Leo kulikuwa na uzinguzi wa kongamono la QUALITY IN THE PROVISION OF TECHNICAL AND VOCATIONAL EDUCATION AND TRAINING nchini ambapo vyuo vyote vilivyo katika kanda ya VETA na NACTE vilikutana MovenPick Royal Palm Hotel jijini Dar ambapo kamera ya mdau iliwanasa waandishi wa habari wakimdadisi Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Ladislaus Komba mara baada ya kufungua kongamano hilo.
Katibu mkuu huyo alieleezea changamoto mbalimbali zinazoikumba sekta ya utalii kutokana na elimu duni wanayopatiwa pindi wawapo vyuoni hali inayowafanya washindwe kudominate soko la ajira katika sekta ya utalii na kuwapa nafasi wageni has kutoka nchini kenya kutawala soko la ajira kutokana na kuwa na ufahamu mkubwa wa lugha zinazotumiwa na watalii hasa kiingereza na mambo mbalimbali.

Komba laiwataka wadau wa kongamano hilo kuhakikisha wanajadiliana kikamilifu jinsi ya kuweza kutatua changamoto mbalimbali zinawakabili wadau wengi wanaoingia kwenye sekta hiyo hivi sasa mara baada ya kumaliza vyuo. Changamoto hizo alizitaja kuwa nia:Huduma kwa wateja, Lugha, na uaminifu
picha ya pamoja baada ya kongamano kuzinduliwa


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. ha ha ha ha ha ha ha ha!!Brother Michu,kulikua na UZINGUZI!Ha ha ha ha ha ha.Hiyo maana yake ni kwamba walikua wanazinguana tu na hakukua na lolote la maana.Kaka naona swaumu imekubana sana mwaka huu.


    Mkulima-Kijijini Gezaulole

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...