Dkt. Augustine Mahiga

Na Mwandishi Maalum

Balozi wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Dkt. Augustine Mahiga atatunukiwa Tuzo ijulikanayo kama ‘ “The Spirit of the United Nations” kwa mwaka wa 2009.
Balozi Mahiga anakuwa mwana-diplomasia wa tatu kutunukiwa tuzo hiyo tangu kuanzishwa kwake mwaka 2007.

Waandaji na watoaji wa tuzo hiyo ni Kamati ya Taasisi isiyo ya kiserikali inayojihusisha na masuala ya kiroho, maadili na mambo yanayo hususu ulimwengu katika ujumla wake (CSVGC-NY), ikishirikiana na taasisi nyingine isiyo ya kiserikali ya Umoja wa Mataifa inayo husika na masula ya mikutano na uhusiano.( CONGO)

Aidha kuanzia mwaka huu wa 2009 waandaji wa Tuzo hiyo ya “The spirit of the United nations”, wameamua iwe inatolewa kwa makundi matatu ambayo ni wana-diplomasia,wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa, na wawakilishi wa taasisi zisizo za kiserikali ambazo zinauhusiano na Umoja wa Mataifa kupitia Kamati ya inayohusika na masuala ya Uchumi na Maendeleo ya Jamii (ECOSOC) au Idara ya Mawasiliano ya Umma (DPI)ya Umoja wa Mataifa.

Balozi Mahiga atatunukiwa tuzo hiyo Oktoba 26 katika wiki ambayo taasisi hiyo huadhimisha wiki ya kiroho, maadili na masuala yahusuyo ulimwengu. Maadhisho ya wiki hiyo yalizunduliwa rasmi mwezi Octoba mwaka 2007 kama sehemu ya kuendeleza utamaduni wa amani kama inavyotambuliwa ndani ya katiba ya Umoja wa Mataifa.

Kwa mara ya kwanza Taasisi hiyo ilimtunuku Tuzo hiyo mwaka 2007, Balozi Anwarul K. Chowdhury, (2007) aliyekuwa kwa wakati huo Katibu Mkuu Msaidizi wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia masuala ya nchi maskini na zinazoendelea, nchi zisizokuwa na bahari, na nchi zinazoendelea za visiwa vidogo.

Balozi wa Pili alikuwa ni Balozi wa Kudumu wa Ufilipino katika Umoja wa Mataifa, Hilario G. Dvide, Jr. aliyetunukiwa tuzo hiyo mwaka 2008.Watunukiwa wote hao waliteuliwa kupokea tuzo hiyo kutokana na juhudi zao za kutangaza na kuendeleza masuala kiroho na maadili katika Umoja wa Mataifa.

Wanaopatiwa tuzo hiyo ni watu ambao pamoja na sifa nyingine wanatakiwa wawe wameonyesha kwa vitendo dira na maadili ya kiroho ya Umoja wa Mataifa kama ilivyoainishwa katika katiba ya Umoja wa Mataifa na Tamko la haki za Binadamu kama msingi mkuu wa kuanzishwa kwa Umoja wa Mataifa.

Aidha anatakiwa awe ni mtu ambaye amefanya kazi katika Jumuia ya Umoja wa Mataifa kwa takribani miaka mitano mfululizo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 16 mpaka sasa

  1. Ahmed SheriffOctober 20, 2009

    Pongezi Dr. Mahiga. Tunakutakia kila la heri. Mdau Ahmed.

    ReplyDelete
  2. Eti nasikia yeye ni Balozi wetu wa kudumu katika UMOJA WA MATAIFA.teh teh teh sasa sijui ni vigezo gani vinavyotumika katika serikali yetu ya Tanzania kuchagua hawa viongozi?!!!waosha vichwa wenzangu nisaidieni.Hongera kupata hiyo Tuzo
    Mdau-Ukerewe!!!

    ReplyDelete
  3. Pongezi za dhati kwa Mheshimiwa Balozi! Tunafurahi kwa kuipatia sifa Tanzania. Mdau wa Ukerewe, uliza nini maana ya 'Balozi wa kudumu Umoja wa Mataifa' uelimishwe na siyo uulize swali lako kwa kebehi. Nafasi hiyo ina maana zaidi ya hivyo unavyofikirikuwa ni ya upendeleo. Ninatumaini utaeleweshwa na wenye kufahamu.

    ReplyDelete
  4. Hongera kwa Dk.Mahiga. Kwa ufahamu wangu kidogo jina au neno la balozi wa kudumu ni kwa sababu tu ya tafsiri ya kiingereza kwa mabalozi wote wa umoja wa mataifa. Fuatilia http://www.un.org/members/missions.shtml utakuta zile ambazo kwa sehemu nyingine zinaitwa 'Embassy', kule UN zinaitwa 'Permanent missions', na kwa faida zaidi waingereza zao zinaitwa 'High comissions' na wawakilishi wa hizo sehemu wanapaswa kujulikana kutokana na jinsi ubalozi unavyoitwa, mfano Embassadors, Permanent repreentatives, na High comissioners. Kazi inakuja sasa ukifanya translations kwa kiswahili, maana inaweza kupotea. Kifupi yeye ni balozi tu kama walivyo wengine, na uchaguzi/uteuzi ndiyo uleule tu.
    Nawasilisha.

    ReplyDelete
  5. ale bela mnyalukolo..inguluvi itange hongera sana

    ila iyo ya balozi wa kudumu ata mie hainiingii akili kabisaa,tueleweshwe

    ReplyDelete
  6. PETER NALITOLELAOctober 20, 2009

    MICHUZI WEWE UMENISTUA KWELI NILIVYO ONA PICHA NA MWANZO WA MANENO BALOZI AUGUSTINE MAHIGA BASI MIMI NIKA FIKIRI AMEAGA DUNIA...WEWE MICHUZI USIWE UNATUPA PRESSURE WENZAKO HATUZIWEZI

    ReplyDelete
  7. Hiyo tafsiri ya habari haiko sahihi.

    Wewe mshamba hapo juu balozi wa kudumu ni jina linalotumika kwa mabalozi wote walioko UN, hata kama atakaa siku moja.

    Michuzi hawa watu wengine uwe unawajibu huko huko, wanatuchafulia siku.

    ReplyDelete
  8. kabagabaho! kafanya nini cha maana???

    ReplyDelete
  9. Kaka MICHUZI namjibu huyo annoy wa 20 oct saa 04:40:00 kama ifuatavyo.tuko katika blogu ya jamii kuchangia mada na wala si kukosoana PUMBAVU MKUBWA WEE.sasa kinachokushangaza ni nini mtu kuuliza maana ya ubalozi wa kudumu?!!.Kaka MICHUZI usinibanie post hii coment yangu ili huyo mdau aione alaaah.
    Mdau-Ukerewe!!!

    ReplyDelete
  10. Tuliowahi kufanya kazi na Balozi Mahiga tunajivunia heshima aliyopewa. Sio tu anastahili bali pia ni heshima kwa nchi yetu.

    ReplyDelete
  11. Huyu mzee alimpa vidonge vyake yule balozi wa marekani UN wakati wa Bush alikuwa anaitwa john bolton, jamaa ndiyo wale mlengo wa kulia kabisa. Nawapa homework wadau mtafute alichomwambia wakati muda wa john bolton umekwisha na hakuweza kupitishwa tena na senate ya marekani. Baada ya hapo nikamuheshimu sana....

    ReplyDelete
  12. Wakuu hivi ukitaka kujiunga na chuo cha diplomasia kigamboni requirements ni zipi? Umri umekwenda lakini I wouldnt mind kuspend miaka 2 hivi pale, vilevile itanisaidia kujuana na future foreign ministers/presidents.

    ReplyDelete
  13. SIZANI KAMA KUNA BALOZI AU KIONGOZI WA AFRICA ANASTAHILI KUPEWA TUNZO YOYOTE DUNIANI...KWANI HAKUNA WANACHOSAIDIA AFRICA CHOCHOTE.
    MDAU MONEY UK.

    ReplyDelete
  14. HILI JAMAA NI LINYALUKOLO LILILOKWENDA SHULE, KAMA MAREHEMU BALALI, ISIPOKUWA DR. MAHIGA HANA KASHFA YA KUIBA HELA ZA SERIKALI. DR. MAHIGA ALISHAKUWA BALOZI CANADA, MWAKILISHI KWENYE NGAZI ZA KIMATAIFA NA BALOZI NCHI ZINGINE. SOMA HABARI ZAKE ONLINE. MTANGLULIZI WAKE NAYE ALIKUWA MNYALUKOLO DAUD MWAKAWAGO. HUU SI UBALOZI NCHINI MAREKANI, BALI NI UN. BALOZI WETU USA YUKO D.C PALE.

    ReplyDelete
  15. Anon wa Oct 20 07:50 ninafikiri unamaanisha Chuo cha Diplomasia Kurasini. Ninavyofahamu umri siyo kigezo ila kuna programu ambazo sifa za kujiunga ni kuwa na elimu ya kidato cha sita au 'equivalent qualification' na zipo ambazo utahitajiwa kuwa na degree ya kwanza. Nilisikia kuwa wana mpango wa kuanzisha programu nyingine mwaka huu, ila sina uhakika. Kwa programu zote kuna kiwango cha kufaulu ambacho utategemewa kuwa nacho.

    ReplyDelete
  16. Asante kwa msaada wako anon wa Oct 21, 11:21:00 AM, nitajaribu kufuatilia. Nipo kwenye late 20s. Ila nadhani admission inaweza kuwa strict sana, sitashangaa kukuta nchi kama msumbiji na drc wanategemea chuo hicho hicho.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...