Jumuuiya ya watanzania waishiao Korea Kusini (TALIKO), kwa niaba ya uongozi napenda kuchukua nafasi hii kuwajulisha kuwa mkutano wetu utafanyika jmosi (Oct-03) 12:05pm ndani ya PEARL REST. & VINTAGE PUB 126-16 Itaewon-dong Yongsan-gu Seoul. -
Msiopafahamu wala msikonde huwezi potea kabisa, ni opp. na Manhattan Rest. /Goldfish Pub ukikata tu kona kulia baada ya UN Club kama unatokea Subway Satation Exit 3, Pearl Pub ipo jengo moja na Reggae Pub na Latin American Pub, kushoto ni 7eleven mart na kulia ni jengo la Cuncun Club.
Bahati mbaya ukipotea piga number hii. 010 51155703 (Manager) au 01031457025 Paul Nzuki -
Nadhani hapo ni sehemu poa kwa Chakula na kinywaji kwa bei poa kabisa! !- Muda, Agenda vyote katibu atawarushia hivi punde hivyo msikonde! - Kufika kwenu ndio mafanikio ya kikao chetu!!
Paul Nzuki
Ha ha ha ha ha kumbe korea kusini nako ni tambarare.Maelekezo kama upo Tandale.
ReplyDeleteUdumu Paul Nzuki!
ReplyDeleteJumuiya ya wabongo tulioko huku Afganistan tunapenda kuwasiliana na promoters wa miziki ili wasanii kama akina Ali Kiba na wengine watutembelee.
ReplyDeleteHali ya mabomu si mbaya sana hasa upande wa kusini na tunaweza kufanyia concert letu kwenye sehemu ya wazi mchana ili kuepuka mshtuko wowote wa milio ya silaha ama uvamizi wa namna yoyote
Tunaomba msitutenge kwani maisha popote na kwakweli tumezoea na tunafurahia sana maisha ya huku.
hatujihusishi na mambo ya vita ila kazi za mitaani ambazo zinalipa sana kutokana na jamaa kukosa manpower kwa woga wa vita
If u think am kidding u might be wrong
Akchuali am joking
Mkuu jinsi unavyoelekeza sidhani kama kuna mtu atapotea. Maana umetaja land marks zote muhimu: bar, pub, club, danguro, jumba la kamali nk. Hapo hapotei mtu! Na watafika wengi wakijua baada ya kikao si mwendo mbali kwenda kwenye viwanja vya starehe ya kila aina.
ReplyDeleteMkutano mwema wakuu.
mmhhh wee Paul Nzuki ndio nini watu wa huku huku hawajapata taarifa mpaka wajionee kwa michuzi?
ReplyDelete