Mwenyekiti wa Chama Cha Netiboli Tanzania (CHANETA) Mama Anna Bayi akiongea na wanahabari na kutangaza kuachia bodi kwa katibu mkuu wake Anna Kibira leo. Hakutoa sababu za kungátuka kwa Kibira zaidi ya kusema kwamba kapokea barua isiyoeleza sababu toka kwa veterani huyo kwamba anaachia bodi. Juhudi za kumpata Anna Kibira kuelezea kilichosibu zimegonga mwamba.

taratibu chaneta, pesa si msingi wa maendeleo ... bado mnahitaji busara na kujitolea kwa maveterani kama anna kibira.
ReplyDeleteHili ni pigo kubwa sana katika maendeleo ya netiboli Tanzania. Itakuwa ni busara kwa Mama Bayi pia kuachia ngazi ili kutoa nafasi kwa mabadiliko ya msingi ndani ya Chaneta kuchukuwa mkondo wake.
ReplyDeletemimi si mpenzi wa netball lakini tangu niko mtoto namsikia anna kibira kwenye netball hadi nikawa nadhani ndie rais wa TFF yao muhimu kuwaenzi waasisi wanapokosea waonywe maana ni hazina
ReplyDeletenadhani ni wakati sasa BMT wakawa na meno ya kutosha kukabiliana na matukio kama haya ya kufukuzana ovyo...tunajua chanzo nini sisi tulio katika sports admin ila wananchi wengi hawajui...lasivyo ndoto za Tanzania kuwa nchi ya michezo haitakuwepo...mama kibira si ulipue tu jamii ikusafishe maana naona kama wewe ndio unaonekana mbaya vile!!
ReplyDeleteNaona kama ufisadi unanyemelea hata netiboli, mama Kibira yupo ktk netiboli siku nyingi toka wakati ule hakuna hata senti yeye amehangaika nayo, sasa neema inakaribia naona mafisadi udenda unawatoka wanaamua kumwondoa. Nadhani hawakumtendea haki. Hata BMT tayari wamewashangaa akina Mama Bayi!!!!
ReplyDelete