Ndugu yangu Michuzi naomba niwaulize Watanzania wenzangu hasa wale wanaoongea english.
Hivi lugha yetu ni swahili au kiswahili? Jana nilipokuwa naangalia Big Brother Africa, mwakilishi kutoka Tanzania alikuwa anamuelimisha mwakilishi kutoka Angola akamwambia "You see we in Tanzania our national language we call it Kiswahili but in Kenya they call it Swahili.
Sasa mimi ninachoelewa Kiswahili ni lugha na watu wake ni Waswahili. Ukiongea English unasema "our national language is Kiswahili and our people are Swahili (Mswahili/Waswahili kwa lugha ya Kiswahili).
Naomba mchango wenu ndugu zangu juu ya hili. Imekaeje hii?
Naitwa Petro,
mswahili.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 25 mpaka sasa

  1. Ndugu petro nadhani hata wewe mwenyewe bado hujaelewa kabsaa pamoja na kujaribu kufafanua....Hakuna watu wanaoitwa waswahili...kuna Lugha ya kiswahili....na waafrica...

    Swahilli - in English
    Kiswahili - in Swahili

    Na ndio maana ukiwa nje ya africa ukiulizwa unatoka wapi unasema from Africa..which country?..Tanzania...tunaongea Swahili language....swahili ni LUGHA na sio watu...KISWAHILI kama unaongea ukiwa unaongewa in swahili language...nadhani utakuwa umenipata.

    ReplyDelete
  2. kutokama na elimu yamgu nikwamba , kiswahili ni kiswakili ila lugha yenyewe inaitwa swahili ukiwa umaongea lugha nyingine kwamfano, kihaya,kipare au kichaga ukiomgea kiiingereza utasema chaga tribe na si kichaga soo ukisema we speak kiswahili hapo utakua umekosea unapaswa kusema we speak SWAHILI... bila shaka tuko pamaja, utakua umeelewa .

    ReplyDelete
  3. salaaaam.
    kwa jinsi nijuavyo mimi 'kiswahili' ni wakati unapoongea lugha ya kiswahili na'swahili' ni wakati unatumia kiinglish.
    mfano; lugha ya taifa letu ni kiswahili.
    'our national language is swhili' NI HAYO TUUUUU

    ReplyDelete
  4. Kwa mtazamo wangu Swahili ndio mzizi wa neno lenyewe. So you have to say "Our language is swahili". Unapo weka 'ki' unakuwa umeongea kiswahili zaidi kuliko english. mara nyingi 'ki' inakuwa imetumika kama 'adjective'. Ni neno tunaloongezea kabla ya neno lenyewe (sijui kisifa au kivumishi....sikumbuki, mi najua kuongea tu)kama ambavyo unaweza kuongezea neno 'u' ukasema 'uswahili' au 'wa' na kusema 'waswahili'.Maana kwa mtazamo mwingine "swahili" is a region, from "Swahili land", eneo la pwani ya Afrika mashariki na visiwa vyake. Kwa mfano mtu hawezi sema "naongea Sukuma", atasema "naongea Kisukuma" au "I speak English" and not "I speak England". Au mtu husema "nakula kisukuma" (ugali mkubwaaaa....lol)akimaanisha namna watu wa "Sukuma land" wanavyokula. Vivyo hivyo kwa Kiswahili tunasema "naongea Kiswahili" kwa maana ya 'kwamba' naongea kawa watu wa swahili land waongeavyo.

    Nadhani nimejitahidi kidogo kujieleza ingawa mambo ya nomino na vitenzi nilishasahau tangu form one mwaka 47.Mdau mwingine ataongezea

    Mdau
    Cardiff

    ReplyDelete
  5. ukweli ni kuwa lugha ya tanzania ni SWAHILI, lakini unaposema KISWAHILI inamaana umeunganisha na ngeli "KI-VI" ambapo "KI" inasimamia umoja na "VI" inasimamia wingi. na kwa vile lugha ya SWAHIKI ni moja ndio inaanza na ngeli ya "KI" ukiunganisha unapata KI-SWAHILI, na ndio maana wengine utawasikia wakisema VISWAHILI wakimaanisha lugha ya SWAHILI kwenye wingi. kwa kumakizia ni kuwa kila neno la kiswahiki lina mzizi wake ambao haubadiliki hata hila neno ukilibadilisha kwa namna tofauti mfano neno "ANACHEZA" mzizi wake ni "CHEZ" kwa hio unaweza kusema CHEZEANA,CHEZESHA,ANACHEZWA,ANACHEZEA nk lakini juu ya kubalidilisha kote huko mzizi unabaki pale pale " "CHEZ", na ndivo ilivyo kiswahili mzizi ni SWAHILI ndio lugha lakini kwenye umoja unaweka ngeli ya "KI" kwa hio inakuwa KI-SWAHILI.
    MWISHO NAPENDA KUKWAMBIA KUWA WATANZANIA NDIO WANAJUA LUGHA YA KISWAHILI SANIFU KULIKO WA KENYA.

    ReplyDelete
  6. MH NAONA NA WE NA HUYO BIG BROTHER WOTE MNACHEMKA, LUGHA YETU KISWAHILI UKIONGEA KINGEREZA UNAITA "I AM SPEAKING SWAHILI" UKIANZA NA KI NI SAWA NA "KIINGEREZA" "KISWEDESH" "KIGERUMANI" LAKINI UKIONGEA KISWAHILI UNASEMA i AM SPEAKING "SWEDESH, "GERMANY ETC. sO KISWAHILI IT TIPICALLY UNAONGEA KISWAHILI NOT IN ENGLISH.

    ReplyDelete
  7. BWana petro kweli we mswahili na huyo mshiriki wako mswahili vile vile.

    English = English
    Kiswahili= Kiingereza

    Swahili = English
    Kiswahili = Kiswahili

    Sambaa = English
    Kisambaa = kiswahili

    Haya = English
    Kihaya = kiswahili

    kiswahili ni kwa kiswahili, swahili ni kwa kizungu, upo hapo!

    Mdau No 5 !

    ReplyDelete
  8. PETER NALITOLELASeptember 16, 2009

    KAKA HILI SWALI LA KIZUSHI MPLEKEE KAMUSI YA WEBSTER YAANI SHAKESPERE MTAKATIFU, NABII MTEULE MESIAH YOHANNA MASHAKA. YEYE NDIYE ANAYEELEWAGA MANENO KAMA HAYA KWA MAANA AMESOMA MUZUMBE CHUO CHA UNIVESITY YA ECONOMICS NDIO MAANA ANA AKILI NYINGI KULIKO NYWELE. WATU WOTE WA MUZUMBE MARA NYINGI NI WATU MAKINI SANA WENYE HEKIMA NA BUSARAMKAYA YOHANNA MASHAKA AMBAYE YUKO KWENYE VEKESHENI DARISALAMA. LAKINI KWA MKENYA KUSEMA KWAMBA KISWAHII NI SWAHILI NDO YALE YALE YA KANUMBA

    ReplyDelete
  9. Kaka michuzi lugha inaitwa Kiswahili na wanaozungumza ni waswahili.Umenipata
    Haya lete swali jengine???

    ReplyDelete
  10. Michango imeenda shule kweli...nimeelimika.

    Ahsante Wadau.

    ReplyDelete
  11. Mdau No 5..naafikiana na wewe
    "English = English
    Kiswahili= Kiingereza

    Swahili = English
    Kiswahili = Kiswahili

    Sambaa = English
    Kisambaa = kiswahili

    Haya = English
    Kihaya = kiswahili"

    very clear and imple!!!!

    ReplyDelete
  12. Kwa uelewa wangu naomba na mimi nichangie hapa. KISWAHILI na SWAHILI ni maneno yenye maana sawa kabisa ila yanaonekana ni tofauti kutokana na lugha ambazo zinatumika kutamka maneneo hayo.
    Mfano.
    1.- Nimejifunza kuzungumza KISWAHILI
    - I learn to speak SWAHILI
    2.- Lugha ya KISWAHILI
    - SWAHILI Language
    Ahante!!

    ReplyDelete
  13. Habari zenu,
    Lugha yetu jin lake ni SWAHILI, ambalo ndio asili ya Kiswahili yaani Ki- ni kiunganishi cha mwanzo tu kuonyesha ni lugha, kwa mfano China, wachina wanaongea lugha gani, KIchina, waingereza KIingereza, wamatumbi, kimatumbi, ki- ni kuonyesha ni lugha tu.
    Hata katika lugha zingine ni hivyo hivyo,England wanaongea English, Poland Polish -sh mwishoni ni kuonyesha ni lugha, ktika kiingereza ipo mwisho si lugha yetu inaweza mwanzo.

    ReplyDelete
  14. Swali linauliza alivyo sema Watanzania tunaongea Kiswahili na wakenya wanaonge Swahili..ni sawa....?Nahisi angesema wote tunaongea Swahili. kenya na Tanzania...

    ReplyDelete
  15. Naomba nitofautuane na wengi mliokuwa mnaounga mkono kwamba lugha yetu ni Swahili kwa kiinglishi.Watu wa pwani wanaitwa Waswahili kwa kiswahili na Swahili people kwa Kiinglish.Lugha ya Kiswahili inaitwa Kiswahili kwa kiswahili na Kiinglish hakuna tofauti
    Wako Mpemba

    ReplyDelete
  16. Nitoe mfano wa lugha mbili kufafanua.
    Endapo unaongea Kiingereza, lugha yetu ya taifa ni "Swahili". Endapo unaongea Kiswahili basi lugha yetu ya taifa inaitwa "Kiswahili".
    Ni sawa na ambavyo kama unaongea Kiswahili basi yai huitwa "Kiingereza" lakini kama unatema yai basi yai huitwa "English".

    ReplyDelete
  17. Huyo mwakilishi wetu BBA ni yaleyale ya kina KANUMBA!!!!!tutafika tuu hamna shida.

    ReplyDelete
  18. HAPA NI NGELI TENA KWA WALE WALIOSOMA KISWAHILI HATA CHA DARASA LA SABA, LUGHA YETU NI SWAHILI UNAPOONGEA KWA KISWAHILI NA KUWEKA KI MWANZONI NI UNAMAANISHA UMOJA WA HIKO KITU KWANI SWAHILI IKO MOJA TU HAMNA SWAHILI INGINE MAHALA POPOTE DUNIANI NA KAMA KIKO NDO HICHI HICHI SO THAT IS WHY TONAWEKA KI MWANZONI KAMA VILI KIHAYA, KINGONI. NA KAMA UNAZUNGUMZA KATIKA ENGLISH UNATAMKA SWAHILI KWA VILE KI HAIKO KATIKA LUGHA YA ENGLISH NA LUGHA YA TAIFA NI SWAHILI

    ReplyDelete
  19. Petro MswahiliSeptember 16, 2009

    Ndugu zangu wachangiaji ninawashukuru sana kwa kunielimisha wala sitanii. Asante sasa nimeelewa. Kumbe maneno haya ninayaandika kwa Kiswahili and correctly put I have written these words in swahili. Asanteni sana.

    Petro mswahili.

    ReplyDelete
  20. Ni nini asili ya neno 'swahil'?
    Ni neno litokanalo na lugha ya kiarabu 'sahel' likimaanisha 'pwani', 'ufukweni' au 'coastal' kwa kimatumbi cha ulaya. Likiwa ni neno la kuazimwa toka kiarabu, swahili linamaanisha pwani, na mtu aishiye pwani ni m'pwani' au m'swahili'. Halikadhalika, lugha izungumzwayo na watu wa pwani ikaitwa ki'swahili' . Kwa mantiki hiyo, ni sahihi kuita lugha 'kiswahili' regardless which languange is employed.kama kungekuwa na umuhimu wa kuongeza au kupunguza maneno au viunganishi, basi ni bora neno lote linebadilishwa kwa kiingereza (homework kwa waingereza kutafuta neno mbadala la 'swahili' au 'kiswahili' kwa lugha yao!kama ambavyo akina Shaban Robert walivyoyatunga maneno kama 'Uingereza', 'Ureno'etc ambayo hayamo katika kamusi yoyote duniani zaidi ya ile ya kimatumbi.

    ReplyDelete
  21. kaka michuzi chei chei !

    hapa kinachoendelea wengi wameelekeza kuhusu kiswahili ama swahili. kwanza ieleweke nini maana ya swahili. si kila mtu ni mswahili hapa kuna kila aina ya watu hata petro pengine hafai kuitwa mswahili ! swahili maana yake ni mwambao wa pwani ama costal area kwa kimombo sasa kwa vile tanzania imetawaliwa na wa pwani ndo mana ikawa inazungumza kiswahili lugha ya taifa hili wengi hawataipenda lakini ukweli utabaki kuwa ukweli.
    ndio maana ukiangalia maoni mengi utakuta yana matatizo ya uandishi .

    sasa kama wewe ni wa pwani ndio mswahili wengine ni wahaya wamasai na lugha zao zitakua kiswahili, kihaya, kimasai na kadhalika HII NI KWA KISWAHILI kama itakua kwa lugha nyengine basi itakua sawa kusema swahili , haya na masai.

    mdau kutoka bwagamoyo mzaramo mswahili.

    ReplyDelete
  22. MLIKUWA MNAMCHEKA KANUMBA BURE KUMBE HATA ELIZABETH HAJUI TOFAUTI YA KISWAHILI NA SWAHILI LOL.

    ReplyDelete
  23. DADA YETU KACHEMKA HAPO.

    ReplyDelete
  24. Mwaushe Ohiwa, SverigeSeptember 17, 2009

    yote sawa lakini ukisoma lugha ya kiswahili kama somo lako basi utajua ya kuwa Kiswahili kama lugha kinatokana na lugha za mwambao wa pwani ya bahari ya Hindi na waarabu waliita Sawa-hili na hapo wakoloni kwa kushindwa kutamka sawahili walitamka swahili na tukapata Kiswahili nadhani nimeeleweka.

    ReplyDelete
  25. wabongo saa ingine tuakiamua kuacha kuosha vinywa tuna akili! Hizi komenti za akili sana kama alivosema mdau hapo juu zimeenda shule hasa!
    Tujipe big five kwa kuchangia hoja bila mswaki leo,
    subilaga

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...