Shoto ni mcheza filamu nyota steven kanumba alipokutana na mwanaharakati wa mambo ya jamii john mashaka hivi karibuni. wadau hawa wana jambo moja linalotaka kufanana. mmoja hushambuliwa sana anapotumia kiinglishi katika maandiko yake, na mwingine anasakamwa kwa kinachodaiwa kutoongea kiinglishi vyema.
raha yake ni kwamba ni hao hao wanaobeza mashaka kuandika kiingereza ndio wanaombeza kanumba kwa kutoongea kiingereza kwa jinsi na namna wanavyotaka wao.
sasa haijulikani wamatumbi wanataka nini haswa, maana hawana dogo, hawana jema, hawana zuri, wao kila kitu kwao ni kusagia tu. Ni nani atayebisha kwamba kwa Bongo kiinglishi ni janga la taifa na hata vigogo huchapia?
Globu ya Jamii haina kawaida ya kuingilia mijadala labda hadi pale inapobidi saaaaaana kama wakati huu ambapo maskini Kanumba anapigwa mande na karibu kila mdau. Kwa kweli inakatisha tamaa na hata haijulikani wamatumbi wana roho gani toba yaillahi! Inakera. Inaudhi. Inakatisha tamaa, hasa ukizingatia kwamba wengi wa wakosoaji ni weupe katika kiinglishi kama mie hapa anko nanihii. Acheni hizo wadau husika! Bongo itakuwa ngumu kujengeka kwa mtimanyongo wa aina hiyo!
Ukitaka kumuona na kumsikia Kanumba akiwa Big Brother Africa IV:
BOFYA HAPA
-Michuzi
NIKUTO KUJUA (IGNORANCE) KINGEREZA NI LUGHA TU KAMA KIBENA, KIHAYA AU KIHA. MBONA WATU WANACHAPIA KISWAHILI CHENYEWE NA LOCAL LANGUAGE HATUONGEI? ACHENI ULIMBUKENI WABONGO.HAO WAZUNGU KISWAHILI WANACHAPIA TUKICHPIA KIZUNGU WABONGO MNAMIND. ULIMBUKEN TU. KANUMBA NA MASHAKA KAZENI BUTI WACHA WASEME AS LONG UNAFIKISHA MSG.
ReplyDeleteNa wewe bwana michuzi "as a matter of principle" endelea kutoyaingilia haya ya wadau, kama ukiamua kujiita "mlesabriti/mselabriti" basi "uselabriti" una bei yake, na hii ndiyo bei ya "ulesabriti"
ReplyDeleteViwango mwanangu
well said michuzi!!!!
ReplyDeleteMh Michuzi unachanganya mambo. Mashaka ana-address Kiswahili audience kwa Kiinglish - which is inappropriate. Kanumba ana-address Kiinglish audience kwa kutumia Kiinglish kilichotafsiriwa moja kwa moja toka Kiswahili - which is not appropriate either.
ReplyDeleteDah!Ka Kanumba hicho kilemba basi sasa!pia naomba receipt ya kiatu chako kimeniacha hoi!chapatikana duka gani au online nini?special order teh teh teh!!!!!!
ReplyDeleteWanaita Low self-esteem, insecurity kwa pande zote mbili.Wanaotumia english kujiboost waonekane wako juu (status-wise)na wanaoshindwa kuongea english wanatumia udhaifu wao kupiga madongo.
ReplyDeleteIm different I take pride speaking my Swahili language.Lugha ya mababu zetu.Hakuna aliyesema kwamba dunia nzima lazima tuongee kienglish.Lugha zote ni sawa mbele ya mwenyezi Mungu.Lugha zote ni laana.Biblia inasema kuna watu walitaka kujenga Mnara ufike mbinguni.Mungu na malaika wakaja kuwapiga laana wanadamu wakaanza kuongea lugha tofauti.Mpaka leo kuna lugha mbalimbali duniani.
In serious note.Huwezi tumia lugha moja kufikisha ujumbe angali watu unaowapa ujumbe hawaielewi lugha hiyo.
Waafrika wengi wana mtazamo finyu juu ya lugha ya kiingereza. Wengi wanafikiri kwamba kuongea lugha ya kiingereza kuna onyesha jinsi gani mtu alivyo elimika. Kiingereza ni lugha kama lugha nyingine tu (kifaransa,kirusi,kijapani). Nafikiri tatizo letu sisi watanzania ni kwamba lugha ya kiingereza imetawala sana kwenye mashule, ndiyo maana vijana wengi wanafikiri elimu ni kujua lugha.Tatizo lingine ni mfumo wetu wa elimu, tungeweza kabisa kufundisha masomo yote mashuleni kwa kutumia lugha ya kiswahili. Watu wanao kwenda kusoma inje ya nchi, mfano urusi, wanatakiwa kujifudisha lugha ya kirusi kabla ya kuanza masomo.Ukweli ni kwamba umasikini tulionao unatufanya tuwe watumwa wa akili.
ReplyDeleteNafikiri sasa ni zamu ya WEMA SEPETU kuchekelea.. although inasikitisha kwao wote!!
ReplyDeleteNgoma draw:
ReplyDeleteWEMA 1 : KANUMBA 1
Sasa na wewe brother Michuzi unakuwa kama hujakaa Bongo, kwani hutujui wabongo?
ReplyDeleteWabongo hatujui nini tunachotaka. Ukiwa mtaaramu sana wa kitu wewe bitozi, unajifanya unajua, wewe ni machi nowa na dunia itakuumbua.
Na kama hujui kitu, hata kiingilishi (ambacho ni lugha tu kama lugha nyingine, tofauti yake inaongewa na watu wengi); basi wewe ni mjinga, shule hujaenda, huna maana na unaaibisha taifa.
Kwahiyo, wabongo tunaosha tu vinywa......Na guess what??? maendeleo tuyasahau!!!
Watanzania tunatakiwa kusaidia katika kukuza lugha ya kigeni sio kukosoana. Lugha hii kwa watanzania ni ya kujifunza sio lugha mama. Hakuna aliye perfect kwani kuna watu wamekaa nje ya nchi hususan Marekani kwa zaidi ya miaka 30 lakini hata wajitahidi vipi kuongea lafudhi ipo pale pale utajua huyu ni wa kuja. Swala la msingi sio kumcheka au kumbeza mtu asiye flow kiingereza badala yake tumtafute na kumsaidia.
ReplyDeleteNajua Star huwa hapendwi, ila uzuri ni hapendwi na wachache wenye roho ya kwanini, wengi wanampenda kwani anawaburudisha nyoyo zao.
Kanumba you need to prove people that they are wrong, jipige tuition za nguvu hasa katika kuongea I wish I was near you ningekupiga msasa wa nguvu na baada ya miezi 6 utakuwa unaongea kama mmarekani. Usijisikie vibaya kwa jinsi watu wanavyokubeza kwani hiyo lugha kwa watanzania wote tumejifunza ukubwani hatujazaliwa nayo, hivyo hakuna mtu yeyote wa kujidai kwamba naflow kiingereza. wengi wanaokubeza ni "malimbukeni" wamesoma lakini hawajaelimika!
Mdau USA
ANKO MICHUZI ACHA KUTUHUKUMU KWA BAADHI YA WADAU AMBAO WALIOCOMENT HOJA ZAO NA VILE U-SUPER STAR HAUJI HIVIHIVI MPAKA MTU AUMIE KIDOGO AU SANA, KWA HIYO TAKE IT EASY GUY.UNAAMBIWA UKUBWA JARARA KILA BAYA UTUPIWA ILA KUMBUKA MAISHA YANAENDELEA WA-TZ WENGI WALIOSOMEA ENZI ZA KANUMBA ZE ENGLISH 50-60% LABDA UWE UMEKAA KIDOGO EUROP
ReplyDeleteDawa yao uwaendee TUITION ya maimuma kisiri siri, then siku moja uwashtukize kwenye vipindi vya EATV ukilonga SLANG na big man SSEBO... Hapo ndo watajua kumbe Kanumba ni GREAT kweli!
ReplyDeleteMichuzi, inategemea na icho kiingereza unakitumia wapi. Sasa wewe unaandika makala unawalenga wananchi wasio na uelewa mkubwa wa kiingereza bado unataka kutumia kiingereza kigumu kweli ujumbe utafika kwa walengwa? Tukubaliane kuwa kwenye jumba la BBA lugha inayotumika ni kiingereza sasa unapokwenda pale na hujui kiingereza unategemea nini?
ReplyDeleteAnko nanihii nimeangalia mtiririko mzima wa habari za Kanumba nimeona unatabia ya "Kung'ata" na "Kupuliza". Eti "Bwana Kanumba anything to say?". Noma hiyo anko nanihii...
ReplyDeleteUkiibania comment yangu shwari tu, ila habari ndo hiyo.
Samweli
Honesty! MImi siwajui hawa wote na sijui yaliyotokea huko nyuma mpaka ifikie hatua ya kusemwa yote hata....Ila baada ya kusoma hii passage yako nimekwenda kusikiliza huyu mtu anaongea nini lakini maoni yangu ni kuwa.
ReplyDeleteI think all of them they need to spend their money to hire a therapist. Faida ya kuwa kwenye public eyes ndio hiyo. Unahitaji kuwa na steel iron heart or a thick skin.
That is a very small price to pay..."KUSEMWA" ...Wajiulize macelebrities wa USA wanatembea na mabody guard wa nini? Wao hawaogopwi kusemwa tu bali hata wakati mwingine wanaogopa mkong'to.....Kusemwa jambo dogo sana....kwanza most of the celebrities they don't give a shit mtu akiwasema...kwanza wanafurahia kwavile ni two more minutes of publicist there...and the free publicist one....
Kwani wao hawaoni macelebrity wa USA wanavyosema nao? Imetokea hawa wanasemwa kwa "LUGHA" lakini hiyo ni just a patch lakini kona ya yote ni KUSEMWA TU kwa vile wao ni public figures.
Wameshaingia kwenye public life (STAR). Hizo ndio consequences zake na inatakiwa sasa hivi kuwe na career nyingi sana ...hawa macelebrieies badala ya kuweka sympathies zao hadharani wanatakiwa kwenda kuwaona specialist wakuwasaidia how to deal with this. Halafu wakiappear hadharani wanakua na smiling face kama vile hamna lilotokea.
Sioni sababu ya kuweka hii iwe big issue au imlaze mtu macho wazi....They should take it as a challenge and go on with their lives.
Kwanza watu wakiwaona wanalia lia ndio watajua weakness zao ziko wapi na kuzidi kuwakanyaga.
Hapa macelebrity kila siku gossip za ukweli na uongo zipo mitaani lakini hamna hata mmoja anaita press release.
Waache kulia lia kama watoto ...AS I SAID that is the very little price to pay when you are a celebrity.
PUBLIC LIFE is good but tough NA SIO KUWA HII NI TABIA YA WABONGO TU ...kila mahali ni hivyo hivyo....kwanini haya magazeti ya umbea hapa USA yapo kila kona na yanauzwa sana tu au kwa vile yameandikwa kwa kidhungu...it is all the same guys just in the style.....na different culture ndio maana umbeya unakua wa tofauti...photoshop kila siku wanawafanya watu wanenene sana au wembamaba sana na kuwasema.... ...sasa sie kwetu unenene au wembamba sio funny hivyo twaweka mambo mengine kam LUGHA kupata porojo....
I hope hutaibania manake na wewe una roho ya plastic ukisha stick na rafiki zako hutaki watu waongee other way around or what they think it should be done......
Just take it easy guy.....Hayo ndio maisha....
sawa uncle nanihii tunakuelewa sana unapomtetea huyo kanumba.na pia hatukatai kuwa english ni janga la taifa ila inapokuja suala la mtu kuteuliwa kwaajili ya kuiwakilisha nchi yapaswa kuteua mtu ambae ataweza kusimama na kuzungumza kwa ufasaha ikiwa ni pamoja na kujenga jina la nchi,sasa anapoteuliwa mshiriki ambae hawezi hata kuelezea nchi yake au kuwasiliana na wenzie inatia aibu sana si kwake yeye pekee bali kwa nchi nzima kwa ujumla.we unafikiri waliokuwa na kanumba jumbani wameitafsiri vipi nchi yetu?mbona mwisho na richard watu hawakukebehi kiasi hiki?tatizo bongo mnapenda kubebana hata katika masuala ya kinchi mnataka muweke watu wenu.so hata umtetee huyo kanumba haitasaidia maana aibu imeingia kilichopo ni kujirekebisha next time mchague watu watakao leta sifa ndani ya nchi.msituletee hapa.mnafanya madudu alafu mnajitetea eti english ni janga la taifa,unatuuzi na wewe michuzi.usinibanie mawazo yangu hata kama ni blog yako.
ReplyDeletemdau scandinavia.
Ngano ya 'safari na punda' mdogo ni mfano uonyeshao kuwa binadamu huwezi kumridhisha.
ReplyDeleteBaba alikuwa safarini na mwana wakitembea na punda wao, watu wakasema badala ya kupanda punda wapekua tu.
Wakaona wapeane zamu kupanda punda. Wakapita kijiji cha kwanza baba akiwa kapanda mtoto anatembea, wakasema baba mkatili huyu apanda punda na mwanae apekua juani.
Baba akamuwachia mtoto apande yeye atembee, watu wakasema mtoto ana laana apanda punda wakati babake apekua juani. Wengine, baba mjinga atembea wakati punda hajasheheni.
Wakaona wote wapande punda, watu wakasema mijitu isisyo huruma yaani watu wawili kupanda punda mmoja mdogo mpaka asota. wakaona wambebe punda watu wakasema badala ya punda kubeba abebwa.
Baba na mwana wakaona wasisikie la mtu maana maneno na ushauri havikuwa na faida wala muafaka wala mwongozo.
Watu kila siku wako upande wa hasi.
Teh teh teh teh!!!Michu nawewe bwana unakuza tu mambo,unataka hii kitu endelee kuwa Ligi.Dogo nashangaa kawa mpole,ina maana hajui wapo wanaomkubali na wanaomkataa?yeyeachukulie tu km challenges asimind wala nini,mbona mwenzie Vicent Kigosi kapondwa sana alivyojiita the most great na akabadilisha na kuwa sahihi the greatest?Huyo dogo alitakiwa afurahi tu tena angecheka sanaaa kwani wabono tumejaaliwa kuongea so haa akijitiamnyonge hapo wataendelea kuponda tu.Mbali na hivyo si alionaga raha mis wetu 'Kind Sepetu' alivyouzaga magazeti alivyompelekaga ndani,sasa hiyo ndio malipo yake kaka,hebu onja kidogo nawewe inakuwaje kuongelewa vibaya midomoni mwa watu.Teh teh teh teh!!Ukinipiga ya mbavu Michuzi sitakuachia na wewe,nitaanzisha topic tudiscuss Ule MTV wako km mtungi ulioturekodia Rais alivyoongea na wananchi!!!
ReplyDeleteNa wewe anko nanihii huwa unachapia hata hicho kiswahili kama hapo acheni - umeweka cheni, na hAusika sijui ulikuwa unamaanisha nini, kwa kifupi LUGHA NI JANGA LA TAIFA KWA UJUMLA.
ReplyDeleteMgwadu.
kaka na wewe unaanza kuchemka sasa!! umeshindwa kujua kuwa hadhira kubwa ya mashaka ni waongeaji wa kiswahili, watanzania tunaongea kiswahili na ndio maana wengi humpinga mashaka anapotumia kiigereza tena kile cha kwenye kamusi. Hii ni tofauti na kesi ya Kanumba ambaye yeye hadhira yake siku ile ndani ya bigbrother ilikuwa ni afrika nzima na si kenya na tanzania peke yake. lugha inayotumiwa bigbrother ni kiingereza so kanumba hakuwa na jinsi zaidi ya kutumia kiingereza kilichonyooka. so usimtetee alichemsha!!! na wewe pia unataka kuchemsha. haya bwana saidianeni kuchemsha
ReplyDeleteWapi wabeba box wajibu swali hili? Michuzi for precidency!!!!
ReplyDeleteMichuzi umemkejeli jamaa Eti -ANY THING TO SAY!! kwahiyo ulikuwa una mdeshi kama kinapanda.Any way zote ni lugha tu,kinachotakiwa ni kufikisha message tu.J mashaka anaandika kiingeleza kama NGUNGI WATHIONGI(kigumu).Kanumba hiyo ni challange tu,ambayo unatakiwa kuifanyia kazi.Kweli hakipandi lakini bado unanafasi kubwa ya kusawazisha ili uwe international figure.
ReplyDeletemkataa wengi mchawi!!
ReplyDeleteweka hiyo clip ya interview yake basi sio kutetea pumba tu
ushakula rushwa kumsafisha kayumba eeh. kanumba kama unataka kukubalika nenda inglishi coz
ReplyDeleteMICHUZI UMETOA POINT NZURI SANA NA MFANO MZURI SANA HAKUNA.NAONA UMEWANASA KWAMBA KUNA WADAU WENGI HUMU WANAFIKI WAKUBWA MNO.JOHN MASHAKA ANASHAMBULIWA KUONGEA ENGLISH HUKU KANUMBA ANASHAMBULIWA KUTOJUA ENGLISH HA HA HA KWELI WATANZANIA KILA KITU KWAO NIBAYA.
ReplyDeleteTATIZO LANGU HAPA HAWA ANAOFANYA HIVI NI VIJANA WADOGO ,SASA TUKIWA NA VIJANA WENYE ROHO ZA KICHAWI KAMA HIVI KWELI TUTAFIKA POPOTE?
MCHAWI SIO LAZIMA ATUMIE TUNGULI,MCHAWI ANAWEZA KUKUZURU HATA KWA MANENO NA NDIO UCHAWI WANAOTUMIA VIJANA WENGI WAKITANZANIA.
mdau "cha mtu mavi"
yes Kanumba smile namna hiyo mtoto wa kisukuma smile wabaya wako wajinyonge.....tuko pamoja daimaaaaa. Kitu kimoja unahitaji kuelewa: challenges za watu wabaya zinakupeleka juuuuu zaidi zingatia tu kwamba no giving up forever Mungu amekupa bure fanya kila uwezavyo kutumikia talanta yako hata kama itabidi uongee kichina au kirusi we sema tu vile uwezavyo. Hii tabia ya kubabaikia lugha iko huko kwetu tu kwa sababu ya ushamba lakini huku majuu hata ukijaribu tu kuongea watu wanakuheshimu mradi ujumbe una contents za maana na zinazojibu swali ..HUKU WATU WANAANGALIA CONTENTS YA SPEECH ULIYOSEMA YAANI KUNA WISDOM KIASI GANI NA SI KUSEMA SEMA TU KAMA KASUKU MRADI UMEONGEA INGLISH. MWANAWANE WEWE UMESEMA NA UMEELEWEKA ZAIDI YA YOTE UMESEMA BUSARA GO ON MY DEAR AND MAY THE LIVING OD UIDE YOU ALWAYS......
ReplyDeletehao ndo watu wanaoishi kwenye nchi yenye AMANI isiyokuwa na UPENDO,
ReplyDeletetunaomba mtuonyeshe hizo clip za yaliyofanyika huko Big braza, anyway whatever happened... not knowing English should never be the case.
Wabongo mnapenda sana kutukuza kiinglish. Kibaya zaidi hata Media inafagilia Kiinglish we mwenyewe Michuzi unafagilia Kiinglish ndo maana mwanao anapiga buku Uganda ili kiinglish kiwe rechabo
Nimefurahi sana kwamba upo pamoja mr kanumba kwamba inglish siyo big dili kwa viiiiiiiiiiile na nadhani media nyingine zitaungana na wewe kuwaarifu watu kwamba waikonde kama hawajui hiyo lugha na wala isiwe ujiko kwa mtu anayejua wachukulie kama bb yangu Mtabutwa anavyo ongea kimatumbi
KISWAHILI OYEEEEEE
TUKOSOANE KWA MISINGI YA KUELIMISHANA NA WALA SIYO KUUMBUANA.
THANX.
Michuzi Akhii
ReplyDeleteWajaribu kuficha na kutumia lugha diplomatically but its overt that these feisty wadaus get your hackles up. Pole sana walakin tafadhal kumbuka ni mwezi gani huu na hasa sasa twaingia kwenye kipindi cha lailatul kadri
Ramadhan njema
Wakatabahu
Kiinglish chake kigumu..Jaribu Maimuna...mie naitwa Maimuna mmh Kiinglish chake kigumu!! Kwi kwi kwi !!
ReplyDeleteMr kanumba wewe sasa ni Super Star, usikubali hata siku moja mtu akakuvunjia hadhi yako for any reasons. Watu kama hawa inabidi uwachukulie hatua za kisheria siyo kusema NAMWACHIA MUNGU(watu wenye msemo kama huo wa 'namwachia mungu' huwa ni wachawi,mtu kama wewe uchawi siyo hadhi yako, Mr Kanumba wewe ni CELEBRITY, celebrities use LAWS NOT JUJUs)... unamwachia mungu kitu gani ndugu yangu, siku hizi mungu yupo busy sana hana muda wa kudili na mambo kama hayo, kinachotakiwa KUFANYA ni kufuatilia kwa makini vyombo vilivyohusika na kushusha hadhi yako,TAFUTA WAKILI (acha ubahiri wa kutaka kwenda kumaliza kwa mganga maana kwa mganga ni cheaper kuliko Wakili), Mpe ukweli halisi then yeye ndo atakwambia kama kuna kesi ya kufungua ili ulipwe kwa kudhalilishwa au la!(kwani inawezekana ikawa ni feeling zako tu)
ReplyDeleteWewe unaweza dhani kwamba hili ni suala dogo lakini kutokana na kazi yako ya USANII hili siyo suala dogo hata siku moja. Sasa hivi UPOJUU kwenye FILM INDUSTRIES hivyo vyombo vya habari husika vinajaribu kukuporomosha sasa wewe unaposema unamwachia mungu maanake ni kwamba unamruhusu adui yako akuporomoshe!!!!!!!
Unajua Mr Kanumba hali ya uchumi nymbani siyo nzuri lakini ingekuwa ULAYA kama Uingereza ungekuwa ushapigiwa simu na Mawakili kibao ambao wangekuwa tayari kushughulikia kesi yako UNDER NO WIN NO FEE(Huwalipi mpaka ushinde kesi) Lakini kwa bongo yetu ya sasa inabidi Ujitutumue umuwekee mtu bastola ya kichwa(umpeleke mahakamani).FAIDA utakayopata ni kwamba: KESI ITATANGAZWA KARIBU NA VYOMBO VYA HABARI VYOTE IN WHICH UMAARUFU WAKO UTAONGEZEKA MARA DUFU NA VILEVILE WALUGA WENGINE WOTE AMBAO WANAFIKIRIA KUFANYA KITENDO KAMA HICHO KWAKO AU KWA MSANII MWINGINE YEYOTE UTAWAOGOPESHA(which is good for bness)
Ongea na wasanii wenzio kama kina Ray na wengineo Pitisheni mchango kidogo mpate pesa za kumlipa lawyer kama mfuku wako utakuwa mdogo.
MNATAKA SERIKALI IWASAIDIE WASANII WAKATI WENYEWE HAMJISAIDII??!!! siyo rahisi, inabidi muonyeshe mfano, mlinde HESHIMA YA MSANII ambayo kwa sasa haipo.
mungu ibariki Tanzania
Mungu mbariki mdau no;1 (i.e Mr Michuzi)
Thanx.
HAPO NI WAKATI KANUMBA AKIOMBA DARASA LA TWISHENI YA KIINGLISHI KUTOKA KWA NABII YOHANA MASHAKA ILI KUJIANDAA NA SAFARI YAKE YA SAUZI AFRIKA..... teh teh he he teh teh
ReplyDeletewamatumbi tunataka hivi, kama ni kiinglish kiwe fasaha sio chai maharage hapa kwenye ishu kubwa kama ile ya big bro africa nzima inaangalia pale laivu bila zengwe hakupaswa kwenda maimuna kama kanumba na kwa blog ya jamii huyo mashaka aandike kiswazz tu itanoga zaidi hii ni blog ya jamii na kila mwana jamii anapaswa kujua yanayojiri humu ndani hii sio big brother kiinglish tuu ni blog ya jamiii kiinglish kina mahala pake na wakati wake na kadhalika kiswahili hivyo hivyo
ReplyDeletemiss michuzi
sasa jamani sinema gani kacheza huyo jamaa!!!ndo denzeli washingitoni wa hapo ubongoni!!!!
ReplyDeleteJamani Michuzi mbona nasikia Kanumba alituwakilisha vyema tu. Walimuuliza kwanini hali chakula mchana akasema " I am closing" jamani mmesahau kuwa huu ni mwezi wa Ramadhani na watu wana close jamani?
ReplyDeleteKanumba ifanyie kazi changamoto ya kuinua kiwango chako cha lugha ya kigeni.
ReplyDeleteMnaombonda mnadhani mastar wote wa Hollywood wanajua kuongea Kihispania, licha ya kuishi mazingira yaliyo na ndugu zao wa Mexico wengi tu? Lugha ni lugha tu, sio kila mtu ana kipaji au amepitia mazingira ya kuwa nguli katika lugha za kigeni. C'est la vie. La vida es dificil.
This comment has been removed by the author.
ReplyDeletewalahi Kanumba toto bwana sikuwahi kulitazama vizuri toto hili nyie semeni tu hadi mchoke na kesho tunaanza story mpya ya kuosha vinywa na kusahau mwezi huu tulishauri nini maana klabu ya michuzi nayo haina mtunza takwimu sijui tunapimaje kama maoni yanafanyiwa kazi ama tunacheza mchiriku ila KB (KANUMBA) yuko mbali anaita jamani wadau tuwe wakweli...
ReplyDeleteHabari za jioni waungwana.
ReplyDelete1.Bwana Michuzi naomba nikushauri hili,kama unaamua kuwa neutral kwenye issue yeyote unayoipost hapa,basi uwe neutral kweli kweli.Na sio kuhubiri kwamba upo kwenye neutral ground ilhali maongezi yako yanaonekana kabisa kwamba yameelekea upande fulani.
2.Lugha kama "KANUMBA ANAPIGWA MANDE" zinatupa shida kidogo sisi watu wa mwambao
3.Lugha ya mawasiliano ndani ya BB4 ni kiingereza,hatukatai kwamba kiswahili ndo lugha ya taifa,lakini when it comes to issue kama ile,hakutakiwa kuwa na mjadala bali ni kupeleka mtu aliye compitent kwenye lugha hiyo tu!and thats it!
Mkulima-kijijini Gezaulole
I love TZ thats all I can say maana nimecheka humu ndani mpaka uuuuh.
ReplyDeletekwendeni zenu kiwango cha lugha atanyanyua kwa wakati wake...hata asiponyanyua mtaangalia tu kazi zake maana zinalipa kwa maburdani sasa mnabisha? hata mkibisha kwani mko wangapi? huhitaji kuwa umeenda shule ili ukubali kuwa kazi za KB zinalipa...up up up up shoto kulia moja mbili tatu Kanumba tembeaaaaa endelea na kazi achana na roho koroshoooooo lete mapicha tunayasubiri.....
ReplyDeletemitchu, acha hizo! Kwa nini hizi kauli fyongo (chonde, sijakutukana, nataka kusema ‘misguided comments’ kwa ‘kilugha mama’- lol!) mbona twapenda kutafuta majibu rahisi kwa matatizo yetu? ndo mtazamo huu ulotufikisha kwenye ma-EPA na mengine hata kichef2 kuyaorodhesha ‘apa. yaani wafikiri tuna nongwa na K ama mteule JM?, Japo Big Brother (BB) nahisi sio muhimu kiasi hicho, lakini ya kaisari mpe kaisari, mbona Richard alipochemsha kivingine (sio kwa lugha) watu pia walisema? Mbona watu wanamsema Maximo humu ndani (kuhofia aibu ya taifa?). kama wewe Mitchu, ze globber na kanumba, ze great na wachache, ze few hamkuelewa mjadala wa kanumba hapa (na pia kwenye bongo celebrity) na ukosoaji chanya, basi hapa pesa zangu mbili:
ReplyDeletehaijalishi BB ina maadili ama la, tukubali kuwa kwa namna yake (sababu ni vigumu mtu mmoja kuuwakilisha umma wote) ni kioo cha taifa analotoka mshiriki, kitabia, kitamaduni na haiba. Kwa kiasi chake haya huwasilishwa kwa njia ya mazungumzo/kujieleza kwa mshiriki, aidha mazungumzo na wenziwe ama nyakati za diary. Jee Kanumba ama walompeleka walielewa hili. Kama ndivo jee alijipima/pimwa ubavu?..majuzi wanasheria ‘washomile brazaz’ wetu wenyewe walisema ‘wanajinyea’ kwa wakenya na waganda- mmeona wao wapumbavu na Kanumba mjanja. Kama hujui, kujua tatizo ndo nusu ya utatuzi wake. Wadau walichofanya ni kulalamika na kutuma madongo sababu wanachukulia kuwa ilikuwa wazi katika namna yoyote, kuwa K hata kama ni mmojapo wa nguli na galacha wa hapa nyumbani, labda hakuwa tayari kwa sasa kutia timu mjengoni..zingepatikana tu namba zingine mujarabu kuliko yeye. Wengi wa wadau walikosoa kujenga si kusaga wakishauri K sasa abuni mipango ya kujiongezea maarifa binafsi..Angle nyingine ya kukandia lazima ijitokeze sababu kwa kukubali kuingia mjengoni K alikuwa anajiacha uchi kwa mara ya kwanza kwa wengi wasomjua binafsi ila kwenye ‘big screen’. Na hawa ndo walodhani amekamilika, sababu ya kuona edited shots za muvi ambazo pengine zinampendelea K. ni vigumu kumtetea mtu anayeshindwa kupambanua katika ya nomino ‘Africa’ na kisifa ‘African’. ata kama elimu si ya watoto wa EPA, lakini jamani? Mkuu wa Wilaya ya nanihii, sitamaliza hapa, lakini ya mambo ya ‘mwenzetu’ ndo yanatufanya tunaandamana kuunga mkono mafisadi, eti kuogopa usenene. Na ukae ukijua kuwa uvivu wa kujifunza, kutafuta maarifa na ujanja-ujanja ndo uliofikisha kwa upande mmoja wananchi wenzetu kusaini mikataba mibaya ya madini na ubinafsishaji. Tafadhali tumia blogu yako kuhamasisha ujanja wa maarifa, ili tuje kuwa ‘wabongo wa kweli’ siyo ‘walongolongo’, mwishowe ndo kuumbuka kwani nguo ya kuazima haisitiri matako. Hili neno ‘usenene’ linaenda kinyume kabisa na demokrasia ya kweli, samahani kwa kusema hili lakini linanuka kuburuzana na u-dikteta mkongwe. Wacha watu walonge, msikilize Voltaire (Letter, 1770 – akina K mjifunze kiingereza ili msome hii): "I disapprove of what you say, but I will defend to the death your right to say it."
is this news jamani??ahh kaka michuz sa nyininge unaniuzz..ssa mambo gani tena haya?obama anasemwa ije kuwa kanumba..ahh nexttt bwana...
ReplyDeletekanumba...kiatuuu ahahahahaha!cheka sana!jamani mmeona kiatu cha kanumba??niko hoi hapa!alafu nimependa color codination yani kiatu grey, shati white and black alafu kofia na shawl yellow safiii ila ze kiatu ahahahaha
ReplyDeletejamani huyo john mashaka is he a normal guy? au ndio wale midget(andunje)? swali lakizushi tu
ReplyDeleteHiyo, ni kweli kaka Michuzi, lakini kwa upande wa Kanumba sioni sababu ya watu kumpigia kelele mimi kwa upeo wangu naona kijana kawakilisha na tena nampa ongera. Huo ndo mwanzo next time atakuwa safi we are learning from mistake. kuhusu bwana Mashaka tatizo kwake bado liko pale pale yeye ni mtu ana lengo la kuwasaidia masikini na hao masikini awajaenda shule je watajuaje anachokiandika kwa lugha ya kiingeleza? Asante kaka michuzi nakutakia Ramadhani jema...
ReplyDeleteMdau,,, Malaysia
Hii njaa itatupeleka pabaya...meechooz umekatiwa kidogodogo na Kanumba unaanza kumsafisha...UFISADI MTUPU. Lugha ya mawasiliano BBA ni kiinglishi hivyo washiriki lazima wajue lugha hiyo ndo mawasiliano yatakuwa rahisi na si kupeleka vihiyo wa kiinglishi eti kwa kuwa wanatamba kiusanii umatumbini. Mbona wewe ukienda vekesheni zako huongei kikwenu huko ughaibuni? Badala ya kuwahamasisha vihiyo hao wa kiinglishi ili wajibidishe kujifunza lugha kama wanataka kuuuza kazi zao nje ya nchi unawapaka mafuta kwa mgongo wa chupa.
ReplyDeleteMichuzi grow up...ukiweza minya lakini message sent!
WaChagga wana msemo mmoja, 'lekana nawo'.
ReplyDeleteNasikia wanataka kutoa waraka kupeleka serikalini ili wasanii wasisemwe...sijaelewa?
ReplyDeleteHuyu jamaa ni msanii binafsi sijaona hata maigizo yake hata moja lakini nadhani ana washabiki wake pia anao watu wanaompinga...Kwa mtu muelewa ni jambo la kawaida kupongezwa na kupingwa hivyo ningeshauri tu atulie na awe na amani kwa kuwa dunia ya leo kila mtu ana akili na kila mtu anazungumza anachotaka ili mradi tu havunji sheria tunaita 'agree to disagree'.Na asikate tamaa bali achukulie kama challenges ili aende mbele zaidi katika jambo ambalo anaona litamsaidia katika maisha yake...JAMANI TUSILALAMIKE TU ukubwa ni jamvi tuwe tayari kupokea changamoto.
What goes around,comes around!
ReplyDeletePole sana kaka Kanumba maana naona umeumia sana!
ReplyDeleteWatu hawana haja ya kukutusi wala kukutungia yale ambayo hukusema. Kujua au kutojua kiingereza ni mitazamo ya kila mtu na husasani kwa wale walioangalia hicho kipindi.
Hata hivyo, Wachambuzi wengine wa harakati za maendeleo ya jamii wanaona kuwa hata mapokezi uliyoyapata kwa kutoka kupasha joto BBA hayakuwa ya lazima!
Rai ilishatolewa kuwa watu wanaorudi nyumbani wakiwa na shahada za uzamivu za vyuo vikuu au nishani za kutukuka kwao katika tafiti za kisayansi na au ujasiriamali ndio wanafaa wapokelewe kwa nderemo hapo JKN Airport na pia wakaribishwe Wizara yenye dhamana na hata Ikulu ikiwezekana kuwasilisha Tasnifu na au mafanikio yao kwa KISWAHILI kwa jamii ya Watanzania.
Ni watu kama hao wanatakiwa kupewa 'exclusive inteviews' ili tusaidiane nao ama kupunguza umaskini au kuboresha maisha ya Mtanzania kwa kutumia dhana, mbinu mpya na mashauri wanayoyawasilisha kupitia maandiko na au kazi zao zilizokubalika kimataifa.
BBA kamwe haituboreshei maisha Waafrika! Hata kama ni kwa ajili ya kufurahisha basi akina joti na hata Makamaredi wa Redikulasi wa Kenya na wenzao mbona wako juu kinoma kuliko yatokayo mjengoni mwa BBA?
Tupendane na tupende KWELI na KWELI itatuweka huru maishani.
Ndugu Watanzania,
ReplyDeleteLugha zipo nyingi duniani na kuna ambazo ni zetu Watanzania. Kwa nini tung'ang'anie kuongea lugha ambazo hatuwezi. Unajua kiswahili, ongea kiswahili. Watatafsri hao wanaotaka uongee. Hakuna sababu ya koungea lugha za wengine na kuharibu! Huu ni ukoloni mamboleo kutaka kuongea kiinglish eti kwamba ndio utaonekana ni mtu wa kileo au anaejua. Mtu maarufu kama Kanumba atangaze kiswahili chetu.........
Noona www.kanumba.com not reachable, sijui ime-expire au ndo mdau kaamua kuishusa fasta baada ya kuona watu wana sehemu ya kuthibitisha mchemko wake katika kugonga ngeli?Jamaa na wenzie wakubali kujifunza kama wanataka hiyo international audience na pia wasifarijike kijinga eti kupeleka tamko sijui waraka serikalini, suala la kwenda kumpokea kwa wingi halina maana yoyote zaidi ya kujifariji maana wote hawajui au kanumba ndio mjanja wao katika kutema lugha ya kiingereza.
ReplyDeleteKama ilikuwa planned kwanini hawakumsindikiza kwa kishindo kama yalivyokuwa mapokezi yake? Hawa watu wakubali kwanza kiingereza hawajui na wasikalie kusema eti sio issues, sio issue wakati kanumba ana dream ya kucheza na movie na Denzel? Sio issue wakati wanataka acceptance ya kazi zao duniani? Mwingine akadai mbona wachina wanatumia kichina, kama ndivyo wakubali kutotumia kiingeereza kabisa na wakipewa mialiko waseme wao kiingereza hawajui, hawatumii na hawana mpango wa kukitumia. Wanakuwa ndumila kuwili, wawe na msimamo mmmoja sio vijisababu vya kujustify ujinga.
Kukua hukuko moja kwa moja...unapitia mapito kama haya, ka kujifunza naamini kajifunza. zilizobaki ni story tu......
...UTAPANDAJE MNAZI NAWE SI MGEMA, WAACHIE WAGEMA MINAZI WAIGEME!
ReplyDeletekaka Michu kama unataka kumsafisha Kanumba vile!! lakni utakuwa haumpendi wala hupendi maenedeleo yake. ulitakiwa umwambie jamaa shutuma tayari zipo hivyo alitakiwa atumie wakati huu kama challenge ya kuweza kurekebisha pale penye dosari na pia iwe ni wake up call na kwa wengine pia.kama tunatka tuw kimataifa basi tuwe kimataifa tusinganganie kuwa kiswahili ni lugha yetu pale kulikuwa na mataifa mbali mbali na makwao pia wana lugha zao lkn lugha ya mawasiliano pale ilikuwa moja, jamani tusitetee ujinga.
ReplyDeleteMichu, hebu tubonyezee kiji-clip Kanu alipolonga "I don't eat I am closin' I'm Islamic" - Wizi mtupu!
ReplyDeleteMSHAKA anafagiliwa sana na mademu huku USA tukianzia na H-TOWN nasikia jamaa anapesa kama nini. Vijidemu havijali kama yeye anduje $$$$ talks.Mashaka naona unatesa tuu na hawa mademu wajinga ambao wameshindwa shule kazi kutafuta wanaume wenye pesa haya kaka kama hautakuwa makini utaibiwa.
ReplyDeleteHuyu ndio John mashaka LMAO kweli yuko handsome hehehehe kazi kwenu madada nasikia yuko single.
ReplyDeletekumbe john mashaka ndio kafupi hivi halafu kanaonekana kamekula chumvi nyingi je ana umri gani?pole sana dada yangu ulivyokuwa unasema umepata mume sikujua kuwa ni andunje...kwikwikwikwiiii, kweli huko houston kuna shida...hapendwi mtu linapendwa pochi dada yangu una moyo
ReplyDeleteTarehe Thu Sep 10, 10:58:00 PM, Mtoa Maoni: Anonymous wewe naona unataka kumdanganya Kanumba na wadau wa blog hii. Nani kasema sheria inaweza kukifunga chombo cha habari kwa "fair comments". Vyombo vya habari vinafanya kumkosoa na kumwambia ukweli Kanumba kuwa alichemka na anatakiwa kujifunza kutokana na makosa. Yeye sasa hivi ni staa wa kimataifa hivyo anatakiwa kuijua lugha ya mawasiliano ya kimataifa vizuri. Atakishtaki chombo gani cha habari tena kwa grounds zipi? Kama hujui sheria ya defamation sema tukufundishe kuliko kutaka kupotosha watu hapa!
ReplyDeleteUkweli bado unabaki pale pale tu wavivu wa kiingereza, kujifunza ni nia ya mtu tu jamani,kuwa hata tufanye wengi wa watanzania tunaongea Kiingereza cha Class three, ni ngumu kusimama, kwenye umati wa watuamiaji wa hiyo lugha tukaweza kubishana, ni mara chache hata wenzetu kutukuta tuko nchi zao tunaongea Kiingerea sahihi hushangaa na kuuliza asili yetu au tuliko soma, kwakusema ukweli kiingereza Tanzania bado hakipo lakini bado kuna watu wanasimama popote nakukipigania ipasavyo wako tayari, bado Maulti choice Tanzania haichukui muda wa kutosha kuandaa watu wa ku compete kimataifa. Mfano mzuri ni Yacob ambaye ni mu- Ethiopia, nayo ni nchi inaongea kiingereza kibovu kama sisi tu, lakini Yacob wamemtoa wapi?.. Kanumba alibaki anacheka kila kitu hata vizivyochekesha coz hana point ya kujibu au kuchallenge kinachozungumziwa, Basi Multi choice walipoona anahitaji kunolewa hata Britich council ni ngumu kuihusisha. Naamini Kanumba angekuwa bubu wa masaa mengi sana kama angeendelea kukaa mule ndani, so Ukweli ubaki ukweli. Hakuwa mshindani sahihi, either kwa maandalizi mabovu ya multi choice au kutojua mlengo mzima wa BBA kila mwaka.... Tuangalie mambo kimataifa na sio Kiingilish Kuwa janga la taifa. Tuki chukulia mapungufu yetu ni ya lazima ... hatusongi ingawa watu tunao... Hata hao waliotangulia walijitahidi sana. tuangalie jinsi ya kusonga mbele sio kupongeza mapungufu... tuwe wakweli ili tusonge mbele. Toka enzi za shule za mkoloni nchi gani isoweza pata mtu sahihi kwa jambo fulani kwa wakati sahihi.
ReplyDeleteMsikilize K1 anaongea english yanye accent mbaya sana ya kwao Botswana lakini ana uewelewa mkubwa ajabu. Sisi nani bwana tuna kaa class za mwisho kwenye kila kitu... kila kitu kipeni uzito wake kitafanikiwa sio kutimiza wajibu wa ushiriki tu.
Kweli siwezi kumaliza maumivu yangu juu ya ukweli wa kiingereza nchi hii. Kwasababu sio tatizo kam a tunavyo liweka tumezidi kuendekeza ujinga na kuridhika na vitu vya low quality.