Kaka Michuzi heshima yako, ulifanyalo haina haja ya kukomenti, upojuu, kazi yako ipo juu. Nna ombi kaka nirushie hii mdau wako.
Mie nilikuwa nafanya kazi kampuni fulani kama IT Expert wao ila sasa nimeacha kazi najifanyia mambo yangu mwenyewe. Nawatangazia wote wenye kuhitaji kuwa na website (tovuti) basi nitawafanyia kwa bei chee kabisa.
Mtu akilipa Tsh 199,000/= (laki na tisini na tisa elfu) tu, basi mi namtengenezea static website ya
kisasa kabisa na yeye ataikubali. Kwa ela yake hiyohiyo namsajiliajina (domain registration) na kumwekea tovuti yake hewani (hosting)kwa miezi 6 bure kabisa.
Yeyote mwenye kutaka website ya kampuni au ya binafsi asisitekuwasiliana nami kwa email yangu.
Kazi njema mkuu wa wilaya.
Email:
jisajili@gmail.com

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. Habari,
    Mimi ni designer kama wewe na nina website yangu ambayo ipo tayari, kwakuwa narudi Uni...sitokuwa na muda sasa nakupa tender, swali unaweza uka redesign website nzima? je mfano wa kazi zako ziko wapi? Nioneshe kazi zako na tenda ni yako. Thanx

    ReplyDelete
  2. tuonyeshe kazi zako kwanza.....

    ReplyDelete
  3. kaka biashara sio maneno,kama wewe ni mtaalamu ungetujulisha haya kwa kuwa na simple website,lakini naona kaka unachonga zaidi,website ya Tsh 200000, miminatia shaka uwezo weko.Tunaomba utupe reference ya kazi zako.

    ReplyDelete
  4. NILIJUA TU KUNA MTU ATAULIZA SWALI KAMA HILO!!!!!

    NI KWELI UKITANGAZA BIASHARA YA WEBSITE LAZIMA UWE NA MFANO WATU WARIDHIKE!!!

    KWA KWA KWA

    ReplyDelete
  5. swali hili lako bwana michuzi,
    mimi nataka kublog nifanyeje?
    lazima niende darasani? wapi?
    au nikishafungua blog ni mswano tu? na nani anaweza kunifungulia? nifanyeje?
    please naomba nijibu najuwa watafaidika wengi kama mimi.

    ReplyDelete
  6. Unayeulizia kuhusu blog...kuwa nayo ni free na unaweza kufungua kwa wakati wowote ili mradi unajua unachotaka kublog....

    Kublog ni fun lakini sio easy. The hard part inakuja pale unapotafuta watu wakusoma blog yako na jinsi ya kuwakeep wale watu wawe wanarudi kuja kusoma kila siku. Zipo blog nyingi sana tu na kila siku zinaanza mpya lakini hazikai au waandishi wanakata tamaa au kuishiwa nguvu/hamu ya kuandika kitu kwenye blog yao hata mara moja kwa week.

    Blog hosts za kuandika na kuweka picha ninazozijua ni www.blogger.com, www.LiveJournal.com, www.typepad.com na www.wordpress.com. Free blog ya kuongea ninayoijua ni www.podcast.com na free video blogging ninayoijua ni www.vidilife.com

    Lakini kama wewe ni beginner ningekushauri uende na blogger.com ni user friendly, easy to edit and maneuver around.

    nadhani hii takusaidi na nadhani kuna wengine wenye maelezo zaidi wataongezea

    MMB

    ReplyDelete
  7. MMB Shukran sana Mungu kujaze heri. Amin.

    ReplyDelete
  8. jisajili@gmail.comSeptember 14, 2009

    Nashukuru sana kwa maoni yenu.
    Naweza kuredesign haina shaka
    Wewe wa blog nitumie email tu nitakufungulia blog bure tu usijali, pia nitakuelekeza online jinsi ya kuiendesha.

    KWA WOTE
    Kazi ninazo, nyingi sana, ila MKATABA WA KAMPUNI NILIYOFANYIA KAZI HIZO ZOTE UNAKATAZA MIMI KUJINADI/KUDAI/KUCLAIM KUWA NI KAZI ZANGU BINAFSI, KWA HIYO ZOTE ZINABAKI NA LEBO YA KAMPUNI. WANAOFAHAMU MIKATABA YA KAZI WANAJUA HILO. Kama una imani nami leta kazi yako kama huna basi usiwe na hofu. Kuhusu bei ni ndogo kweli kwa vile nna muda wa kutosha, sifanyi kwa nguvu nafanya kwa kujinafasi tu.
    Ahsanteni sana
    Jisajili@gmail.com

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...