Meneja Uhusiano na Mawasiliano wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Maneno Mbegu akibandika stika kwenye gari Dar yenye maneno yanayotahadharisha madereva kutoendesha magari huku wakiwa wamelewa. Stika hiyo ni moja kati ya 4000 zilzotolewa msaada na TBL kwa Kamati ya Wiki ya Nenda kwa Usalama leo. Pia TBL ilitoa msaada wa fulana 800 kwa kamati hiyo. Wa pili kushoto ni Kamanda wa Kikosi cha Polisi cha Usalama Barabarani, James Kombe,
Meneja Uhusiano na Mawasiliano wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Maneno Mbegu (kushoto) akimkabidhi moja kati ya fulana 800, Kamanda wa Kikosi cha Polisi cha Usalama Barabarani, James Kombe, ikiwa ni msaada kwa ajili ya maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama itakayoadhimishwa mkoani Mbeya kuanzia Septemba 28 hadi Oktoba 3, Mwaka huu. Katika hafla hiyo iliyofanyika Dar leo, TBL walikabidhi pia msaada wa stika 4000, vyote vikiwa na thamani ya sh. milioni 10.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. we maneno mbegu, huo ni msaada wa tangazo la kilevi? umaskini mbaya manake usalama barabarani na pombe wapi na wapi.

    ReplyDelete
  2. TBL acheni kufunika macho watu kwa kujifanya nyinyi mnasaidia kuimarisha usalama barabarani. Kama kweli muko serious katika hili acheni kutengeneza ulevi ambao mara nyingi umehsishwa kuwa ndicho chazo cha ajali.

    ReplyDelete
  3. Hivi James KOmbe anaweza kukimbia huyu na li kitambi hilo kweli????AIBUUUUUU tupu mwanausalama kuwa na li kitambi dizaini hii.mmmmh tutafika tuu.

    ReplyDelete
  4. Sticker 4000 kwa magari milioni 1

    ReplyDelete
  5. HIVI MIMI SIJAELEWA VZR AU? INA MAANA KAMA ILIVYOKUWA STIKA YA ZAIN MWAKA JANA NDIO MWAKA HUU ZINABANDIKWA ZA TBL(TANGAZO LA POMBE)? KAMA NDO HIVO KOMBE UNATUTAKA LAWAMA KUZINUNUA HIZO, PLS TUKO TAYARI KULIPA HATA BEI GANI LAKINI SIO KUITANGAZA POMBE..KAMA KUNA NJIA MBADALA SAWA YA STIKA NA SIO YA TBL. HATUNUNUI KUBANDIKA KNY MAGARI YETU HATA SIKU 1

    ReplyDelete
  6. Mimi huwa nashangaa hata kwenye tule tu jacket tunatoreflect mwanga usiku wanausalama huvaa juu ya uniform zao tumebeba matangazo ya CELTEL hii ni sawa kweli

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...