Madaktari nchini China walipigwa na butwaa baada ya kugundua kuwa Kang Mengru, mtoto wa kike mwenye umri wa mwaka mmoja ambaye alipelekwa hospitali baada ya tumbo lake kuzidi kuwa kubwa, alikuwa na mimba ya kichanga kingine.Baada ya mtoto huyo kufanyiwa ultrasound, madaktari waligundua kuwa mtoto huyo wa kike alikuwa amebeba kitoto kichanga kwenye tumbo lake ambacho kilikuwa kikiendelea kukua.
Mtoto Kang Mengru na mama yake.

Mtoto Kang Mengru na baba yake

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 20 mpaka sasa

  1. Huyu mtoto ana pacha wake ambae anakulia tumboni, na anamnyonya chakula na damu. Inabidi afanyiwe upasuaji haraka ama sivyo maisha yake yapo hatarini jinsi umri wake unavyozidi kuongezeka.

    ReplyDelete
  2. Hee! makubwaa!

    ReplyDelete
  3. mdau wa philySeptember 10, 2009

    hizi ni dalili za kiama

    ReplyDelete
  4. jamani mi sina hata la kusema.yani namwogopa mungu maana haya ni maajabu yake yeye mwenyewe ndo kaamua iwe hivyo na yeye mwenyewe anaujua mwisho wake.just imagine huyo mtoto ni wako.daaaah.

    ReplyDelete
  5. No i cant believe it.

    Stellah

    ReplyDelete
  6. Mmh, Kweli mwacheni Mungu aitwe Mungu!

    ReplyDelete
  7. MWACHENI MUNGU AOTWE MUNGU JAMANI!!!!!!!! MUNGU NA ZIDI KUWATIA NGUVU NA IMANI WAZAZI WA BINT HUYU.AMEN!

    ReplyDelete
  8. Fetus in fetu may be a parasitic twin fetus growing within its host twin. Very early in a monozygotic twin pregnancy, in which both fetuses share a common placenta, one fetus wraps around and envelops the other. The enveloped twin becomes a parasite, in that its survival depends on the survival of its host twin, by drawing on the host twin's blood supply. The parasitic twin is anencephalic (without a brain) and lacks some internal organs, and as such is almost always unable to survive on its own. As the normal twin has to "feed" the enveloped twin from the nutrients received over a single umbilical cord, it usually dies before birth.

    ReplyDelete
  9. kaka nanihii ya leo kari,nadhani mtoto anaumwa kansa sio mimba.nadhani interview imesikia vibaya au kichina kinakupita mbali kaka. mimba na umri huo haiwezekaniiiiiii.

    carlos M

    ReplyDelete
  10. Waafrika tuna utajiri wa IMANI za ajabu ajabu.Na imani ingekuwa inaonekana basi waafrika tungekuwa tunaongoza dunia hii. Hapa hakuna cha Mungu kafanya haya yatokee wala nini.Vitu vingine ni vya kuangalia na kufikiria ni kwa nini imekuwa hivi.Huyu dogo hana mimba bali pacha wake hakuweza kuzaliwa kwa njia ya kawaida.Haya mambo yanatokea kila siku duniani.Hili halina tofauti sana na mapacha wanaozaliwa wameungana viungo.

    ReplyDelete
  11. HUYO NI TWIN WAKE BAHATI MBAYA ALIKAA SEHEMU ISYOTAKIWA (TUMBONI KWA MWENZIE).

    ReplyDelete
  12. Ajabu na kweli. Sipati picha atajifunguaje? atanyonyeshaje? na je baada ya kujifungua atakuwa anapata menstration periods kama wanawake wengine? maana sielewi nimuweke ktk kundi gani la watoto hayumo yumo zaidi kwa wanawake maana ana uja uzito.
    Ee Mungu wee!

    ReplyDelete
  13. Most likely a hoax.

    ReplyDelete
  14. Hii itakuwa mchezo wa kufanya mapenzi na mke wakati mjamzito haswa kipindi karibu na kujifungua! Matokeo yake baba kamtia mimba mtoto wake tumboni! Wakina baba mnaona madhara yanayoweza kutokea mkiwa ving'ang'anizi kwa wenza wenu pingi wajawazito? Najua hii itakuwa ticket ya wakina baba kujiruhusu kutoka nje ya ndoa kisingizio madhara ya kujamiina na wajawazito!

    ReplyDelete
  15. Wabongo haoo...hehehehh imani zetu mbona kazi. Tembea uone...this is not common lakini its happens sometimes and this is not the first time. Kama huyo aliyesema hapo juu....Ni parasitic twin wake. Na hii ina happen sana kwa nchi ambazo hawana good prenatal care. Kam angekua anakwenda kwenye prenatal care zenye kufanay ultrasound wangemuona huyo mwingine siku nyingi tu.

    Google FETUS IN FETU uone wanavyotokea kwa nyia tofauti

    ReplyDelete
  16. BABA WA HUYO MTOTO AMBAYE YUMO TUMBONI NI NANI? AMA NDO MIUJIZA KAMA YA BIKIRA MARYAMU?? SABABU HUYO MTOTO NI BIKIRA IWEJE AWE NA MIMBA AMA NI KWA UWEZO WA MUNGU? HOW IS THIS SITTING???

    ReplyDelete
  17. eheee hapa hapa ..mnamcheka KB hajui kiinglish sasa nyie mbona hamjui sayansi..yaani mnashangaaa mnamsingizia na Mungu..yaani hamjui probability za miujiza katika reproduction...hahahaaaaaa ama kweli nyani hajui KUNDULE.....!!!! UWIIIIIII YALAAAA KB songa mbele humu duniani lazima kila mtu kuna kitu cha muhimu ambacho hajuiiiii..oi ..oi..oi....aibu mlisomea miembeni ama ? kama siyo basi acheni kumnanga KB.....

    ReplyDelete
  18. sasa najiuliza mtoto huyu kabalehe tokea tumboni au...?
    kichwa kinanizunguka naomba Daktari atupe ufafanuzi hapa.

    Thanks Arsenal fans.
    wanaume kama panya wanakimbia kimbia wakitafuta mashimo wajifiche.

    ReplyDelete
  19. kaka nanihii,
    wachina nao kila kitu feki mpaka mimba feki ziko kwao, noma!!!!

    carlos M.

    ReplyDelete
  20. kuna vitu vingi ambavyo hutokea,na kwa sababu ya watu hasa waafrika wengi ambao hawana habari juu ya nini chanzo chake na hawataki kuchukua nafasi hata kujua kama jambo hilo linachanzo chake,basi mara moja huelekeza sababu kuwa ni MUNGU KAFANYA HIVI au UCHAWI.na hili linafanya afrika inashindwa kuendelea kabisa!!!najua hamta amini lakini nimejaribu kufanya utafiti mdogo tu,nikagundua kunatofauti kubwa sana kati ya mtizamo ukilinganisha lets say mtoto aliyezaliwa ktk nchi zilizo endelea na mtoto wa umri huohuo aliyezaliwa afrika,mathalani ukawatishia kuhusu kiumbe cha ajabuajabu ambacho hawajawahi kukisikia au kukiona,utashangaa 100%ya watoto waliozaliwa afrika wanaogopa na kujihisi vibaya,wakati labda 0.5%ya watoto wa kizungu ndio wataonyesha kuogopa kidogo! think about that!!!!!hii nimeitafiti mwenyewe na kuithibitisha.
    matokeo yake kilakitu waafrika wanalaumu na kukiona kiko juu ya uwezo wao,hawataki kuchukua muda kidogo kujiuliza na kufikiri kuwa lazima kuna sababu inayofanya hivyo japo wao hawaijui,ils ipo. su kusmini kwamba wanaweza kupata suluhisho la jambohilo kama watafikiri kwa makini na kuchukua hatua kidogo mbele. umaskini wetu unaanzia mbali jamani sio tu ktk ufisadi,tuna kazi kwelikweli hasa ktk elimu na tamaduni ili kubadili mitazamo ktk mambo.niliona mlemavu mmoja kawekwa ktk post zilizopita watu wakaibuka na MUNGU NDIYE KAMUUMBA HIVI!LEO HII HAPA tayari mungu kahusishwa,kesho mtu anakuwa maskini kwa kuwa hataki kujituma na kuwa na mipango mizuri ikiwepo family planning MUNGU NDIYE KASEMA NIZAE HADI MAYAI YAISHE utadhani anajua binadamu wa jinsia ya kike ana mayai kiasi gani!sasa ukizaa hadi mayai yaliyopo kwa kawaida yaishe unadhani utakuwa hai!!na hata kama ungepewa uwezo wa kuwa hai unadhani unaweza kuzaa hadi yaishe yote!hahaha haya jamani kazi kweli!we need to change.mungu yupo ila kashauri kuitafuta elimu,maana kasema mshike elimu na wala usimwache aende zake.

    mdau.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...