siyo ya kina karne hizo.
    Hata mfanyaje sheria imepita labda muweke wanasheria wenu waicheleweshe adhabu mpk January halafu mjisuke vizuri ndiyo sheria ichukue mkondo wake. Au mkapigane mpunguziwe iwe msimu mmoja kama Roma na itakuwa mnabahati ya mtende kama mtafanikiwa.
    Poleni sana CHELSEA NA UJIO WA UMRI.

    ReplyDelete
  6. Sio darajani tu manu nao wanafata kwa kumuiba mchezaji ktk timu ya norway adhabu ni hiyo hiyo
    mdau
    kisiju pwani.

    ReplyDelete
  7. FIFAS wanachanga. Wachezaji wa mpira wakulipwa hawaibwi bwana. Wao wanaonyeshwa michuzi (samahani mzee wa libeneke) kisha wanafuata. Kwanini FIFA wasiwafungie hao wachezaji kwa kukosa maadili? Kwani Chelsea walimuonyesha huyu mchezaji kisu ili aihame klabu yake? FIFA gere tu kwani hawana hila ya kuzizuia England-based clubs. Chelsea mpango mkali. Kwa taarifa yenu, youth academy ya pale darajani itatuletea wachezaji wengine kibao tu. Wembe ni ule ule.

    ReplyDelete
  8. HAKUNA KANUNI YOYOTE YA FIFA INAYOSEMA HIVYO HUU NI UBABE WA HICHO KIZEE CHA FIFA HAPENDI TIMU KUNUNULIWA NA MATAJIRI NA HAMPENDI KABISA ABRAHMOVICH, KAMA UTAFUATILIA COMMENTS ZAKE JUU YA DARAJANI TOKA INUNULIWE NA ABRAHMOVICH UTAONA HAMPENDI, REAL MADRID HIZO NDO ZAKE LAKINI HATII MGUU PALE, AFTER ALL MPIRA SASA KWA WACHEZAJI NI KAZI SI BURUDANI, NI BURUDANI KWA WATAZAMAJI TU, WACHEZA NI KAZI/CAREER KAMA VILE KARANI WA BANK ANAVYOHAMA BANK MOJA KWENDA BANK INGINE KUFUATA MASLAHI BORA. HIZI KANUNI ZA MIAKA 47 ZA FIFA ZINZFAA KUONDOLEWA, NA HICHI KIBABU KIPO MDA MRAFU SANA HAPO TOKA ENZI ZA AVALANGE AKIWA MAKAMU RAIS WA FIFA HADI AMEKUWA RAIS, ANATAKA AFIE HAPO KITINI ANAFAA KUONDOKA, ANATAKA KUWA AVALANGE ALIYEONDOKA KWA AJILI YA UZEE.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...