JamiiForums.com/The Home of Great Thinkers
inapotimiza miaka 3 tangu kuanzishwa kwake, inapenda kuwatakia watanzania wote pamoja na wadau wote mitandaoni mfungo mwema na kuwatakia kila lililo jema katika mwezi huu Mtukufu wa Ramadhani.

"Enyi Mlioamini! Funga ya Ramadhani imefaradhishwa kwenu kama ilivyokafaradhishwa kwa wale waliokuwa kabla yenu ili mpate TAQWA"
(QURAN Surah Al-Baqarah 2:183)

Unakaribishwa kwa mijadala huru
ili ushiriki na wazalendo wenzako.

Tembelea
www.JamiiForums.com
JF Management
-----------------------------------
Globu ya Jamii, kwa niaba ya wadau wote, inatoa mkono wa pongezi kwa JF miaka mitatu ya libeneke lililotukuka. Pia asanteni kwa kututakia mfungo mwema wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani. Mbarikiwe.
Martin Luther King jnr. aliwahi kusema katika spichi yake ya "I have a dream" kwamba ufanyapo kazi yoyote ile, hata kama ni ya kufagia barabarani, ifanye kwa uadilifu na uzuri ili watu waje wakukumbuke kwa kazi nzuri uliyokuwa unaifanya. JamiiForums mtakumbukwa kwa yote mnayoyafanya na kwa kuleta mapinduzi katika nyanja ya TEKNOHAMA.
Ingawa hamjasema kama kutakua na mnuso ama la, Globu ya
Jamii inatoa saluti kwa Libeneke lenu ambalo ni mfano wa kuigwa. Miaka mitatu si haba, hass ukizingatia milima na mabonde, vijito na mifereji mliyopita katika safari yenu hiyo ambayo najua fika ndio mwanzo mmeanza.
-Michuzi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 24 mpaka sasa

  1. Kaka Michuzi pamoja na mambo yote,Lakini wewe binafsi na Jamiiforums ndio mmekuwa watanzania wa kweli kwa kutekeleza kwa vitendo,Nyanja hii ya kuifahamisha Jamii kupitia vyombo vyenu, Blog ya Jamii (IssaMichuzi Blogspot) na Mtandao wa Jamii forums.Tumefahamu mengi na tunajifunza mengi kupitia Kazi zenu.Uhuru huu wa kujieleza tuutumie vizuri ili kujenga jamii yenye ufahamu....Hongereni sana...Na Hongera Mkuu invisible kwa kutufumbua macho!

    ReplyDelete
  2. TATIZO LA JAMII FORUM NI KUIFANYA KAMA MALI YA CHADEMA.VYAMA VIGINE HAVIPEWI NAFASI YA KUONGELEWA VIZURI.
    KINGINE WASIMAMIZI WENGI NI CHADEMA NA KUNA WATU WANATUMIA MAJINA MENGI HUKO NI KUJIDANGANYA.
    WAMEKOSA MWELEKEO NAOMBA WABADILIKE.
    WAACHE UDINI HASA WA KUWACHUKIA WAISLAM MKIBADILIKA MTAKUWA CHOMBO KIZURI.

    ReplyDelete
  3. Kaka michuzi habari,
    Kuna wakati fulani uliwahi kuweka tangazo la antenna flani ambazo zilikuwa zikilipiwa kwa account kama DSTV.....lakini sasa kwa bahati mmbaya nilipoteza contacts za watu hao naomba sana kama utakuwa nalo au mtu yeyote mwenye contact za watu wale anitumie kaka anuani na maelekezo yangu yote yapo hapa chini.

    andendekisye@gmail.com

    ReplyDelete
  4. jamii forums wana upendeleo sana ni wamimi sana huko sitiagi timu kabisaa tutabanana humu humu kwa nahnihino mfano baba ni mkali utakuta watoto woote wako upande wa mama kwa sababu huko wanajiachia vulivyo inshort wanadekezwa wanakuwa huru zaidi
    mdau canada

    ReplyDelete
  5. Tunahitaji liberal blog. Huku ni too much CCM kule ni too much of CHADEMA

    Mnatunyima freedom of speech bongo.

    ReplyDelete
  6. Kaka Michuzi maneno yako haya ya menifariji sana .

    "Martin Luther King jnr. aliwahi kusema katika spichi yake ya "I have a dream" kwamba ufanyapo kazi yoyote ile, hata kama ni ya kufagia, ifanye kwa uadilifu na uzuri ili watu waje wakukumbuke kwa kazi nzuri uliyokuwa unafanya. JamiiForums mtalumbukwa kwa yote mnayoyafanya na kwa kuleta mapinduzi katika nyanja ya TEKNOHAMA.
    Ingawa hamjasema kama kutakua na mnuso ama la, Globu ya Jamii inatoa saluti kwa Libeneke lenu ambalo ni mfano wa kuigwa. Miaka mitatu si hapa, has ukizingatia milima na mabonde, vijito na mifereji mliyopita katika safari yenu hiyo ambayo najua fika ndio mwanzo mmeanza.
    -Michuzi"

    Wacha ni fanye kazi yangu ya kufagia kwa bidii zote....

    we Anonymous wa Tarehe Tue Sep 01, 04:33:00 AM,

    un uzibitisho wa maneno yako ? mtu unapotaka kuongea jambo ni vizuri kwanza ukalifanyia utafiti kuliko kuropoka tu,JF haina mwenyewe,mwenye JF ni mwanachame yoyote yule.Napenda kukujulisha ya kuwa JF haipo upande wowote wa chama au kiuongozi.Umewahi kuona forums yoyote iliyo open kama JF?

    Hapa kwa Mtani wangu Bro! Michu ukituma tuma comment ya kuiponda gvmnt inawekwa kapuni.....karibu sana JF.

    ReplyDelete
  7. Balozi wa tegeta, hongera kwa kazi nzuri unayoifanya pia nawapa hongera JF lakini wapunguze umbea siku hizi umekuwa mtandao wa umbea maana inaonekana wanachama wote wa zeutamu wamehamia huko.

    ReplyDelete
  8. Kule siku hizi sitiagi timu kabisa!Wana chuki na WACHAGA kama nini.

    ReplyDelete
  9. jamii forums si kweli ina pendelea chama cha chadema bali ni kwamba watu wengi wanaongia mule ni wamechoka mambo ya ccm sasa wanaona chadema kama ndio inaweza kuwa mkombozi wake na kujikuta wanakifatilia sana kile chama.HAKUNA KITU CHOCHOTE KUHUSU CCM AMBACHO MTU UNAWEZA KUKITETEA KWENYE MTANDAO WA UWAZI NA UKWELI KAMA JAMII FORUMS NDIO MAANA UNASHINDWA KUWAONA WAFUASI WENGI WA CCM WAKIJIBU HOJA ZOZOTE MULE NDANI.KAMA WEWE NI MTU WA CHAMA KINGINE NA UNADHANI UNA HOJA MUHIMU KUWAAMBIA WANANCHI MLANGO UKO WAZI MULE NJOO UWEKE POST NA WATU WATA DISCUSS LAKINI KUSEMA JAMII FORUMS INAENDESHWA KI CHADEMA SI UKWELI KABISA.HAKUNA MTANDANO UNAONGOZWA KWA UHURU NA HAKI KAMA JAMII FORUMS.NA WOTE MNAKARIBISHWA KULETA HOJA ZENU HILI JAMII HITOE MAONI YAO BILA UBAGUZI WOWOTE.

    ReplyDelete
  10. HAWA JAMIIFORUMS NI "GREAT THINKERS IN A BOX".
    WANA MAWAZO YA KITOTO, WENGI WAO HAWAJUI/HWANA EXPERIENCE HATA KUONGOZA VIJIJI AU MITAA YAO SEMBUSE JAMII YOYOTE YA UMMA.
    UKITOA MAWAZO YAKO HUKO YANAYOPINGANA NA MLEGO WA MAWAZO YA UHAKUKA BASI UTAFUNGIWA TU.
    HIYO NI BLOGU YA WATOTO WADOGO.WANAOCHAKURACHAKURA MAKABRASHA NA KUPASTE

    ReplyDelete
  11. Ndio maana mkaambiwa Jamii forums is the home of great thinkers, mtanzania yeyote mwenye akili timamu hawezi acha kuingia kwenye ile site, maana unajifunza ishu nyeti zaidi zinazotokea kwenye taifa hili. Tatizo wengi wetu sisi hatupendi mambo ya kutumia akili, bali ni kupumbaza akili ndio maana tunaishia kujihusisha na mambo yasiyo na maana afu at the end of the day tunataka maendeleao, inafurahisha kama si kusikitisha, talking of bias, tunajua fikra kwa blog hii ni kuhusu CCM tu, sasa mbona na hapa hamkimbii, watz smell the coffee!!

    ReplyDelete
  12. Wadau ni kitu cha kumshukuru Mungu kwa blog hii kutimiza miaka mitatu.Ila sikubaliani na wale wanaosema inawananga waislamu sio kweli.Uhuru wa kutoa maoni pale wanaona kama unawaonea,wakati uhalisi ni kuwa waislamu Historia inawasaliti.Elimu ya duniani kama masomo ya Sayansi wapo nyum,wapo mbele katika elimu Ahera sasa mtu akishika nafasi ya juu kwenye nchi, wizara,au siasa mnasema serikali imempendelea kwa kuwa ni mkristO!.Sio kweli angalia watoto wa kiislamu na kikristo mashuleni,seminari za Kiislamu Kama Ubungo,Kirinjiko au shule ya Al Haramain linganisha na Seminari za Kikristo kama Rubya,Lutheran Morogoro au shule kama St Marys.Perfomance zao kwenye mitihani ya kidato cha 4 hazifanani miaka nenda miaka rudi.Au hata vyuo SAUT na cha Waislamu cha Morogoro.Nchi yetu haina dini kwani ni SECULAR STATE so hakuna dini yoyote inayopendelewa.Sio sawa na RELIGIOUS STATES kama Iran,Vatican kwa Papa.
    Wadau ni mawazo yangu sina chuki na mtu Baba wa Taifa ametuachia Upendo na Amani tusivuruge .Tutalia kilio kisicho na mnyamazishaji.Nawakilisha mzee wa nanihii....

    ReplyDelete
  13. Unayesema Chadema Haina mwenyewe (Sorry Jamii Forum) ni sawa na kusema CCM haina mwenyewe. Hakika kila mtu anaweza kuwa mwanachama. Lakini kama hukubaliani na sera yao ya ufisadi, hata kama wewe ni Kada Sita, utaondolewa tu! Sera za Jamii forum ni tukuza Chadema, Tukana CCM, Ukabila Udini nk, lakini kila mtu aweza kujiunga!

    ReplyDelete
  14. Jamani source nyingi ya habari Tanzania kwenye magazeti kwa taarifa zenu nyie wa hapo juu inatoka JF kama unabisha fuatilia pale JF mtu yeyote upo huru kutoa maoni na mada sio unaleta habari ambayo haina source unatunga uzushi uzushi ndo unakutana na magreat thinker wanakukosoa nakuomba uweke evidence.
    Karibuni JF mjimwage njoo msome nyaraka za meremeta,EPA,RICHIMONDULI na zingine nyingi ambazo mkuu wa wilaya ya nanihii hawezi bandika hapa kibarua kitaota nyasi hahahaha

    ReplyDelete
  15. Jamii Forum ni ya Chadema kwani ndio wanaoifadhili hili halina ubishi.
    Michuzi BLOG ilipotokea sakata la Rostam NA MENGI ALIWEKA PRESS CONFERENCE YA MENGI NA ROSTAM HAPA.ALIWAPA HAKI YA KUSIKILIZWA WOTE WAWILI KULE ILIKUWA NI KUMSIFU MENGI TU

    LAKINI JAMII FORUM IKAWEKWA HABARI YA MENGI TU KWA VILE MENGI ANAISADIA BLOG HIYO NA KUNA WATU WANAOTUMIWA NA MENGI KUMSHAMBULIA ROSTAM.
    WATU HAO NDIO VIRANJA WA JAMII FORUM MMOJA WAPO ANAISHI MAREKANI AANANDIKA SANA MAGAZETINI KWA JINA BANDIA.

    KUKIWA NA MADA YA KUMKOSOA MBOWE ITAFICHWA KAPUNI.

    PIA WAZEE NA WATENDAJI WOTE WA CHADEMA KAMA MTEI,SLAA,MBOWE,MNYIKA ANAYETUMIA-MPAKA KIELEWEKE, KITILA MKUMBO WANACHAMA KWA MAJINA YAO HALISI.WAMEFANYA NI PLATFORM YAO.

    SIKU AKIINGIA HAMAD MASAUNI WA UMOJA WA VIJANA WA UVCCM BASI ATAKULA MATUSI TU.

    JAMII FORUM HAINA UHURU KAMA WA MICHUZI AMBAYE UBNAWEZA KUMTUKANA NA AKATOA COMMENTS ZAKO.

    PIA JAMII FORUM SANA WANAJADILI WATU NA MATUSI VITU AMBAYO HAZINA MAANA.

    KUTHIBITISHA HILO MICHUZI AMEKUWA AKIPATA TRAFIK KUBWA YA WATU, JAMII FORUM WANALIJUA HILO.WATU WATAZIDI KUISHUSHA MAANA JF KWA UDINI MFUMO KRISTU,UKABILA YAANI KULE KUSIFIA UCHAGA TU.

    ALIPOHITILAFIANA NA MBOWE MAREHEMU WANGWE ILIKUWA FURAHA KWA JAMII FORUM NA IKAWA NJIA YA KUKAKASHIFU NA KUMTUKANA. KWANINI WASIWAJADILI WOTE KWA PAMOJA?

    MWANAKIJIJI ANA MAJINA KIBAO HUO NI UTOTO NA UJINGA.

    ReplyDelete
  16. Nakubaliana kabisa na non 4:16 hapo juu.Ukisikia mtandao wa mabishoo ndo Jamiiforums wanapost ujinga, wanajisifu ujinga na wanapongezana ujinga.Kujiunga na ujinga huo sawa sawa na kuoga maji taka ya Msimbazi.

    ReplyDelete
  17. MUNGU SI ATHUMANI WAKATI JAMII FORUM IKIJIKWEZA KWA UHURU NA UWAZI WALIONAO.

    LEO ZITTO KABWE KAANIKA UOZO WAKE CHADEMA NA JINSI ANAVYOPIGWA VITA NA KUELEZA KUWA WATENDAJI WA CHADEMA WENGI NI WACHAGGA.MADA ZAKE NIMEFINYWA FINYWA NA KUWEKWA KWENYE MPANGILIO USIOELWEKA.

    TANZANIA DAIMA GAZETI LA MBOWE LIMEKUWA LIKIMSAKAMA ZITTO TOKA ASEMA ATAGOMBEA UENYEKITI LAKINI HABARI YA TANZANIA DAIMA KUMSAKAMA ZITTO TAYARI IMEFICHWA.
    NJIA YA WAONGO NI FUPI.JF BADILIKENI.

    ReplyDelete
  18. Jf wanajitahidi,naimani wanakosoa kwa uwazi kile wanachokiona ndio maana wanaonekana wapinzani.CCM wanatakiwa wawe mbele pia kupinga na kutetea wanachofikiri ni sawa na sio ubabe ubabe tu.Nafikiri wakitumia nguvu ya hoja debate zitakua kali.Tatizo langu kwa watu wa JF nimekua nasoma mara kwa mara lakini wengi wanaochangia mind zao bado zinaonekana ni za mfumo dume.Ukitaka kuproof hiyo angalia post ambazo wanadiscuss kuhusu uteuzi wa kiongozi mwanamke na uteuzi wa kiongozi mwanaume.Hata ukiangalia wakikosoa ministers wanawake au wabunge hawatumii scale ileile kwa wanaume.Naona wengi wana-sexism na pia nakubaliana na anon aliyesema wanachukia sana wachagga.Nafikiri agenda zenu zinajichanganya pale mnapoamua kuingiza udini,ukabila na gender.It puts me off nafikiri na wengine pia.Lakini sitachoka kuwapa thumbs up few of the people ambao wanachangia ukisoma post nyingine utajua huyu ni independent minded,lugha za matusi hamna na kuongea facts and not fiction.Naona mkiweka masahihisho madogo madogo mtafika mbali sana .All the best to you all!

    ReplyDelete
  19. Jamii Forum kuna Injili juu kabisa lakini hakuna Kaswida za waislam ni kweli ina udini mkubwa na waislam hawapewi nafasi .hapa kama kuna kipaimara michuzi anaweka.tena kule ukiwa unawashambulia Chadema kina mwanakijiji wana disclose IP adress ya computer yako.watu makini msinde kule.

    ReplyDelete
  20. Hao wamiliki wa Jamii Forum ni nafisadi wakubwa sana. Huibuka na kudai kwamba "tumeelemewa na gharama karibu Jamii itafungwa" basi huchangiwa mamilioni ya pesa na Watanzania nje na ndani ya nchi, lakini cha kushangaza hata siku moja hawajawahi kuonyesha gharama zao za kuendesha forum yao kwa mwezi/mwaka ni kiasi gani.

    Hakuna uwazi kabisa wa pesa wanazokusanya kwa mamilioni wanazitumia vipi na inaelekea huo ni mradi ambao unawaneemesha wamiliki wa jamii. kinashongaza hawa wachangiaji hawaulizi hata mchanganuo wa matumizi ya ya Jamii.

    Ndiyo narudia tena wamiliki wa Jamii Forum ni mafisadi kwa kukusanya mamilioni ya pesa lakini hawako tayari kutoa matumizi yao.

    ReplyDelete
  21. KWELI KABISA MANENO YA ZITTO DHIDI YA CHADEMA WALIVYOMUHUJUMU WAMEYAFICHA.HATA KIBARAKA WA MBOWE THE SO CALLED MWANAKIJIJI HAJACHANGIA KITU KWANI BOSI WAKE ANASHAMBULIWA NA ZITTO.ZITTO KALELEZA HADI HUJUMA ZA MBOWE KWA WANGWE.
    SHAME ON U JF.

    ReplyDelete
  22. huko hakuna mvutoo too complicated badilikeni muwe flexible tutawatembeleeni tukishamaliza kuperuzi humu kwa mkuu wa blog bongo

    ReplyDelete
  23. hahahahaaaa annons bwana??

    hahahahaha...asanteni

    ReplyDelete
  24. JF ni binaadamu kwa hiyo mtegemee watafanya makosa, cha muhimu sisi jamii tuyachukue yaliyo mazuri na yanayoelimisha na yaliyo pumba tuachane nayo. Chadema wana problem kubwa na nichama kichanga mjue palipo na wengi hapakosi mengi vilevile ccm mjue ndio wameifikisha nchi hapa ilipo ambapo hakuna solutions ya kero ya ajira kwa vijana waliojaa vijiweni hadi mtu unaogopa kupita kwa kuogopa kuporwa japo wengi sio waporaji lakini ukikuta watu waliochoka sana wamekaa corner kuanzia mawio hadi usiku wa manane lazima unaingiwa na natural uoga. Iwe hili kundi la vijana wanabana mlangoni mwako au jirani na nyumba yako huwezi kuwa na amani na mali zako au watoto ulioacha nyumbani. JF, Issa michuzi na jamii kwa ujumla tuamke tuikosoe serikali kwa kuaddress mambo muhimu yanayotukabili ili nchi yetu iwe mahali salama. Tujaribu kuwa na uzalendo wa kuipenda nchi yetu na kuwa proud to be Tanzania na serikali yetu itekeleze majukumu yake ili na wao wasiumbuliwe kila kuchwapo.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...