
Mapema leo, Afisa Uhusiano wa Multi Choice Tanzania Bi. Furaha Samalu, aliiambia Globu ya Jamii kuwa Kanumba na mastaa wenzie walialikwa kwa muda huo wa saa 24 ndani ya jumba hilo kwa nia ya kuzindua shindano lenyewe. Alisema Kanumba keshamaliza muda wa kuwa huko jana na huenda akarejea leo. Duru za karibu na Kanumba zimethibitisha kwamba keshatua na yuko kwao Temeke anapumzika baada ya kazi ya masaa 24....
Kuwamo kwa Kanumba kwenye jumba la Big Brother kulileta msisimko wa aina yake, hasa kwa wabongo wa ndani na nje ya nchi, wengi wakisema haya na yale kuhusu mbinu za mawasiliano alizokuwa akitumia SupaStaa huyu. Wengi wamemsifu kwa kuweza kuonesha kipaji cha ku-act kama hamnazo wakati yuko fiti ile mbaya, ikizingatiwa kwamba yeye ndiye staa pekee wa filamu aliyepata mwaliko Hollywood na pia London ambako ameshuti filamu za kimataifa itayotoka muda si mrefu ujao.
Bongo tuna historia njema katika Big Brother, ambapo awali mdau Mwisho Mwampamba aliwahi kushika nafasi ya pili katika shindano la ukweli la Big Brother kasha Richard akifanikiwa kuibuka kidedea katika Big Brother Africa na kulamba dola 200,000. Safari hii inasemekana mwakilishi wetu ni mwanadada, lakini jina limehifadhiwa.
Redio mbao zimekuwa zikimtaja Wema Sepetu na mwingine anayejulikana kama Ghandi. Jumapili hii wasichana washiriki wataingia mjengoni na ndipo mwakilishi wetu atajulikana.
THE BRAIN CHILD OF BIG BROTHER - CHANNEL 4 UK - GONNA DO THE LAST ONE NEXT YEAR AND CALL IT A DAY, THEY GONNA NOT DO IT ANYMORE AS MORALLY CORRUPT AND ECONOMICALLY NOT VIABLE AS THIS YEAR THE RATING WENT DOWN THE DRAINAGE AND SPONSORS ARE PULLING OVER. I DON'T KNOW WHAT GONNA HAPPEN DOWN UNDER (SOUTH AFRICA- AFRICA VERSION).
ReplyDeletenawaonea huruma sana hawa wabongo na huyo staa wao Kanumba kwakweli ama kweli nchi ya vipofu chongo watamwita kengeza,hivi kwanza mcheza maigizo toka lini akaitwa mcheza sinema?yaani kazi ipo na cjui kama tutafika sisi au watoto wetu sisi au wajukuu wa wajukuu zetu sisi nchi utasema imelaaniwa bwana kila sekta ubabaishaji dazeni tu mambumbu kila idara ujuaji mwingi mbele giza,na mtamkoma huyo mjamaa huko uswazini ndio maana kuna nchi nyingine kama hizo ninazozijua mm mtu kama huyo sijui ataanzia wapi kujielezea hadi wamuelewe kwa ukweli sio lugha tu namaanisha kilakitu anachokijua yeye kitakuwa kimekaa kiistiafricaafrica tu haswa bongo
ReplyDeleteWataingia mjengoni? hivi wewe misupu mtu wa wapi? hayo ni matusi huku kwetu pwani.... mtu wangu kuwa careful man! u know am saying?
ReplyDeleteWaafrika tunapoiga upuuzi, huwa tunawapita hata hao tunaowaiga. Hivi kwanini nguvu hizi hizi za kuiga upuuzi haziwezi kutumika katika kuiga mambo ya maana?
ReplyDeleteMimi nampongeza sana Kanumba kwa kuichukulia fani ya sinema siriasi na kuinyanua hadi kwa kiwango kilichofikuiwa hapa nchini kwetui kiasi kuwa sasa hivi inatoa ajira sana na huenda itaendelea kutoa ajira kubwa kubwa kadri siku zinavyokwenda kwani baadaye tunaweza kuwa na vyoa vya kujifunza sanaa hii ya maigizoa katika kiwango cha kimataifa. hiyo ni pamoja na fani ya upigaji picha za video. Ila ningemshauri sana ajifunze kiingereza kwa bidii sana kwa sababu sasa hivi ameshafikia ngazi ya kimataifa; inakuwa ni aibu sana kwake anapojikanyagakanyaga kwa kushindwa kuelewa au kwa kutumia kiingereza ambacho kina makosa ya grammar.
ReplyDeleteOYAA NANIHII, RICHARD ALILAMBA DOLA 100,000 NA SIYO 200,000 KAMA ULIVYOLONGA HAPO JUU. PILI, TOKA NISIKIE TETESI KUWA WEMA SEPETU NDO ANAWEZA KUWA MWAKILISHI WA BONGO MJENGONI, MI NASALI SANA ILI ASIWE YEYE (AIBU ALIZOITIA FAMILIA YAKE HAPA HOME, ASIJE WATIA WATANZANIA HUKO BIG BRITHER) PLIIIIIZ MULTI CHOICE. MKIKOMAA NAYE SHAURI YENU MI SIMO.
ReplyDeletemdau chiggs, deslam
ANON SEPT 9, 07:40...u know am saying?...YALE YALEEEE
ReplyDeleteHALAFU NA WEWE 07:29:00 AM ACHA UJINGA. SINEMA UNAONA NDO REALITY??!!! NAYO NI MAIGIZO TU. SOMA KABLA HUJAKOMENTI UPUUZI
mdau chiggs,deslam
ANON SEPT 9, 07:40...u know am saying?...YALE YALEEEE
ReplyDeleteHALAFU NA WEWE 07:29:00 AM ACHA UJINGA. SINEMA UNAONA NDO REALITY??!!! NAYO NI MAIGIZO TU. **@!@**
mdau chiggs,deslam
Mimi binafsi ningemshauri ajitahidi kusoma magazeti ya kingereza, hasa kurasa za michezo ambazo zina coverage za michezo na sinema za kimataifa, pia angalie international news and sports, ili aweze kuwa well informed kwenye maeneo hayo. hii itamsaidia kuwa na ufahamu wa kuweza kujibu waswali yanayohusu field yake. pia mazoezi ya kuongea kingereza na hata akiwe aende sehemu kama british council kujiendeleza. bado hajachelewa na asikate tamaa. unaweza kukosea kingereza watu wakakuelewa lakini unapokuwa ujui mambo amabyo yanakuzunguka watu wanajiuliza huyu anakuwaje star???? watanzania lazima tukubali kukosolewa ili tuweze kujifunza zaidi. kumtetea Kanumba ni kufuga ujinga.
ReplyDeleteHabari za saa hizi,
ReplyDeletekuhusu ushiriki wa Kanumba kusema ukweli haikuwa mbaya ila kwa ushauri tu British Council wanatoa kozi mbali mbali mojawapo ikiwa maalumu kwa ajili ya kuwasiliana ambazo ni kati ya wiki nne mpaka kumi na mbili hivyo nadhani ingekuwa busara kwa bwana Steven Kanumba angeenda japo kupiga msasa ili aweze kuwa na mawasiliano mazuri katika lugha hii ya kigeni. Kuhusu snema za kiswahili wanajitahidi ila kuna mengi ya kujifunza kwa mimi binafsi naweza kusema inabidi waende darasani kujifunza kuanzia editing, acting classes na hata ku-direct a movie. Kwa utaalam wangu kiasi kwa kweli huwa siwezi kuangalia snema hizi mwanzo mpaka mwisho bila ku-forward kwa sababu unakuta kuna scene ambazo hazina maana yoyote kuwekwa kwenye movie au hata kingine ni ku prolong a scene na movie yenyewe naweza kutolea mfano nishawahi kushuhudia snema imetengenezwa(jina kapuni) take ya kwanza ya scene jamaa kashika panga mkono wa kushoto take ya pili kalishika mkono wa kulia na editor bila KUTAZAMA HILI AKAUNGANISHA TAKE HIZI ZIKAWA SCENE MOJA. MAONI YANGU BINAFSI JAMAA WAKUBALI KWENDA KUJIFUNZA PIA WANA MAPUNGUFU KATIKA VISUAL EFFECTS. NI HAYO TU
My advice to Multichoice Tz Ltd. Be very careful when selecting somebody who is going to represent our country so that they do not embarass us as Kanumba has done. There are some issues that are beyond your knowledge, but its obvious that the guy could not speak proper english. I salute you for selecting Sauda Kilumanga many years ago to participate in the famous soap Egoli, she did a great job and we were very very proud of her.
ReplyDeletewanna cheka guys? go to www.kanumba.com then biography...tehe tehe tehe...
ReplyDeleteJamani mimi naona DSTV wamaefanya vizuri Kumpeleka Kanumba lakini tukubali tukatae Kanumba English is not hm kma waliangalia ile siku ya Ufunguzi aliulizwa hiki akajibu kile katika kile chumba kam walitaka Star kwa nini Wasingempeleka Nancy Sumari "Miss World Africa" au Seven Mtangazaji wa MTV au Emal Chris wa Choice Fm ,Kina Bobby Mongi etc etc wako Marepresenter wazuri bongo ambao wao wanaongea Ungenge safi kam walivyochaguaga kina Mwisho,Rich hawakwenda kututia Aibu jamni hii Nchi Cjui ikoje jamani Mngeomba hata Ushauri looh,South Africa walipeka mtangazaji wao wa Channel O sisi si tungepeka mtangazaji bas Furaha naomba umake hatukatai Kanumba ndio ni Actor lakini jueni Bado Kizungu toka Kaole mpk BBA ,Tuwe Serious jamni
ReplyDeleteYaani star wetu mr mithupu star wa nani huyo?nakuunga mko0no mpaka mguu Anony wapili yaani kweli waonee huruma wa TZ na muimba ngonjera wetu Kanumba!Duh!sipati picha eti Star!naye anajiita Celebrity sijui wa busweru usukumani labda!Kuvaa nako zero hata sijui tumuweke ktk fungu gani huyo star wenu!
ReplyDeleteChannel4 UK sio waasisi wa Big Brother.
ReplyDeleteChannel4UK wame- kopi toka kwa waanzilishi yaani waasisi wa Big Brother huko Holland.
Hivyo hata Uingereza pia huchukua mawazo toka nchi zingine.
Mdau
Strasser
kaka michu naomba ukikutana na kanumba mwambie asome maoni ya wanablog, mengi yatamsaidia na ayachukulie positive tu, na asifikiri watu wanamchukia. ajue tayari ameshakuwa mwakilishi wetu na sisi tunakuwa so proud kama tunawakilishwa vizuri. asijione amefika, bado ana kazi, tena si ndogo. na kama ataweza achukue ile part ya clip ya mahajiano aangalie vizuri ni wapi panahitaji improvement, na angalie macelebrity wenzake walivyokuwa wanaongea na walivyojibu maswali. nafikiri fans wa kanumba wa nje ya Tz hata wao watakuwa wameshangaa na kuwa dissappointed. sasa kama wakati wa kujitambulisha kwa house mates, akasema sisi hatukuja hapa kwa sababu wameona tuna hela ila kwa sabau wao ni macelebrity. sasa mimi nikashangaa huyo aliyemdanganya kanumba kuwa ana hela ni nani?? kama kuendesha used car ya japan in utajiri basi watanzania karibia wote ni matajiri.
ReplyDeletekitu kingine, macelebrity wetu hawawezi kuwa international celebrities, ingawa nafasi hiyo wanayo kama hawatabadilika na kujiweka kimataifa zaidi, kuanzia kwenye kazi zao mpaka wao wenyewe. celine dion, angeliq kijo na wengineo walikuwa hawajui kingereza kabisa lakini walijifunza ili wawe global na wakafaulu, wangekaa na vifaransa vyao nani angewajua???? Asante sana wadau.
we kanumba kazi yako kujichubua tu na kujiona uko juu kumbe si lolote si chochote. Embu nenda ukakae darasani usome hasa kiingereza ni aibu. kwanza kuna siku ulikuwa unasema ulisoma chuo kikuu mambo ya sanaa sasa kiingereza gani ulikuwa unatumia huko chuo kikuu??? chhaaaaaa fyaaaa unanichefua kabisa na grama yako. kwaheri kwa ushauri wa kukusaidia zaidi nenda shule
ReplyDeleteMbona PM Japan, Rais Korea, China, Ujerumani, Ufaransa, Vietnam etc etc hawaongei Kiingereza? Acheni utumwa wa kimawazo huo. Mswahili haongei Kiingereza - inakushangaza nini? Colonial mentality.....
ReplyDeletekingereza mayelo!
ReplyDeletehivi tumekosa watu wanaojua lugha zetu mbili (kiswahili na Kiingereza) kwa ufasaha? haya ni matatizo ya kutokwenda shule! angekuwa amesomea SANAA hiyo, nina matumaini lugha isingemsumbua kihivyo
kanumba kutokujua kiingereza sio kosa kwani sio lugha yetu chamsingi sasa kwa kuwa umeanza kujulikana anza kujifunza kiingereza ili upate madili kimataifa south africa wanapendwa sana kwenye movie za hollwood kwa sababu wanasoma pia wanajifunza kiingereza kama umeona maactor wengi wa kisouth wameshatokea kwenye hotel rwanda,blood diamond, na movie mpya inayovuma sasa skin na nyingine nyingi.ni kwa ajili wako competent usirizike mapema
ReplyDeleteHUYU JAMAA (KANUMBA) KATUAIBISHA SANA WA TZ, YAANI KUNA RAFIKI YANGU WA NAIROBI ALINIPIGIA SIMU AKINIAMBIA NIMUANGALIE MTZ MWENZANGU ANAVYOTIA AIBU, KWA KWELI NILITAMANI KUZIMA TV, KWELI KIINGEREZA NI LUGHA TU KAMA NYINGINE, LAKINI KWENYE HADHARA INAYOTUMIA LUGHA HIYO UNAPASWA KUMPELEKA MTU ANAYEIMUDU, NA NDIO MAANA MWL. NYERERE HAKUMCHAGUA MZEE. SHABAN ROBERT KUWA BALOZI WA TANZANIA NJE, INGAWA ALIJUA NI HAZINA KUBWA KWA TAIFA NA KWA WAKATI HUO ALIKUWA MWANAZUONI ANAYEHESHINIKA SANA, KWA HIYO TUSIJIDANGANYE, TUNAPOTAFUTA WAWAKILISHI WETU WA KWENDA NJE NA HASA KWENYE MAZINGIRA AMBAYO LUGHA NDIO KIUNGANISHI KIKUU, BASI LAZIMA TUZINGATIE KIINGEREZA
ReplyDeleteWatanzania kweli tumelogwa, mnataka watu wote tuwe sawa wajinga,wazembe hili sijui nani atatuokoa. Mkiona mtu kanyanyuka kidogo au anaanza kunyanyuka mnamponda kweli kweli, wasanii wamelilia serekali iwasaidie hamna kitu. Kama kweli Wizara ya utamaduni inaona wawakilishi wake nchi za nje hawawakilishi vizuri ni muda muafaka kwa wao kuandaa programu za kuwanoa wawakilishi wa Tanzania kimataifa hata kama hawapati udhamini wa serekali moja kwa moja katika uwakilishi huo wawe basi na chombo cha kusaidia. Kwa mapungufu aliyoonyesha Kanumba ,yeye si wa kulaumiwa na mfumo mzima kuanzia elimu ya msingi hadi sekondari na hata vyuoni pia. Sio sababu ya mnyooshea kidole na kusema sijui lugha hajui mshamba blah blah wasanii wabongo feki wanatuaibisha wewe uliyeaibika umechukua hatua gani ya kuondoa aibu hiyo? Kama kuna mtu anamapenzi mema na nchi yetu mabaya yote na mengine tunayofanya kimakosa ama kwa kujua au kutojua yanahitaji marekebisha na wa kufanya marekebisho hayo ni mimi na wewe na wa serikali yetu tukufu iliyokuwa ngumu kama jiwe.Si vizuri hata kidogo kwa Tanzania kuwa na sifa ya umbumbumbu halafu kuna mtu anawacheka wenziye huko anakobebea boksi akijiona yeye ndio bora.
ReplyDeleteMwenye masikio na asikie na mwenye kutenda na atende.Obama jana kasema ukiona mtoto anakipaji kiendeleze kwa hiyo kama muigizaji wa tamthilia anaonyesha dalili za kuwa mcheza sinema kwanini asipewe msaada na yeye ajisaidie? Kuna shule ngapi za kuendeleza lugha ya kigeni kwa waigizaji mlizofungua nyie wakosoaji wacha kabisa hiyo! Michuzi weka vitu tuendelee kuijenga nchi yetu
Celebrity Kanumba hongera kwa juhudi zako. usiwajali wanaokuponda wao hakuna walichofanikiwa kuionyesha jamii. Lakini sasa hiyo fasheni ya ushungi inatosha na huko nyumbani joto kali, mimi naskushauri wewe bila hata ushungi unaonekana tofauti. WELL DONE BIG BOY!!!!!
ReplyDeleteMY NEM IZ TANZANIA…OOO SORI KANUMBA FROM TANZANIA AFRICA,,YES YES,,,EEEM PEOPLE SEE ME NOT EATEN BIKOZ AM CLOSED(ETI NDO KAFUNGA)..DONT LOOK AT ME VERY(MSINIANGALIE SANA ) COZ AM SHY FROM MY CHILD(TANGU UTOTONI NINA AIBU)…DUUH
ReplyDeleteMisupu usiibane hii...
Ndugu yangu kanumba , hongera kwa yote yaliyokukuta kwa kweli unamoyo mgumu wa pekee
ReplyDeletenatumaini hutarudia tena ...
ha ha ha ha .....chamoto ulikipata kwi kwi kwi kwi kwi kwi uwiiiiiii
kan`gaaaaaaaa!!!!!!!!
michu usinibanie hii comment !!pls
heri kumjua .....bwana...roho huamka aniita..anitambua mali yakeee...yeye ni.....tumtukuzee...! haya itikieni sasa acheni ushamba wa kumtukuza kanumba...hovyooooo
ReplyDeletehukiwa makini unaweza ukaona tofauti ni kidogo sana kati KANUMBA na KAYUMBA.....si mnakumbuka mambo ya HAKI ELIMU
ReplyDeleteDammmmmn dis niga aint say even ONE english word.
ReplyDeleteMbaya zaidi ni MUHAYA. hahah mashauzi kwishneyyy.
Kacheza movie au documentary?
ReplyDeletejamani nilipotembela wesite yakanumba nilitamani kulia, yaani english utafikiri ameandika mtoto primary, my goodness yaani ni ametranslate from swahili tu english, nadhani angeandika kwa kiswahili ingependeza ziaidi, jamani wabongo shule ni muhumu sana hebu tubadilikeni watu tunapenda kuwa masuperstaa wakati lugha hazipandi kabisa
ReplyDeleteMWANDISHI WA HABARI: KANUMBA WHY ARE YOU NOT EATING?
ReplyDeleteKANUMBA: I MA CLOSING BECAUSE I AM A MUSLIM
MUANDISHI WA HABARI: WHAT IS LEVEL OF YOUR EDUCATION:
KANUMBA: I PUPLIED IN SHINYANGA PRIMARY SCHOOL.
Mdau wa "www.kanumba.com" Thanxs. Ujust made my evening, ahahahahaha!!! Pips check out that site yani Kanumba ana freestyle tu NGENGE mbofumbofu!
ReplyDeletesasa natumaini kanumba umeona mwenyewe what fans think of you. now go back learn japo kiinglishi tu.... hii itakutowa mkuu wangu. sifa za kucheka tu na yes yes nyingi bila kelewa nini unambiwa au unasema si u-super star huo.... just simple go learn either einglishi, french or spanish...
ReplyDeleteWEWE,uliyesema kanumba muhaya ukome,toto la kihaya linajua english toka liko tumboni,yaani kabla ajazaliwa english inapanda
ReplyDeleteMi naona angeongea lugha anayoijua halafu wangempa mkarimani tu...mambo ya kutaka kuzungumza lugha ya watu tena usiyoijua vizuri...ni ngumu sana....Ze Ze zinakuwa nyingi wakati unatafakari maneno ya kuongea....
ReplyDeletekwi kwi kwiiii.....
Mimi na issue moja nataka niongelee...Hivi Kanumba anajua maana ya pink t-shirt? anatoa zawadi ya pink t-shirt kwa mwanaume??? yeye ni mwana sanaa, anafaa ajue cilture mbalimbali duniani.
ReplyDeleteHuku kwa wenzetu ukitinga na pink lazma wakucheki. and its everywhere all over the world.
A color pink is for little gals and ladies. thats why u see barbie is in pink.
kama mlikuwa makini, angalieni Kanumba alivyotoa ile zawadi ya t-shirt nyekundu hlf participants walivyocheka...we have our own culture bt we should try learn other people's culture.
Big up Kanumba...i dnt care much about about language either u knw english or not. wangapi hawajui english and are still superstars na hamna anayemcheka??? especially soccer players.
But naomba uingie tu school, au ukialikwa sehemu ujitayarishe. kama kusoma culture za watu wa hiyo sehemu, huna haja ya kuongea English, chapa kiswahili tu au watafute mtu to translate.
Binafsi siku zote naomba tupate mtu imara atangaze lugha yetu. Wakenya watatuibia...
kuna mtu ana link ya video ya hiyo interview? am curious to see it.. I know the guy is arrogant but lacking the basics
ReplyDeletemtalii koko karudi baada ya kuitangaza saaana nchi manake alikuwa anaongea na kushinda woote mle ndani ati celebrity nakuomba tu kwa sasa usione aibu kujiunga na kozi ili ujue mawili matatu elimu haina cha mkubwa wala mtoto elimika ndo uuze sura vizuri mbu mbu mmoja wakati up stairs siro!!!!
ReplyDeleteHivi wadau nyoote mnaomponda kinumba eti hajui english hamjui kama ni lugha ya wazungu?wewe mwenyewe unayejiona wamaana kwa kingereza naomba utembelee London au USA au nchi nyingine ya kingereza utaonekana wa bure tuuu,,sasa hapa kuna mabwege wanamponda mwenzao kanumba kipindi wenyewe hapa kiswahili chenyewe bado kinawasumbua kuandika!angalieni kama huyu mtu wa sep 09,08:16:00 anaponda wenzake tu eti wesite nini hii?,,ziaidi ni hii? muhumu ni hii?Dharau wengine ukijianzia,mimi najua nyoooote mnaomponda jamaa steve hamwezi kuongea english sahihi, atakae jua kati haya maneno aniambie.samahani michuzi usnikwangue!
ReplyDeletekaka,,michu,,,naoana wadau wamechachamaaa kumponda kanumba,,,mimi sipo upande wowote ule,,,ila maoni yangu ni kwamba kama ungeweza kutusaidia tukapata,,iyo clip ya kanumba japo ya dakika tano ndani ya ilo jumba,,,hapo tutajua ilo jambo lina umuhimu gani,,,eithee tumewakilishwa ama tume aibishwa,,,,Mdau ukerewe
ReplyDeleteTough guys wear pink! Acha porojo wewe Annon hapo juu.
ReplyDeleteKanumba Usione aibu wengi English kwishney ndio maana kuna English courses. C hata Mke wa Raisi na Lady Jay Dee walienda ili angalau hata cha kuombea maji wawe wanajua.
Kuna Mtanzania kanikuna kiukweli Dada Furaha wa DSTV umechemsha kiukweli hatukatai kam kanumba ni Actor ila kama mlitka Celebrity Mngechagua kina Chris wa Choice Fm,Penny wa XTREM Channel ten,Ruben Ndege wa Clouds FM,Seven wa MTV,Jokate ,Nancy Sumari ingekuwa vyema kumtangaza Miss Africa from TZ ,Please You Guyz muwe serious jamani kama ni macelebrity hata South wanajau and dat why TZ hatusongi tunapenda mbebesha mtu Mzigo asiouweza Furaha please wear Tabasamu Ngongoseke Shoes Pliiiz maana una boil tuu naona Shelukindo mshauri mdada huyo si mngewaconsult kina Kevin Twissa jamani
ReplyDeleteJAMANI WASWAHILI ACHENI WIVU. KUONGEA ENGLISH SIO LAZIMA, NA HAIMAANISHI MTU HANA ELIMU YA KUTOSHA. MTAKUFA NA WIVU WENU!!!!!
ReplyDeleteKANUMBA, USISIKILIZE YA WATU.KEEP IT GOING!! YOU CAN DO IT!!
Cheers,
mdau, canada.