Ulaya na Africa Bw Morten Lundal.
Mahojiano kati ya Mkurugenzi wa Vodafone Barani Ulaya na Africa Bw Morten Lundal na Mwandishi maalumu MATINA NKURLU juu ya ujio wake nchini Tanzania.
Q.Unaweza kuwaambia Watanzania ni nini hasa kilichokufanya uje hapa nchini wakati kuna ofisi nyingi tu za Vodacom duniani kote?
A.Kitu kilichonifanya nije Tanzania ni kutaka kuweka mikakati bora ya mawasiliano na uchumi hapa nchini tukishirikiana na Serikali ya Tanzania kwa ukaribu zaidi.
Q.Kuja kwako hapa Tanzania umepata nafasi ya kipekee ya kuonana na Mh Waziri Mkuu wa Serikali ya Muungano wa Tanzania,Je ni vitu gani muhimu zaidi mlivyoongea?
A.Kwanza kabisa nilifurahi sana kupata nafasi ya kukutana na Waziri Mkuu wa Tanzania na tuliongea mambo mengi muhimu ya kuweza kuendeleza uchumi wa nchi hii kiujumla.
Q.Baada ya kukutana na Waziri Mkuu ulienda kuzindua mradi wa mifugo pamoja na jengo lake wenye thamani ya Milioni 12 kwa ajili ya watoto yatima, Yatima Trust Fund,Je unaonaje mfuko huu wa kusaidia jamii wa Vodacom Foundation unavyofanya shughuli zake hapa nchini?
A.Mimi napenda sana watoto,nilifurahi kuwaona watoto yatima, wa Yatima Trust Fund wakionekana na nyuso za furaha na nimeahidi kuwasaidia misaada mingine mbalimbali ili waweze kujikimu katika masomo yao kwani wanafanya vyema katika swala la masomo kuna baadhi ya watoto wapo vyuo vikuu kwa mjibu wa mlezi wa kituo hicho na wengine watatu wanajiunga na chuo kikuu mwaka huu,Pia nimefurahishwa sana na Vodacom Foundation inavyofanya shughuli zake hapa nchini Tanzania na ninaweza kusema ni mfuko unaofanya kazi zake kiumakini na ubora zaidi kupita mingine yote niliyotembelea.
Q.Wewe kama Mkurugenzi wa Vodafone Barani Ulaya na Afrika, nini wito wako kwa watanzania kwa watoto yatima?
A.Wito wangu kwa Watanzania kwa ajili ya watoto yatima ni kuwajali na kuwasaidia hawa watoto kwani hawana wazazi,na wazazi wao ni watanzania wenyewe kwa hiyo wawasaidie nao watakuja kulisaidia Taifa lao siku za usoni.
Angalau umetafasiri kwa kiswahili ili hata sisi wakina nanihii tusome na kuelewa...
ReplyDeleteMie nafikiri Hamujamuuliza maswali vizuri wamekuja kipi kuwekeza ili kije kuwasaidia watanzania Zaidi?
ReplyDelete