Nafasi za kazi Kampuni ya Usafi inatafuta watu wa kufanya kazi za usafi maofisini na mazingira kwa nje ( wanaume kwa wanawake),Wenye uzoefu au waliosomea watume CV zao kwenye e mail:
au wapige simu no:
0754 80 88 40
kwa maelezo zaidi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Yaani hata kufagia wanataka CV, dah bongo ufisadi kweli...

    ReplyDelete
  2. hata kufagia au kupiga deki lazima uwe na CV! makubwaaa! sasa hebu fafanua muombaji hiiyo kazi anatakiwa awe amesomea fani gani ili aweze kupata nafasi hiyo?

    ReplyDelete
  3. Wanaoshangaa kuhitajika CV yawezekana ni wale wanaopata kazi kwa kujuana.
    Kabla ya kufanya kazi yoyote ile lazima upate mafunzo ya kazi husika. Mathalani usafi wa mahotelini unahusisha kupata mafunzo ya housekeeping. Kwa usafi wa nje yawezekana kukawa na mafunzo ya kuendesha malori ya taka, mitambo ya kufagilia barabara, usalama kazini nk. Bila kuona CV yako watajuaje kama ama una ujuzi unaotakiwa au unafundishika??? Isitoshe kuna swali juu ya uaminifu. References hupatikana kupitia CV. Ni kawaida kwa references kupatikana kupitia CV.

    ReplyDelete
  4. NYIE MNASHANGAA NINI??. HUKU MAMTONI KAZI YOYOTE BILA CV HUPATI. CLEANERS, LEAFLET DISTRIBUTORS, MAIL SORTERS, KITCHEN PORTERS, RECYCLING OPERATIVES, PARK KEEPERS, DELIVERY ASSISTANT, DRIVER'S MATE, WAREHOUSE OPERATIVES, ORDER PICKERS, PACKERS, HOTEL FRONT OF HOUSE ETC ZOTE MNAWEZA KUZIONA NI KAZI ZA KISHENZI KWA BONGO LAKINI AMIN NAKWAMBIA MAMTONI BILA CV YA KUELEWEKA UTAPIGWA CHINI KWANZA COMPETITION NI KUBWA SANA SANA KUPATA KAZI HIZI, KWENYE INTERVIEW MNABANANA NA WAZUNGU BWERERE. HIZI NDO BOX LENYEWE MNALOLISIKIA NA UKILIPATA KAMA WAREHOUSE OPERATIVE UKAPATA MASAA 50 KWA WIKI BASI WE UJUE KIMSHAHARA MKUU WA WILAYA BONGO HAKUPATI. HILO TANGAZO LIKO SAHIHI SANA NA LIMEKAA KIMAMTOMTONI.LIMEKWENDA SHULE. NDO KAZI ZETU UGHAIBUNI HIZO, NDO BOX LENYEWE HILO NYIE MKITUONA TUNATUA BONGO AIRPORT TUMEIVA KAMA LUDACRIS AU BEYONCE MJUE HIZO NDO KAZI TUNAZOKAMUA HUKU. NDO ZINATUWEKA MJINI UGHAIBUNI HIZO TENA UNAWEKA PESA KWENYE SIMU KABISA ILI KUPIGA KUOMBA KAZI HIZO NA ZINAPATIKANA KWA MBINDE VILEVILE!!! WE NJOO TU HUKU UJIONEE LIBENEKE LA BOX LILIVYO MWANANGU. SEMA UKILIPATIA FRESH NDO VILE UKITUA BONGO UNAONEKANA KAMA MDOGO WAKE OBAMA VILE KWA JINSI UNAVYOKUWA UMEKWIVA NA KWA BONGO WAWEZA KWENDA KIWANJA CHOCHOTE SI MAMBO YA DOLALI BWANA? HATA UKIMTAKA MTOTO MKALI KWA BONGO KAMA NANCY SUMARI UNAMPATA TU UNAMDANGANYADANGANYA WEEEE MZEE KITU NA BOKSI AU HATA JOKATE MWEGELO SI NDO MASUPASTAA WENU HUKO NYIE INAKUWA NGUMU KUWAPATA LAKINI MIE NIKIPIGA DEKI HUKU MWAKA NIKIDONDOKA HAPO BONGO AKINIONA NILIVYOKWIVA NIKAMWAMBIA NATOKA ZANGU ATLANTA NIPO BONGO LIKIZO DOLALI NYINGI MTOTO HARUKI MZEE NAJINYOSHA TU KA SIO MIMI MPIGA DEKI VILE.
    KWAHIYO HILO TANGAZO HALINA TATIZO LOLOTE LIKO MWAKE LIMETULIA NA LINA AKILI NI KAMA MATANGAZO YA BOX HUKU YALIVYO.
    AHSANTENI.
    Mkosa kazi, ATL, GA USA.

    ReplyDelete
  5. Bongo imeshabadilika sana siyo kama ya "enzi za Mwalimu", sasa hivi hata kama ni kufyeka nyasi CV na interview ni muhimu, na Kampuni zingine tracing ya criminal records inafanywa hasa hizi kampuni za kigeni tatizo ni kwa wanaodhani kuna kazi inapatikana kirahisi siku hizi, labda zile za kupitishana milango ya nyuma (kujuana) na zenyewe siku ni chache sana. Hilo tangazo liko sawa mno. zile zama za mimi form four/six au nina degree haisaidii ni lazima usotee kazi haziji hivihivi tu eti kwa vile una ka digrii kako, wa hivyo ni wengi tu hapa bongo.

    ReplyDelete
  6. nafikiri mmetafsiri vinginevyo. Kinachotakiwa hapa ni maelezo binafsi ya mwombaji na ujumbe umejieleza aliyesomea au mwenye uzoefu. Sidhani kama unaweza ukampa mtu kazi bila kuwa na maelezo yake binafsi, contact yake na wadhamini.kampuni itamjuaje kama hatajitambulisha.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...