Bofya link hiyo hapo chini umsikilize msanii Ali Kiba akiongelea
umuhimu wa shule kwa vijana, hususan wasanii, katika Sporah Show

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 31 mpaka sasa

  1. kaka MICHUZI hiyo intaviyuu magumashi sana.jamaa anahojiwa kingereza yeye anajibu kiswahili kaazi kweli kweli.ni hayo tu.
    MDAU-UKEREWE.

    ReplyDelete
  2. Ali kiba english is not reachable...I remember him in Orlando, Houston, Seattle and Kansas....all he can say is this is Ali Kiba tuko pamoja....dogo ni kama kanumba anahitaji elimu zaidi..

    ReplyDelete
  3. EBu Acheni ujinga sasa, enterview yenyewe imechanganywa kiswahili na kiinglish, Naona Ali Kiba amefanya vizuri kuongea kiswahili!!!! kama radio ya kiswahili then ongea kiswahili.

    ReplyDelete
  4. WaTZ tujivunie lugha yetu. Tuchukue mfano wa nchi za Asia kama Japan, China. Wenzetu hawa baadhi yao wanajua Kiingereza lakini ukikutana nao wanaongea lugha yao. Mimi swali langu kwa huyo mwana dada, yeye anajua kabisa mtu anayemuhoji anaongea kiswahili kwani yeye amuhoji kwa kiengereza au anatuambia nini? Ndugu zangu kwa dunia ya leo kujua lugha za kimataifa ni vizuri lakini sio maendeleo au usomi. Na maanisha kuongea Kingereza sio kwamba ndio umefanikiwa kwa kila kitu. Tukipende na kukienzi kiswahili, tujivunie kwani ukisafiri nje ya mipaka yetu wenzetu wakisikia kiswahili wanajua wewe Mtanzania, hata watani zetu wa jadi wanatuhemu kwa hilo.

    ReplyDelete
  5. ndio ndio ali kiba hapo umewamaliza waosha vinywa, unaelewa swali, kisha unadumisha lugha ya kibantu.

    ReplyDelete
  6. sikujua kama kiingereza ndio elimu. kwahiyo waingereza wote ni maprofesa!

    ReplyDelete
  7. Kitu kidogo cha kufanya...kama unaona kimobmo kitasumbua fanya mahojiano kwa kiswahili kitupu...na mwambie anayekufanyia hayo mahojiano.kama kimobo kinapanda fanya kwa kimombo na SIO KUCHANGANYA!na kwa hapo kaka Kiba umeogopa kukanumba...poa tu.

    ReplyDelete
  8. Wasanii wa bongo jamaaani, kwa nini mnakuwa hivyo, nendeni angalau tuishion ya kiingereza jamani, mnatuaibisha

    ReplyDelete
  9. Stay in school kids!

    ReplyDelete
  10. jamani hapa ! waosha vinywa mna nongwa!kwa ustaraabu sio lazima KIINGILISHI kipande,acheni ulimbukeni wabeba mabox ,chuki za nini? Ali Kiba akijitaidi kiasi chake,mbona wasanii wengine wanaongea lugha za kwao na kuwekewa tafisiri ya maandishi chini.

    ReplyDelete
  11. VISA za kuja kufanya tour UINGEREZA na MAREKANI alipata vp?au ndio aliomba mkalimani wa hizo BALOZI mbili atafisiliwe wakati wa intaviyuu.wasanii wa BONGO mhhhhhh
    kaazi kweli kweli.
    MDAU-ukerewe!!!

    ReplyDelete
  12. KWANZA KABISA NATAKA KUOSHA KINYWA CHANGU KWA KUSEMA KWAMBA KUOONGEA KINGEREZA SIO USOMI,KWANA NAWAFAHAMU WATA KIBAO WAMEMALIZA CHUO LAKINI KIINGILISHI BADO MUSHKELI.
    SASA HIVI BONGO TULITAKIWA TUKIENZI KISWAHILI ,KWENYE MAMBO MENGI
    ASILIMIA 80 YA WATANZANIA HAWAJUI KINGEREZA NAAMANISHA WATU WANAOTOKA VIJIJINI,WANAMUZIKI WANATUMIA KISWAHILI KWENYE NYIMBO ZAO,WANASINEMA WANATUMIA KISWAHILI KWA NINI WAOJIWE KINGEREZA KAMA UJUMBE UNATAKIWA KUFIKA KWA WAHUSIKA ALIOWAIBIA.
    ALIKIBA UMEFANYA VIZURI KUJIBU KWA KISWAHILI INGAWA MAJIBU YAKO HAYAJAJITOSHELEZA

    ReplyDelete
  13. Hata Kanali Ghadafi alihojiwa wiki hii www.cnn.com/GPS alitumia lugha ya kiarabu kujibu mwaswali ya mtangazaji yaliyokuwa ktk lugha ya kiingereza.

    Kanali Ghadafi alikuwa anataka watu wake wa libya na Mashariki ya kati waelewe nini anaongea ugenini.

    Hivyo Ali Kiba pia amefanya vizuri ili sisi wamatumbi tuelewe anaulizwa maswali gani huko ughaibuni.

    Pia ni njia mwanana ya kukienzi lugha kubwa ya kiswahili inayoongelewa Tz, Kenya,Uganda,Rwanda, Burundi, DRC, Comoro, Somalia, Mozambique, Zambia, Sudana.

    Hivyo Kiswahili tukienzi kimataifa , asante Ali Kiba kwa kuonyesha mfano. Bado viongozi wetu wawe wanaongea kiswahili ktk dhifa za kitaifa wakati wa kuwapokea wageni Tanzania.

    ReplyDelete
  14. huyu demu vipi! anajua kiswahili alafu anamuhoji jamaa kwa kiingereza na hapo hapo nae anapiga kiswahili!!!!

    Kipindi ni zero (0), sijui dhumuni cha kipindi ni nini!!! kama watu wawili wakiongea lugha tofauti, pia hakuna ata maandishi yenye kuonesha tafsiri ya kiswahili kwenda ktk kiingereza au kinyume chake wakati kiba au huyo dada akiongea!!! Mlengwa ni nani? Mmatumbi au muingereza? Au ni kujionesha mnajua kiingereza?

    Kwa ufupi naona ni upotezaji wa muda!! Na kujionyesha. Onesha ubunifu! Ningekuwa Kiba, kamwe nisinge kanyaga hapo.

    ReplyDelete
  15. chingaz wanasema "Bah!" mimi nilidhania huyu dada hajui kiswahili, kumbe anajua! sasa kwanini ameanza kuuliza maswali kwa kiingereza?

    ReplyDelete
  16. Na mbona huyo dada anamkatisha sana Ali Kiba?!! Hamwaachi hata amalize anachotaka kukisema wajemeni?! Kha!

    ReplyDelete
  17. wewe dada kwakweli umeboa sana yaani ni kichefu 1x2, kwani lugha yako sio kiswahili? au ndio misifa tuu, ndugu yangu jina alitangazwi kiivyo mwe!? umetokota kijana utetezi huko katika lugha yako!!!!!
    mwenyewe misiiiifa fyuuuuuuuuziii!?


    Dr. Mongi USA

    ReplyDelete
  18. Hata hao wanaolaumu na kupomponda Kiba wenyewe baadhi yao pia kiswahili ni kibovu mno. Angalia post zao. 'Kutafsiliwa' ndiyo nini?
    Mwaona kibanzi cha Ali Kiba, Boriti zenu vije?

    Pana kazi kweli kweli

    ReplyDelete
  19. duu, dogo una kazi kweli kweli mdada anakutega.,,, kwani lazima akusogellee kihivyo, hajui weye ustathi nini" afu ananiuzi kuongea commu wakati walengwa ni wabantu,, ama basi angeweka tafsiri, heri yake kiba kaelewa maswali kuliko The G a.k.a K.
    kiswahili asikuambie mtu ni kitamu haswa ukikiweza kama mzee Gorogosi vile wangenikoma, maana huhitaji kufikiri hivi nimepatia au la yaani unakitema tu. Dogo nimefupenda nahisi unajiheshimu vilivyo hata kama sikujui sana.

    ReplyDelete
  20. Advocate JashaOctober 02, 2009

    Jamani kujua kingereza sio kipimo cha elimu kwa bahati mbaya hii kasumba ya kuamini kua kuelimika ni kutema ug'eg'e.Hii inanikumbusha wakati kiongozi mmoja wa juu huko Zanzibar alipotembelea Uingereza bada ya kurudi akaja na maneno yafuatayo "Nimegundua watoto mashuleni Hamsomi!na walimu mashuleni hamfundishi!Juzijuzi nilikua Uingereza mtoto miaka mitatu anatema ug'eg'e kama mtu mzima!

    ReplyDelete
  21. Bravo Ali Kiba,
    Mdada kakuletea kimombo chake ukampa jibu kwa kiswahili.
    Kwa maana hio ulikua unajua anachoongea.

    Hapa ninayemuona mshamba ni huyo mdada.
    Unamhoji mswahili mwenzako halafu watumia kimombo? kwa ajili gani?
    Na hata hao watoto kama wangekua wanapitia hii blog na hawajaenda shule wangemuelewa huyo mdada?
    Kiba kama ni mtihani umepata 10 juu ya 10.

    ReplyDelete
  22. wasiojua kiinglishi ndio hawa wanaotetea kiswahili eti tundumisha utamaduni. Kuongea kiinglishi ni lazima ktk dunia ya sasa hivi, hamjiulizi ni kwanini tz inaogopa kuingia EAC?
    hata hao waarabu kizazi kipya sasa hivi wanasoma nje ya nchi zao ili tu kujifunza kiinglishi, msije mkajikuta baada ya miaka 10 duniani ni bongo pekee ngeli matatizo.

    unaesema kwanini mtangazaji anauliza kiinglishi jua kwamba malengo yao ni kuvuka mipaka ya tz.

    aliamua kumix na kiswahili ili kuepuka balaaa

    ReplyDelete
  23. MIMI SWALI LANGU KWA HUYO MTANGAZAJI KWANINI ATUMIE KIINGILISHI????

    NA ANAJUWA ANAEONGEANAE ANAJUWA KISWAHILI NA ANAMJIBU KISWAHILI AU KIINGILISHI KWA HUKO NYUMBANI NI KITU CHA KUJIVUNIA SANA??????

    AU NDIO MBWEMBWE ZA MTANGAZAJI AJIONYESHE KUWA ANA ELIMU SANA KWA KUONGEA KIINGILISHI PASIPO NA MAHITAJI YAKE??????

    NA HUYO ALI WA KIBA NAE SIO KAMA AMETAKA KUJIBU KISWAHILI KWA KUPENDA AU KUTAKA KUJIVUNIA LUGHA YAKE HAPANA..........HUYO KIJANA KIINGILISHI IS NO RICHABO

    KWANI TUNAMJUWA VIZURI HATA ALIPOKUJA HUKU KWETU UHOLANZI TULIMUONA ALIKUWA HAJUI KIINGILISHI.......LAKINI SIO MUHIMU SANA MUHIMU YEYE NI MSANII WA MUZIKI WA KIZAZI CHETU CHA FLAVA ZA BONGO BASI KISWAHILI NDIO KINATUMIKA KWA VINA NA MASHAIRI......mdau uholanzi nawakilisha.

    ReplyDelete
  24. British Council in Dar reiterates stance on English language test

    By Angel Navuri
    2nd October 2009

    The British Council in Dar es Salaam has reiterated its stance that all Tanzanian students applying for further studies in British universities would have to prove their language capability through English test to asses their proficiency.

    Sally Robiman, the British Council Director made the statement when responding to questions from journalists during a press conference held in Dar es Salaam on Tuesday.

    The question was about complaints raised by Tanzanian graduates who undergo English test when they want to join British universities, something many of them believe “is unnecessary.”

    “The issue of Tanzanian graduates undergoing English test to prove their proficiency has not been brought up by the British Council, but the British universities themselves,” she said.

    Robiman added that as long as English test is a must requirement by the British universities there is nothing the British Council could do about it.

    She said that English test has been there for British universities and this is one way to prove capability of English language both oral and written since it plays a big role for the studies.

    SOURCE: THE GUARDIAN www.ippmedia. com

    ReplyDelete
  25. IS HE A BATTY MAN????

    ReplyDelete
  26. Kuna mambo kazaa inayotaka kuyasema kwenye hii mada:
    1) Ali Kiba anaulizwa kwa kiingereza, yeye anajibu kiswahili. Tatizo angekuwa anaongea kiswahili fasaha basi..lakini anajidai kiswahili kama akipandi vizuri vile.Sijui ndio mbwembwe hizo au?

    2)Sporah anajua kiswahili fasaha kwa nini anamuuliza maswali kwa kiingereza wakati anajua Ali Kiba, hayuko sawa na lugha hiyo ngeni?

    3)Kwa wataarishaji, kama mnataka watazamaji wenu kwa lugha ya Kiswahili au kiingereza wawaelewe vizuri, kwa nini msiwe na mkalimani wa kutafsiri mahojiano?
    Ili muweza kutumia lugha ambayo muojiwaji anaiweza vizuri? Kwa sababu mahojiano yanakuwa hayajitoshelezi kwa sababu muhojiwa anakuwa hana uweleo wa kutosha kwenye Lugha unayotumia mtakazaji

    Ahsante!

    ReplyDelete
  27. ALI KIBA UMENIFURAHISHA----

    HUYO DADA HAPO ANAJIFANYA KUONGEA KIENGEREZA WAKATI KISWAHILI WOTE MNAJUWA.

    KISWAHILI LUGHA YA TAIFA.

    ALI KIBA- UKIWACHA YOTE ULIYONIFURAHISHA SANA ANAKUULIZA SWALI AMBALO ANALO JIBU. NAUMEMPA MAJIBU KIMIKATO TU SAAAAAAFI.

    ReplyDelete
  28. Kama hao graduate wa kibongo hawaoni umuhimu wa huo mtihani wa kiingereza hapo british council kwa sababu huo mtihani unagharimu pesa, kwa kweli wana sababu ya msingi ya kutokukubali kufanya huo mtihani.
    Lakini kama kuna graduate yoyote aliyewahi kufeli huo mtihani wa kiingereza, basi tuombe mungu atusaidie.

    ReplyDelete
  29. Huyo Sporah ndio anajifunza kuwa talk show host, sasa wadau hebu mwacheni dada aendeleze libeneke.

    Kitu ambacho kiliniudhi na hii ni pale anajaribu kuelezea anachosema Ali Kiba kwa kiingereza, bora angeweka subtitles.

    Vilevile nimeangalia hizo interview zake, kingine kinachoboa ni hiyo editing, yaani clips zinakatika katika, sasa sijui kwanini wanakatakata hovyo (kama mnataka different angles za shots basi nunueni camera nyingine).

    Mfuate taratibu za kufanya interview kwa mfano kuwapa wasanii maswali mtakayosema na sio mbaya hao wasanii wafanye pre-test.

    Usifikiri wasanii wa kimataifa kama Wyclef, etc wanapokwenda kwenye radio na tv, wanajibu papo hapo na wao pia wanapewa ile script ili wajibu vizuri.

    Hiyo ni senti hamsini yangu tu kwa Sporah na timu yake.

    ReplyDelete
  30. Huyo DADA ni ZERO ZERO 000 ALi KIBA 100% Umefanya vizuri kaka. Huyo mtangazaji should know better kama unamuhoji mtu anaeongea kiswahili kwanini basi usiongee kiswahuli chote. Mtangazaji unachanganya ya nini? ALI KIBA UMEFANYA VIZURI SANA KUMPITA HUYO PROFESSIONAL REPORTER OR JOURNALIST WHATEVER SHE CALLS HERSELF> WAY TO GO KIBA!!!!!

    ReplyDelete
  31. Wewe mdau hapo juu acha lugha zenu za London (Batty man!!!?) maeneo Ladbroke Grove, Brixton, Tottenham, sio vizuri kama huna la kuchangia ktk blogu ya jamii kaa kimya.

    Mdau
    J.Boris
    Royal Borough of Kensington & Chelsea.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...